Vijana wa Agape Evangelical Singers wikiendi ilopita walikuwa na harusi moja ya kitamaduni ya mwenzao mdau Kamala James Lutatisinibwa na mai waifu wake Vaileth Ajuna Magezi.
Kwa kuwa vijana wengi wanadhani harusi ni lazima uwe na ma milioni, tunataka waone mfano huu. Harusi hii ilikuwa ni ya kipekee sana haijawahi kutokea na gharama yake ilikuwa chini ya laki tisa.

mchungaji Ernest Kadiva akiwameremetesha maharusi katika kanisa la Azania front

maharusi na wapambe pamoja na wasindikizaji
maharusi na wapambe wao
waalikwa wakifurahia champeni ya asili ya madafu
bendi ya agape ilitumbuiza
mchungaji Kadiva na maharusi wakiwa meza kuu iliyokuwa ya vigoda na jamvi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. A well planned wedding. No artificial stuff; all natural and healthy. I love creativity. God bless all of you richly.

    ReplyDelete
  2. hongereni maharusi mmependeza wenyewe si lazima ndoa iwe ya gharama ndoa yenu ipo simple na nimeipenda jamani mungu awajaalie ndoa ya baraka na upendo.

    ReplyDelete
  3. Hongera bloga na mwanaharakati Kamala kwa kufunga arusi na mkeo Vaileth. Mbarikiwe kwa maisha marefu na yenye mafanikio mema.

    ReplyDelete
  4. Hongereni Bwn Kamara na my wyf yako, kwakweli nimeipenda harusi hii maana ni mfano Kuna vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na gharama ambazo wanaona hawaziwezi na hivyo kuishia kuwadanganya watoto wa watu na kuwaacha solemba, siwalaumu wanaoshindwa kutokana na gharama kwa sababu mwenyezi Mungu katujalia uwezo tofauti tofauti lakini pia nafikiri kwa sehemu kubwa watu tunapenda ufahari hata ambao hatuwezi ukizingatia wadada wengine wanaweka presha kwa hao waoaji ili harusi iwe bakubwa,afadhali nguvu kubwa ipelekwe wenye kuanzia maisha kuliko siku moja ya harusi,jamani tuige mfano huu wa kuigwa TUFANYE KADRI YA UWEZO NA MWENYEZI MUNGU ATABARIKI MAANA CHA MSINGI NI NIA ZETU.KWA WENYE UWEZO SINA NENO LKN TUSIO NAO SWALA HILI LA UFAHARI LISIWE KIGEZO
    HONGERA BWNA HARUSI.BIBI HARUSI HONGERA PIA KWA KUKUBALI KWANGU MIMI HII INAONYESHA KUNA UPENDO WA KWELI. MUNGU AWAJALIE UPENDO NA AMANI KATIKA MAISHA YENU.

    ReplyDelete
  5. Kamala na Ajuna HONGERA SANA. Nimependa sana hii kitu na ninafikiri kitakuwa mojawapo ya kuwatoa tongotongo machoni wabongolese kuachana na utamaduni uliochoka wa harusi za mamilioni ya kuchangisha na baada ya miezi miwili tunasikia oh mara piga ua, ugoni, magezeti ya udaku, oh mara talakiana, nk. Hizo za mabilioni waachieni watu wa Richmond (maana hao kila mtanzania ameishawachangia apende asipende)na sie akina pangupakavu tufanye harusi zinazolingana na uwezo wetu - na ninauhakika ndoa yenu itakuwa ya furaha kwa kipindi chote itakapokuwa iko hai!!!

    ReplyDelete
  6. Jamani naomba kuuliza, eti Madafu yanaleta mabusha? Naomba vile vile lugha ya kitaaluma (medical)ya Mabusha

    ReplyDelete
  7. Watu wengine bwana. Wangetumia na mirija ya mianzi basi

    ReplyDelete
  8. simple and beautiful
    hongereni sana maharusi
    mungu awabariki

    mdau Canada

    ReplyDelete
  9. mungu awabariki harusi hii iwe na kil amafanikio waliojipangia musiwe na wasi maana hata mimi yangu itakuwa hivi hivi na pesa nitakazo pata nitafanya kitu kwa jamii maana harusi hii aina presha ya kurudisha madeni na kuanza kuishi maisha magumu baada ya ndoa kisa kutafuta fahari ya kuuza sura tu

    ReplyDelete
  10. SAFI SANA VIJANA GOOD WORK

    ReplyDelete
  11. Raha ya dafu bwana ukatiwe kisha uchokonolewe na unywee humo humo tena wala si kwa mrija mmechanganya madawa waungwana

    ReplyDelete
  12. hongereni maharusi mmependeza mmekuwa tofauti kabisa na harusi nyingine nimependa huo ubunifu wenu safi sana simple and nice mungu awajalie muishi maisha yenye raha na baraka tele, mmpendane daima, welcome to the club.

