kocha wa Taifa Stars Marcio Maximo yuko katika lala salama ya mkataba wake na hivi sasa anaifundisha timu ya bara Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya chalenji ambapo baada ya kutolewa na Rwanda kwenye nusu fainali itapambana na ndugu zao Zanzibar Stars kuwanua nafasi ya tatu. wadau karibuni katika mjadala wa kumjadili kocha huyu bila kutumia maneno ya jazba na pia tuje na mawazo mbadala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 73 mpaka sasa

  1. mie sioni tatizo la kutoa nizamu kwa wachezaji ni vibaya ankubaliana na maximo,wachezaji lazima wawe na nidhamu na kueshimu profesheno zao.ila nataka kujua wachezaji wa taifa Star wanachaguliwa vipi na je wanapimwa vipi kuonekana wako fiti kuchezea Taifa Stars,manake sio tunamlaumu sana Maximo kwa kuchagua timu mpya kila siku,ila tujiulize maswali je Hawa wachezaji wetu je wanauwezo kweli wa kucheza kabumbu la kitaifa.Manake kabumbu sio lele mama na sio nguvu za Soda unatakuwa uwe super talent na super fit.je wachezaji wetu wanayo hayo au? na sio majigambo na kumlaumu kocha kila siku.

    ReplyDelete
  2. maximo hana jipya timu imemshinda kwa kucheza mpira wa kisasa na nidhamu mbovu kila siku wachezaji wanapewa kadi nyekundu. tumuombe partick phiri afundishe kwa miaka miwili tuone matunda yake kwani soka la kiafrika analijuwa sana.

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi mambo vipi awali ya yote Amani ya bwana iwe nawe pole na shughuli za maisha ya ikla siku.rai yangu kwa leo ninakuomba kwa heshima yako futa huu mjadala kwenye ukurasa huu kwasababu
    1.wakati tulipokuwa tunajaribu kurusha hisaia zetu na maoni hakuna aliye jali matokeo yake tulionekana tunachuki na kocha.leo hii tujadili nini zaidi ya kumsifia kocha wetu. nilitamani kuendelea sana lakini naomba kuishia hapa.
    danny finland

    ReplyDelete
  4. ebwana eeh yule golikipa wetu wa starz kama mchezaji wa timu za shule za msingi kwa makosa yale huwezi kumlaumu kocha hatuna wachezaji wazuri full stop

    ReplyDelete
  5. NDUNDULU A.I.December 11, 2009

    Hakika sasa muda umefika,Maximo anatakiwa ajipime mwenyewe kwa yale anayoyapata na aliyowa ahidi Watanzania na akipata jibu najua atatangaza kung'atuka HARAKA sana!!Timu inapimika kwa utovu wa nidhamu,isiyokuwa na tija wala mategemeo,ni bora apewe shule ya soka la vijana ainoe kuanzia mwanzo then tuone matunda yake kwa falsafa yake ya Kuijenga timu!!Lakini timu ya TAIFA amekuwa ni kimeo!!Its now not then!!

    ReplyDelete
  6. I hate him! Huyu jamamaa mm sijaona changes yoyote aliyoifanya kwenye soka la Tz, labda pesa nyingi anazolipwa na kupelekwa kwao Brazil. Hajuu kutafuta vipaji, yeye ni majungu tu na kujifanya anafull confidense! Eti alisema kuwa Zanzibar hakuna vipaji, anafikir vipaji ni yanga na simba! Timu gani anayounda kila siku anabadilisha timu, mm!!! sijapata kuona ukocha wa aina hii. watu wanshindwa kujuwa Eti wanasema timu yetu imepata mafanikio kwa kuingila Mashindano ya Chan! mm nishangaa sana kuona jinsi ya mpira mbaya, mbovu usiovutia unaochezwa na timu yetu, tuseme ilikuwa ni bahati tu kufika pale na sio ubora wa timu. Maximo hafaii, aondoshwe, na tutafuta kocha wetu wa kizanlendo!

    ReplyDelete
  7. Mr. Michuzi,
    Hopefully things on your side are wonderful and smoothly,but unfortunately on national side particular on soccer issue, one of the most prominent sport not only in Tanzania but also in the world things are not doing well.Why so? Because of the followings main two reasons;Tanzania national soccer team does not have a professional football coach but we have a joker and a very unprofessional man known as Maximo,it is my hope now the time has come for us to change this altitude of calling Maximo a coach but let us remove this Joker from the post forcefully because Maximo does not want to quit peaceful!!!!
    Secondly The TFF does not have a powerful Secretary General who can lead this most prestigious instrument in Tanzania so Mr. Tenga and his members have to act upon this matter by taking Mwakalebele out from the post.I think any formar football prayer like Mtemi Ramadhani or Mwalusako could be a best candidate on this post than having a very bogus secretary genaral of TFF like Mwakalebela.

    ReplyDelete
  8. Tunamshukuru kwa alipotufikisha ila kwa sasa tunamuomba atuachie timu yetu uwezo wake kiufundi umeishia hapo

    ReplyDelete
  9. hatumtaki uwezo wake umeishia hapa ila tunamshukuru kwa alipotufikisha

    ReplyDelete
  10. Maximo ni kocha mzuri,alipotufikisha ni pazuri na ni kwenye stage nzuri,na maximo hapo ndio mwisho wake hawezi kutovusha zaidi ya hapo kwasababu ndio mwisho wak, kwa hiyo ni kutafuta kocha ambaye atatupeleka katika hatua nyingine ne yeye atamwachia mwingine ambaye atakuwa bora zaidi.

