Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe, (Katikati), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Standi linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Corridor Spring mjini Arusha jana.

Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, imepewa changamoto ya kupanua wigo wa elimu kujitegemea, kwa kuongeza stadi za ujasiliamali, biashara na usimamizi wa fedha, huku ikipanua elimu ya ufundi stadi kufikia kiwango cha ngazi ya Diploma ya FTC na kuongeza idadi ya vyuo hivyo kufikia angalau kila wilaya iwe na chuo kimoja cha VETA.

Changamoto hiyo, imetolewa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Standi linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Corridor Spring mjini Arusha.

Prof. Maghembe amesema vyo hivyo vya kila wilaya, vitatumika kama chachu ya kuondoa umasikini, kwasababu elimu inayotolewa na VETA, huwapatia vijana stadi za maisha kuweza kujiajiri na kujitegemea.

Prof. Maghembe amesisitiza VETA, isiishie kwenye utoaji wa elimu tuu na kuwapatia vitendea kazi, bali pia iwapatie jinsi ya kupata mitaji na namna bora ya kutafuta masoko ya bidhaa zao, hivyo mhitimu akimaliza VETA, anaanza kujitegemea moja kwa moja. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof.

Idrissa Mshoro, amesema VETA, imeishaanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zilizoko mbele yake, ikiwemo ya kuboresha mafunzo wanayoyatoa kwa kuanzia na kuwajengea uwezo walimu ili kupata walimu bora watakaotoa wahitimu bora.

Prof. Mshoro amesema VETA imeshaanza mkakati wa kujisambaza kila wilaya, kwa kuanzia, imeshagharimia andiko na mchanganuo wa vyuo kila wilaya, na tayari imeishatenga Shilingi Bilioni Nne katika bajeti yake kujenga vyuo vipya viwili katika wilaya ya Makete na Ludewa na kuviboresha vyo vya Karangwe, Korogwe na Mwanga.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi, amesema lengo la kongamano hilo la siku mbili ni kupokea taarifa za utekelezaji wa malengo waliojiwekea kwa mwaka huu toka kanda zote 9 za Veta na kujadili changamoto zinazoikabili Veta pamoja na ufumbuzi wake.

Kongamano hilo, linahudhuriwa na wenyeviti na wajumbe toka kwenye kanda zote 9 za VETA,Wenyeviti wa Kamati za Kiufundi za Ushauri (TACs) na wadau mbalimbali muhimu wa VETA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...