    ReplyDelete
  13. Anony wa Tue Jan 05, 03:31:00 AM umesema kweli kabisa.
    Hiyo mirija imetibua. Au kama walikosa mirija ya mianzi walitakiwa watumie MABUNDA YA MPAPAI hapo ndo ingenoga

    ReplyDelete
  14. ndoa kama hizi ndio zinazodumu hongereni sana , nawatakia maisha marefu yenye afya njema na furaha ,

    ReplyDelete
  15. thanx people. lengo lilikuwa ni simpo, na gharama kiduuchu lakini pia utamaduni wa mtu mweusi.

    kwaniaba ya vaileth, namshukkuru kila alliyesaidia katika kufanikisha hili

    Kamala L

    ReplyDelete
  16. Watu wengine bwana kila kitu lazima atafute cha kukosoa tu!hebu wasifieni ubunifu wao,ni harusi ngapi umeziona za aina hii?binafsi hii ndo ya kwanza na nimependa sana!mambo ya mirija ni uamuzi wao,sasa ulitaka kila kitu kiwe kama unavofikiria au unavotaka wewe?we yako ulimpendezesha kila mtu?si ulifanya ulivopenda wewe?narudia tena si lazima kutafuta cha kukosoa hasa pale ambapo kitu kimeonekana ni kizuri machoni pa wengi.

    ReplyDelete
  17. Hii nzuri sana na ndio inayotakiwa. Gharama za harusi kiduchuuu... huku mkibalance mtikisiko wa uchumi na maisha halisi ya Mtz. Uzalendo unaanza taratibu namna hii, kisha kujiamini na kujitegemea. Kwa mtindo huu wa kujitegemea kimawazo tutaibua mawazo chanya ya kuthamini chetu na hivyo utu wa Mwafrika utakula bata na ufisadi utatoweka. Sisi asili yetu vitu simple ufisadi tumeshobokea kwa sana kimtindo baada ya Mwalimu kututoka. Nimeikubali mpaka nawasamehe hiyo mirija. Safi sana na kuleni FIVE.

    ReplyDelete
  18. Hii nzuri sana na ndio inayotakiwa. Gharama za harusi kiduchuuu... huku mkibalance mtikisiko wa uchumi na maisha halisi ya Mtz. Uzalendo unaanza taratibu namna hii, kisha kujiamini na kujitegemea. Kwa mtindo huu wa kujitegemea kimawazo tutaibua mawazo chanya ya kuthamini chetu na hivyo utu wa Mwafrika utakula bata na ufisadi utatoweka. Sisi asili yetu vitu simple ufisadi tumeshobokea kwa sana kimtindo baada ya Mwalimu kututoka. Nimeikubali mpaka nawasamehe hiyo mirija. Safi sana na kuleni FIVE.

    ReplyDelete
  19. Kwa taarifa ya wale ambao wanaodhani hii ndo harusi ya kwanza ya mtindo huu mmekosea hawa wameiga tu, ilishafanywa harusi ya mtindo huu ambayo sidhani kama irekodi yake ilishavunjwa, ilikuwa ni ya mrisho mpoto ambapo keki ilikuwa ni boga lililochemshwa na watu waliketi kwenye mikeka, ikaja harusi ya mgunga mwa-mnyenyelwa(tangulia mwalimu),ikaja ya mnju msita(david Manju joseph - roots and culture kwa sasa ni designer) kwa hiyo hawa wameiga tu, tunawapongeza kwa hilo na wengine pia tuige ili tusiwe tunatumia gharama kuuubwa kwenye sherehe za harusi. tupunguze

    ReplyDelete
  20. kaka Michuzi Kweli wamependeza na ni mfano wa kuigwa. Hongela mdau Kamala na 'mai' waifu wake.

    Hata hivyo mdau kusema kuwa kila kitu ni 'natural' ni kuweka chumvi tuseme tu kuwa hii ni arusi ambayo kwa kiwango fulani imeenzi utamaduni wetu na kwa gharama walizozimudu wao bila kusababisha michango mingi toka kwa watu; tusiseme gharama hiyo ni ya chini.