    Joseph(Dar)

    ReplyDelete
  11. ebwana eeh yule golikipa wetu wa starz kama mchezaji wa timu za shule za msingi kwa makosa yale huwezi kumlaumu kocha hatuna wachezaji wazuri full stop

    ReplyDelete
  12. Namkubali sana Maximo, ila kwa sasa itabidi tu aende na TFF watafute kocha mwingine kutoka nje wala wasithubutu kutafuta kocha hapa nyumbani kwani hakuna wa kuifundisha Taifa stars kwa kiwango cha kimataifa

    ReplyDelete
  13. Kuna vitu vizuri Maximo amechangia kama vile
    1. Kupata ticket ya kushiriki CHAN
    2. Kuifunga Burkina Faso n.k

    Kuna moja tu ambalo naona haliko sawa kidogo, nalo ni kushindwa kuharmonize uhusiano wake na some of the key players like Kaseja, Haruna Moshi, Athumani idd n.k

    Halafu uteuzi wake wa wachezaji umekuwa ni wa hivyo hivyo tu ...kama pale alipomteua Ali Mustapha "Barthez" ambaye hakuwa amedaka mech yeyote ya ushindani katika siku za hivi karibuni

    Amepewa support kubwa ambayo kwa kocha yeyote yule ingemuwezesha kufanya Maximo alichokifanya

    ReplyDelete
  14. Mi sijali sana huyu jamaa kama anaondoka au la,Kinachonisumbua mimi ni hawa watu wa TFF,hivi inakuaje kocha ambae amepewa jukumu la kuwa kocha mkuu wa timu ya JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA anapewaje jukumu la kuinoa timu ya BARA pia????,,,Watu wa TFF lazima wawe wanafikiria zaidi,kwanini wasimpe timu kocha yeyote mzalendo,akachagua timu yake mwenyewe,na akaikochi,na bwana mkubwa huyu MAXI aende kwenye challenge kama mtoa ushauri kwa timu zote mbili(ie TZ Mainland na TZ island),na ikibidi kuchagua timu nzuri zaidi tokea hapo,lakini matokeo yake mnaenda kumpambanisha na timu ya ZENJI,hivi timu ya BARA ikigongwa na ZENJI itakua inaonesha nini???,you TFF ppl,you get to think BIG now.

    ReplyDelete
  15. Mimi nazani huyu jamaa amefika mwisho hatusemi hajatusaidia japo si kwa mpira hata kutuhamasisha alau ameweza huyu nazani ni kada sio kocha wa mpira ni kada wa mpira ameweza kuunganaisha nguvu za wapenzi mashabiki na kingenge si timu na hasa ile iliyocheza jana ni kingenge cha wahuni fulani nazani muda umefika huyu tumbadilishe tupate kocha wakuunda tuma sasa itakayo itwa timu ya taifa aende tu huyu tumeshahamasika vyakutosha aendel

    ReplyDelete
  16. Chamuhimu ni kwa maximo kuelewa anawajibika kwa nani,anafundisha timu ya nani na wenye timu wanataka nini?

    Tatizo tulilonalo ni utaifa wa mtu. kwani hata wakina Dr. Msola wangepewa nyejo (rasilimali) kama anazopatiwa Maximo timu ingelifika mbali saaaaaaana kuliko ulipofika.

    ReplyDelete
  17. I dont see much problem in Maximo kwa sabababu wachezaji wetu ndio hao hao Tanzania nzima....nchi yetu bila kuwa na Soccer academies nationalwide, we going nowhere ...
    Kama maximo ataongeza mkataba wake basi tumuombe yafuatayo:
    1.Ajaribu kusikiliza ushauri mzuri kutoka kwa makocha wetu locally na wachezaji wa zamani kama kina Juma Mkambi,Jela Mtagwa,Jamhuri Kiwelu nk

    2.Atuonee huruma watanzania na umaskini wetu tulionao akubali kupunguziwa mshahara wake japo kwa 30% ya kiwango anachopata sasa.
    Kwa kweli mshahara anaopata ni mkubwa sana kulinganinisha na uchumi wetu ulivyo

    Mdau wa michezo
    Rodrick Mwambene

    ReplyDelete
  18. Sioni sababu ya kumjadili Maximo. Kama ni kufungwa, basi imefungwa Liverpool mara kibao lakini hujasikia watu wanamjadili Benitez. Huu ni mchezo wa mpira, Maximo sio mchezaji, kama wachezaji hawachezi vizuri yeye aingie acheze? Tujadili mambo ya maana ya maendeleo ya Taifa na sio kumjadili kocha wa mpira wa miguu

    ReplyDelete
  19. Sisi siyo wa kumjadili Kocha wa Timu ya Taifa. Mwajiri wake ni TFF. Kwahiyo kujadili suala lake katika blog ni kupoteza muda. Kwasababu hakuna mtu yeyote ambaye anajua :

    1. Mpango Mkakati ya Kocha wa Timu ya Taifa.

    Kama huujui au hatuujui utajadili nini dhidi ya mafanikio/mapungufu yake ? Ni lazima uwe na Mpango Mkakati wake uulinganishe na utendaji wake (kwa sababu unaweza kukuta katika huo Mpango Mkakati akawa amefanya zaidi ya yaliyomo) !!!

    Acheni hizo, mmepata mwamko wa mpira wa miguu lini ? TFF ina vichwa vyenye akili na bado imeridhika (ina angalia kazi yake dhidi ya mpango mkakati)iwe sisi Wapenzi kama siyo Washabiki !!!

    ReplyDelete
  20. Watu wengine wana mambo ya kiswahili sana. Yaani kwa sababu tumefungwa na Rwanda ndio tumjadili Maximo. Kama tungeshinda na kuchukua kombe kweli tungeambia tumjadili?Acheni mambo ya kiwashili,ndio nyinyi mnarudisha nyuma maendeleo.

    ReplyDelete
  21. Aende salama muda wake ukiisha. Tunamshukuru kwa aliyofanya na kusikitika kwa aliyoshindwa. Kila mtu amefurahi baadhi ya mida na kuchukia muda mwingi wakati huyo jamaa yuko benchi la ufundi. Sio yeye pekeyake hata ligi yetu na yenyewe mbovu ndo maana hata wanaoitwa stars wabovu na hata wachache tuliokuwa nao kama akina boban na chuji(kaseja simtaji) hawaitwi. Nadhani ni Muda wa kutafuta Kocha mzawa atakayesaidiwa na Mgeni kutoka Ujerumani.

    ReplyDelete
  22. Wadau,
    Ni kweli Tanzania tuna kiwango kidogo cha kabumbu, lakini tukipata Mwalimu mzuri tunafundishika. Kwa bahati Rais wa awamu ya nne ni mpenda michezo na amejitolea kuiinua. Maximo amefungua pazia tu, na sasa amefikia ukomo wa uwezo wake hivyo atuachie nafasi tujaribu kocha mwingine. Mbona Simba wamejaribu na Phiri na wanaendelea vizuri? TFF waanze mkakati wa kumpata Kocha mwingine. Sio ajabu kwani mataifa mengi huajiri na kufukuza makocha wanapokosa mafanikio. Maximo amuachie JK amalize awamu yake ya uongozi kwa mafanikio bila yeye.
    Mdau wa Soka

    ReplyDelete
  23. Twajadili kwa lipi?

