Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga, katika mkutano wa
hadhara wa uzinduzi wa Operesheni Sangara, uliofanyika katika
Uwanja wa Tangamano jana jioni.
Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA Mh. John Mnyika akiwahutubia maelefu ya wakazi wa jiji la Tanga, katika mkutano wa uzinduzi wa Operesheni Sangara,
uliofanyika katika Uwanja wa Tangamano jana
Helikopta inayotumiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, ilipotua katika Uwanja wa
Tangamano jijini Tanga, ambako ulifanyika mkutano wa uzinduzi wa
Operesheni Sangara jana. Picha na mdau Joseph Senga



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. watu wamekwenda kuishangaa helikopta na si kumskiza freeman...ila pametisha

    ReplyDelete
  2. Hii manayake ni kwamba the more you tell them the more they open their eyes! na mwisho wa siku idadi kubwa ya wananchi watafunguliwa macho. si kazi rahisi Mr Freeman, lakini naamini wewe ni kamanda na mjumbe wa matumaini, Piga kelele usiache paza sauti kama tarumbeta uwahubiri watanzania ubaya wa CCM na shida tunazopata kwa sababu ya ufisadi huu!

    ReplyDelete
  3. tutafika na tutalikomboa taifa letu.Mjitokeze basi kujiandikisha na kupiga kura kwa maslahi ya vizazi.

    Maana nasikia wanaojiandikisha 200,000 wanaopiga kura 46,000.
    Watu wamekuja kumshuhudia kamanda si helikopta toeni mawazo ya kipuuzi

    ReplyDelete
  4. MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE APEWE.

    HUO UMATI KAMA UNGEKUWA UMEFUATA HELIKOPTA BASI WASINGEKUWEPO KWENYE JUKWAA LA WATOA HOTUBA NA MACHO YAO KUELEKEZWA KWA WAZUNGUMZAJI.

    BADO WANA SAFARI NDEFU LAKINI HATIMAYE WANAYOYAONGEA YATAKUJA KUNASA KWENYE VICHWA VYA WATU NA KUJA KUYAONDOA TENA ITAKUWA SIYO RAHISI NA HAPO NDIPO TANZANIA ITAPOANZA KUBADILIKA.

    INAKUWA KAMA BONGO FLAVA ILIVYOANZA VILE WATU WAKIUPONDA KUWA NI MUZIKI WA KIHUNI AU WAHUNI LAKINI WAKAJA KUUTEKA MUZIKI KISAWA SAWA.

    ReplyDelete
  5. Zitto kafulia.

    ReplyDelete
  6. Inawezekana kabisa sehemu ya umati imevutiwa na kopta. Lakini kama kopta inaweza kuvutia watu na hatimaye wakaondoka na fikira mbadala, basi hiyo kopta idumu, ni mbinu muafaka.

    ReplyDelete
  7. chadema kwishney,hakuna kitu hapo,chama cha ukoo hicho,alivyosema marehemu wangwe watu walimsakama anatumiwa na mafisadi,lakini uchaguzi wa ndani ya chama mwaka huu umeonesha wazi chama hiki kina wenyewe,zito na manaosuport wato wameanza kusulubiwa,bahati zito ni njanja,kwa maana hivyo elfu 2010 hamna jimbo tena chadema,labda tarime peke yake,maana kigoma na nccr wanaichukua mazima,matokea ya vijiji mwezi ulopita yameonesha moshi mjini chadema imeambulia viti 3 na ccm 7,kwa maana hiyo 2010 ndesamburo aote,ukiangalia karatu vile vile ccm imerudisha vijiji vingi huku dr slaa akijidai ataishitaki serikali kimataifa,sasa naanza kuamini cuf kitabaki kuwa chama kikuu cha upinzani tz kwa muda mrefu,japo na matatizo yao sera zao zinaeleweka.namuhurumia sana rwakatare,nadhani anajutia uwamuzi wake.

    ReplyDelete
  8. Jamaa hapo anamzungumzia ZITO aliyetulizwa na CCM, wanasiasa njaa! Jamaa ooh nataka kuwa mkufunzi! Uliingia siasa kufanya nini in the first place! Someday somewhere tutapata tu viongozi watakao simama for Tanzania no matter what! Sio hao wenye njaa zao baada ya mwakani you are gonne wala hutakumbukwa kwa lolote! Yaani wewe sawa tu na mafisadi wakina ENL, BPM, GM, etc.

    ReplyDelete
  9. Hawa jamaa wanahitaji michango ya kuendeleza kazi hii tukufu na takatifu. Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 ili kuwachangia, kwa wateja wa zain na vodacom. Au tembelea tovuti yao www.chadema.or.tz. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke

    ReplyDelete
  10. CHADEMA MNACHO HARIBU MNASHINDWA KUELEWA BASICS HAKUNA SIKU HII INCHI ATAJA ENDESHWA NA MCHAGGA WATANZANIA SIO WAPUMBAVU SELIKARI SI ITAKUA YA WACHAGGA MAANA WAHAGA HAWANA AKILI MMOJA AKIWA JUU ANAENDA KUWACHUKUA WENZIE WALIO BAKI UCHAGANI HATAKAMA HAWAJA SOMA WANAKUA KAMA WANAIGERIA WACHA WAIBE LAKINI WACHA AMANI IWEPO

    ReplyDelete
  11. anonymous wa Mon Dec 14, 03:31:00 AM unashindwa kuelewa hawa wenzetu wametuzidi wapi,ni kuwa waligundua umuhimu wa elimu toka miaka mingi iliyopita na hii ilitokana na historia wakati wa wakoloni wamisionari walihamia Kilimanjaro walipenda Kilimanjaro kutokana na hali ya hewa ilifanana na yakwao na ardhi yenye rutba na wakakaribishwa kule wakawaletea dini ya kikristo na wakajenga mashule,hii yote ili kuwashawishi wawakubali na wawe na hofu ya mungu ili waweze kuendelea na unyonyaji,na hii ikasababisha wachaga wengi kusoma na wengi kujali umuhimu wa elimu,sasa matokeo yake wachaga weng sana wameenda shule na wakaanza kuwah nafasi za ajira ukienda kwenye kila secta utawakuta wachaga nenda TRA utakuta wachaga kibao ukichunguza utakuta wako na qualifications zao nenda BOT utawakuta pia wameingia na qualifications zao,nenda vyuo vikuu Madocta na maprofesa kibao sasa kutokana na hiyo imefanya watu wengi wahis kuwa wachaga wanachukuana makazin lakin ni shule ndio inawatoa.Hivyo hivyo itakuja kutokea kwenye East Africa community wakenya weng sana wamesoma na wao watachukua nafasi nyingi sana za ajira Tanzania na tutaanza tena kulalamika na pia watatuzid kibiashara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...