    Nasema hivyo kwa sababu hata Tsh. 900,000 kwa wengine si ndogo bado ni kubwa sana hiyo. Kuna wengi tuna kipato cha chini ya laki kwa mwezi hapa.
    Pili neno natural nalo ni relative sana yaani hapo naona maji ya chupa, kidani shingoni, viatu made in .... kora ya mchungaji, saa mkononi, lipstick kwa mbali, gari walilopanda, matumizi ya PA system n.k sijui ni 'natural' kwa kiwango gani.

    ReplyDelete
  21. nice one mate,veru nice one!

    ReplyDelete
  22. Hongera sana Kamala, twakutakia maisha mapya mema, mapate watoto wa kike na wakiume

    ReplyDelete
  23. -Great wedding ceremony!I love creativity too!The first comment said it all for me!

    ReplyDelete
  24. Culturist na wengine jitahidini kuwa na mawazo chanya, hivi kuna kitu kisicho na kazoro humu ulimwenguni?
    Watanzania wengine hamuwezi kubadilika kwa kuwa mmeshamezwa na tamaduni zisizo zenu, mimi naona la msingi hapa ni kujifunza maisha ya sasa vijana tubadilike, kama unaona hajafikia kitamaduni kabisa si uongezee kwako au ushauri wengine baadala ya kuponda? Muwe wazalendo jamani mwenzetu amefanya alichokiona ni sawa kama kuna cha kuongeza mpongeze kwanza kisha washauri wengine. Hongereni sana kina kamala na vailet kwa kuwa hamkujali elimu kubwa mlio nayo lakini mlijali maisha ya sasa na asili yetu watanzania. Jamani tuige mfano tuachane na harusi za mamilioni halafu baada ya asali ya mwezi mnaanza kutazamana hela hakuna wakati mmewaweka watu ukumbini kwa mamilino.
    Tuamke watanzania wenzangu.

    ReplyDelete
  25. mdau hapo juu umesema wameiga? Hiyo siyo kweli labda hujui maana ya kuiga.Alichotumia Mpoto kama keki si ndicho hawa wametumia.Hapo suala la kuiga halipo kabisa wao wamefanya vile walivyobuni.

    Nawapongeza sana Kamala na Vailet.Huo ndiyo ustaarabu wa kuoa na kuoana.Hata mimi nilifanya ya kwangu kijijini kabisa tulijenga kibanda cha mianzi na kutundika majani ya migomba pakawa ndiyo ukumbi.Lakini tunaishi kwa furaha na amani na hatujapungukiwa kitu.

    Vijana wengine igeni huo mfano ili mjikoe na gharama zisizokuwa za lazima na mbwembwe za kujimbwembweza tu.

    ReplyDelete
  26. Naomba vyombo vya habari vionyeshe harusi hii ili iwe mfano kwa taifa letu maana watu wanatumia mamilion kufunga ndoa wakati kuna watu wanakufa na njaa
    Mdau Kutoka Marekani.

    ReplyDelete
  27. anony- ulouliza kuhusu mabusha vs madafu - ukweli ni kuwa madafu hayaleti mabusha bali wadudu wanosababisha mabusha wanapatikana maeneo ya pwani ambapo kuna pia minazi kwa hiyo ni kuhusishwa kihisia zaidi kuliko ukweli
    medically inaitwa Lymphatic filariasis- inapoaffect sehemu za siri kwani pia yaweza affect miguuni nk ----------The worst symptoms of the chronic disease generally appear in adults, and in men more often than in women. In endemic communities, some 10-50% of men suffer from genital damage, especially hydrocoele (fluid-filled balloon-like enlargement of the sacs around the testes) and elephantiasis of the penis and scrotum. Elephantiasis of the entire leg, the entire arm, the vulva, or the breast - swelling up to several times normal size -
    ---Cause
    The thread-like, parasitic filarial worms Wuchereria bancrofti and Brugia malayi that cause lymphatic filariasis live almost exclusively in humans. These worms lodge in the lymphatic system, the network of nodes and vessels that maintain the delicate fluid balance between the tissues and blood and are an essential component for the body's immune defence system. They live for 4-6 years, producing millions of immature microfilariae (minute larvae) that circulate in the blood.

    ReplyDelete
  28. Hawakuiga wazungu kama wengi walivyozoea.

    Hongereni kwa kuoana na hongereni kwa kuwa funzo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...