    ReplyDelete
  24. Mi nadhani tumjadili Prezida,kwanini kamshikilia. Hana jipya yule

    ReplyDelete
  25. Mkuu wa nanihii!

    Ni wazi kwamba huyu kocha amefikia kiwango chake cha mwisho. Anahitajika kocha mwenye uwezo mkubwa zaidi ili tuweze kuendeleza vipaji vya vijana wetu na soka letu kwa ujumla. Kututoa porini isiwe sababu ya kutulaza barabarani!!

    ReplyDelete
  26. INAWEZEKANA ANAZO SHUGHULI NYINGINEZO NYINGI ZAIDI YA UKOCHA AMBAZO ZIMEMFANYA ASIWEZE KUFANYA VIZURI KATIKA KAZI ILIYOMLETA NCHINI, LABDA TUANZIE HUKO.

    ReplyDelete
  27. Ni kitu gani wanachoshea makocha hawa mashuhuri duniani? Martin Jol, Luiz Felipe Scolari, Claudio Ranieri, Gerald Houllier, na Sven-Goran Eriksson? Jawabu: Walipoajiriwa na klabu zao walitoa ahadi fulani fulani na ndipo mikataba ikasainiwa. Waliposhindwa kutimiza ahadi hizo, pamoja na umashuhuri wao walionyeshwa mlango na waajiri wao, wengine baada ya muda mfupi tu. Je, sasa huyu Maximo vipi, katimiza ahadi? Tujulishane. Na haya si majungu ila ni swali tu.

    ReplyDelete
  28. Hatuna kocha Mzawa mwenye uwezo zaidi ya Maximo. Kama mnadhani wapo basi hata waende nchi jirani tu kufundisha mpira lakini wala hawafikiliwi.

    Hebu angalia Simba, Yanga wote hawataki makocha wazalendo kwanini ? Sembuse Timu ya Taifa ? Maximo ndiyo anayetufaa hadi tutapopata displine ya mpira. Sasa kucheza timu ya taifa raha tupu ndiyo maana unaona kelele kibao ooooo !

    Kocha wa Timu ya Taifa alikuwa mmoja tu Joel Bendera wengine hawa ni Makocha wa viungo tu na kuogelea !

    Teh teh eeh ! Teh teh !

    ReplyDelete
  29. Soccer limeingizwa mno kwenye siasa, Maximo si mbaya sana, amejitahidi kwa uwezo wake, but inaumiza sana kwani tunaomlipa ni sisi wakatwa kodi na uwezo wake umeishia hapo. hakuna haja ya kuendelea naye. Arudi kwao kabla hatujamlazimisha. TFF pia wajipange wasikalie siasa tu wajue wajibu wao

    ReplyDelete
  30. Habari Kaka Michuzi,
    Awali ya yote nashukuru kwa kuuweka huu mjadala hapa, kwa kifupi tusitoe maoni kwa hisia bali tunahiataji kutafakari kwa kina kuwa Maximo is the best Coach whether you like or not. Kawapa mbinu zote wachezaji ila hawakuzitumia sasa nyie mnao mlaumu mlitaka yeye acheze? Pia huu si wakati wa kuangalia mapungu ya mchezaji mmjoa mmoja bali kama kufungwa imefungwa timu na sie sote tukihusika humu maana baadhi ya watanzania mmejaliwa unafiki sana na wala sisiti kusema hivi, acheni hivyo kwani team ikishinda mnawabeba wachezaji na Kocha ila ikishindwa manakuwa wanafiki acheni kabisa.
    Hebu jiulize wewe binafsi kabla ya kumpa lawama Maximo na team nzima ni kipi umechangia kuakikisha team inashinda?
    Acha kunyooshea kidole kimoja Maximo wakati vinne ninakuatazama wewe.
    Mdau wa mpira,
    jtwangala@gmail.com

    ReplyDelete
  31. Jamani tuache kumsema Maksimo....matatizo ni yetu. Ukweli ni kwamba Tanzania hatuna wachezaji wenye uwezo na vipaji, tuna wacchezaji wanaotengenezwa na magazeti tu kwa kusifiwa bila maana, unasoma sifa za mchezaji gazetini halafu ukimwona uwanjani unashangaa jinsi hamna kitu. Kwenye vilabu nako hakuna cha maana zaidi ya majungu.Kwa kawaida mchezaji anatengenezwa na klabu na sio timu ya taifa, naamini kabisa hata huyo maksimo huwa anapata Headache wakati wa kuchagua timu. Watanzania hatufahamu uwezo halisi wa wachezaji wetu na ndio maana tunamlaumu maksimo..ninavyoamini mimi hii timu hata apewe Ferguson, Morinho au Wenger au hata wakija wote kwa pamoja mambo yatakua hivyo hivyo hadi pale wachezaji wetu watakapokuwa na uwezo. Kwa leo ni hayo tu.

    Mdau

    ReplyDelete
  32. Mie nafikiri ni wakati sasa wa Maximo kufikiria kuachana na soka la bongo na kufikiria kutafuta timu ingine ya kufundisha, kwani miie nafikiri kuna mawili, either Maximo hajui kufundisha, au wachezaji wa Tanzania wameshindikana, kitu ambacho sidhani, kwani wachezaji hawahawa walifanya vizuri sana siku za kwanza hata kufikia hatua ya kuifunga mali nyumbani kwao.

    Tuache kumbeba Maximo, hebu tufikirie kutafuta kocha mwingine.

    ReplyDelete
  33. WAKATI WA MABADILIKO UMEFIKA SASA. MAXIMO GO HOME NOW.

    ReplyDelete
  34. www.tanzaniasports.comDecember 11, 2009

    Issues with Tanzanian football.
    Tanzania is a British colony and this is one of the reasons why its football never developed. The British did not help their colonies developed football post independence. Except for Ghana and Nigeria, most English speaking countries in Africa have enjoyed very little success in football on a continental level. The French on the other hand invested in countries like Cameroon, Ivory Coast, Mali, Senegal and also scouted these countries for talent who eventually where developed at French clubs.
    Lack of Competition
    Tanzania has not got much in terms of regional competitions that serve as a recruitment vehicle.
    Lack of Investment
    There has been very little investment in the game at Grassroots level. The Country still does not have any football academies in the regions and its league remains extremely underdeveloped.
    Lack of scouting activity
    Tanzanian enjoys no scouting activity at all. If a talented player emerges from Tanzania, they most often end up in the local leagues and hardly ever make it to Europe. This hugely affects the national team who often lack the experience of teams with European players in their ranks.

