Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametaja nguzo kuu sita ambazo amesema kuwa zikitekelezwa ipasavyo zitaharakisha kasi ya maendeleo ya Bara la Afrika.
Miongoni mwa nguzo hizo ni Bara la Afrika kuhakikisha kuwa linabuni njia bora zaidi, endelevu zaidi na za uerevu zaidi wa jinsi ya kutumia raslimali zake muhimu kama vile madini na mafuta kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Bara hilo.
Rais Kikwete ametaja nguzo hizo sita wakati aliposhiriki katika mdahalo kuhusu Fikra Mpya za Mkakati wa Maendeleo ya Afrika – Rethinking Africa’s Development Strategy - kwenye siku ya kwanza ya Mkutano wa 40 wa Taasisi ya Uchumi Duniani ya World Ecocomic Forum unaofanyika mjini Davos, Uswisi.
Mkutano huo unaoshiriki viongozi kutoka zaidi ya nchi 30 duniani na baadhi ya viongozi maarufu na mashuhuri wa nyanja ya uwekezaji, biashara, uchumi na maendeleo duniani, umeanza leo, Jumatano, Januari 28, 2010, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Congress Centre.
Miongoni mwa washiriki wenzake katika mdahalo huo wa kwanza wa Mkutano huo wa WEF alikuwa ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Donald Kaberuka, Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Exim ya China Li Ruogu na Maria Ramos, Mtendaji Mkuu wa Kundi la Benki ya Absa ya Afrika Kusini ambaye aliendesha mdahalo huo.
Akifafanua kuhusu nguzo hiyo ya kwanza ya Bara la Afrika kutumia vizuri, kwa njia endelevu na erevu raslimali zake, Rais Kikwete amesema kuwa uchimbaji wa madini na mafuta katika Afrika lazima uwasaidie Waafrika.
“Ni jambo lisilokubalika kuwa madini ama mafuta yanachimbwa katika Bara la Afrika, lakini jamii zinazozunguka machimbo hayo havinufaiki na uchimbaji huo. Baadhi ya makampuni ya uwekezaji katika machimbo yanathubutu hata kuagiza maji ya kunywa, ama kuagiza chakula, ama hata kukodisha malori ya kusomba mchanga kutoka nje ya Bara hili,” amesema Rais Kikwete.
Nguzo ya pili muhimu kwa maendeleo ya Afrika, kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni umuhimu wa Bara la Afrika kuendeleza na kudumisha mageuzi ya kiuchumi ambayo yameuwezesha uchumi wa Bara hilo kukua kwa namna ya uendelevu kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo kabla ya misukosuko ya karibuni ya uchumi duniani.
Rais Kikwete ameitaja misukosuko hiyo kuwa ni pamoja na kupanda ghafla na kwa kiwango kikubwa kwa bei za mafuta duniani, kupanda sana na ghafla kwa bei ya chakula duniani kabla ya kuanza kunyumba kwa kiasi kikubwa mno kwa uchumi wa jumla wa dunia.
Rais Kikwete ameitaja nguvu kuu ya tatu kuwa ni umuhimu wa Bara la Afrika kuendeleza uwekezaji wake katika sekta ya miundombinu, ili kuboresha kiwango cha uzalishaji wa wakulima na kuwawezesha kufikisha mazao yao haraka sokoni.
Rais Kikwete amesema kuwa nguzo kuu ya nne kwa uchumi wa Afrika kuweza kukua kwa haraka zaidi ni Bara la Afrika kuwekeza katika kilimo ambacho ni muhimili wa kati ya asilimia 70 na 80 ya Waafrika wote wanaoishi kwa kutegemea kilimo.
“Kilimo kitatuwezesha kuwa na usalama na uhakika wa chakula. Tunaweza kuuza akiba nchi za nje ili kujipatia fedha zaidi za kilimo,” amesema Rais Kikwete katika mdahalo huo.
Rais ameongeza kuwa nguvu kuu ya tano ya uchumi wa Bara la Afrika ni ulazima wa Bara hilo kuwekeza katika mtaji wa maendeleo ya binadamu yaani kuwekeza katika elimu na afya.
“Tumewekeza sana katika elimu ya msingi. Tumefanya vizuri katika elimu hiyo, lakini elimu ya msingi ni elimu ya kufuta ujinga. Lazima sasa tuelekeze nguvu zetu katika elimu ya sekondari na elimu ya chuo kikuu. Na hasa katika elimu ya sayansi. Ni elimu ya namna hiyo itakayokabdilisha Bara letu,” Rais Kikwete amewaambia watazamaji na wasikilizaji katika mdahalo huo.
Nguvu ya sita na ya mwisho, kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni kukuza haraka ushirikiano wa kikanda (regional intergration) kama kukusanya nguvu za pamoja za nchi mbali mbali kukabiliana na changamoto za maendeleo.
Akijibu swali kuhusu rushwa kama kikwazo cha maendeleo katika Afrika, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu nje ya Afrika wakiamini kuwa kila mtu katika Afrika, kila mtumishi wa umma katika Afrika, anakula rushwa.
“Lazima tukumbe kuwa Bara la Afrika linalo mataifa 53 na mataifa haya yanatofautiana kwa namna nyingi. Ni kweli ipo rushwa katika Afrika, kama ilivyokuwapo rushwa katika sehemu nyingine duniani.
Lakini siyo kwamba kila Mwafrika ama mtumishi wa umma katika Afrika anakula rushwa. Ni vizuri tunachukua muda kujifunza mema yanayotoka katika Bara hili,” amefafanua Rais Kikwete.
Changa moto ya Mhs Rais Kikwete ni nzuri sana. Ila nafikiri utekelezaji ndiyo tatizo kubwa. Basi naona ngoja tusubiri sisi kama watanzania tutafanya nini baada ya changa moto hii.
ReplyDeleteInawezekana kuanzia sasa wale wote ambao wako karibu na sehemu zinazo chimbwa madini wakapata faida nazo!!
Ahsanteni sana.
Jamani!!!!!!!!!!!!! seriously nashindwa elewa!! Mbona anachosema mheshimiwa ni sahihi kabisa!!! sasa inakuwaje anashindwa kuyatekereza nyumbani????
ReplyDeleteFirst of all, how can a meeting about Africa be held in Europe, You hypocrites could not find a country in Africa "luxurious" enough to hold your meeting. Talk will not build that bridge between have-not and the have everything. We can not continue to be dictated on how to develop our humble continent by those who have exploited it to bones...Why do we always see outsiders as the only hope for us when we have populous which can be turned into skilled labour as well as consumers of our own produce....if u wondered it is me who is coming with new kind of revolution that will spark the brain-wave of change in Africa..
ReplyDeleteKaka Michuzi,
ReplyDeleteNampongeza Rais kwa ujumbe alioutoa. Nina swali la ki-ufundi. Nini ilikuwa lengo la Tanzania katika mkutano huo. What was the key issue/message Tanzania wanted to achieve in that Forum. Maana Rais amezungumzia Afrika..je Tanzania ilitaka kupata au imepata nini katika ajenda iliyopeleka huko.
Nashukuru kaka
NGUZO YA KWANZA #1. Kupiga vita Rushwa, Ufujaji, na uporaji wa mali za umma. (vita dhidi ya corruption) ndo namba moja Africa. Kinachoturudisha nyuma si kingine ni hicho..na Rais anajua sana..hayo mengine ni gelesha tu na politics...!!
ReplyDeleteHongera Mheshimiwa Rais. Uliyoyasema yote ni kweli na nyumbani tunayatekeleza. Mkutano wa Davos unazungumzia masuala muhimu ya kibiashara duniani. Ni mahali muafaka kuzungumzia mustakabali wa Afrika na Tanzania ni nchi mojawapo Afrika na yote uliyoyasema yanatuhusu Tanzania. Tunafurahi na kujigamba tukiona mchango wako wa hali ya juu. Ahsante sana Mheshimiwa Rais.
ReplyDeletemimi naona kichefuchefu tuu na naona bora nikae kimya kwa sababu maoni yaliyo akilini mwangu kuhusu huyu "mtukufu lahisi" weni; ndugu yake mkuu wa wilaya ya libeneke hatoyatundika anyway.
ReplyDeleteSimply
"Lazima tukumbe kuwa Bara la Afrika linalo mataifa 53 na mataifa haya yanatofautiana kwa namna nyingi. Ni kweli ipo rushwa katika Afrika, kama ilivyokuwapo rushwa katika sehemu nyingine duniani.
ReplyDeleteLakini siyo kwamba kila Mwafrika ama mtumishi wa umma katika Afrika anakula rushwa. Ni vizuri tunachukua muda kujifunza mema yanayotoka katika Bara hili,” amefafanua Rais Kikwete."
