Woinde Shizza,Arusha
Jumuia ya Afrika ya Mashariki(EAC) katika mwaka ujao itakabiliwa na changamoto kubwa za kuhakikisha inaondoa kero wakati wa kuanza kwa Umoja kamili wa Forodha na pia kuhakikisha nchi wanachama zina ridhia kwa wakati muafaka itifaki ya kuanzishwa kwa soko la pamoja.
Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa jumuia ya Afrika ya mashariki Balozi Juma Mwapachu wakati wa salamu zake za kuuaga mwaka huu wa 2009 kupitia vyombo vya habari ambapo jumuia hiyo imefunga shughuli zake mpaka mwezi Januari Mwakani.
Balozi Mwapachu alisema kwa Marais Jakaya Kikwete(Tanzania)Yoweri Museven(Uganda),Mwai Kibaki(Kenya),Paul Kagame(Rwanda) na Pierre Nkurunziza(Burundi) kusaini itifaki wa Soko la pamoja mwezi uliopita sasa itakuwa kazi ya mabunge ya nchi hizo kuridhia itifaki hiyo.
Alisema kuwa utekelezaji wa soko la pamoja unatakiwa kuanza kwa kasi katika kuelekea kwenye hatua inayofuata ya kuwa na sarafu moja ya Afrika ya mashariki.
Aidha Balozi Mwapachu alisema katika mwaka huo nchi hizo zitakuwa na jukumu la kuandaa mpango mkakati wa nne wa jumuia ya Afrika ya Mashariki wa mwaka 2011 na 2016 utakaolenga katika kuandaa programu za kiuchumi,ushirikiano wa kisiasa pamoja na sekta za kijamii.
Balozi Mwapachu alisema umekuwa na mafanikio makubwa hasa katika katika kupitishwa kwa sera muhimu na uboreshaji wa miundombinu. Alisema kuwa katika sera kubwa za pamoja zilizopitishwa zilikuwa ni pamoja na mikakati ya uboreshaji wa barabara,reli,usafiri wa maji na anga,bandari,mawasiliano ya simu,nishati na usalama wa anga
Balozi Mwapachu alisema kuwa mafanikio makubwa yalipatikana katika barabara baada ya kuzinduliwa kwa ujenzi wa barabara kati ya Arusha-Nambanga hadi Athi River Mapema mwezi Machi na wakuu wa nchi hizo katika eneo la Lengijave wilayani Arumeru mkoani hapa.
Alisema barabara hiyo ni muhimu katika kuunganisha kati ya Kenya na Tanzania mpaka Unganda na baadhi ya maeneo ya Rwanda na Burundi. Balozi Mwapachu alitaja mradi mwingine ni wa kuunganishwa nguvu ya umeme kati ya Kenya na Tanzania katika mpaka wa Namanga.
Mipango mingine ni pamoja na Mradi wa Kilimo na program za maendeleo vijijini,program za maendeleo za Bonde la ziwa Victoria. Alisema pia katika mwaka huu kumekuwepo na kazi kubwa ya ya kuhamasisha eneo hilo kuwa la soko la pamoja na uwekezaji ambapo mkakati huo ulikamilika kwa nchi hizo kukamilisha mchakato na hivyo kuanza rasmi kwa umoja wa forodha ifikapo Januari mosi mwakani.
Balozi Mwapachu alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakuu wa nchi zote tano zinazounda jumuia hiyi,baraza la mawaziri pamoja na asasi zote na taasisi za jumuia hiyo pamoja na wafanyakazi wote kwa kufanikisha malengo ya kazi za jumuia.
Aidha Balozi Mwapachu amewashukuru wadau wengine wa karibu ndani ya jumuia hiyo likiwemo baraza la Biashara la Afrika ya Mashariki,wananchi panoja na washirika wa maendeleo wa jumuia hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali ya hali na mali
MMELIWA, BAO LA KISIGINO HILO, WENZENU WATASUKUMA TEMBO KWA UBUWA, MTASHANGAA FELI WAKATI WENZETU WANAMBURUZA MLEVI KWA KIDOLE KIMOJA, MUNGU AWAPE NINI GUNIA LA CHAWA WAJIKUNE!! MKASHANGAE MATAA YA FAYA
ReplyDeleteje, na huu mpaka wetu wa forodha kati ya bara na visiwani pia utafunguliwa??
ReplyDeleteTHE BRAIN
Tanzanian exports to Kenya have registered 17% increase in value, narrowing the trade balance gap between the two countries.
ReplyDeleteKenyan High Commission to Tanzania, Mr. Mutindo Mutiso said Tanzanian revenue from exports to Kenya has grown to US$95.8 million (KShs7.3 billion) in 2008 compared to $86.6 million (KShs6.6 billion) in 2007. He said this was a 17% increment.
In 2006 Tanzania's exports to Kenya revenue stood at $59.1 million (KShs4.5 billion); in 2005 it stood at $36.8 million (KShs 2.8 billion) and in 2004 at only $26.3 million (KShs2 billion).
"The volume of exports from Tanzania to Kenya rose by 17% in 2008 while Kenya's export into Tanzania rose by 27% during the same period," said Mr. Mutiso.
Ambassador Mutiso added that Kenya's exports into Tanzania in 2008 were valued at KShs29.3 billion which is up from KShs22.3 billion in 2007. The value of exports from Kenya into Tanzania in 2006 stood at KShs18.3 billion.
Mutiso added that the fast rising of Tanzania's exports to Kenya will work to narrow the trade balance gap between the two
countries due to the increasing of cross-border trade and investments.
The move signifies that Tanzanian products have the competence to cater for the Kenyan market and trade between the two countries is expanding.
The major exports from Tanzania to Kenya include raw cotton and seed cakes, hides and skins, live animals, timber and timber products, fish and fish fillets.
Other major exports are milk, cereals (mainly beans and maize) fruits, onions, tyres, detergents, gemstones, groundnuts and power transformers.
Kenyan exports to Tanzania include fuels and oils, beverages and spirits, soap and other washing preparations, paper and paperboard, machinery and mechanical appliances, Other major exports from Kenya to Tanzania are motor vehicles, iron and steel and articles thereof, rubber and articles thereof, milled products, financial and banking services, and human and technical skills. High Commissioner Mutiso said another important aspect of the bilateral relations is with respect to Tanzania being major receipt of foreign direct investment (FDI) from Kenya with an overall investment portfolio of $ 2,087 million.
The multi-million dollar investment portfolio came from 346 investors as at December 2008 making Kenya the second largest injector of FDI into Tanzania after the United Kingdom. "Currently, there is more than 346 Kenyan companies operating in Tanzania which have cumulatively created over 45,737 jobs," said Mutiso. These investments are spread out in various sectors ranging from manufacturing, tourism, services, financial institutions, agriculture, construction, transport, petroleum and mining, natural resources, human resources and telecommunication.
Tanzania Investment Centre (TIC) Director of Investments Promotion, Mr. Raymond Mbilinya said recently most investments from Kenya have targeted the industrial and construction sectors.
Source: