Habari za leo wadau wa globu ya jamii,

Leo kuna kisa ningependa kuwashirikisha tubadilishane mawazo. Kwa walewenzangu na mie ambao mlikuwa vikojozi utotoni bila shaka mnakumbukazile ndogo za unaota unakojoa halafu unashtuka umeshalowesha shuka.
Halafu kulikuwa na ndoto zile unaota unadondoka halafu unajikutaumeshadondoka chini sakafuni ... au ukiwa na bahati unajikuta ndio ukoukingoni mwa kitanda bado kidogo tu udondoke.

Ndoto za aina angalau ni rahisi kuzielewa maana zinaambatana namovement za mwili (kama kukojoa au kudondoka).

Sasa leo nimeona maajabu. Nimeota niko kwenye computer nachat narafiki yangu. Halafu nikamuomba anipigie simu ili tuongee vizuri maanachat iko slow. Akasema haya napiga sasa hivi.

He! Simu yangu ya ukweli ukweli ikaita bwana ... na kunikuamshausingizini. Kucheki ni rafiki yangu (japokuwa sio yule niliyekuwanachat naye kwenye ndoto) kapiga. Nikapokea na kuongea naye.

Ila nikawa nashangaa inakuwaje kwenye ndoto wakati nasubiria simu marasimu yangu ya kweli inaita? Utafikiri ubashiri fulani vile.
Je wadau wengine huwa mnaexperience ndoto kama hizi?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Nenda kamuulize Sheikh Yahya atakusaidia kutafsiri ndoto yako.

    ReplyDelete
  2. DUh kweli jamaa kikojozi!!!!!!!!!! unakojoa mpaka ukubwani nini?? Dah kulalek.
    Ila inaelekea unataka kuwa mganga wa kienyeji maana unachoota ndio hicho hicho kinatokea!! fungua ofisi mdau!!!!!!

    ReplyDelete
  3. tuna msiba sie nenda U-TURN au kwa DINA MARIOS ndio kuna mambo kama hayo huko mtayajadili mpaka vidole mtatiana ila huku kwa siku ya leo sio mwake

    ReplyDelete
  4. Miujiza,kuna mambo mengi we cant explain, what about this,the other day I thought I had not spoken with my brother for a long time,as I was reaching for the phone it rang, it was my brother and his first words were,Hey its a long time since we had a chat!!

    ReplyDelete
  5. wakati ukiwa usingizini simu ilishaanza kuita, sauti ikakudistabu, ndoto yako ya kuchati ikibadilika kuwa kusubiri simu, mlio ukakushtua ukakuta simu lakini sio ya yule uliechati nae ndotoni. hakuna tofauti na zile za utotoni(mkojo unakusumbua unaota uko chooni unalowesha shuka).

    Rich - Trondheim

    ReplyDelete
  6. Unafahamu huyo simu kutoka kwa rafiki yako iliita mara ngapi? au kama iliita mara moja, iliita kwa urefu wa muda gani? Ninauliza kwasababu yawezekana ile 'part' ya ndoto yako ulipokuwa unaexperience problem ya internet connection, ni wakati huo huo ndipo simu ikaanza kuita (kiukweli). Kwahiyo ubongo wako ukiwa ndotoni ukaweza ku'relate experience ya "ukweli" (simu kuita) na haja yako ya kuongea na huyo chat friend wako kwa simu ndotoni. Hivyo kwenye ndoto uka'suggest akupigie, ilihali tayari simu yako ikawa inaita kiukweli. Hii ndio hypothesis yangu. The brain is the most fascinating part of the human body.

    Mdau,
    Vienna

    ReplyDelete
  7. Haa. mambo yako ya nyumbani unayaleta barazani. acha utoto bana.

    ReplyDelete
  8. hahahahaha ndoto yako haijasababisha huyo jamaa apige simu, kili chotokea ni kwamba simu ilianza kuita kwanza ikiwa inakuamusha kwa mbaaali wewe ukazani umekuwa ukiota mambo ya simu.

    ila nilishasikia ati smart people think alike, yani kama vile wewe unamfikiria rafiki kuhusu kitu fulani afu at the same time na yeye anafikiria kitu icho hicho, ama unafikiria umpigie simu rafiki ako mara unapokea simu kutoka kwako hahaha.

    Ila kusema la ukweli nilipokuwa darasa la tano/ la sita nalikuwa naota jinsi mwl anafundisha masomo yoote all nite long, na mitihani nalikuwa naiota vile vile, ila mahangaiko ya dunia yakaingilia mara nkaaza kuota mambo mapenzi wakati nalikuwa sina hata huyo mupenzi ila ndotoni tu lol

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli experience ya ndoto kama hizo sina. Mara chache chache huwa naota nipo honeymoon. I like those dreams.

    ReplyDelete
  10. hiyo inaitwa telepath.

    ReplyDelete
  11. Yaa.. mi sishangai..
    nadhani simu iliita mara ya kwanza, ule mlio ndio ukatengeneza ndoto, ingawa we hukusikia hadi baadaye...

    Mi huwa naota nataka kufanya jambo, afu mtu anagonga mlangoni, halafu ni kweli kunakuwa na mtu anagonga..

    sijajua ndoto inachukua muda gani kutungwa, kuota, na kumalizika.. kwani ingesaidia kutengeneza mtiririko wa matukio

    ReplyDelete
  12. Kawasimulie watoto wenzio, hadithi za ukojozi, hapa tunataka mambo ya msingi, kama ulikuwa kikojozi utotoni mwako sisi inatuhusu nini??? Au nenda Muhimbili wanaweza kupa sababu za kisayansi kama zipo ama laa nenda kwa shehe Yahaya!!!

    ReplyDelete
  13. Wanasema hizo za watoto kujikojolea kutokana na Umri hata mpaka 12, inatokea na mtoto kama Wazazi wanakorofishana au wanahamahama majengo na mashule, wanamuhamisha sana mtoto basi hilo tatizo mtoto rahisi kumtokea. Itakuwa una Mawazo sana kwenye kichwa Mpaka ukilala kama hukosi usingizi mzuri basi ndoto yako inakuchanganya bado kwenye wazo lako. Jaribu kuomba kbla hujalala au utakuwa na mawazo ya kazi sana. Seif.

    ReplyDelete
  14. Una jini mahaba, nenda kwa mnajimu mkuu Magomeni DSM

    ReplyDelete
  15. Mdau ukweli ni kwamba simu iliita zaidi ya mara mbili wakati ukiwa usingizini, mara ya tatu ndo ukaisikia kwa mara mbili ilikuwa ni kama ndoto lakini ulikuwa kwenye usingizi mzito kiasi kwamba uliona uvivu kuamka na kupokea simu. Sio muujiza wala connection yoyote hapo!

    ReplyDelete
  16. Hiyo mbona cha mtoto? mimi mpaka sasa nnajiogopa sana? huwa nnaota vitu vya hatari au msiba ukitaka kutokea:-
    siku moja mchana jirani yetu alikuja na kusema kuwa baba yake anaumwa na amekwenda hospitali alikuwa anawasimulia ndugu wengine mimi nnapita kuelekea chumbani kulala, nilipo lala nikaota yule baba amefariki kule hospitali na maiti imerudishwa nyumbani watu wanalia nikashtuka usingizini hata saa nzima haijatimia, ile natoka chumbani sijakaa vizuri yuleyule jirani akarudi analia baba yake kafariki kule hospitali.
    siku nyingine niliota nyumbani kwetu bongo nyumba inaungua, kuamka ikawa kila saa inanijia kuona nyumba inaungua nikiwa macho, nikawaza kuna umuhimu wa kukata bima ya moto, kufika usiku nnapigiwa simu nnaambiwa nyumba inaungua!
    Na mimi inanitisha kuwa vitu vingine huwa vinanijia nikiwa macho kabisa na vinatokea! Sijui kuna mwenye msaada nini sababu na kuna tiba?! nnaogopa sana!

    ReplyDelete
  17. Hata mim naungana na mdau hapo juu huaga nikiota tuu tumekutana ndugu wote na tunafanya mkutano fulani ambao mara nyingi kwenye ndoto huaga inakua hainionyeshi ni mkutano wa nini lazima msiba utokee na msiba wenyewe unakuaga wa ndugu hiyo imeshanitokeaga kama mara 6 hiv toka mwaka 2000 na wakat wote nilikuwa naadisia watu baada ya msiba sasa wakaniambia niwe nawaadisia kabla ya msiba,kwa hiyo mim kitu nilichofanya nilipoota ule wa 5 nikamwadisia ndugu yangu kabla,baada ya kama siku mbil hiv ukatokea hakuniamini sana baada ya kama mwaka hiv nikaota wa 6 nikamwambia jioni tukapigiwa sim mtoto wa baba mkubwa kafariki hapo akaniamin akashangaa sana niliogopa kutangaza kwa watu zaidi kitu kama hicho maana wangeanza kuniogopa na kuniona kama mchawi na mpaka sasa hiv msiba wa ndugu yetu wa karibu wowote ambao unataka kutokea lazima niote,ni kitu cha ajabu sana.

    ReplyDelete
  18. ....unahitaji 'Maombezi'

    ReplyDelete
  19. Wewe una umri gani?unatuletea mambo ya kitoto tujadili mtandaoni,wewe kama una zaidi miaka 15,basi utakuwa na kichwa kidogo kishenzi.

    ReplyDelete
  20. Yusuf bwana ndotoJanuary 25, 2010

    TAFSIRI:

    Ndotoni : unatamani kuanzisha chama feki kuzuga watu wakati wa uchaguzi

    Halisi: Chama kinaanzishwa kwa jina la CCJ. Ukijaribu kutafuta ni cha akina nani unakuta si wale uliowafikiria.


    UNABII SIO UTABIRI:

    Ni kweli Kutakuwa na upinzani mkali lakini toka kwa wale usiowategemea

    ReplyDelete
  21. Rich alivyosema amepatia. simu ilikuwa imeshaanza kuita ndio maana ndoto ikahama kutoka kwenye chatting to the phone ringing. It happens all the time

    ReplyDelete
  22. Umenikumbusha mbali,90's nilipokuwa Boarding school,Namfua. Nikiota plate yangu ya chakula imeibiwa dinning, ni kweli siku hiyo nikienda dinning kuchukua msosi siikuti,au naikuta, ni tupu watu wamejiongezea kwenye sahani zao. Au nikiota ndoo yangu ya maji imeibiwa, nikiamka sikuti maji yangu ya kuoga,inabidi nipange foleni ya maji asubuhi baada ya mchaka mchaka.
    Mimi,uk.

    ReplyDelete
  23. Mdau, Mon Jan 25, 07:29:00 PM
    Piga magoti umuombe Mungu,na kukemea mambo yote mabaya unayoyaona. Mungu ni muaminifu.

    ReplyDelete
  24. Siku ingine utaota unazaa kisha ukatoa haja kubwa sijui na hiyo utauliza tafsiri yake?. Hizo ni ndoto tu wala hazina tafsiri kaka. Acha kuamini wala kutaka kujua tafsiri ya ndoto utaishia kwa mchawi au mganga kama sheikh yahya. Huku shinyanga watu kama nyie tunachoma moto

    ReplyDelete
  25. NDOTO MARA NYINGI HUWA ZINA UHUSIANO NA MAMBO UNAYOWAZA MCHANA BEFORE KEMDA KULALA. MAMBO YALIYOKUKABILI, KWA MFANO KAMA UNAOTA UNAKOJOA NA UNAKOJOA KWELI NI KUWA MKOJO ULIKUBANA, AU UNAOTA UNAKULA CHEJEA UJUWE, BALLS ZIMEJA WATOTO SASA WANATAKA KUTOKA. NA VITU KAMA HIVI. NA HIYO YAKO NI KWAMBA ILIKUWA INAKUAMUSHA ILI USIJE UKOIKOSA SIMU YA RAFIKI YAKO

    ReplyDelete
  26. MAMBO YA NDOTO WE YAACHE TU, MIMI MWENYEWE WIKI2 ZILIZOPITA MKE WANGU KASAFIRI NA MAJUZI NILIENDA ARUSHA KIBIASHARA TULIFIKA USIKU SANA NA JAMAA YANGU HOTEL TUNAYOFIKIA HAWAKUELEWA ODA YANGU BADALA YA KUNIWEKEA VYUMBA VIWILI WAKAWEKA KIMOJA KWASABABU ILIKUWA NI USIKU SANA TUKALAZIMIKA TULALE TUU KIBISHI KITANDA KIMOJA NA MSHIKAJI ILI KESHO TUJIPANGE UPYA. BASI SASA USIKU MIMI NIKAOTA NIPO NA MKE WANGU KITANDANI NIKAANZA KUMPAPASA BILA KUJUA KUMBE HATA YEYE AKIWA USINGIZINI AKAHISI KALALA NA MKEWE TULIPAPASANA SANA BAADAYE JAMAA AKASITUKA NILIPOTAKA NIINGIE HATUA INAYOFUATA NA AKANIPIGA KI-PEPSI ILI NIACHE KUOTA, NIKALALAMIKA "HEY BABY WHAT'S WRONG?" THEN NIKAPATA FAHAMU KWAMBA NILIKUWA NAOTA.

    ReplyDelete
  27. Unajua urefu wa ndoto hauendani na urefu wa tukio halisi.....kwa mfano unaweza kuota umepanda basi toka Dar hadi Mbeya kwa muda usiozidi dakika 5!
    Kwa hiyo simu ilianza kuita na ukasikia, akili yako ikahusisha na mambo mengine uliyowahi kufanya (kama hili la kuchati n.k), kwa hiyo ukaota unachati na baadae ukaelewa kwamba simu inaita na ndipo ulipoamka.
    Kwa mfano waweza kuwa umelala mchana na kukawa na mtu anagonga mlango....basi ukaanza kuota upo kwenye safari unarudi nyumbani na unapoingia tu kukawa kuna mtu anagonga! Then ukaamka

    ReplyDelete
  28. NDOTO NI NINI? NDOTO NI HALISI. YAANI NINACHOWEZA KUSEMA NI KWAMBA, UNAPOLALA ROHO YAKO HAILALI MWILI TU NDO UNALALA. NA PIA MAMBO YOTE YANAYOTOKEA YANAANZA KWANZA ROHONI KABLA HAYAJATOKEA KTK MWILI. MFANO UNAWEZA UKAOTA UNAONGEA NA RAFIKI YAKO WA SIKU NYINGI BAADA YA KAMA SIKU MBILI UNAKUTANA NAYE.
    MFANO MWINGINE MZURI KWA WALE WAKRISTO MALAIKA ALIPOMTOKEA MARIAM ILIKUWA NI NDOTO, yUSUPH NAYE HEROD ALIPOTAKA KUMUUA MTOT YESU MALAIKA ALIMTOKEA KATIKA NDOTO, NA PIA NDOTO INAWEZA IKATOKEA KUTOKANA NA MISONGO YA MAMBO MENGI YA SIKU AU UNAYOYAWAZIA AMA TAARIFA YA MAMBO YATAKAYOTOKEA.
    KAMA HILO LA SIMU MI SI MSHANGAI HATA KIDOGO NI KWELI AMEOTA, NA INAWEZEKANA WAKATI ANAOTA HUYO RAFIKI YAKE NAYE ALIKUWA ANAWAZA KUMPIGIA HAYO NI MAMBO YA KAWAIDA KABISA. NA NDIO MAANA KABLA HUJALALA UKAWA UNAMUOMBA MUNGU HAIJALISHI DINI GANI UTASHANGAA KARIBIA KILA SIKU UNAOTA NA HAYO UNAYOOTA UNAONA YANATOKEA.
    NI HAYO TU KWA UCHACHE.

    ReplyDelete
  29. mimi haya ya ndoto sina uhakika, but what i would like to say, and is my scond time am saying this, when someone posts something, would you please discuss it with maturity, if you cant then leave it, dont allow your adult mind to discuss nonesense on a public blog, like "mtatiana vidole....." Jameni jameni!

    ReplyDelete
  30. Kwa ufahamu wangu mdogo ni kwamba, Binaadamu anapokuwa usingizini, mfumo wake wa fahamu huwa unabaki macho. Yaani unaendelea kufanya kazi kama kawaida. Na mara nyingi ukiwa makini ,utagundua kuwa ndoto nyingi ni matukio ambayo yametokea kabla, ima umeota tukio lenyewe au limefanana na tukio halisi,
    Matukio yanayo ambatana na kuanguka na ukajikuta upo ukingoni mwa kitanda, ni kweli ulikaribia kuanguka , mfumo wa fahamu uko macho na umehisi hilo lakini mwili umerelux kiasi hauna controll ya kuepuka tukio. Hivyo hutumwa ujumbe kwenye ubongo wa tukio ambalo litakuogopesha ili mwili urudie uzima na tayari kujiokoa na tukio la kuanguka. Unaweza kuota unakabwa koo na jitu, mara nyingi hutokea wakati unapolala umepindisha shingo kiasi kwamba misuli ya shingo inaporelux inatokea kupunguza mzingo wa koromeo, inafanya hewa inayopita kooni kuwa kidogo kutosheleza mahitaji ya mwili. Hivyo hutumwa ujumbe kichwani utakao kufanya kuamka ili kupata hewa ya kutosha. Unapolala umekunja miguu, inatokea kuwa damu inayo toka juu kushuka miguuni inakuwa kidogo. Kiasi miguu inakufa ganzi. Kuepuka tatizo la kuweza kupooza, ubongo unaliona hilo, na kutuma ujumbe unao ashiria kuwa unakimbizwa na mnyama mkali ili uweze kunyoosha miguu kuruhusu flow nzuri ya damu Inayo kwenda na kutoka kwenye moyo.
    Madakrati wanajua zaidi. Japokuwa inasemekana kuwa binaadamu anamifumo mingine ya fahamu ambayo watu hawajaipatia maelezo. Mtu anaweza kuhisi matukio ambayo hayajatokea kwa kuona mambo mwilini mwake "Machale". Mtu anapata 'Uncontrolled tremors' sehem fulani ya jicho,sikio au mkono basi anatarajia kitu fulani, na kweli hutokea, japo kuwa wakati mwingine hakitokei hicho alicho kitarajia.
    Zote hizi ni jitihada za binaadamu. Lakini Mungu anajua zaidi.

    ReplyDelete
  31. Ni kawaida as a human being kuota vitu ambavyo gonna happen, sometimes huwa tunaota what is gonna happen to us, although huwa haviji moja kwa moja kama ulivoota, but 90% of it!!!!!!!!

    ReplyDelete
  32. mimi nilishawai kuota yanga imemfunga simba 2-1 naikaja kutokea kweli kwenye kombe la tusker na wafungaji niliota walewale Tegete na shamte Ali kwa kweli hii ndoto niliipenda sana napenda iwe inajiludialudia

    mdau
    H Dalali

    ReplyDelete
  33. Haya ni mambo yaliyofichika juu ya uumbaji wa Mungu juu ya vipawa vya watu. Binadamu kila mmoja ana kipaji chake alichopewa na Mungu. Nakumbuka hata nami huwa inanitokea hali nikimfikiria mtu kuwa hatujaonana siku au miaka mingi huwa nashangaa huyo mtu naweza kutana naye baada ya muda mfupi au nakutana na mtu anayemfahamu na kunieleza alipo au alishakufa! Kumbukeni yule dogo aliyeuzwa na kaka zake wakiwa machungoni wanachunga kondoo (wale watoto wa Mzee Yakobo kwenye kitabu cha Mwanzo cha agano la kale katika biblia) mambo aliyowafanyia Mapharao kule Misri, aliota hali ya miaka 14 iliyofuata, miaka 7 ya mavuno mengi na miaka 7 ya njaa kali. Ushauri wangu kwa wale wenye ndoto za aina hiyo msali sana mwambie mungu juu ya ndoto hizo atakuelezea kwa njia yoyote kwa nini anakufanya uwe njia ya kutolea taarifa za mambo yatakayotokea. Sali kwa imani yako uliyo nayo ili mradi inaamini katika kweli 'katika Mungu mmoja. Msiwaulize wanadamu kwa kuwa walio wengi wamepotea katika giza. Watakuambia aaaaaaah unaleta mada gani hapa, mara sisi tunajadili mambo ya maana, mara ukijinyea utamuuliza nani! Eti wanajifanya wao wameendelea sana hawana ndoto za kishenzi, kumbe Mungu yuko mbali na wao.

    Mdau tu

    ReplyDelete
  34. Kuna ngazi nne za ndoto. (1) Ndoto za hali ya mwili (reflection of physical state); k.m. njaa, kutaka kwenda haja, kulala vibaya, n.k.
    (2)Ndoto za fikira au akili. Yaani, vitu ulivyoona, ulivyovisikia, unavyovifikiria, n.k. ambavyo mchakato wake unaendelea hata usingizini. (3)Ndoto za hisia (emotional). K.m. utashi, matamanio, woga, wasiwasi kuhusu jambo fulani, upendo, chuki, n.k. ambavyo vinaweza kujitokeza kwa sura nyingine ktk ndoto. (4) Ndoto za "kiroho" ambazo zinaweza kuashiria au kubashiria jambo litakalotokea na "telepathy". Mwenyezi Mungu akitaka kukufunulia jambo atafanya hivyo. Kama wewe ni Myahudi, Mkristo au Mwislamu au hata kama unafuata dini za jadi utaelewa ninasema nini. Ili uweze kukuza vipaji vyako visivyoonekana alivyokupa Muumba, jaribu kwa dhati yafuatayo : Mwamini Mungu, tenda wema, wapende wenzako, wasaidie wahitaji, huruma kwa viumbe, kuwa na subira na msamehevu,kuwa mkweli na usimshirikishe Muumba (acha ushirikina kabisa), usizini, usiibe, usisengenye, usidanganye na baada ya muda, Mwenyezi Mungu akipenda, utashangaa kuona utakavyopanda daraja.