HIKI ndio kikwazo kikuu ktk maendeleo ya afrika. Waafrika tukielezwa ukweli, tunajitetea kuwa rushwa sio tatizo la afrika tu!!! Hatuwezi kutafuta dawa kama hatutaki kutambua ugonjwa tulio nao! Na ugonjwa wa afrika si rushwa - bali ni ufisadi. Ufisadi (kleptocracy) ni mfumo ndani ya mfumo - na ndio maana watu wa nje wanashindwa kujua ni nani yumo na nani hayumo! Ufisadi ni janga la Afrika na linachochewa na watawala wa afrika kuendelea kufichaficha maradhi! Vifo vitatuumbua!!
kama mzee hakuiwekea rushwa kipaumbele basi tusahau maendeleo kabisaaa
ReplyDeleteRaisi JK amesema kweli, Lakini kusema kwamba sio viongozi wote ni walarushwa lakini naamini kwamba asilimia 90 ya viongozi afrika ni walarushwa Na hiyo ni asilimia kubwa sana. Ulaya pia kuna rushwa, wanakula, lakini maendeleo pia yanaonekana. Afrika viongozi wanakula mpaka wanadidimiza nchi. Mahosipitali hayana dawa wala vifaa vya kutibu, Barabara zetu zina jengwa miaka kumi. lakini viongozi wakienda kwenye ziara zao wanafutana na watu 100. wanakaa kwenye hotel kubwa na ghali. wanakunjwa pombe na kula mpaka wanalewa na kuvimbiwa. yote hiyo ni hela za wananchi. wananchi hawana kazi, hawana dawa, wananchi hawana chakula. Jamani viongozi kuweni na imani kidogo. Hata kama mnakula lakini oneni aibu. It can be done, just play your part.
ReplyDeleteMh Raisi,
Kwanza kwa nchi yoyote kuendelea lazima kuwe na infastructure nzuri, Barabara zijengwe, usafiri wa uma uwe mzuri, watu wataweza kutoa mazao yoa bila matatizo kwenda kwenye masoko, watu wataweza kwenda kazini bila matatizo, watu wataweza kwenda kutafuta kazi bila usafiri kuwa mgumu. watu waweze kupata hudumu mahosipitalini bila matatizo. Hapo ndio watu watakuwa na nguvu hata ya kulima na kulisha familia Zao. kama ulivyo sema kwenye Kampeni yako. Maisha bora kwa kila mtanzania. Tuwe mfano kwa nchi zingine za Africa. Basi kama viongozi wanataka kula, Wale kwa kiasi lakini sio kwa uroho. Mwisho wake utakuwa mbaya, Viongozi ogopeni MUNGU. WANANCHI WANALIA.WASIKILIZENI.
Ndugu Mheshimiwa Raisi Kikwete,
ReplyDeleteNchi yetu itaendelea endapo kuna nia inayofuatalia na kitendo cha serikali yako kuthibiti haki za wananchi kuheshimika. Kwa mfano, kuhakikisha mahakama wanawapa haki wananchi haraka. Mpaka hii leo, mahakama zetu zinachukua muda kutoa haki. Kuna wananchi wengi wa hali ya chini bado wanafungwa kwa makosa madogo madogo kwa kuwa hawana uwezo wa kujitetea. Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya maofisa wa serikali na wakubwa wengine wanaiba na hakuna sheria imechukuliwa dhidi yao.
Pili, kwa kuwa umesafiri an kuona dunia, utakuta nchi kama Chile na Brazil, wanatumia na kuwasikiliza wasomi wao. Kuna wasomi wengi Tanzania lakini hawana sauti. Kama ukitumia vivhwa vya hawa wasomi, basi naamini kuwa nchi itakuwa mbali. Nchi kama Chile na Brazil walibadilisha maofisa wao wote na kuwaleta wasomi mbalimbali serikalini ili watunge upya sheria za kibiashara, uchumi, elimu, sheria,na kadhalika.
Mheshimiwa Raisi, tunataka kuona maendeleo sio tu ya maneno bali ya vitendo. Kwa mfano, mpaka leo, serikali inawaruhusu walimu kufundisha watoto wetu bila ya elimu ya ualimu. Mpaka leo, sheria za kibiashara ni ngumu kuzifuata, mpaka leo wananchi wa hali ya chini hawapati haki zao mahakamani, na mpaka leo tunategemea misaada ya nje katika bajeti ya serikali.
Ahsante kwa kunisikiliza.
Mzalendo.
Anonymous wa Ijumaa 29, 06:11pm umenena na nina kuunga mkono moja kwa moja. Nguzo ya kwanza ni Uongozi bora na vita dhidi ya rushwa. Halafu serikali zinatakiwa kuwekeza katika Elimu. Kama watu wanaelimu, wanaweza kutatua mambo mengi.
