ZANZIBAR HEROES LEO IMEIONESHA UBABE TIMU YA TAIFA YA TANZANIA BARA KILIMANJARO STARS KWA KUICHAPA BAO 1-0 NA KUCHUKUA NGAO YA MSHINDI WA TATU KWENYE MICHUANO YA CHALENJI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
GEMU HILO LILILOPIGWA KUANZIA SAA SABA MCHANA LILIFUATIWA NA LILE LA FAINALI KATI YA RWANDA NA UGANDA AMBAPO UGANDA WALINYAKUA UBINGWA KWA KUWACHAPA WAPINZANI WAO BAO 2-0
tujadili nini tena
ReplyDeleteMAYOOOOOOO!!!!!!
ReplyDeleteMAXIMO LEOO,LEOOO,LEOOOO
sasa zile mbatat za urojo na chipsiza muhogo mlizokuwa mkizikejeli zitatafunwa pale kwa Adinani kama kawaida yetu Mnakaribishwa (mala maleo ,lajana kala nini ??)
ReplyDeleteHONGERENI ndugu zetu wa Zanzibar kwa ushindi mlioupata. Hii inaonyesha kwamba mlidhamilia kupata ushindi ktk mashindano haya. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteLazima kuna hujuma, Loh! Nadhani tungewakilishwa na Lipuli F.C Tungeweza kufanya vizuri zaidi Loh! Lunyamila yuko wapi? Nina imani timu ingefundishwa na Lunyamila tungefanya vizuri zaidi Loh!
ReplyDeleteChakujadili ni Maximo atolewe tushachoka na kuanza kuchanganya wachezaji waliofanya vizuri Bara na Visiwani basi pia wachezaji wanaochezea mipira Visiwani na Mikoani wasisahauliwe. Asilimiak ubwak ila siku Wachezaji wanaocheza Vilabu Dar-es-salaam tu. Mwaipopo
ReplyDeleteZenji oyeeee na siee tumo pia.
ReplyDeleteuk.
Hongereni ZnZ Taifa stars tushachoka na maximo.
ReplyDeletemaximo asiondoke,abaki kuact movie ni muugizaji mzuri wa movie kwakweli tusije kukosa kipaji.ila kwa mpira sijui manataka mpaka afanye nini zaidi.atembee uchi uwanjani, ndo mumuondoe jamaa hafai kwakifupi kuondoa wakongwe wote kwenye timu imetucost kinoma!!!
ReplyDeleteHahahahahaha...! Naona leo watanganyika mkiongozwa na ISSA MAROST,mko kimyaaa, hata habari imekuja robo...hatuambiwi goli kafunga nani dk ya ngapi! Duhh ...ndo basi tena, haikufaa lami, litafaa vumbi la mkaa? Mdau Mathew Mndeme naomba u report haya matokeo kwa makeke kama ulivyo report ile mechi ilopita! Wallah napata ushungu! Kocha wenu wa tanganyika analipwa kwa kodi za wazanzibar na nyinyi watanganyika, tena analipwa mamilioni ya shilingi, halafu matokeo ndo kama hayo, sisi kocha wetu tuna mlipa wenyewe kwa pesa zetu za karafuu na nazi, wala hatoki brazil huyu..!
ReplyDeleteIngekuwa zanzibar inapata nafasi ya kuwakilisha Tanzania, kama Tanganyika inavyopata nafasi basi tungekuwa mbali sana hivi Watanzania kimichezo. Lakini huyo kocha wenu fundi bomba kutoka brazil ana hubiri chuki na majungu badala ya mpira. FUKUZA HUYO
La kufanya sasa ni kuifanya Mapinduzi Stars iwe Taifa Stars.
ReplyDeleteBaya Zaidi,Ni kwamba huyu kocha aliwekwa majungu hata Abdi kassim akawa hapewi namba ni benchi lakini huyu huyu ndio alowafunga leo kwa freekick,na ingelikua kuna Beki mwengine bora kuliko Canavaro basi pia na yeye asingepata namba,sasa MAXIMO asione haya kuchanganya wachezaji,yeye aliiponda sana Znz before sasa leo sijui atasema nini,insemekana huyu maximo sio kocha,ni mtu wa kawaida lakini ni moja kati ya serikali kuiba fedha za wananchi wanamlipa dola 1000 wansema ni elfu kumi.
ReplyDeleteMACOMPUTER GREECE
Yaani leo nmefurahi saaaaana duh moto zenji ndio taifa kubwa teh teh teh heh heh heh ila si tunajua kwa nn zenji wanaminywa kisoka sababu ni moja tu KIPAUMBELE KWANZA KWA TANGANYIKA TU......ah nsiseme sana wacha nende KFC kula kuku na washkaji kusherehekea ushindi
ReplyDeletecomment yangu isibaniwe
mdau 999
Hahahaaaa kweli wala urojo wamewashinda wala sembe?
