Kaka michuzi hii ni habari ya muhimu sana kwa wadau wa Globu ya Jamii kufahamu maana kupitia Globu hii wananchi wnegi wataelewa kinachoendela hapo uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JKN) .. naomba uipost..
Umekua ukisikia mara kwa mara vituko vya uwanja wa ndege wa JKN
kuanzia kuibiwa , kusachiwa kwa baadhi ya abiria , kulaghaiwa na aina
nyingine nyiingi sana za uharamu ndani ya uwanja huo kutokana na
ukuaji wa tekinologia hata hawa wezi na matepeli nao wanapandisha
viwango hata aina nyingine za uharamia wao .
Kwanza ni kwenye sehemu za kupitisha mizigo inayotoka na kuingia
nchini sehemu hiyo imejaa watu mbalimbali wanaohusika na usalama wa
uwanja na watu wanaotumia uwanja ule watu hawa kushirikiana na maduka
ndani ya uwanja huo ya kuuza vitu ambao ni wadau wakubwa wa wizi unaoendelea ndani ya uwanja .
Kama umewahi kuibiwa kitu kama laptop hatua ya kwanza ni kutoa taarifa
hapo uwanjani mara nyingi watasema vitu vyako vimeibiwa Nairobi au
Kilimanjaro na Ethiopia ukweli ni kwamba vitu hivyo huibiwa na watu wa
(majina kapuni kwa sababu maalum za maadili), sehemu za kwanza kuuzwa au kuhifadhiwa ni Duka namba nanihii ambao kuna Huduma za Internet. Duka hilo hujaa mali zilizoibwa ndani kwa kujidai Used Vimetoka Ulaya na Bara Asia .
Duka hilo hilo kama una haraka na kupanda ndege watakuuzia hata Vocha za
simu ambazo zimeshatumika na ukiondoka umeliwa
Saa zingine Abiria anaweza kua amefanya kosa badala ya askari
kumchukulia hatua anaweza kulazimishwa kuachia Laptop yake au Kamera
ili mradi ni kifaa kinachouzika haraka ndio maana ndani ya maduka hayo
vifaa vile havina charge , battery na vifaa vingine vya kuviwezesha
kufanya kazi kwa uhakika .
Ukizunguka upande wa Pili kuna duka la kuuza vyakula kuna mtanzania
mwenye Asili ya ki-Asia ukizungumza nae kwa upole na vizuri anaweza
kukuuzia laptop hata kamera ambazo husahauliwa au huibwa katika
mgahawa anaousimamia uwanjani hapo kwa jina la (kapuni) .
Umekua ukisikia mara kwa mara vituko vya uwanja wa ndege wa JKN
kuanzia kuibiwa , kusachiwa kwa baadhi ya abiria , kulaghaiwa na aina
nyingine nyiingi sana za uharamu ndani ya uwanja huo kutokana na
ukuaji wa tekinologia hata hawa wezi na matepeli nao wanapandisha
viwango hata aina nyingine za uharamia wao .
Kwanza ni kwenye sehemu za kupitisha mizigo inayotoka na kuingia
nchini sehemu hiyo imejaa watu mbalimbali wanaohusika na usalama wa
uwanja na watu wanaotumia uwanja ule watu hawa kushirikiana na maduka
ndani ya uwanja huo ya kuuza vitu ambao ni wadau wakubwa wa wizi unaoendelea ndani ya uwanja .
Kama umewahi kuibiwa kitu kama laptop hatua ya kwanza ni kutoa taarifa
hapo uwanjani mara nyingi watasema vitu vyako vimeibiwa Nairobi au
Kilimanjaro na Ethiopia ukweli ni kwamba vitu hivyo huibiwa na watu wa
(majina kapuni kwa sababu maalum za maadili), sehemu za kwanza kuuzwa au kuhifadhiwa ni Duka namba nanihii ambao kuna Huduma za Internet. Duka hilo hujaa mali zilizoibwa ndani kwa kujidai Used Vimetoka Ulaya na Bara Asia .
