TIMU YA TAIFA YA TOGO

TIMU YA TAIFA YA TOGO LEO IMEJITOA RASMI KATIKA KUSHIRIKI MICHUANO YA SOKA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA HUKO ANGOLA, BAADA YA MTU WA TATU KUFARIKI DUNIA KUFUATIA SHAMBULIZI LA BASI LILILOBEBA WACHEZAJI HAO KUSHAMBULIWA KWA RISASI NA WAPIGANAJI A MSITUNI WANAODAI KUJITENGA JIMBO LA CABINDA.

HABARI TOKA RWANDA ZINASEMA KOCHA MSAIDIZI, AFISA HABARI NA DEREVA WA BASI WAMEKUFA NA WACHEZAJI WAWILI WANAUGUZA MAJERAHA KADHAA, NA KUIFANYA KAMBI YA TIMU HIYO KUJAWA NA FADHAA NA KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA. TOGO ILIKUWA INAINGIA DIMBANI KUKWAANA NA GHANA KWENYE MECHI YAO YA KWANZA HAPO CABINDA. TIMU ZINGINE ZILIZO KWENYE KUNDI HILO NI IVORY COAST NA BURKINA FASO.

KOCHA WA TOGO HUBERT VELUD AMENUKULIWA AKISHAURI KWAMBA MICHUANO HIYO IAHIRISHWE MOJA KWA MOJA.

HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. It is a shame on how we treat each other in Africa...when will this end?

    ReplyDelete
  2. sijui ni vigezo gani vilitumika kuichagua angola, hii nchi bado haijatulia kisiasa na ni juzi tu hapa wametoka vitani chini ya savimbi. hili ndio kosa pekee lililofanyika

    wazungu wamepata ya kuongea maana hawataki kbs wachezaji wao waende CAN na zaidi timu za UK

    TOGO wamepata sababu ya kukimbia aibu

    ni wanne mpaka sasa waliopoteza maisha pia tujilaumu kwa hawa mgaidi waafrika wenzetu wasiokuwa na akili na huruma.

    MUNGU AZIPUMZISHE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.AMEN.

    ReplyDelete
  3. TUWAPE POLE KWA MAUAJI NA MAJERUHI

    Tunasikitishwa na maafa yaliyowatokea,hakuna aliyoyatemea, tunavyoelewa haya yanaweza kutokea popote ulimwenguni,tunaheshimu uamuzi walioupitisha.

    Ningemshauri raisi wa TFF Mzee Tenga haraka saana kupeleka ujumbe wa kutoa salaam za rambirambi kwa viongozi na wachezaji wa Togo.
    Wakati huo huo angeitumia nafasi hii kwa mapendekezo ya haraka kupeleka maombi kwa kamati kuu ya kombe la Afrika na FIFA kwa Taifa Stars ya Tanzania kuchukuwa nafasi ya kuwawakilisha Togo.
    Muda ni mfupi lakini kimtazamo timu yetu kwa sasa kimchezo ipo kiwango cha juu hatuhitaji matayalisho ya muda mrefu kuwawakilisha Togo,zaidi ya hapo hatuna cha kupoteza,hata kama hatutofanya vizuri kuleta matokeo ya ushindi,tutachukulia kama mojawapo ya imani yetu kwa maafa ya Togo na matayalishso ya michezo ya kombe la Afika na ulimwengu kwa miaka ijayo.
    Mzee Tenga "please act fast" peleka kikosi chako cha wawakilishi katika kambi ya Togo na kamati kuu ya kombe la Afrika na FIFA.

    Mickey Jones Amos
    Denmark

    ReplyDelete
  4. hii ni aibu kwa angola,sasa tanzaniaa tujipange kuandaa kombe hili,tunao uwanja mzuri dar,zanzibar uwanja uko kwenye matengenezo,tff na serikali waviboreshe viwanja vya mwanza na arusha tuwe wenyeji wa kombe hili.linawezekana

    ReplyDelete
  5. Safi sana Togo.. kwa wote waliopoteza maisha..R.I.P, wachezaji warudi nyumbani wakapumzike tu

    ReplyDelete
  6. Angola inapaswa kulaumiwa. wakiwa wenyeji wa michuano mikubwa kama hiyo na ambayo inakusanya wachezaji maarufu sana kama drogba, kalou, toure, yaya toure, adebayor, essien, muntari nk walitakiwa kuandaa ulinzi mkali sanasana katika miji yote na mipaka. halafu ukizingatia hapo mji wa cabinda yalipotokea mashambulizi ndipo kundi lenye ghana, ivory coast, togo lilipo. yani hapo ndo wachezaji wakubwa woote watakapochezea. mimi nadhani wangamisha kabisa hiyo venue wakaipeleka kwingine manake huo mji umeshaprove unsafe. anyway hii itafanya world cup south africa kuwe na ulinzi tight kupindukia.
    Martin

    ReplyDelete
  7. Nawapa pole sana Togo kwa hali hii wasingeweza kucheza kwa sababu akili ilishaathiriwa na hilo shambulizi

    Tujiulize kwa nini hii imetokea? inahusiana nini na hao waasi kujitenga?