    ReplyDelete
  35. ivi inakuweje tunafungwa na rwanda?me hainiingii akilini,

    kama tulivosema: taifa stars vs zanzibar heroes,,,jamani huu upinzani si ndio mmomonyoko wa muungano kabisa??tushangilie wapi tuombee baya wapi!!!

    ovyo sana system za bongo

    ReplyDelete
  36. Wachezaji wetu hawana vipaji,nidhamu mbovu,miili kama watoto wa shule ya msingi,viongozi wetu mafisadi...halafu mtamlaumu kocha?...mkulima mbaya humsingizia jembe kila siku!

    ReplyDelete
  37. MDAU HAPO JUU ULIYESEMA KUWA INAWEZEKANA KUWA "MASIKIO MASHIMO" ANA SHUGHULI ZINGINE...... NI KWELI. JAMAA ANACHEZA SINEMA ZA KIBONGO INGAWA WEK PAMIT YAKE IMESEMA KUWA ANAKUJA KUFUNDISHA MPIRA.
    MI SIJAWAHI KUONA HII... KOCHA WA NESHNO TIMU ANACHEZA SINEMA!!!! ANAPATA WAPI MUDA WA KUKARIRI SKRIPT??!!! SAA NGAPI ATAPANGA MIKAKATI YA KUKUZA MPIRA?!!! JAMANI HIZI NI KODI ZETU ZINAZOCHEZEWA HAPA (najua huwa zinachezewa sehemu kibao), TUAMKE. HUYU JAMAA AONDOKE TUU SASA, HANA JIPYA TENA, ALIPOTUFIKISHA (sina uhakika sana ni wapi??) PANATOSHA... TUMWAGE APATE MUDA MZURI ZAIDI WA KUCHEZA MAIGIZO.... AAAHHGGGHHHHHH

    Mdau Chiggs, Deslam

    ReplyDelete
  38. shughuli yake ingine si actor wa bongo basi aendelee asitutie aibu na kumaliza pesa zetu tu

    ReplyDelete
  39. Maximo katusaidia sana tena sana nikikumbuka raha tulizopata kipindi chake kwa kweli ni nyingi ila kwa sababu binadamu hana shukrani siku zote ndiyo hivyo.

    Kama binadamu ni lazima uwe na mapungufu ndiyo maana anamapungufu yaliyoonekana nadhani sio wakati wakuongea mengi.

    Watanzania twatakiwa kumshukuru na pia mukaa naye na kumwambia kuwa kwa muda huu hatumuhitaji ili tupate wengine. Tusijifanye tunajua kuongea sana kwa sababu hata hao ma kocha wataogopa kuja wakisikia sifa zetu au wanaweza wakaja na wakafanya kazi kwa ku paniki kwakutuogopa na midomo yetu.

    Ikiwa nidhamu huwezi mfundisha mtu mzima nidhamu ni yeye mwenyewe kujipanga na kutambua yuko uwanjani hapo pia tuseme maximo??

    Mimi binafsi namshukuru sana Maximo Mungu akujalie ulipotufikisha ni pazuri.

    ReplyDelete
  40. Kabla ya kusema Kocha anatufaa au la, inabidi turudi nyuma kidogo.
    Je, wakati Kocha huyu anaajiriwa kulikuwa na malengo aliyopangiwa? Je kulikuwa na vigezo vya kupima mafanikio yake?
    Mathalan, kama kwenye mkataba wake alitakiwa ashinde mashindano ya Challenge or CHAN baada ya muda fulani, basi apimwe kwa vigezo hivyo.
    Kuna sababu nyingi zinazochangia timu kutofanya vizuri kama baadhi ya wadau walivyoeleza, lakini pia ni jukumu la kocha kutengeneza mazingira ya kuibua, kuendeleza na kujenga timu imara. Basi kocha huyu apimwe kwa mapungufu hayo.
    Kwa kumalizia, badala ya kutumia jazba, noaomba turudi kwenye mkataba wake, Maximo alitakiwa atufanyie nini sisi watanzania? Kama hakukuwa na vigezo au malengo tutakuwa tulikosea.
    Naomba kuwasilisha
    Mdau
    Faustine
    drfaustine.blogspot.com

    ReplyDelete
  41. TFF imefurahishwa na matokeo mazuri ya Kilimanjaro Stars, tumeamua kuwapatia zawadi zote watakazopata kama timu wagawane wachezaji wenyewe kama motisha kwao," alisema Mwakalebela.

    Mwakalebela alisema hatua waliyofikia Kilimanjaro Stars wanapaswa kupongezwa kutokana na kiwango walichokionyesha hasa baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Uganda ambapo walifungwa goli 2-0.

    ReplyDelete
  42. Kocha anayepigana na utovu wa nidhamu vipi sasa timu yake ipate kadi nyekundu tatu katika mechi tano ilizocheza?

    ReplyDelete
  43. Tatizo nchi hii imepigwa laana na aliyeilaani inaelekea amekufa hatuwezi kufanikiwa mpaka hii laana itutoke. UBINAFSI UNATUMALIZA kwenye nyanja zote.

    ReplyDelete
  44. Jamani naomba tupunguze jazba na tujuekua asilimia kubwa ya wachezaji wetu nidhamu hamna. Kuna makosa mengine wanafanya ambayo unaangalia marambili utamani kuvunja TV.

    Kwa huyu jamaa mimi namuita MAKISIO muda wake umepita. Nilichoona kwake ni kua anaonekana ni mwalimu wa kufundisha vijana wadogo na kwa sehemu timu yetu ilipofikia hawezi tena. Tunahitaji mwalimu mwenye kuelewa malezi ya wachezaji wa Kiafrica ila kama ataendelea kuwafungia maisha wachezaji kama anavyofanya sasa hatuwezi kumvumilia. Nadhani tukubali kua mchango wake umetufikisha hapa tulipo ila sidhani kamaa tunamuhitaji tena. Kwa wale ambao wanadhani tunamuonea tunaomba mjue kua kipimo cha mwalimu ni matokeo mazuri na sio mpira wa seed wala pasi nyingi, leo hii wazee wa bwawa la maini wanataka kumchomoa Benithez sio kua ni mbaya ila uwezo wake umefikia kikomo.