Duka hilo hilo kama una haraka na kupanda ndege watakuuzia hata Vocha za
simu ambazo zimeshatumika na ukiondoka umeliwa
Saa zingine Abiria anaweza kua amefanya kosa badala ya askari
kumchukulia hatua anaweza kulazimishwa kuachia Laptop yake au Kamera
ili mradi ni kifaa kinachouzika haraka ndio maana ndani ya maduka hayo
vifaa vile havina charge , battery na vifaa vingine vya kuviwezesha
kufanya kazi kwa uhakika .
Ukizunguka upande wa Pili kuna duka la kuuza vyakula kuna mtanzania
mwenye Asili ya ki-Asia ukizungumza nae kwa upole na vizuri anaweza
kukuuzia laptop hata kamera ambazo husahauliwa au huibwa katika
mgahawa anaousimamia uwanjani hapo kwa jina la (kapuni) .
Ukienda mbele kidogo Kuna duka la ziada Nalo la vitu vidogo vidogo
kuna kijana mwenye asili ya visiwani kazi yake kubwa ni kununua simu
zilizoibwa uwanjani hapo ni mtaalamu wa kubadilisha hizo simu ziweze
kutumika Tanzania .
Ndani ya duka iloilo wauzaji wa Tiketi bandia za kusafiria wapo na
ukitaka ni bwerere haswa za mashirika yetu ya ndani kama Air
Tanzania , PrecisionAir na ZanAir .
Ukikaa uwanjani usishangae kuona askari polisi anatoka kwenda kwenye
gari ya msafiri mara nyingi ni kwenda kupeana cha Juu..
HASWA HIYO NI PICHA KAMILI YA BONGO YETU.JAMAA WANADHANI NDO UMJINI HUO KUMBE WASIJUE NI GHASIA KWA WAGENI.INATIA AIBU KWA KARNE HIZI DOLA ZIPOZIPO TU;.
ReplyDeleteNilishajisemea kuwa hii nchi yetu imeuzwa. Wenyewe si wazawa tena.Ngoja niendelee kupiga box tu.
ReplyDeleteGood intelligence, sasa vyombo inavyohusika vifanye kazi yake mtu amekwisha watafunia nanyi mtumie mafunzo mliyonayo kumalizia kazi. Kuhakikisha nchi inasafisha uoza huu. Jamani msifurahie kununua vitu vya wizi ujue mwenzio analia nawe laweza kukufika kama jamii imepotoka kiasi kikubwa. Mkuki kwa nguruwe kwa.............
ReplyDeleteMdau.
Is this true? Mbona mimi naitumia sana hiyo airport na maduka yaliyopo pale mbona hayafanani na hili analolisema huyu mdau. Pale nyingi ofisi za airline. Au anamaanisha upande wa departure for international travel? Kule juu? Kama ni kweli namshauri awasiliane na Prosper Tesha ambaye ni CEO wa Tanzania Airports Authority juu ya upuuzi huo.
ReplyDeleteHuu ndio upuuzi unaoleta aibu kila siku. Wakati wa kuweka majina kapuni ulishapita. Hayo maadili unayofuata ndio yanayotuletea matatizo yote haya. Weka majina hewani ili watu wajue na kuanza kufuatilia la sivyo utaonekana mtu wa porojo tuu kama magazeti mengine ya udaku.