    ReplyDelete
  8. habari za wikienda ankalll?

    nashukuru kwa kutuhabarishaa maana hiki kitendo si cha ungwana kabisa walo fanya hao mauji walaaaniwe na wasakwe juu chini.mungu wape moyo wa uvumilivu walo fiwa na walo salimika.rip ma shujaa wa kiafrica.watakuaaa wale nderahamwe wa kirwanda ndo wamefanya unyama huo aaaii inaskitishaa saani.

    mdau kigali makazi boksini

    ReplyDelete
  9. Nafasi ya kuingia kombe la African Cup iko wazi Watanzania ombeni tukajifunze Tofauti ya mechi na mechi za kweli.

    ReplyDelete
  10. Rating:he International Federation of Football History and Statistics (IFFHS) has appointed Japanese Shinij Okazaki of Shimizu FC, world best striker 2009
    .1. .1. Shinij Okazaki (JAP, Shimizu FC) 15 (15/0) Shinij Okazaki (Jpn, Shimizu FC) 15 (15 / 0)
    .2. .2. Didier Drogba (CIV, Chelsea) 15 (8/7) Didier Drogba (CIV, Chelsea) 15 (8 / 7)
    .3. .3. Abdelmalek Ziaya (ALG, Entente Sportive) 15 (0/15) Abdelmalek Ziaya (ALG, Entente Sportive) 15 (0 / 15)
    .4. .4. David Villa (ESP, Valencia) 14 (11/3) David Villa (Spa, Valencia) 14 (11 / 3)
    .5. 5. Carlos Alberto Pavón (HON, Real España) 14 (9/5) Carlos Alberto Pavon (HON, Real Spain) 14 (9 / 5)
    .6. 6. Luis Fabiano (BRA, Sevilla) 13 (11/2) Luis Fabiano (BRA, Sevilla) 13 (11 / 2)
    .7. 7. Mrisho Alfani (TAN, Young Africans) 13 (8/5) Alfani Mrisho (TAN, Young Africans) 13 (8 / 5)
    .8. 8. Alan Kaluyituka (CON, TP Mazembe) 13 (5/8) Alan Kaluyituka (CON, TP Mazembe) 13 (5 / 8)
    .9. 9. Edin Dzeko (BHZ, VfL Wolfsburg) 12 (8/4) Edin Dzeko (BHZ, VfL Wolfsburg) 12 (8 / 4)
    10. 10. Milan Baros (RCH, Galatasaray) 12 (6/6) Milan Baros (CZE, Galatasaray) 12 (6 / 6)

    Nimeipata marca.com BInya translate. Hao ndio best striker wa 2009/10

    ReplyDelete
  11. jamani poleni wapenda soka sasa hawa jamaa waangola kama hamna amani kwanini walipendekeza huo wa cabinda utumike nani anawafadhili hao watu kukaa mwituni kuna mataifa ya magharibi yanawafadhili ili wapate shaba kwa wingi shane on them inauma sama jamani africa ehe mungu tunusuru.

    ReplyDelete
  12. as of 1258hrs eastern Us time, yawezekana watajitoa.
    No confirmation yet .
    Personal opinion, ni muhimu kujitoa.

    ReplyDelete
  13. WALAANIWE HAO MAGAIDI WA MSITUNI!! Inasikitisha vijana wetu wanashambuliwa vibaya namna hii, hao magaidi waelewe,ugaidi sio njia ya kuleta amani Afrika. MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE!!

    ReplyDelete
  14. Lidumu Globu la Michuzi!!!!!!
    LIDUMUUUUUUU

    Badala yake waiweke Taifa Stars! one mans trash is one mans treasure! au kufa kufaana! kwa nia nzuri tu!

    ReplyDelete
  15. Tuombe taifa stars ikawa replace hawa jamaa huko

    ReplyDelete
  16. ALHAJ ABUBAKARYJanuary 10, 2010

    PENGINE WATANZANIA NDIYO NAFASI YETU HIYO JAMANI MSILALAMIKE KUFA KWANI KUKO KILA SIKU. PIA KUMBUKENI TOGO WANA ZERUZERU PENGINE NAO WANGEWEKA KAMBI TANZANIA NAO WANGEUWAWA TAMBUENI KILA NCHI INA MATATIZO YAKE CHA MUHIMU TU VIONGOZI WA TFF WAWAHI KUOMBA ILI TAIFA STAR IENDE HUKO.

    ReplyDelete
  17. nao kwanini wachukue bus?si wange fly?kote huko nikupenda udokozi kwa vigogo wa afrika cha juu kinatuponza haya sasa ,mdau greece

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...