    ReplyDelete
  45. MCHEZA SAMBA YUPO KWENYE OPTIMUM POINT,

    ReplyDelete
  46. acheni kumlaumu maximo. kazi ya kocha wa timu ya taifa ni kuwaunganisha tu na kuwaelekeza wachezaji vitu vidogo.
    kazi kubwa wanatakiwa makocha wa clubs ndio wawaelekeze wachezaji. tabia yetu ya kutofanyia kazi kisayansi haitatupeleka mahala popote. Mimi naona maximo anafanya kazi proffesionery lakini sisi tuahangaika kutafuta mchawi badala ya kubadili mfumo mzima ili twende kisayansi zaidi

    ReplyDelete
  47. mie kwa kweli nasikitika tusivyokuwa na uzalendo kwa timu yetu kwa kumkumbatia maximo. huyu kocha hana deliverables? coz kila mfanyakazi anatakiwa kuwekewa malengo ili kama hakukuweza kuyafikia basi inabidi kuchukuliwa uamuzi wa eidha kumwachisha au kumbadilishia malengo. bwana maximo haja weza kudeliver tangu aajiriwe na mkuu wa nchi na moja ya mafanikio ya timu yoyote ya michezo ni ushindi, hapo ndipo kocha anapimwa. hebu tuseme ukweli maximo tangu ameingia ameshinda kombe gani? yeye ana mshahara mzuri, wachezaji wako highly motivated na mazingira mazuri ya kufanya mazoezi bado hatushindi, kwa nini? zamani timu ilikuwa haina hata posho wala vifaa na kocha alikuwa analipwa kama kibarua bado tulikuwa tunashinda vikombe na hata wakati tukafika fainali ya kombe la Africa. jamani kuna tatizo watz tuamke tuache siasa kila mahali.

    ReplyDelete
  48. Jamani sioni la kumlaumu Maximo hapa. Hivi hao wachezaji wa kutumainiwa wako wapi? Watanzania kama walivyo waafrika wengine ni kupenda vitu vya haraka.

    Mnao mlaumu maximo mjiulize ni wachezaji gani mnao fikiri hakuwapanga hadi timu ikashindwa?

    ReplyDelete
  49. unajua sie wabongo tunaona kabumbu ni kwa wachezaji wawe na kocha mzuri siku zote ,kwa nini amu msapoti maximo kwa kutoa nizamu kwa wachezaji wanaosamini ngono ,kuvuta bangi na kunywa mipombe na kuchelewa au kukacha mazoezi...mnamtolea macho maximo wa watu...afu mnamshangaa akitoa nidhamu..jiulizeni kiini cha chanzo na sio kutoa maoni ya kipuuzi au mnaona bora kila khalfani kucheza kabumbu canada daraja la nne na mnaona hiyo ni bora kuliko kuweza angalau kutoa mchezaji mmoja wa tz angalau kucheza ligi daraja la kwana ughaibuni na sio mineno tuu.tatizo wachezaji bongo usiku mzima kwenye mabaa na asubuhi anatakiwa atinge zoezini na aonekani siku mbili sababu ya hang over..apo pia mnamlaumu kocha sio..think again tz ppl

    ReplyDelete
  50. kama kweli watanzania tunaipenda nchi yetu basi ´tuwe waungwana kama ni suala la kocha mimi nadhani watoa maoini wote hapo juu wmezungumza mengi lakini kwa kiasi fulani wanamlaumu kocha na wachezaji ukweli ni kwamba kocha ndio mwenye uwezo wa kujua mchezaji anafaa au la kwa kuzingatia kigezo hiki na kocha wetu amekuwa akifanya mabadiliko mara kwa mara na ahadi ambazo hazina mafanikio hii inaonyesha uwezo wake umeishia hapo tunamshukuru kwa kazi aliyoifanya wapewe wengine nafasi nao watusogeze
    tangu lini mchezaji ambaye hujawahi kumuona unamwita timu ya taifa ? uliowaona unasema hawana nidhamu.jamani tuwaige hao simba mwaka jana au kwa kipindi cha miaka miwili walishindwa kufanya vizuri kwenye ligi wamekuwa wakibadilisha kocha na kocha mabaye waliye nae sasa ndie aliyeipokea timu tangu mwaka jana na kazi yake kila mtu anaiona iweje stars washindwe? Tenga na wenzie wanalakujibu hapa;na nyinyi waandishi wa habari hususani za michezo mnatuangusha samahanini sana wajomaba ukweli mnaufahamu .taifa stars na ya kwetu wote na siyo timu ya wachache hebu tuondoleeni huyu kocha tafadhalini sana wahusika
    mdau Haambiliki bin mkuchu

    ReplyDelete
  51. Maximo si lolote na katuletea ugonjwa wa moyo tu..kila siku tunaacha kazi zetu na kushabikia timu yetu na tunatolewa kila mashindano.

    pia timu haibadiliki..kila siku watu wanacheza kivyao..leo Ngasa anawika ,kesho flani..hakuna team cordination.


    kinachouma zaidi ni jamaa analipwa kwa kutumia kodi zetu.

    kazi anayoiweza ni kufundishwa kucheza filamu..awatumie kina kanumba wamfundishe jinsi ya kucheza filamu za kibongo//

    kama vipi nikikutana nae pale sweety easy namwambia..wamezoea na maximo ni fisadi wa mpira!

    ReplyDelete
  52. Mimi kwa kweli sina tatizo na Maximo . Maximo ni kocha mzuri sana tangu mprira tupate uhuru. Lakini sisi wantanzania wenyewe tuna matatizo makubwa kama ifuatavyo;
    1. Tumepagwawishwa sana ushabiki wa timu za nje hasa Ulaya na timu zingine za mataifa mbalimbali .

    2. Tunatumia lensi za mpira ya nchi zingine and clu za kimataifa kuangalia mpira wetu wa ndani bila kujali kwamba tune ya lensi ya kumuangalizia TEMBO huwezi kuangalizia INZI and get the same results, in short kama umeshatune darubini yako kwa mithali ya TEMBo kimsingi INZI hutomwona unless you magnify the lens to the tune ya INZI. Acheni hizo ! ndivyo pia tuvyomwaangalia MAXIMO na SIR ALEX na wengenie ... Ndio maana lawama ni nyingi kuliko mazuri, Acheni Hizo.

    2. Watanzania zaidi ya SIMBA NA YANGA hakuna uzalendo ... Brazil au Invory coast wacheza na Taifa Stars wengi wetu watakuwa wanashabikia hizo timu zingine ... Ni ushamba halafu it will never change that facts.