ReplyDeleteilikuwa ni tarehe 2june 2009 saa tano usiku niliwasili na ndege ya klm toka amsterdam,wakati nasubiri mizigo yango kwenye ule mkanda unaozunguka[conveyer belt] nilishangaa kuona mizigo yote imetoka kasoro mabegi yangu..baada ya kuuliza wahusika wakanambia nisuri kidogo kisha beg langu liliwasili na ndipo mjamaa wakakagua na kuniambia natakiwa nilipie ushuru kwa kuwa nilibeba sm nyingi.walipocalculate wakanipa hesabu nami nikawaomba nilipie kwa hela za kigeni.tukiwa kwenye proces akatokea jamaa ninayemfahamu tuliposalimiana akaondoka.wale jamaa wakaniuliza unamfahamu vp yule jamaa? nikawajibu kuwa aliwahi kuwa classmate wangu.wakanambia basi tumekusamehe..nilipofika nyumbani nikabwaga mabeg nikalala.kesho yake ndo nashtukia kuwa sim sita hazipo.nimebaki na charger na earphone.kwenda kuriport wakadai watafanya uchunguzi na mpaka leo sijapata jibu na watu walioniagiza simu wananidai kama mwizi..ni aibu sana kwa matukio kama haya..tunaomba wahudumu wa eaport muache wizi.mna dhamana kubwa sana kwa kuaminika kufanya kazi hapo..mdau uk
ReplyDeletenaomba mnisaidie nyinyi mnaoibiwa, hivi masanduku yenu mnafunga na kufuli au mnaacha wazi?na zile digital locks mnafunga kwa namba zenu za siri?kama mnafunga wanavunja au kuchana???mimi napita sana DIA na sijawahi kuibiwa sababu nafunga na locks,kama UNAACHA BILA KUFUNGA NA KUFULI AU DIGITAL CODES LAZIMA UIBIWE SIO DIA TU,HATA HEATHROW WANAIBA LAPTOPS,CAMERAS N.K,nishaona programu on tv wakishika wezi heathrow....wizi uko kila mahali jitahidini msirahisishe kazi ya hao wezi,FUNGENI MASANDUKU YENU NA KUFULI,KAMA WATAVUNJA KUFUNLI HAPO UNAWEZA KUSEMA WAMEVUKA MIPAKA LAKINI NAJUA WANAIBA MABEKI YASIYOFUNGWA NA KUFULI......na kuhusu kusachi lazima wakague kwani kuna watu wanakuja na bidhaa za biashara hawataki kulipia ushuru..simu 20-50 sio zawadi tusidanganyane lazima mlipie ushuru kwani nyie ndio wa kwanza kupiga kelele kuhusu maendeleo na kodi ndio zinaleta maendeleo
ReplyDeleteHAPPY NEW YEAR,MDAU UK
Kwa kweli wakuu inapofikia wakati unawaza utakapofika J.K.N Airport unajikuta na kizunguzungu kinakupata ,Maana mambo yanakuwa siyo kabisa!Just imagine una ka zawadi cha kawaida tu lakini cha ajabu unakutana na mhusika pale na bila ya hata chembe ya aibu anakuja na anakutolea macho kama mtakattifu fulani na calculator yake akikuuliza ulinunua bei gani?utakapotaja au kuonyesha receipt utachoka kabisa maana itatajwa pesa ya ajabu ajabu tu!Inatia simanzi na huzuni kuona tunavyopelekwa pelekwa na wezi hawa. Ila next time ni bora mtu upitie Nairobi kama vipi uanze kula border la Namanga utajua huko ila pale hapana jamani kha!Ni aibu hii!Kha!
ReplyDeleteAirport yetu is a joke,kabla hujafika kwenu unaanza kujiuliza leo nitakuwa na tafrani gani, it's sad kwamba safari ya nyumbani inkuwa na mashaka just because of few stupid people at the port. Uongozi wa airport unayajua yote haya but it's all part of our ignorance, no one is responsible. Nyerere amekufa now nchi haina mwenyewe,our country won't change mpaka uongozi ubadilikie, from top to bottom. It's sad but going home is just a nightmare nowadays.Do you know how many people were sent to Copenhagen ???, what the f&*%$#&, things like that really hurt.
ReplyDeleteHIYO YA TIKETI NI KWELI KABISA MAANA HATA MIE WAMEWAHI KUNIUZI TIKETI YA ATCL KWENDA MWANZA KWA BEI NAFUU. NIMEFIKA DARASHANI, MUUZAJI AKANIAMBIA ONGEA NA YULE PEMBENI KWANZA. AKAJA KIJANA AKANIAMBIA 150,000 MPAKA MWANZA. NDIO WAKANIPA TIKETI. HII DHAMBI NAIJUITIA MAISH AYANGU YOOTE MAANA NA MIE NIMESHIRIKI KUIUA NDEGE YETU. WATANZANIA NISAMEHENI. NA FEEL SO GUILTY. MUNGU PIA ANISAMEHE NI MIAKA 2 SASA IMEPITA
ReplyDeleteITS NOT AS BAD AS YOU,RE TRYING TO MAKE IT LOOK LIKE,HIZO NI CHALLENGE TU LAZIMA MZIKABILI,SIO WOTE WANASUMBULIWA NI RANDOM SEARCHES POLE IKIKUANGUKIA KILA UKISHUKA DIA
ReplyDeletejina kapuni au duka fulani maana yake ninini?mi nashindwakuelewa nyie watu mnamaana gani nahii misemo yajina kapuni inaonyesha mnapendakuibiwa taja jina husika la duka nadhani utakuwa umefanya jambo lamaana sana kulikokufichaficha watu tunakuona mzushi,labda nawewe nimmoja wao mmezinguana katika mgao ndiomaana unaonanoma kutaja jina la duka,ningekuwa Mr Curry(MICHUZI) nisingeweka malalamiko kamahaya.
