



Kwa miaka mitatu mfululizo NMB imedhamini maendeleo ya soka nchini Tanzania. Udhamini wa NMB umegawanyika katika maeneo matatu Timu ya Taifa, Maendeleo ya soka la vijana na Shughuli za TFF. Katika kuendeleza soka la vijana kila mwaka NMB inatengeneza na kugawa mashuleni zaidi ya mipira 5,000, hugharamia mafunzo ya makocha ambapo hadi sasa zaidi ya makocha 700 wameshapata mafunzo kupitia mkakati huu, pia NMB hutoa udhamini kwa timu ya vijana chini ya miaka 17.
Mwishoni mwa wiki NMB ilitumia ziara ya timu ya Taifa ya Ivory Coast yenye wachezaji wengi wa kimataifa kutia ari zaidi ya maendeleo ya soka la vijana kwa kuendesha kliniki na kugawa mipira na jezi kwa timu za vijana.
Akizungumza baada ya kutoa vifaa hivyo kwa kushirikiana na Timu ya Ivory Coast, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula alisema ‘’ ili kupata maendeleo ya soka ni lazima kuwekeza kwenye soka la vijana, ziara ya timu ya Ivory Coast na hususani uwepo wa wachezaji maarufu wa kimataifa nchini unaongeza hamasa kwa vijana wa Ki-Tanzania wenye malemgo ya kuwa wachezaji wa kimataifa hapo baadaye’’.
Licha ya kupata mipira na jezi wachezaji wa timu hizo walionyesha vipaji, kupiga picha na kupata nafasi adimu ya kuchanganyika na wachezaji wanaowapenda na kuwaona kama mfano wa Ivory Coast.
MNAONAJE SHUGHULI KAMA HIZI MNAZOFANYA MKAZIFUNGULIA WEBSITE ILI MUWEZE KUSAMBAZA HABARI ZENU ZAIDI?? hAMUONI KUWA HUMU NAFASI INABANA SANA? NDIO YALE YALEEEEE!!
ReplyDeleteGood stuff. Kweli wengi hawajui kama juhudi kama hizi zipo. Hongera NMB. Ni vema kuwatumia wakongwe wa soka mikoani pia ambao wanaheshimiak na jumuiya zao ili kusaidia kuendeleza vipaji kama hivi. Kwa miaka mingi hapa Musoma na Mwanza zimekuwepo juhudi za binafsi kwa miaka nenda rudi (Sylliverster Marsh anaweza kutoa maelezo mazuri zaidi) na japo hutokea vipaji hapa na pale mara hufifia kwa kukosa muelekeo. Juhudi za kitaaluma zikitukima ufanisi utakuwepo.
ReplyDeleteNi kweli kabisa maendeleo ya soka huanza na vijana. Kwa hili nawapongeza sana NMB hususani Imani kwa ubunifu. Ila program hizi zije na mikoani hadi wilayani.Jamani Haruna Kone kijeba zaidi ya Mrisho Ngassa!!!.
ReplyDelete