    3. Watanzania ni hodari sana kuongea kuliko realities on the ground, kwanini msingalie msidadisi ukweli wa mambo, wachezaji wetu hawajapata elimu ya mizecho " Sports Academi ni GAS zanzibar haipo " nchi nyingine hizo ambazo mnashabikia zina historia nzuri ya sports tangu enzi za mjerumani . You do not see those, why ? LENSI hizo !

    Kwa Wachezaji wetu.

    1. Kiburi ni kubwa kuliko uwezo wachezaji wazuri dunia wanaadabu na heshimu hata kushinda viwango vyao vya mpira ... Maximo akisema ...mnapiga kelele ...kadi nyekundu kama mvua ndio maanake .

    2. Mentally affected wengi hapa hamtoelewa lakini habari ndio hiyo, nitatoa mfano wa mwili ... Maximo has done som much mpaka sasa lakini capacity ya kupekea na kudigest kwa wachezaji wetu haipo... kukosa shule ya shule ya sports utotoni ndio chimbuko... wale mnaosema Maximo aondoke ni sawa lakini hata SIR ALEX name it akiletwa kesho SIFURI ... the capacity ya wachezaji haipo...like an old modern computer kama mnataka kuelendea kimichezo anzeni kuandaa watoto ..Sarakasi haianzii ukubwani !! South Africa Rugby vs. Mpira wa Miguu what do you think is a problem. Rugby ni WORLD champions lakini mpira wa Miguu hata sisitunaweza kuwafunga ... why ? habari ndio hiyo

    3. Kwa Serikali ya awamu ya NNE

    Kama kuna kitu kizuri cha kukisifu Serikali hii katika swala zima la Michezo, ni kumleta Maximo lakini mimi ningeshauri Serikali, kwa sasa wanainchi sorry wanainchi wamelilia wembe kwa muda mrefu .... please allow Maximo to go kama hatujaondoka kwenye anga ya Michezo .. Yaani ni aibu kama kila wakati mnataka Mh. Rais amtetee Maximo Mh. Rais anamjukumu makubwa na Mazito zaidi ya hayo..

    Maximo Hoyee ! Maximo Hoyee !

    ReplyDelete
  53. NADHANI MAXIMO SOKA YA FITNA BONGO IMEMSHINDA NI BORA AENNDE MLIMANI CITY AKAENDELEE NA FANI YAKE YA KUCHAGUA MAMISS,MAANA NDIO FANI YAKE AU LA ARUDI KWAO AKACHEZE ILE NGOMA YAO YA .....LAKINI NAONA AMEISHIKA TFF SANA KAGANJANI MWAKE.

    ReplyDelete
  54. MI NAONA TATIZO SIO MAXIMO,,TATIZO NI SISI WATANZANIA KWANI HATUJUI TATIZO LETU,,TATIZO TUNATAKA KUJENGA NYUMBA YA GHOROFA ANGALI MSINGI WAKE HATUJAJENGA VIZURI,,MPAKA SASA HATUNA ANY SOCCER ACADEMY IN TANZANIA,,WACHEZAJI WAZURI WOWOTE DUNIANI WAMETOKEA KWENYE ACADEMY,,HAKUNA MCHEZAJI YOYOTE ALIEANZIA MTAANI KAMA WETU,,KWA STAILI HIYO WACHEZAJI WETU HAWATAKUWA NA NIDHAMU WALA HAWATAELEWA WANACHOAMBIWA,,KWA STYLE YETU HATA AKIJA ALEX FERGASON HATUFANIKIWI.....

    ReplyDelete
  55. Watanzania huwa hatueleweki siku zote,juzi tumeshinda 4 tukasema kocha mzuri jana tumefungwa kocha hafai,now which is which,kuna kamati ya ufundi ambayo kwa maoni yangu ndio ya kuilaumu,inashindwa kufanya kazi yake vizuri na kutoa mawazo au ushauri.Nadhani kamati ya ufundi ituambie kama ni kweli maximo hashauriki au ni redio mbao zinatudanganya

    ReplyDelete
  56. Maximo hana tatizo.Tatatizo ni kuwa wachezaji wetu siyo professional kwa maana kuwa wanaanza kufundishwa mpira wakiwa wakubwa.Nchi ambazo wamefanikiwa ni kuwa wanawaandaa wachezaji wao toka wakiwa chini ya umri wa miaka 10.Maandalizi ni pamoja na kupewa balanced died.Niliwahi kusikia kuwa baadhi yao walitapika baada ya kupewa orange juice asubuhi.Hata tupate kocha wa timu ya taifa ya Brazil,hatuwezi kushinda maana huwezi kumnenepesha ng'ombe siku ya mnada,wala huwezi kum-overfeed materials mwanafunzi siku moja kabla mitihani.Let the nation start investing with 5th graders because learning is a continuos process othewise we will be talking over and over but our current formula is not gonna work.Let's lay the foundation ground before rooffing.Lazima tukubali kuwa sasa hivi tunachokifanya ni sawa kuficha sura wakati makalio yako wazi.Nashukuru kwa wote mlichangia na ninataofautiana na wngi lakini ninaheshimu mawazo yenu.
    Toto tundu-DC

    ReplyDelete
  57. MAXIMO NI KOCHA WACHEZAJI NDIO HAWANA UWEZO.DUNIA SI TANZANIA HAIJAWAHI KUWA NA KOCHA BORA KAMA MAXIMO.
    NAPENDEKEZA MAXIMO AKAE TU HADI SIKU YA KIAMA.

    KUNA MTU HAPO JUU KAULIZA KUWA KAMA KUNA MCHEZAJI WA MCHANGANI AMEWEZA KUWA MCHEZAJI WA KIMATAIFA?JIBU NI GEORGE WEAH AMETOKA MCHANGANI ANA AMEKUWA MCHEZAJI BORA DUNIANI.
    MDAU KISIJU KIPENZI CHA MAXIMO
    MDAU KISIJU.

    ReplyDelete
  58. Kwa mtazamo wangu naona tumepiga hatua kutoka tulipokuwa awali na tulipo sasa, kila mmoja kwa nafasi yake amechangia katika hilo kuanzia viongozi wa serikali, TFF, mashabiki, wachezaji na kocha mwenyewe. Hata hivyo baada ya hatua kadhaa tulizopiga tumesimama mahali flani, hatupigi hatua kama tunavyotarajia; hapo ndipo inabidi tumshukuru Maximo kwa maneno machache tu '' asante sana, umefanya kazi nzuri, tunashukuru kwa kazi nzuri ila pumzika tunahitaji mtu mwingine wa kutuvusha hapo tuliposimamia wewe nenda kapumzika''.
    Jazba tuziweke pembeni.