ReplyDeleteWANAFUNZI TUNAOSOMA NJE TUNATESWA SANA HAPO JK AIR PORT.HADI NATAMANI KUJA HOME KWA USAFIRI WA TREN.TUNAOMBA VIONGOZI MUANGALIE HILI!!!!!!
ReplyDeleteMWAKA HUU MWEZI WA SITA MIE JAMANI MWAKA HUU NIMEKUJA NYUMBANI KUNA BABA MKAKA HAPO ALINIKERA SANA.PALE ALIPONIAMRISHA KUFUNGUA BEGI LANGU KWA LAZIMA,PAMOJA NA KUMWAMBIA KUWA MIE NI DENTI NA SINA KITU NDANI NI NGUO TUU.NLIVUNJA BAG LANGU NA KUFUNGUA ALICHOAMBULIA NI KUONA ALWAYZ TUU.ALINIKERA NA NILIMWEKA ALAMA NA HADI LEO NNA CHUKIA TZ UWANJA WA NDEGE.WIZI,UCHAFU,ULAGHAI UMEJAA,VIONGOZI MNAONA HILI JAMANI.Tunapita nchi zaidi ya 5 na tunapita salama kama wanafunzi na ukweli ni hatuna chochote ila home hapo ndo hao wavaa nguo za blue wanatutesa.Jamani HII MADA IMENIGUSA SANA,WENGINE WANAPITA NA KILO 50-60,WE MWANAFUNZI NA VIRASTA VYAKO VIWILI VIMEZIDI HAPA KANUSU KILO WANAKUBANA ETI TOA USD 250 KWA RASTA ULIZONUNUA TZ KWA 1500TSH.ITS SHAME!!!MNATUJENGEA CHUKI TAIFA LA KESHO
Seriously wewe uliyeuliza kama watu wanafunga na codes unamaanisha hujui kama airport yoyote ile wanaweza kufungua zile code, na kuzifunga tena, na huwa wanafanya hivyo randomly na ni legal.
ReplyDeletemimi nimeondoka tar 23dec na kenya airways, nimefika airport saa nane ndege ilikuwa inaondoka saa tisa nikakuta wameondoa kibao chao na wakasema hawataweza kuni-check in since nilikuwa natakiwa ku-connect another flight in nairobi ikabidi nimbembeleze huyo mama aliyekuwepo hapo KQ jamani akaanza kwa kusema kweni una nini??kwanza sanduku lako lina kilo nyingi(lilikuwa na 21kg) nikamwambia naweza nikatoa viatu nikaweka kwenye hand-luggage akasema hand-luggage hairuhusiwi kuweka viatu since nilikuwa na shida ilibidi nikae kimya nikasema poa naweza nikaondoa nguo alivyoona niko flexible mbeba mizigo akaniambia unakitu gani ili ni kusaidie kupeleka bag yako faster i told hm sina akasema shauri yako naacha bag yako anyway wat to do nikamwambia nina voucher za voda za 5,000 akaniambia nimpe so i had no choice zaidi ya kumpa
ReplyDeletebut i was so dissapointed with the black lady in kq na mbeba mizigo later on people who were behind complained the same u can imagine wanaondoa kibao mapema ili wapate hela
Hii ni aibu sana kwa Taifa wao wanaona ni kitu kidogo lakini ni kikubwa hatujiharibii jina tu tunajiharibia hata mambo ya utalii,kwa sababu utalii ni rasilimali ya taifa sasa wizi kwenye mizigo ya wageni ni aibu sana kwa sababu hao wageni wanaibiwa na wanawaatarifu wenzao kule wanakotoka au wanaweza kuandika kwenye mtandao ni aibu sana.Na madhara yake ni makubwa sana hayo sio maendeleo bali kuua Taifa la leo la kesho.
