Mama Salma Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Portland Cement, Pascal Lesoinne,wakitoa zawadi za vyakula na vitu mbalimbali kwa vikundi viwili vya watoto yatima vya Mbagala na Mama Theresa cha Mburahati. Vyakula hivyo vilivyotolewa na Kampuni ya Saruji ya Twiga vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20, kwa ajili ya sikukuu ya Krismas, Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za WAMA jijini Dar leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. michuzi mimi ni mtanzania nifanyeje ili niweze kumpata mama salima nikatoe naye zawadi kwa watoto wa mitaani??? please nisaidie....

    ReplyDelete
  2. Mbona jibu lake ni rahisi huna hata haja ya kumuuliza Michuzi. Nenda ofisi za WAMA kawaeleze madhumuni yako, utakutana na msaidizi wake atakupa maelezo ya nini cha kufanya. Na sidhani kama Michuzi ana majibu ya maswali yako unless kama utakuwa umeuliza kwa nia ya kukebehi, lakini kama unataka kweli nenda WAMA, toa burungutu lako kama ni 10m au hata 5M, manake sio tu unataka ujiko uonekana unatoa msaada kwa watoto wa mitaani ukiwa umesindikizwa na First lady msaada wenyewe wa elfu 50.

    ReplyDelete
  3. asante kwa majibu yako my dear, sio utani i real want to do for those kids they need us, hawa watoto wanamaisha ya ajabu sana hapa dunia,
    asante tena kwa ushauri wako na nitaufanyia kazi

    ReplyDelete
  4. Nawapongeza WAMA na Portland Cement kwa kuwakumbuka yatima wengine tufuate nyayo hizo.

    WAZO: WADAU NA SERIKALI IPANGE MIKAKATI ENDELEVU YA KULEA WATOTO YATIMA NA SIO KUWAPA CHAKULA CHA CHRISTMAS NA SIKUKUU NYINGINE TU. KABLA NA BAADA YA CHRISTMAS WALE NINI, WAVAE NINI, WAPATE WAPI MAHITAJI YA ELIMU N.K. TUWAZE KWA HERUFI KUBWA NA SIO KUFANYA MAIGIZO YA KUTOA VICHACHE HIVI ILI TUONWE KWENYE VYOMBO VYA HABARI TU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...