ReplyDeleteRAIS ANACHEKESHA SANA.ANAONGEA SANA,LAKINI MATENDO HAKUNA.ALAFU ANAFIKIRI WATU ANAOKUTANA NAO HUKU AWAIJUI TANZANIA.NDUGU RAIS, AIBU AIBU, SANA.WANAELEWA MAMBO YOTE UNAYOFANYA HAPA.NA KIBAYA ZAIDI NI KUSHINDWA KWAKO KUTUMIA UWEZO WAKO KUKOMESHA UFISADI.NA IMEONEKANA JUZI JUZI TU KUHUSU ISSUE RICHMOND.MAENDELEO YA TANZANIA AU AFRICA ,TUJIFUNZE KUTOKA BOSTWANA NA RWANDA SIO WEWE UELEZEE TUNATAKA KAGAME AELEZE NDIO TUTAMWELEWA KWANI ANAIFANYIA KAZI HUKO KWAKE.WEWE UNAIFANYIA KAZI WAPI?.KAZI YAKO KUBWA KUSAFIRI TU.MAENDELEO YA TANZANIA AU AFRICA INATAKIWA KUBADILIKE NA KUTUMIA FREE AND GREEN ENERGY [WIND AND SOALR POWER] NA MAGARI YETU YATUMIE NATURAL GESI AMBAYO TUNAYO HAPO.AFRICA HAINA MAFUTA YA KUTOSHA ILA TUNA NATURAL GESI NYINGI.TANZANIA INATAKIWA WATU SMART WAKAE SIO MARAFIKI ZAKO WANASIASA .NASEMA WATU SMART KUTOKA NJE NA NDANI.KUNA WATANZANIA WENGI WANAFANYA KAZI KATIKA SEHEMU NYETI HUKU AMERICA NA WENGINE WANASOMA.UWATUMIE KUOVERHAUL KILA SEKTA.WAITE SEMA TUFANYE NINI?SASA WEWE UNAWAITA WAPIGA DEBE WA SIASA,UNATAEGEMEA NINI?????????????????.KWA MFANO ,NILISHANGAA KUONA SIKU ZA NYUMA ETI WAZIRI MKUU ALIYEONDOLEWA KWENYE MADARAKA ANASEMA TUNATAKIWA KUTENGENEZA MVUA KWA KU INJECT CHEMICAL KWEBYE MAWINGU ALAFU TUPATE MVUA.HIVI UTAINJECT MPAKA LINI.NA HIZO PESA UTAPATA WAPI?.NA KWA NINI HUSIANGALIE TATIZO NIN NINI?TATIZO NI TUME HARIBU MAZINGIRA.ALITAKIWA AJE NA SUSTAINABLE SOLUTION YA KUSEMA TUSIKATE MAGOGO SASA TUPANDE MITI KWA WINGI.VIONGOZI WA TANZANIA WANACHEKESHA SASA ,LAKINI NAONA MUNGU ANAWAPIGA SASA.LAKINI UKIONANA NAO WANAONA WANAFANYA VIZURI HIYO NDIO PIGO LAO.
ReplyDeleteASANTE SANA KAKA MICHUZI
Rais wetu kazungumza mambo mazuri sana kwenye huo mkutano,amajaribu kuonyesha matatizo ya Africa Tanzania ikiwemo hayatokani na waafrika tu,bali ni matokeo endelevu ya mahusiano na mchi za nje hasa ulaya na marekani.
ReplyDeleteRushwa katika Afrika au Tanzania inahusika kwa kiasi kikubwa na maingiliano au mahusiano niliyiyataka hapo juu,makampuni ya kimataifa yenye kufanya biashara Afrika na Tanzania ndio yanayoongoza kwa kutoa rushwa,yakishindana yenyewe lili litakaloshindwa ndio uanza kelele kuwa tenda fulani wamepewa kampuni fulani kwa rushwa.Kama rushwa iko upande wao hawatajaribu kupiga filimbi zao.Rais katumia njia ya kidiplomasia kuwasilisha hoja yake.
Kuhusu makambpuni ya madini kuagiza chakula,maji na mbwa wa ulinzi nje,hili serikali ya JK imeanza kulifanyia kazi,serikali imepiga marufuku uaigizaji nyama,maji nje ya nchi na bidhaa zingine zinazoweza kupatikana hapa nchini.
Makampuni mengine kama ya simu ambayo utengeneza faida kubwa.lakini tumesikia hivi karibuni kuwa hayalipi kodi,nayo ufanya-outsourcing kwa makampuni ya nchi za kwao,mfano kuweka mafuta kwenye genereta,kujenga minara ya mawasiliano,hii yote ufanya na makampuni ya kigeni,shughuli ambazo zingewezwa fanywa na makampuni ya kizalendo au kwa ubia.Kigezo kwao ni kuwa kampuni za kigeni hazina uwezo.
Maamuzi yote haya yanafanyika na wahusika serikalini ufumbwa macho (kwa rushwa) wasichukue hatua.Tumeona wabunge wanashutumiana kuwa wenzao wameongwa na makampuni ya simu wasaidie kujenga hoja kampuni za simu zisijisajili kwenye soko la mitaji ili watanzania waweze kumiliki kiduchu hizo kampuni.
Na hii ni mikakati ya wenzetu kwenye vita ya kiuchumi.ambapo tunaona wanatufanyia ugaidi wa Kuchumi.
Nawasilisha.