Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa wa UVCCM, Gabriel Amos Makalla ( wapili kutoka kulia ) akisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi ( hayupo pichani ) wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Chipukizi ulioambanata na uchaguzi mkuu jana mjini Morogoro. Gabriel katika uchaguzi huo alichangukiwa kwa kishindo na wajumbe wa mkutano huo. Alipata zaidi ya asilimia 85 kwa kura 310 wakati wa pili alipata kura 19.
Baadhi ya wajumbe wa Chipukuzi Taifa katika mkutano mkuu kutoka Mkoa wa Ruvuma , Kagera na Mtwara wakiwa na wenzao wa Mikoa mingine ya Tanzania Bara na Visiwani wakisililiza hotuba ya mgeni rasmi wa Mkutano huo

Baadhi ya wapenzi na wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) na Umoja wa Vijana ( UVCCM) wakijipumzisha nje ya ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Morogoro wakisubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa taifa wa Chipukizi ulifanyika mjini humo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huyo mzee kakasiriak kweli, mtoto wake ameshindwa uchaguzi nini?

    ReplyDelete
  2. ......halafu baadae mnauliza kwa nini CCM(Chama Cha Maakuli) wanashinda kila uchaguzi,wenzenu wanajitahidi ku-exploit kila nyanja waliyonayo ndani ya nchi.tatizo vyama vingine vimeshindwa na kukataa kuelewa jinsi Mtanzania anavyojiendesha katika maisha ya kila siku.hivi ndivyo tulivyokuwa sie wengi wa miaka ya nyuma kidogo,mambo ya chipukizi na vitu kama yhivyo kwa hiyo CCM wanaona kuna wanaweza ku-expolit hii opportunity,why not?siasa mchezo,ingia ushinde au ndo hivyo utoke miguu juuu....but remember,''...never trust a politician to grant you a favor,for he will want to control you forever.....'',kuwa mamcho.

    ReplyDelete
  3. Mtandao wa CCM unaanzia mbali sana kwa hili, big up.

    Mnanikumbusha jinsi tulivyokuwa tunafundishwa siasa tangu darasa la kwanza hadi sekondari. Matokeo yake wote tukawa wanasiasa.

    Many years down the road bado imani za mwana TANU bado watu wanaweza kuzitaja kama vile hawana akili nzuri.

    Japo hii imewafanya watz wengi kuwa wabishi, wavivu na watu wa kulalamika lalamika even kwenye trivial issues.

    Otherwise, hongera!!

    ReplyDelete
  4. Papaa Idd nae ni mkereketwa wa CCM??C mchezo unatuwakilisha wadau wa PR camp Kinondoni.Kamua baba mpaka kieleweke ila usimtupe sana mdau mwenzako Yero Masai.
    mdau UK

    ReplyDelete
  5. Ingekuwa bora kama tungewekeza katika kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora, lishe bora, makazi bora na mambo kama hayo kuliko kujenga political foundation ambayo inajenga matabaka kuanzia ngazi ya chini!

    ReplyDelete
  6. HAHAHAHAHAHA Papa Iddi hana lolote ulaji tu unampeleka mbio . hapo kanuna anasubiri posho yake ya mkutano.
    mdau UK

    ReplyDelete
  7. Watoto wa vigogo washinda Chipukizi


    na Andrew Chale, Morogoro




    WATOTO wa vigogo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameibuka washindi katika uchaguzi wa Chipukizi Taifa uliofanyika juzi mjini hapa.

    Watoto wa vigogo waliofanikiwa kutwaa nafasi katika uchaguzi huo ni pamoja na Gabriel Makalla ambaye ni mtoto wa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Taifa, Amos Makalla, ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa baada ya kupata kura 300 kati ya 357 zilizopigwa.

    Mwingine ni Khalifani Jakaya Kikwete ambaye ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa.

    Kwa upande wa Kamati ya Uendeshaji Taifa Tanzania Bara ilichukuliwa na Glory Mwambeleko ambaye ni Mtoto wa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Alfred Mwambeleko na Asnail King huku kwa upande wa Tanzania Visiwani walioshinda ni Abdallah Haji Mgeni na Abdulatif Ramadhan Abdullah.

    Kwa upande wa Tanzania Visiwani walioshinda nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa ni Abdallah Haji Mgeni na Elias Cassion huku kwa upande wa Tanzania Bara nafasi hiyo ilichukuliwa na Gladness Urassa na Ramadhani Guruwe.

    Katika uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kigurunyembe, baadhi ya vigogo ndani ya chama hicho walikuwapo kuongeza nguvu katika kampeni.

    Mbali na vigogo hao pia watoto wao walikuwa wakiongoza kampeni akiwamo John Nchimbi ambaye ni mtoto wa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi, ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa mtoto wa Makalla.

    Aidha, uchaguzi huo uligeuka kuwa mkutano wa kampeni za ubunge wa vijana huku baadhi ya wagombea wanaotarajia kujitokeza kugombea ubunge kupitia UVCCM wakionekana kupigana vikumbo kugombea wajumbe ili kuweza kupata fursa ya kuzungumza na wapiga kura.

    ReplyDelete
  8. narudia tena najua na hii utaibana, swala la chipkizi ni CHILD ABUSE. maana ni kuwaingiza watoto katika kundi la kisiasa ambapo sheria za kimataifa haziruhusu watoto kuingizwa ktk siasa. mambo hayo yalikuwepo zamani hizo ambapo hata watoto pia walitumiwa ktk vita kabla ya kufikisha umri unaostahili kufanya maamuzi. huu ni uvunjaji wa haki za binadamu kwa watoto ambao lazima katiba mpya ije kuuondoa.
    watoto wanapaswa kufundishwa somo la uraia na haki za bindamu na za mtanzania,na kuvalishwa bendera ya taifa kuonyesha uzalendo kwa taifa na sio kuingizwa ktk makundi ya kisiasa huku wakikuwa na mitizamo ya kupingana kisiasa tangu utotoni,huu ni ukatili wa kisiasa unaohalalishwa na serikali. nitaishitaki serikali kwa jambo hili just give me a time.
    narudia let these blessed young ones grow with fresh and healthy mind free of political craps!!tunahitaji wanasayansi,wavumbuzi,na sio huu ujinga ujinga! we want children clubs to improve their heath,learnings and foster their creativity and talents in their development and not politicaly biased craps! narudia naandaaa mpango wa kuishitaki serikali na ccm kwa kitendo hiki,enough is enough!!

    ReplyDelete
  9. True dat anonymous wa Thu Dec 31, 02:03:00 PM. Hayo mambo yalikuwa na nafasi chini ya mfumo wa chama kimoja. Kila chama kikianza kupiga vikumbo vingine kutafuta 'chipukizi' hatutapata wanasayansi, madaktari wala wanasheria. Tutaishia kupata madokta feki bungeni.
    Sasa hivi watoto wanatakiwa kufanya mambo yasiyo na itikadi za kisiasa mfano uskauti. Wajifunze kupenda taifa lao, sio chama chochote cha siasa. Wajifunze kujiamini, upendo kwa binadamu wenzao sio kutafuta kura. Ningekuwa na uwezo ningelipeleka suala kortini.

    ReplyDelete
  10. Nchi isiyo na vipaumbele utaijua tu! Badala ya kuhangaikia mambo ya maana wako "bize" na chipukizi. Watawala: Grow up!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...