ReplyDeletempk mbeba mizigo anataka rushwa.! ATCL imekufa kwa haki, mimi nakumbuka hapo ilikuwa ukitaka ticket wanakwambia ndege zote zipo full lkn ukienda masaa 3 kabla ndege kuruka ukimpata mtu unayemjua unapata ticket naukiingia ndani chaajabu ndege inaruka nusu ya seat zipo wazi, yaani mtu kweli anaona ni bora apate 20,000 yake kuliko shirika kupata 120,000.? hata mimi nilipata sana ticket kwa njia hii kwani bila hivyo nisingesafiri, sorry tz for being dishonest to u!
ReplyDeletewadau wengine full miyeyusho,sasa unazungumzia makufuli na pin lock..kwanini tulazimike kuweka pin na makufuli wakati tunarudi kwetu? ina maana hao wezi wa eaport wanaiba eti kwa sababu tu mabegi nhayana kufuri.kwani beg likikosa kufuri wanashindwa kujizuia kuiba? unanitia mashaka inaonekana hata wewe ungekuwa unafanya kazi pale ungiba na kusamehe mabeg yenye kufuri tu..hiyo heathrow unayodai kuna wezi mimi nimepita zaidi ya mara tano na sijawahi kuibiwa kitu..basi washauri hao eaport ya dar waandike mabago kuwaonya wasafiri wote kuwa wanapotua bongo wahakikishe mabegi yao yote yana makufuri!
ReplyDeleteA/alaikum Mr Curry(Michuzi) pole sana kwakazi ngumu unayoifanya yakutusaidia sisi walalahoi kuondoa kero/dukuduku zetu mbalimbali kupitia Blog yetu hii yajamii Hongera sana,ni muda mwingi sasa tangu wadau wenzangu wameanza kutoa kero zao kuhusiana nauwanja wa Ndege wa JKN lakini nikwelikwamba hakuna lolote lililofanyika,mi ningeombautusaidie kamaunazifaham contacts zawahusika ilitujaribukupeleka malalamiko yetu mojakwamoja kwao huendawakatusikiliza,kwamaana Blog yetu nikama mjumbe huendahawayapati malalamiko yetu nahatakama wanayapata sisi hatunaushaidi najambo hilo so then wanayohaki yakuendeleakukaakimya nawalawashtuke wakadaikuwa hawaelewikinachoendelea kwamaana hawajafikishiwa malalamiko yetu juu yakero hizo,ni hayo tu mkuu.
ReplyDeletemdau uliyeleta malalamiko haya nakushukuru sana na mungu akubariki. maana mimi nilikuwa na duku duku pia na uwanja wetu huu. nilikwenda nyumbani april mwaka huu na wakati nilipokuwa naondoka nilidaiwa rushwa na kila mtu anayeniona. kuna dada mmoja anafanya british airways desk aliniganda hata akawa ananifuata nyuma nyuma. nikampa elfu kumi ili aache kunibugudhi lakini alikuwa anataka more. nahakuna alichonifanyia chochote cha yeye kutaka pesa kwangu. then akaja kaka mwingine tena nae anaomba hela ya chai. hii yote kwasababu waliniona na mkoba wa kiingereza. ni aibu sana soooo shame for a beautiful country like tanzania. i wish mwalimu angekuwepo hai ayaone haya yote . mdau
ReplyDeleteJamanu ehh, mi natoa ushauri ingawa sidhani kama ni wa maana sana. Ningeomba wale waliopo karibu na media especially TV watume watu wao hapo Airport kusubiri habari kama hizo, then Unapotokewa na tatizo kama hilo ulielezee wazi wazi bila woga na kutaja muhusika wako bila woga. mambo yawekwe hadharani nahisi hilo litasaidia kwa kiasi fulani maana kwa watanzania jambo lolote kushughulikiwa ni mpaka impact iwe kubwa. Wadau mwasemaje?
ReplyDelete