ReplyDeletemuheshimiwa muhidini issa, nilisema mrefu wa mbilikimo atakuwa mbilikimo ukanibania lakini inabakia ukweli.muheshimiwa mbilikimo wa akili na atachagua kila kitu kitakuwa kama alivo mwenyewe.kaanzia baraza la mawaziri mpaka makocha. kama unataka kubana bania tu
ReplyDeleteHONGERA MAXIMO.WEWE NI KOCHA BORA DUNIANI.
ReplyDeleteNAPENDEKEZA ABAKIE HAPA HAPA HADI SIKU YA KIAMA.
MAXIMO OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
MDAU KISIJU.
Maximo oyeeeeeeeeeeee...
ReplyDeletemdau KISIJU
MLA MLA LEO, MLA JANA KALA NINI? Nifuraha ilioje hpa Hyderabad, India. Yaani full kujiachia, hongereni kaka zangu Zanzibar heroes, mfundisheni kazi Maximo hana lolote hyo kazi ubaguzi tu.HONGERA ZANZIBAR HEROES
ReplyDeleteNina imani kuwa mshahara anaolipwa Maximo kwa mwezi( USD 15,000) wakipewa makocha wawili wazalendo na timu ikiwezeshwa kwa vifaa na mahitaji mengine kama ilivyo sasa basi tutafika mbali sana. Imani ya kuwa kocha wa nje anajua zaidi imepitwa na wakati kwa vitendo anavyofanya Maximo. Hiyo timu apewe Mziray na Kibadeni au Mkwasa na Bushiri au Marsha na Mziray.
ReplyDeleteMafanikio ya kocha hupimwa kwa ushindi wa timu na sio kwa vyeti alivyo navyo, sasa ni wakati wa kumcharaza bakora huyo Maximo anayekumbatiwa na JK na TFF.
ReplyDeleteKwa taarifa yenu, huyo jamaa tunapanga kumpiga wakati wowote kama atendelelea kuleta majungu yake na kuwaacha wachezaji wazuri kutokana na sababu za mitaani.
Kili Stars ikishinda hela za wachezaji
ReplyDeleteSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema, zawadi watakayoipata wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itakuwa yao.
Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela, amesema, zawadi hiyo itachukuliwa na wachezaji ikiwa ni njia ya kuwapa kifuta jasho kwa kupigana kulitetea taifa.
“ Tangu awali tuliwaambia wachezaji kama wangechukua ubingwa, basi zawadi ingekuwa yao, na katika nafasi ya pili na yatatu pia,” amesema.
Kilimanjaro Stars inatarajia kuumana na Zanzibar Heroes kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo itakayofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.
Mshindi wa tatu wa michuano hiyo ataondoka na dola za Marekani 10,000 ( sawa na zaidi ya Sh milioni 10) wakati mshindi wa kwanza atazawadiwa dola za Marekani 30,000 na wa pili dola za Marekani 20,000.
Stars ilitolewa na Rwanda kwa mabao 2-1 katika mechi ya nusu fainali wakati Zanzibar Heroes iliondoshwa na bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Uganda kwa mabao 2-1.
Fainali za michuano hiyo iliyoshirikisha nchi 12, zikiwemo mbili zilizoalikwa, itazikutanisha timu za Rwanda na Uganda.
**********************************
Huu ni upuuzi mwingine wa TFF, wanataka kutuaminisha kuwa wao kama taasisi walitoa kila aina ya vichocheo vya morali kwa wachezaji ili washinde. Hivyo, kushindwa kwa timu kusitafsiriwe kwamba hawakutoa supoort kwa wachezaji. Ni kweli morali ni muhimu, lakini kwanza morali si pesa tu. Unawaahidi pesa wakati unajua timu haina Mwl aneweza kuwaanganisha wachezaji na badala yake ni chuki na visasi kwa wachezaji. Haya matokeo ni ya JK, TFF na Maximo. Watanzania Bara wengine wote tunaungana na Ndg zetu Mashujaa wa Zanzibar Herous! Zanzibar hoyeeeeeeeee! Hapo mmefanya jambo nzuri sana!
Hii ni kashfa kubwa!
ReplyDeleteItakuwaje kijinchi kadogo cha Zanzibar(watu hata milioni moja hawafiki) na ndogo kuliko wilaya yo yote ile ya TZ bara iweze kutushinda na kutuadhiri ugenini?
