Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda (Kulia ) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC BW. Tido Mhando(Kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya TBC yaliyoko Barabara ya Nyerere jijini Dar leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda (wa pili kulia alievaa suti nyeusi ) akipata maelezo kutoka kwa Mtayarishaji wa vipindi vya TBC1 Bw. Selemani Kisoky alipotembelea kituo hicho,na katikati anaeandaa vipindi ni Bw. John L. Lewanga.

Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda akipata maelezo kutoka kwa Mathias S.Kabisa (Fundi Mwandamizi wa Televisheni) kwenye Studio ya vipindi( TBC1) iliyoko Mikocheni mjini Dar es Salaam alipotembelea leo. Shoto Bw. Tido Mhando Mkurugenzi mkuu wa TBC .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda wa kwanza kulia akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. mathias S. Kabisa ( katikati ) kwenye Studio ya kurushia Vipindi ya TBC1alipotembelea Studio hiyo iliyoko Mikocheni jijini Dar leo.
Picha na Anna Itenda wa Maelezo




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana bwana Tido Mhando, toka kurudi kwako na kuongoza jahazi hili la TBC, siri kuna mafanikio makubwa sana yamepatikana. sasa hivi ukitaka habari za uhakika na zinazotangazwa bila uoga, utazipata TBC.
    umebadili kabisa muonekano mbaya wa TVT mbele ya umma, na hatimaye umeifanya TBC kuwa ni tv pekee inayopendwa sana kwa sasa na kila aina ya rika la watu umewapatia sehemu yake.
    hii ndiyo faida ya kuwa na wataalam wanaofanya kazi nje ya nchi kwa muda mrefu na kisha kurudi kulitumikia taifa lao.
    Natumaini sheria ikipita ya uraia wa nchi mbili, nchi yetu itavuna vipaji vingi vilivyojificha nje ya nchi. hongera sana.

    ReplyDelete
  2. Advocate JashaJanuary 26, 2010

    Ingelikua vizuri kama katibu mkuu angelitua hapo kuzindua tovuti ya TBC hiyo ingelikua habari hapo sioni habari chombo kikuu kama hicho pamoja na maelezo HAVINA TOVUTI ni AIBUI Nafurahi ninaposikia taarifa za habari za TBC kupitia Radio Maria au uchabuzi wa magazeti au baadhi ya Habari mfano Rushwa kwa matrafik huko Iringa kupitia kwa blog ya Jamii TBC mnashindwa nini kua na vitu hivyo?Ilizuka website YaTBC siku Tatu ikapotea ilikua utani?Au ulikua mradi hiyo ilikua demo baada ya cheki kusahiniwa mchezo umekwisha hainiingii kichwani katika ulimwengu wa sasa kwa vyombo kamaTBC au MAELEZO kutokua na tovuti.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...