Meneja uhusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa na wachezaji wa timu ya Taifa walioshika jezi zenye majina yao leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya shangilia taifa stars ishinde leo kwenye kiwanda cha Serengeti jijini Dar.

Promosheni ya shangilia Taifa Stars inaanza kesho kabla timu hiyo kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Cast Januari 4 na 7 jijini Dar.
Ivory Coast inajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Angola.
Promosheni hiyo itawafanya mashabiki mbalimbali wa soka katika baa mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali na jezi za timu ya Taifa pamoja na tiketi za kuingilia katika michezo hiyo neshno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. shangilia stazi kwa lipi la maana walilifanya zaidi ya kuwapa sifa wasizo stahili.
    Vitendo kwanza shangwe baada ya mavuno

    ReplyDelete
  2. Ndio yale yaleee! Nina wasi wasi hawa wanaopost hizi promotion humu katika blog ni viongozi wa TFF au hao Wadhamini. Sasa kama mnatambua umuhimu wa kupost hizi habari humu kwa nini msifungue Websites zenu halafu mkapost hizi habari nasi tukazifuata huko?? Grow up people!!

    ReplyDelete
  3. Hivi mshabahatika kumuona huyo DIDIER DROGBA hilo jimwili lake au huyo HARUNA DINDANE au TOURE wote wawili mkubwa na mdogo hayo majimwili yao ndio mkawapambanishe na hawa watoto sijui wakubwa wamefanya kudumaa tu loool..siajabu kweli wachezaji wetu wanaujua mpira sana lkn lishe duni sana mm naona sometimes huyu Maximo analaumiwaga bure tu jamani MPIRA NI STAMINA,NGUVU,TAKTIK NA CONDITION BAADA YA KUWA TAYARI UMESHAUJUA.wachezaji wetu vimbaumbau sana bwana tuwe wakweli na ndio maana kama ingelikuwa ngumi tanzania ingebidi icheze na timu za yosso weight ndogo mno

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...