Tatizo si Maximo pekee, hata hao makocha wa kienyeji kabla ya Maximo hali haikuwa tofauti sana. Tatizo ni kun'ga'gania wachezaji wa Simba na Yanga ambao hubandikwa majina makubwa kupita uwezo wao.Hata hao vijana wa Zanzibar ambao ni wazuri hawapewi nafasi kweye timu ya Taifa stars(zaidi ya kuchukuwa wachezaji wawili kutoka Zanzibar kila mwaka ili ionekane tu kuwa na Zanzibar ni sehemu ya TZ.
Au anaposema kuwa asilimia 15 ya Watanzania wanamchukia, 15 wanampenda sana na 70, wanafuata upepo ina maana yeye anapendwa na watu asilimia 15 tu, hao wengine 85 si wake na hawamtaki, je, hao ni wa nani? Mfano alisema:
ReplyDelete“Ndiyo kwanza nimerudi nchini, bado sijayapata. Ngoja niyapate sawasawa ndipo nitayazungumzia. Lakini nimesikia...ningeshangaa kama wangenisema vizuri”, alisema Rais Kikwete.
Alipoulizwa kwanini unasema ungeshangaa kama wangekusema vizuri, alijibu “Kwani wewe hujui?”
“Asilimia 15 watakupenda sana, asilimia 15 watakuchukia sana. Asilimia 70 wanaangilia upepo, sasa jiulizeni hao wanaonisema hivyo wanaangukia wapi? Kwa hiyo nitayatazama maneno yao ili kuona kama kuna ya maana, maana najua hakuwezi kukosekana yenye maana. Hayo tutayatolea uamuzi, lakini yale yaliyosemwa kwa sababu ya chuki tu, basi tutawaacha waliosema na chuki zao.”
Hapo mkuu wa nchi anasema kuwa kuna watu wana chuki naye katika nchi anayoiongoza, inatia wasiwasi na kuwaogopesha wananchi hasa raia wema. Ila kwa hili ni changamoto kwa Watanzania wanapaswa kujifunza kuwa mfumo tulionao wa uongozi ni mbovu.
NDIO TULIOWAPA DHAMANA YA KUTUONGOZA, SASA TUSILALAMIKE MAANA TULIYATAKA WENYEWE!
MIMI KISIJU NILIKUWA NAWAELEZA KILA SIKU KUWA MAXIMO SIO KOCHA NI GOGORO NILIPINGWA SANA .LEO WANAFIKI WOTE MNAKUJA KUSEMA MANENO NILIYOYASEMA.
ReplyDeleteACHENI UNAFIKI MLIKUWA MNASEMA KUWA MAXIMO NI BINGWA.SASA MNALIA NINI?
MDAU KISIJU.
matokeo ya Leo..yanathibitisha kauli ya Mbunge--Mh. Hafidh Ali,.. kwamba bara mna upendeleo tu na kuendekeza tabia ya kuwatenga Wazanzibari kimichezo..lakini hamna lolote kubwa...yani hata "kikombe cha kahawa" hamjawahi kupata...!!! ...matokeo haya ni ya kawaida tu. Zanzibar imeifunga tanganyika mara nyingi zaidi. Uwezo wa kusakata kabumbu kwa vijana wa Zanzinbar ni wa hali ya juu...tatizo hawapewi nafasi.
