Mwanamuziki Amani kutoka nchin kenya akiwarusha vilivyo wapenzi wa tamasha la Str8Muzik Festival;Intercollege Special 2009 ndani ya viunga vya hoteli ya Royal Village mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali lililandaliwa na kampuni a sigara TCC kupitia chapa yake ya muziki iitwayo Str8 Muzik.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes a.k.a Mr Misifa akiwaimbia washabiki wake wimbo mpya wa shikide ambao unaonekana kufanya vyema

Joe Makini a.k.a Mwamba wa Kaskazini akionesha umahiri wake wa kuimba free staili mbele ya umati wa watu uliofika kwenye tamasha la Str8Muzik Festival;Intercollege Special 2009 ndani ya viunga vya hoteli ya Royal Village mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo,



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ulimwengu na hususan nchi nyingi za ulaya ziko mbioni kupigana na vita juu ya matumizi ya Tumbaku na kutumia makampuni ya Tumbaku kuwa wadhamnini wa matamasha na mbio za magari.Leo hii kwetu hawa ndio wamekuwa wadhamini wakuu wa matamasha ya vijana??!Ni janja ya makampuni ya Tumbaku kuwaandaa vijana kuwa watumiaji wakubwa wa Tumbaku na kutangaza vita dhidi ya Afya.Makampuni haya ya Tumbaku na Sigara yamekuwa yakitumia nchi masikini na nyingi nchi za Afrika ili kueneza matumizi ya uvutaji sif=gara na matumizi ya Tumbaku.Kuna Ethical issu hapa ambayo viongozi wengi wa Afrika huenda wana hisa katika bidhaa zinazotokana na Tumbaku au kutokujua madhara ya Tumbaku au kupuuza, wamekuwa wakiwapa mwanya haya makampuni ya Sigara ambayo katika nchi zao asili hawawezi kufanya matangazo yao au kufanya udhamini wa matamasha ya vijana kama tuonavyo hii leo na sisi tunakuwa ni wenye kushabikia.Africa tumekuwa Guinea pig Ulaya mtoto ambaye yuko chini ya miaka 16 hawezi kununua sigara au bidhaa za Tumbaku lakini leo tunaona watoto walio chini wa umri huu wakishirikishwa kwenye matamasha ya kupromote bidhaa hizo za Tumbaku...tuko wapi waafrika?tunapelekwa wapi waafrika??Hatuwezi kufikiria?Wasanii ninyi ndio kioo cha jamii kwa nini msigomee udhamini huuu/au mnajali tu matumbo yenu na umaarufu wenu?Issa Michuzi kaka , tunakuomba uwe unaweka kwenye matangazo yako japo kwa dakika moja tangazo la hasara za utumiaji wa Tumbaku.
    Hebu tungalie hawa wenzetu...http://www.cbsnews.com/stories/2008/02/27/eveningnews/main3884821.shtml
    Mwl. Abal Hakam

    ReplyDelete
  2. annon #1 umesema yaliyo moyoni mwangu

    ivi of all kampuni lazima sigara?kweli na ilhali twajua madhara ya sigara kwa mtu?? eeeh kwanini wapewe hii show waidhamini na apo watu wa "marketing" wamemwaga misigara kibao wakiitangaza/kuuza kuua vijana hawa!!!eeh kweli kabisa

    nachukia sana huu ujinga wa mikampuni inayoua watu km hii kudhamini shughuli za kijamii

    nyambaf

    tuige zanzibar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...