    ReplyDelete
  35. NI KAWAIDA BINADAMU KUOTA KITU HALAFU KIKATOKEA EXACTLY AU TOFAUTI KIDOGO MUNGU ALITUPA NDOTO ILI TUYAJUE YA MBELE C WOTE WENYE UWEZO WA KUOTA KUNA WATU HUWA HAWAOTI.NI VIZURI UKIOTA KITU UKAKIFANYIA KAZI MFANO KUNA SIKU MM NILIOTA NIMEPATA AJALI NIKASTUKA USINGIZINI NIKAAMKA NIKASALI NIKIMWOMBA MUNGU ANIEPUSHE KESHO YAKE WAKATI NAELEKEA KAZINI DALADALA YETU IKATAKA KUPATA AJALI NA WATU WALIOKUWA CHINI TULIPOSHUKA WAKASEMA NI MUNGU TU GARI YETU HAWAAMINI KAMA HAIJAPINDUKA KWA JINSI WALIVYOONA IKIYUMBA.HIYO NDOGO CKU NYINGINE NIKAOTA MOTO ILA SIJUI NYUMBA INAYOWAKA NI IPI KAMA KAWAIDA NIKASALI CKU 2 KUPITA MTU NINAYEMFAHAM MOTO UKAWAKA KWAKE NA KWA KUWA NILIMTANGULIZA MUNGU MADHARA HAYAKUWA MAKUBWA NI VEMA UKIOTA USIDHARAU FANYIA KAZI

    ReplyDelete
  36. hayo ni maradhi tunaita kitaalam bourdonnement d'oreille.....madaktari bingwa hawajapata ufumbuzi wala tiba juu yaugonjwa huo....kwabahati mbaya ukachanganya hayo maradhi na mlio wasim iliyoita mudamrefu....

    ReplyDelete
  37. Inaitwa Telepath

    ReplyDelete
  38. Chifu KimweriJanuary 27, 2010

    Ninakupongeza kwa ku-share experience yako nasi.

    Actually, hapo hakuna muujiza kama utavyofikiri au wengine watavyo-relate na miujiza. To be frank, miujiza si lele mama!

    Unajua ndoto zipo nyingi na tafsiri za ndoto nyingine zipo wazi mno. Mfano wa ndoto yako ya kupigiwa simu ni kwamba, the moment simu yako imeanza tu kuita basi ndoto imetafsiri hiyo sekunde in terms of some hours, yaani mda mrefu unaotosha wewe kuwa kwenye computer na kuchati na kufanya mengine hadi network kuwa slow. Hapo ujifunze kuwa ndoto ina-exaggerate muda na mambo. Hapa ukumbuke kuwa waweza kuota umesafiri kwenda ng'ambo na kurudi nchini na kufanya baadhi ya mambo lakini kiukweli huwezi amini nikikuambia hiyo ndoto ime-consume sekunde zako zisizozidi tano.

    Ndoto nyingine zinakuwa na muunganiko na mambo fulani. Kwa mfano waweza kuwa na ndugu au jirani anayeumwa sana au kawaida na kutokana na kuwa mtu wa karibu sana kwako unakuwa ukimuwazia sana then ikitokea ukamuota usiku kuwa amekufa na ikatokea akawa amekufa kweli basi waweza ona ni muujiza lakini si hivyo kwani ni mara ngapi tunaota wapendwa wetu wamekufa lakini tukiamka tunakuta wapo hai. Hiyo ni 'coincedence' tu.

    Ningekuwa na muda ningekujuza mengi sana juu ya elimu hii lakini kwa hapo inatosha.

    My last word to all. Tujitahidi kusoma na kusikiliza na kujifunza tusiyoyajua kwa kuwa wanadamu hatujui mengi sana na inapotokea baadhi ya mambo hukimbilia kuhusisha na miujiza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...