ReplyDeleteMdau,
OHIO-USA
WATANZANIA TUSIENDELEE KUMKASHIFU MAXIMO, WAKATI WA UKOCHA WAKE TUNAWEZA KUONYESHA JAPO MECHI KADHAA ZA KIMATAIFA AMBAZO NI NGUMU NA ALIWEZESHA USHINDI. TOFAUTI NA ILIVYOKUWA KABLA HIVI MNAWEZA KUMZUNGUMZIA KOCHA YEYOTE MZALENDO NA KUONYESHA CHA MAANA ALICHOIFANYIA TAIFA STARS. WABONGO TUACHE MANENO MENGI KATIKA SOKA TUTAFUTE SURUHISHO LA KIWANGO CHETU CHA SOKA, NA TUACHE KUWAPA KICHWA WACHEZAJI WASIO NA NIDHAMU HATA KAMA NI WAZURI KIASI GANI MAANA SIFA YA MCHEZAJI NI PAMOJA NA NIDHAMU NDUGU ZANGU. MIMI NI MMOJA KATI YA WATU TUSIOWAFAGILIA KABISA WACHEZAJI WASIO NA DISPLINI HATA KAMA UWANJANI WANAWEZA KUCHEZA VIZURI, SOKA NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE YEYOTE NDO MAANA HATA WATU KAMA WAHASIBU, WAALIMU, AU WANASHERIA HUSIMAMISHWA KAZI IWAPO WATAMISIBIHEVU NOMATA KAZI YAO NI NZURI KIASI GANI. FOREKZAMPO MWALIMU ASIPOHUDHURIA VIPINDI VYAKE KWA KIWANGO FULANI HUONYWA AU KUSIMAMISHWA KAZI HATA KAMA HUFAURISHA DARASA ZIMA, MUHASIBU AKIWA MLEVI NA HUCHELEWA KUFIKA KAZINI AWEZA KUFUKUZWA KAZI HATA KAMA HAJAWAHI KUIBA WALA KUDUMAZA SHUGHULI FLANI. VIVYO HIVYO MCHEZAJI AKIWA ANAVUTA BANGI NA KUTOKUWA NA NIDHAMU HUSIMAMISHWA KAZI HATA KAMA HUCHEZA VIZURI UWANJANI. MAXIMO HOYEEEEEEEE NA ENDELEA NA MSIMAMO WAKO WAACHE WABONGO NA TABIA ZAO ZA KUYAENZI MAJINA YA WACHEZAJI. CHUJI-CHUJI-CHUJI-CHUJI HUIZI HI BAIZEWEI
ReplyDeleteBaada ya moja ya mechi ilizoshida Stars, mwandishi mmoja kule Nairobi alitumia kiingereza kummwintavyuu mchezaji mmoja mashuhuri wa Kili stars aliyefunga magoli. Basi ilikuwa vichekesho vitupu. Sasa kocha wetu huyu mbrazili kiingereza cha kubabaisha, wachezaji nao kimombo hawakipati, basi matokeo yake sasa ndio haya. Eti watu walitegemea kocha huyu ndiye ataipeleka timu yetuya Taifa World cup! Hahahahaaaaaa Bongo bwana...we acha tu!
ReplyDeleteBonyeeeeeeeeeee, Mdebwedoooo!
ReplyDeletempelekeeni cd ya mchezo huu JK
ReplyDeleteme nshasema kwani soka lipo bongo??hatuna mpira hapa ni mdako tu,,afu uku ndo kuzidi kuchukiana na mpasuko wa muungano....
khaaa zenji wamefunga,hahahaaaaa hongereni jimbo la tanganyika!!
Maximo ni jeuri, ila jeuri hii anaipata kutokana na JK na TFF,ila ajue tu kila lililo na mwanzo lina mwisho wake,kilicho baki ni kuwaachia timu yao Maximo,JK na TFF hio ndio dawa yake.Ushauri wa bure kwa Maximo alipofika pametosha angekuwa muungwa akirudi tu ajiuzuru huo ni ushauri wa bure.
ReplyDeleteJK ahsante sana kutuonyesha njia kuwa tunaweza, hapa JK hana kosa, Kosa lipo kwetu pamoja na TFF, Huyu Maximo keshafikia kikomo cha kufundisha, aliipaisha timu kiasi kabla hawajakaa sawa kuzoeana kabadili timu tokea amekuja miaka zaidi ya 3, kabadilisha wachezaji karibu wote walioenda Brazil wamebaki 2 tuu, chuki,majungu na mademu ndio wamemmaliza na hata chuki na wachezaji ni mademu matokeo anadai hawana nidhamu,yeye keshafikia ukomo wake AONDOKEE!! TFF bado wanamkumbatia JK hana kosa keshatimiza wajibu wake na sasa ameelekeza macho yake ktk RIADHA nao waamke, Kigmb
ReplyDeleteKwanini mnamlaumu kocha tuu? Kwanini hamtaki kukubali kwamba soka la zenjibari ni kubwa kuliko soka la zenjibara? Zenjibari kuna vipaji zaidi, na mimi ninayesema hivi ni mzenjibara.
ReplyDeletekaka michuzi pole sana najua imekuuma ndo maana hii habari ata haina madoido ya aina yeyote. lakini langu moja ukubali kwamba kiwango chenu ni dhaifu na wazenji tuko juu. tizama mifano miwili tu yule mzanzibari mmoja alienda ureno maan baada kushinda mchakato mgumu na yule mcheza bora katika copa cocacola unalo marosti. cha zaidi kinacholeta huu mpasuko ni huyo eti cocha wa kimataifa nimwite masimo na si maximo au mashimo alipokuja huku kwetu na kusema hajaona viwango sasa inakuaje viwango gani ivyo au vya kufungwa kama ivyo kweli huku hakuna teh teh teh teh .
ReplyDeletemdau zenj