Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesogeza mbele kwa miezi sita zaidi tarehe ya mwisho la zoezi la kusajili namba za simu nchini ili kutoa fursa kwa wote wanaomiliki namba hizo kujisajili.
Tarehe ya mwisho ya kusajili
namba ya simu sasa ni Juni 30, 2010.
Awali TCRA ilitoa iliwajulisha wananchi kuwa kuanzia tarehe 1 Julai 2009 makampuni yote ya simu za mikononi yataanza kusajili wateja wao waliopo na wapya ili kuhakiki umiliki wa namba za simu wanazozitumia. Zoezi hili limeendelea kwa miezi sita na mwisho ulikuwa tarehe 31 Desemba 2009.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Mkomwa amesema leo jijini Dar kwamba zoezi la kusajili simu limeenda vyema na kwamba takriban namba za simu milioni 6 zimeshasajiliwa.
Amesema ulazima wa kusogeza tarehe ya mwisho mbele umetokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme na vitambulisho hasa sehemu za vijijini. Akaeleza imani yake kwamba ifikapo Juni 30 mwakani kila mmoja atakuwa ameshasajili namba yake.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawahimiza wananchi kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo ambavo yametayarishwa kwa mfumo wa maswali na majibu kwa mujibu wa tangazo hilo la awali:
1. Swali: Kwa nini usajili namba ya simu?
Jibu: Kwa ajili ya kukulinda wewe na namba yako dhidhi ya matumizi mabaya ya simu.
2. Swali: Kitambulisho cha aina gani kitahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Ili uweze kusajiliwa unahitaji kufika kwenye ofisi ya kampuni yako ya simu au wakala
wake na moja ya vitambulisho vifuatavyo ambapo utawapatia kivuli chake:-
(i) Kitambulisho cha mpiga kura
(ii) Pasipoti
(iii) Kitambulisho cha mfuko wa pensheni
(iv) Leseni ya udereva
(v) Kitambulisho cha SACCOS
(vi) Kitambulisho cha benki
(vii) Kitambulisho cha ajira pamoja na barua ya mwajiri
(viii) Kitambulisho cha chuo cha elimu ya juu
(ix) Kitambulisho cha uanachama kwenye kilabu
(x) Barua ya serikali za mitaa ikiwa na picha, sahihi na muhuri
3. Swali: Nisipojisajili ifikapo tarehe 31Desemba, 2009 nini kitatokea?
Jibu: Namba yako itafungwa ili usiweze kuitumia kwenye mtandao wa simu nchini Tanzania.
Jibu: Namba yako itafungwa ili usiweze kuitumia kwenye mtandao wa simu nchini Tanzania.
4. Swali: Nani na wapi ninaweza kusajili namba yangu ya simu?
Jibu: Unaweza kusajiliwa na kampuni yako ya simu za mkononi au mawakala wao waliopo sehemu mbali mbali nchini.
5. Swali: namba ngapi za simu (simcard) ambazo ninaweza/ninaruhusiwa kusajili?
Jibu: Idadi yoyote kadri utakavyo.
7. Swali: Kuna uhakika gani wa usiri wa taarifa zangu nitakazotoa kwa kampuni ya simu za mkononi au wakala wao?
Jibu: Kampuni zote za simu nchini zinawajibika kwa mujibu wa sheria, kutunza taarifa za wateja wao ikiwa ni pamoja na taarifa za matumizi.
8. Swali: Taarifa zipi zinahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Tafadhali angalia mfaano wa fomuya usajili hapo chini:-
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
SIM card:
ReplyDeleteDefinations of SIM card is:-
Subscriber Identity Module.
A SIM card must be inserted into the user's mobile phone before it can be used. A SIM card identifies a mobile customer and his provider.
In addition, a SIM card may store the mobile customer's personal information as well and contain special functions for the mobile to work according to the service providers systems.
I dont know how it goes/works there in Tanzania, but in Europe if you pick up PAY AS YOU GO SIM CARD when you start using it you will be asked to register it automatically, they will ask you your information and the service provider will put your information in the company's data base, I dont know how it goes in Tanzania! it means you can buy your Sim card and start using it without being asked to register it? if that is the case then the service providers are to blame not customers, they must have that system requires their customers to register before using the Sim card.
Simply not true. My granddaughter has been to Europe twice and she tells me while you may be "advised" to register a PAY AS YOU GO NUMBER you really don't have to do it by law and you are free to simply go and use it straightaway. There are, however, many ways of indirectly enforcing registration - such as offering to send you a Pay As You Go SIM card to your address - in which case it is registered automatically. In any event, so my grand daughter tells me, registering or not registering a SIM card has only limited benefit to service providers - it is probably more beneficial to law enforcement organs and, indeed, the SIM card owner, than to, say, Vodafone. The SIM owner and/or user can always be traced should there be the need to do so.
ReplyDeleteYES! THIS IS AFRICA. HII INAONESHA NI JINSI GANI TUSIVYOPANGILIA MAMBO NA KUJALI WAKATI, BORA LIENDE TUU. TCRA IMEONGEZA MUDA BILA KUZINGATIA UTAALAMU, MIEZI SITA WAMEITOA WAPI NA WAMEZINGATIA NINI, ETI TATIZO LA UMEME WA KUTOA KOPI ZA VITAMBULISHO! HIVYO ONGEZEKO HILI LITAWAWEZESHA WATU KUTOA KOPI! NINAUHAKIKA HATA BAADA YA MIEZI SITA WATAONGEZA MUDA NA MWISHO WA SIKU USAJILI UTAISHIA JALALANI NA HILI LINATOKANA NA KUTOKUPANGA MAMBO YETU KWANI TUPOTUPO TU.
ReplyDeleteTCRA mumechemusha. Kuna watu hata mfanye vipi hawaji ng'o mpaka deadline ikikaribia.
ReplyDeleteSasa hivi si mumeongeza muda sio? Basi wale wote waliokuwa wanapanga foleni kusajili wameghairi. Watakuja tena June 29, 2010.
Halafu mtawasikia wakilalamika "Oooh muda hautoshi" ... "Umeme unakatika" ... "Photokopi zimekufa" na upuuzi mwingine kama huo.
Nyie subirini tu. Ila kwa ufupi mumechemusha.