nadir haroub canavaro alikuwa na kazi moja tu, kumkaba drogba asifurukute
kipa mwalami wa Taifa Stars akitahayari baada ya drogba kupiga bao, kisha kujiangusha na kujifanya kaumia. aliamka na kuendelea na gemu mtangazaji mahiri wa mpira wa TBC 1 Chacha Maginga (kuumeni) akiwa na mchezaji wa Yanga wa zamani aliye masomoni kusaka nondozzz Ali mayai wakichambua mchezo kama karanga

Ankal,
Hii taarifa ya Globu ya Jamii juu ya gemu la leo haiko sahihi. Ukweli ni kwamba Taifa Stars leo imefungwa nusu bila.

Kituko cha leo ni kwamba Taifa Stars imecheza na timu mbili tofauti
zote zikijiita timu ya taifa ya Cote d'Ivoire. Kikosi cha kwanza
(akiwemo Drogba) kilishinda 1-0, halafu ngwe ya pili kikaja kikosi
kingine kipya kabisa cha ma-underground kikatoka kapa.

Naomba kuwakilisha.
Mdau FM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. acha kujiridhisha mtaalam. hapo lingekuwa kombe la maana kwao basi hata hao maandagraundi wangetuchapa tena hata 6. the drogba who plays against liverpool, man-yu, gunners or against barcelona is not the drogba you saw today. toure man city, yaya barcelona drogba cehlsea eboue arsenal dindane portsmouth we wafa'mchezo nini!!. subiri uone moto wao weldi kapu na sio angola sababu drogba hata kwenye african cup of nations huwa anacheza kwa kuibiaibia akiogopa kuumizwa. jamaa akili na maisha yake yote yapo kule anapopatia tonge la ugali chelsea.

    ReplyDelete
  2. ...sasa Drogba kudaivu ndo hadi Bongo, jamani?

    ReplyDelete
  3. Ivory coast wameamua kuwa wapole kwa mwenyeji, hebu tuache kujisifu bure, wangetaka kupiga bao 10 wangeweza. Hivi unazani Drogba angeleta game A hapo? yeye kama super star ametimiza wajibu wake kwa kuwaonyesha wapenzi wa soka mavitu yake, lakini huku akiwa mpole sana, wote mmefurahi kuona na wao wamejipatia tizi. Akili yao yote ni Sauzi tu tuelewe hilo, sie ndo wenye bahati kwa kuweza kujipima na a very relaxed big team.

    ReplyDelete
  4. Thamim, Mikanjuni TangaJanuary 05, 2010

    Ankal, kutufunga wan'tufunga ila chenga tu'nwalaa.
    Asanteni Ivory Coast kwa kutufunga kiduchu na kutulindia heshima yetu. Sisi tulitegemea yakiwa kidogo basi ni matatu tu.

    ReplyDelete
  5. Kwa wale tuliouona mchezo, achilia mbali Ivory kuwa wanajipima, timu yetu inahitaji kwanza pongezi..pili ndo tukosoe, wachezaji wetu wanazubaa sana sasa sijui ndo kuogopa majina makubwa, Ngasa kabaki na kipa akashangaa..beki 3 hivohivo, otherwise defence imecheza vizuri mno na kiungo kiasi..ila forward hatuna..

    ReplyDelete
  6. Hiyo Luning ya TVT ni ya mwaka 47? Huyu TIDO vipi?

    ReplyDelete
  7. Hallo Ankal Michuzi, natumaini hautaibana hii post yangu.

    Kwanza, hiyo picha ya mwanzo, Nadir Haroub "Cannavaro" alicheza bonge ya proffessional tackling toka kwa Drogba, otherwise hilo ndio lilikuwa goli la kwanza. Kwa yoyote aliyoiona live atakubaliana na mimi. Ilikuwa ni the best,naamini hata Cannavaro akihojiwa hiyo ndiyo ilikuwa best moment kwake. Mimi inanikumbusha tackling aliyoicheza Edgar Davids kwa Ronaldo De Lima kwenye nusu fainali ya World Cup 98.

    Pili, Wabongo tusipende kuwa negative tuuu muda wote na hii ndio
    shida kubwa ya watazamaji mpira wa kibongo. Ila kiukweli kwa mjua soka yoyote duniani na aliyeangalia ile game live ni kwamba Taifa Stars walicheza vizuri sana ila tatizo kubwa kama ambavyo mara nyingi timu yetu ya taifa na hata vilabu tunalo ni ukosefu wa goal getters, Tanzania bado tuna tatizo kubwa la umaliziaji, game ya jana tumepoteza two clear chances za kufunga, moja ni ya Ngasa na ya pili ni ya Tegete iliyogonga nguzo ya goli. Ndio maana ni nadra sana kusikia timu yetu imeshinda goli zaidi ya mbili, regardless timu tunayocheza nayo ni ya kiwango gani. Tuna tatizo kubwa kwenye foward.

    Tatu, hapa mchawi sio Maximo wala mfumo wake wa uteuzi wa wachezaji, tatizo kubwa ni mfumo wetu wa soka, hatuna msingi wa soka kabisa. Hakuna nchi yoyote duniani yenye mfumo mbovu wa kukukuza vijana wadogo kwenye soka kama wa Tanzania na ina kiwango cha maana kwenye mpira, na anayebisha hili aniambie ni nchi gani ina mfumo wa mpira kama Tanzania na ina kiwango cha kushiriki world cup. Hakuna.

    Ligi kuu yenyewe ina timu 12, halafu inasimama mwisho wa mwaka toka November baada ya mchezaji kucheza mechi 11 tu hapo ni mpaka February, hivi huyo mchezaji ataweza kuwa na ubavu, pumzi na stamina wa kupambana na akina Drogba? Na kwanini ligi yetu inasimama, wenzetu wanaosimamisha ligi mwisho wa mwaka ni kwa ajili ya kupisha majira ya baridi, hapa kwa nini tunasimamisha ligi? Halafu wabongo mnamlaumu Maximo, hapa hata aje Guus Hiddink kwa mfumo mzima wa mpira wa kibongo hakuna kitu.

    Nawakilisha Ankal.

    International Observer aka IO

    ReplyDelete
  8. Mzee Mayai nakuona mwenyewe enzi zako ulitesa, sasa unaangalia watoto nao wakihangaika bravoo mkuu kula nondozzzz hizo

    ReplyDelete
  9. jamani mnalalamika kwa ivory coast kubadili timu,tushukuru waivory coast sio majigambo.manake wametia timu iliyokomaa mwanzo na wameona watashinda magoli kadhaa na wameamua kuweka timu ammabyo inafanana angalau na ya bongo ili watu wainjoy soccer,manake kipimo cha tz kilikuwa si cha kuweza kucheza na mastaa wengi wa uefa kama kina didier.mie mwanangu wa miaka 13 anacheza kwenye club moja ya premier hapa na tukipambana na wachovu anamuweka kipa kuwa striker sababu anajua awezi shindwa.hao waivory coast watu babu kubwa na wamefanya vema kuja bongo na najua watakuwa wameinjoy kinoma..hongera Taifa stars kugangamaa .maximo kazi poa .

    ReplyDelete
  10. DROGBA TABIA YAKE YA KUGARAGARA KAMA KABEMENDWA MPAKA TANZANIA KAYALETA. MIE NILIJUWA ANAWAFANYIA UK TU. PAZI.

    ReplyDelete
  11. Hii clip inaonekana vizuri sana
    http://www.youtube.com/watch?v=gR1iMA3MXvg
    Tanzania 0 vs 1 Coast on 4 Jan 2010 highlights.flv

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...