    ReplyDelete
  59. Jiulizeni kwa nini Chelsea FC imefukuza makocha wengi toka kina Ranieri,The Special one Jose n.k n.k lakini Chelsea bado inafanya vizuri.

    Nini siri ya Chelsea FC kufanya vizuri, jibu ni wachezaji wenyewe waliokuzwa kimpira toka utotoni kina Terry, lampard, Drogba, Asley Cole, Joe Cole, wote hawa walianza kuonekana wakiwa wana umri wa miaka 15 na kukuzwa na kulelewa kimpira.

    Sasa Simba, Yanga, Kilimanjaro stars, Zanzibar Heroes, Taifa Stars wachezaji wengi hawajapitia mfumo huo wa kugundua vipaji, kuvilea na kuvikuza.

    Hivyo tatizo siyo Maximo bali ni vilabu vyote nchinin hazina academies, shuleni hakuna utekelezaji wa sera ya michezo kisayansi, TFF/ZFF hakuna ubunifu endelezi wa mpira wa miguu.

    Mdau
    Rocky

    ReplyDelete
  60. Maximo aanze hana jipya.amesema hatachagua wachezaji wenye utovu wa nidhamu na sasa timu yake ndio inaongoza kwa utovu wa nidhamu.

    ReplyDelete
  61. Maximo apewa onyo kwa utovu wa nidhamu na CECAFA.
    na Burudani

    Cecafa yamuonya Maximo
    Imeandikwa na Zena Chande, Nairobi; Tarehe: 11th December 2009 @ 23:59 Imesomwa na watu: 18; Jumla ya maoni: 0




    Habari Zaidi:
    Cecafa yamuonya Maximo
    Kili Stars ikishinda hela za wachezaji
    Warembo 10 watinga fainali Kisura wa Tanzania
    Stars, Zanzibar gonjwa moja
    Taifa Queens kujiuliza kwa Singapore
    John Baraza mwanasoka bora Kenya
    Kocha wa Rwanda apalilia kibarua chake
    Zanzibar Heroes watoa visingizio
    Miss Afrika Mashariki kucheza na Jide na Banana
    Taifa Queens yainyuka Canada
    URA wainyuka Simba
    Zanzibar yatolewa Chalenji
    Kazi kwelikweli Kili Stars na Rwanda leo
    Kipa Stars afananishwa na Berko
    Mashabiki kuingia bure
    Kipigo chamduwaza kocha Zimbabwe
    Rwanda yaponda makocha wa kigeni
    Kundi C tishio Chalenji
    Mbunge Morogoro kudhamini mashindano ya vyuo
    Watano kuchujwa leo shindano la Kisura wa Tanzania



    Habari zinazosomwa zaidi:
    Balaa lingine kwa Chenge
    Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
    Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
    Vatican yamvua jimbo Askofu
    ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
    Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
    Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
    Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
    Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
    JK apigilia msumari wa mwisho Dowans


    KAMATI ya nidhamu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) imetoa onyo kali kwa makocha wa Tanzania Bara Kilimanjaro Stars Marcio Maximo na wa Rwanda ‘Amavubi’ Nshimiyimana Eric.

    Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amewaeleza waandishi wa habari kuwa, makocha hao wamepewa onyo kali kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu walivyovifanya katika mechi ya nusu fainali iliyozikutanisha timu hizo.

    “Lakini pia mwingine aliyepewa onyo kali ni mchezaji wa Rwanda aliyekuwa amevalia namba 14 mgongoni (Ndayishime Yusuf) onyo kali kabisa hawatakiwi kurudia tena makosa hayo,”amesema Musonye.

    Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Nyayo mjini hapa, Rwanda iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutinga fainali ambapo itacheza na Uganda kesho.

    Kila Rwanda ilipopata bao, mchezaji Yusuf alikuwa akikimbia mpaka kwenye benchi la wachezaji wa akiba la Kilimanjaro Stars na kutoa maneno yaliyoonekana kuwakera waliokaa kwenye benchi hilo ambapo Kocha Maximo alikuwa akijibishana naye.

    Kocha wa Rwanda Eric alikwenda mpaka kwenye benchi la Stars na kuzozana na Maximo.

    Baada ya mechi wachezaji wa Rwanda wakiongozwa na kocha wao walikwenda kumzonga mwamuzi Thomas Onyango wa Kenya wakidai alikuwa akiwaonea katika maamuzi yake.

    Akizungumza baada ya mechi kocha Maximo,alisema mchezaji Yusuf,alikuwa akienda kwenye benchi lao na kuwatolea maneno machafu.

    “Kila wakifunga alikuwa anakuja na kututolea maneno machafu sasa hiyo ilikuwa kazi ya kocha wake kumwambia aache kufanya hivyo,” amesema Maximo.

    “Lakini si kwamba eti wachezaji wangu hawana nidhamu wao (Rwanda) ndio walianza na unajua mtu akiwa kwenye presha ya mchezo, hakuna wachezaji wenye nidhamu kama wangu si ndani wala nje ya uwanja,” alisema Maximo.

    Kocha Eric aliwalaumu wachezaji wa Kili Stars na kusema kwamba hucheza vizuri wanaposhinda tu lakini wakifungwa huwa na soka ya mtaani.

    “Tunawajua watanzania wanacheza vizuri wakishinda tu lakini wakifungwa wanacheza soka ya mtaani na sisi tulijiandaa na hilo,” amesema.

    ReplyDelete
  62. Tukishajadili Maximo, Kisha tujadili John Mashaka

    ReplyDelete
  63. jaman tusiwe wepesi wa kuwalaumu watu na kuwabebesha lundo ka maneno mbofu kwa vitu vilivyo nje ya uwezo wao!!!wabongo kuchoonga A lakn actions F(0).hapa mi wala cmlaumu kwa mshahra anaopewa mana hata hao wanaoitwa viongoz ktk nyanja tofauti za serikal nao wanakula hela ya walipa kod with no justification at all!!wengine tunawajua lakn hakuna m2 aliyesimama kutetea haki na maendeleo ya nchi zaid ya kupiga majung chinichini!!POLEN!!!

    ReplyDelete
  64. naungana na mdau mmoja hapo juu hata aletwe fegasoni wenga banitezi timu itavurunda tuu huwezi kumfundisha simba mzee kuwinda full stop ataishia kuwa majeruhi manake unaemuwinda naye ni lazima ajitetee kwa mateke meno mieleka hivyo utaumia tu! jamani tujifunzeni hata kwa wanyama tizameni kina mama cheeter simba huwa wanawafundisha watoto wao kuwinda wakiwa wadogo wakiwa wakubwa wanakuwa ni danger tu huko porini tena sie tumebahatika kuwa na mbuga za wanyama nendeni tu huko porini mkaone mfano hai kama naongopa

    ReplyDelete
  65. Hivi kwa nini wachezaji wetu wanapata kadi nyekundu kwenye mashindano ya CECAFA tu???? Wamecheza na Ghana, Cameroon, fainali za CHAN, Burkina Faso, Senegal bila kadi. Wakicheza makombe ya mbuzi kadi zinawamiminikia. Kuna kitu hapo.

    ReplyDelete
  66. Kocha anatakiwa awe na malengo na ahadi na kama timu haifiki ahadia laizo weka basi ni bora aanze kwani ndio mtindo wa makocha wote duniani.Pia anaesema kuwa hatuna makocha nchini sio sahihi, kwani huko zamani walikuwapo na timu zilifika mbali sana ukilinganisha na huyu wa sasa.TFF wasimuone aibu aondoke haraka kwani hii sio ndoa ya maisha.Angalia ghana wameshinda world cup under 20 na kocha amghana tuwaamini na kuwapa ushirikiano kama huyu ambaye hata kwao Brazil hajulikani.

    ReplyDelete
  67. Hivi jamani Tunafikiri kwa kubadili badili kocha kaa mtu anavyobadili viatu ndoo kutaleta mafanikio makubwa kwenye timu ya taifa.La Hasha!!! witinzania wenzingu.Hata kama tukimleta kocha maarufu kiasi gani hakuna kitu kitabadilika.Wachezaji hao tulio nao kusema ukweli wanajitahidi kiasi chao ila tatizo ni umri, na maandalizi mabovu.Cha msingi hapa ni kwa viongozi wa mpira wa miguu bongo kuanza kudream or to think big kwa kuwekeza kwa yosso au next generation.wakiamua kutengeneza system nzuri ya soka hakika nipe 5-10yrs to come bongo kimpira itakuwa juu big time.

    ReplyDelete
  68. Mimi nilikuwa Brazil wakati huo kocha Maximo alipoendwa kutafutwa. Yule jamaaa alieenda kumtafuta alienda kijijini kwao kwenda kumpata mshikaji wake ambae ni Maximo. Maximo hatoki katika miji maaarufu kwa mapira kama Sao Paolo, Maximo alikuwa anafundisha timu za mchangani kama Kawe Rangers, Faru dume na Linnea Messina. Hata ukifuatilia kumbukumbu zake hajawahi kufundisha timu ya jimbo au klabu yoyote kubwa ya Brazil. Timu ya taifa ndio hii ya kwetu ameanza kufundisha. Kwa hiyo Maxomo hana record yoyote ya kufundisha timu ta taifa kubwa kama la Tanzania, sio kwamba kila Mbrazil anajua kucheza au kufundisha mpira wa miguu. Huyu Maximo naona uwezo wake ni kufundisha timu za watoto wadogo. Kocha gani anashindwa kuusoma mchezo na kufanya mabadiliko ya tija. na hawa wakina Leopord Tasso hawamsaidii ushauri au ndio wanamuogopa kwa vile hasikii ushauri wa mtu

    ReplyDelete
  69. Do, mdau wa tanzaniasports amesema kweli. Maoni yake ni kwamba, tunahitaji jitig=hada za ziada kuwekeza katika academy katika ngazi zote.
    tukumbuke historia.
    Hongera tanzaniasport kwa kuweka ukweli

    ReplyDelete
  70. Kwa mtazamo wangu ningependa TFF wasimwongezee muda huyu kocha kwani kashindwa kazi. Kapewa timu ivi sasa ni miezi 18 tangu awe na timu lakini hana 1st eleven sasa unategemea lini Maximo atatukomboa katika hili. Kwakweli Maximo uwezo wake ni mdogo. Tumeshamwona uwezo hana ivyo TFF wasije wakampa mkataba mwingine halafu badae waukatishe mkataba na kumlipa pesa hatutawaelewa. Timu yetu inaufadhili wa kutosha kuliko ilivyokuwa zamani hapa tatizo ni kocha. Hana upeo jamani tusipoteze pesa zaidi.
    Halfan

    ReplyDelete
  71. SASA TUNAMLAUMU KOCHA KWA WACHEZAJI GANI, MPIRA WETU NDIO HUO, HAPA HATA AJE SIR FERGI NA WENGER HAWATAFANYA MIUJIZA. MVUMO WETU WA MPIRA HAIELEWEKI, HAKUNA PROFESSIONALISIOM, NAJUA WATU MLITEGEMEA MAXIMO ATAWAFANYA WACHEZAJI WETU WACHEZE KAMA AKINA RONEY,TORRELS N.K, HIYO SIO KAZI YAKE, WACHEZAJI WANATAKIWA WAANDALIWE KATIKA LEVEL YA CLUB

    MDAU

    ReplyDelete
  72. Maximo is a great coach, hatujawahi kupata kocha wa kutufikisha kiwango kizuri kama cha sasa,kwa kuwa watu hawampendi, aondoke but with respect. Nadhani tutamkumbuka

    ReplyDelete
  73. Hey, hapa watu ni majungu tu, kwani tulikaa miaka takribani 20 bila challenge cup, tukalichukua mwaka 1994. Sasa miaka ishirini mingine haijafika watu wanalalamika nini? Kwani maximo yupo hapa bongo tangu 1994? Kama sivyo mbona hatukuweza kulichukua tena mpaka sasa? Hapa ni commitment za wachezaji, wachezaji kama wa zanzibar ni muhimu timu ya taifa hivyo kuwatenganisha ni tabu. Canavaro unambadili na nani timu ya taifa. Boban au Kaseja mnawaongelea wengine ma model, hamjui ronaldhinho hajaichezea brasil mechi ngapi? Nidhamu ni muhimu zaidi ya matokeo katika soka. Geoffrey Mwavala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...