hivi ndivyo kinavyoonekana kikwangua anga kipya kwenye kona ya barabara ya bagamoyo road na kawawa. zamani hapa palikuwa na gogo hotel iliyobadilishwa jina kuwa ambassador plaza, maskani ya zamani ya njenje. ujenzi wake uko nchani kukamilika na kubadili taswira ya hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Michuzi hicho kimekaa kama MELI.

    Sasa nenda pale barabara ya Ali Hasan Mwinyi rod, wanapolipiaga DSTV ostabei, nyuma yake kuna kikwangua anga kinakaribia kukamilika, chenyewe kinafafana na NDEGE- Airbus.
    Pembeni yake na mbele yake kuna zile Sheli za Gapco mbili pacha zile.
    Utapata picha nzuri kama ukiipiga umesimama kwenye hii Sheli ya Gapco iliyoko upande wa kulia kama unatokea mjini kwenda kwenda Santi Pitaz.

    Jaribu utakuja kuniambia

    ReplyDelete
  2. Alaa!!Ni kama TITANIC fulani hivi (Taswira na mfano wa melikebu)

    ReplyDelete
  3. simchezo pamependeza!! Wanangu huwa wanaiita Meli

    ReplyDelete
  4. Samahani kidogo Michuzi.
    Nisahihishe pozishen ya mahali pa kuchukulia hiyo picha nzuri ya AIRBUS.

    Kama unatoka mjini ni usimame Sheli ya Gapco ya mkono wa KUSHOTO, sio kulia. Sorry.

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Bwana Ankal
    Mimi ni mdau wa marekani,Nimejaribu sana kutafuta nyumba ya kununua bongo bila mafanikio.Moja ni bei yaka ambayo ni kubwa kuliko hata huku marekani,Pili ni watu wa kuwaamini kununua nyumba bongo.Pia ningependa kuelimishwa ni jinsi gani watu wanaamuwa kuuza nyumba zao.Ni nini kinafanya nyumba bongo kuwa aghali sana.Kima cha chini bongo ni laki mbili kama sijakosea, inakuwaje bei ya nyumba ipo juu hivyo.Pia kama kuna website ambayo tunaweza kuona nyumba zinauzwa bongo
    Nashukuru
    Mdau marekani
    Naomba unipostie hiyo kwenye mtandao tafadhali

    ReplyDelete
  6. Hivi barabara ya Ali Hassan Mwinyi inaishia wapi? Nilidhani hapo ni kona ya Ali Mwinyi na Kawawa, au?

    ReplyDelete
  7. Huko ndiko Tanzania, ndiyo maana watu wote mnang'ang'ania kuishi huko hata kama mtu anaishi kama digidigi na kutaabika. Vile huku Tanganyika hamtuwekei mpaka mtu aje kuosha macho Dar, Hilo jiji waachieni wenye kazi na biashara na wazawa.Kubanana hapa hapa si tija.

    ReplyDelete
  8. Mdau unayetaka nyumba ya kununua, kwanza huwezi tena siku hizi kupata nyumba ya bei ya chini, maana kupanda kwa maisha ndio kukua kwa uchumi. Bei za nyumba kama unataka kuona ingia kwenye blogu ya NIFAHAMISHE huko kuna sehemu ya buy and sell, labda utaweza kupata nyumba unayotaka. Bei ya nyumba inategemea na location, kama ni Prime location basi bei yake itakuwa kubwa, maana kiwanja tu peke yake kina cost mamia ya mamilioni.

    Kwenye nyumba za bei ya chini ni Kimara, Mbezi, Kibaha, ndio huko utapata za milioni 40 - 60. Na Kijitonyama pia utapata nyumba kati ya milioni 50 - 80. Tandika utapata nyumba kati ya m 50 - 70, kutegemea na nyumba yenyewe ilivyo.

    Ingia pia website ya "Mutual Developers" wana nyumba Kigamboni, wanajenga, sasa hawa unawalipa kidogo kidogo kulingana na makubaliano yenu, na nyie wa nje ni wanawafaa. Au ingia website ya National Housing nao wana nyumba wanauza, lakini hutapata nyumba kwa bei unayoifikiria uliiacha Tanzania.

    Lau unaona hizo ghali nunua kiwanja ujenge wewe mwenyewe. Mimi nimeanza kujenga mwaka 2005, foundation peke yake kwa wakati huo ilini cost 4m. Nikaenda nayo hivyo hivyo kwa mikopo ya benk, unakopa pesa kama 10m, unajenga unapose, ndio maana unaona watu wana mishahara midogo wanajenga. Mwaka jana 2009 ndio nimeezeka, tena kununua mbao na mabato peke yake kuezeka kumenicost 10m. Nikichanganya gharama zote mpaka sasa nimeishatumia karibu 30m au hata zaidi, sasa hapo bado sijafanya finishing na wala sio nyumba ya ghorofa. Na finishing ndio ina gharama kubwa kuliko kujenga boma, na gharama za vifaa vya ujenzi vimepanda sana. Unafikiri hiyo nyumba nikitaka kuuza nitaiuza kwa kiasi gani kama Kiwanja changu peke yake kina thamani ya kati ya 15m to 20m ukijumlisha na gharama za ujenzi? Kwa hiyo usishangae mabei ya nyumba.

    Mswahili

    ReplyDelete
  9. naomba kuliza hivi pesa watanzania wenzangu wanazipata wapi za kujenga majengo kama haya kama si ufisadi na kodi zetu za wavuja jasho na kututia mchanga wa macho. Nijibuni wadau wenzangu

    ReplyDelete
  10. watu wa marekani tupige pamba tu lakini kununua nyumba daresalaam hatuwezi tusidanganyane labda nje ya mji

    ReplyDelete
  11. Ali Hassan Mwinyi rd,ni wapi na Bagamoyo rd inaanzia wapi?

    ReplyDelete
  12. Nikiliona hilo jengo nawakumbuka wana-Njenje kilikuwa kiwanja changu hicho.

    Wadau mwenye kujua plz nijuze hawa Njenje wanapatikana wapi siku hizi?? they are so quite!!

    ReplyDelete
  13. Kwani huko nje watu wanapata wapi pesa za kununua nyumba? Huwezi kukuta bei ya nyumba inalingana na mshahara wako hata wa mwaka mzima hata siku moja, si popote pale duniani.

    Hivi nyie mnafikiri kuwa kwa kuwa tuko Tanzania basi hatjui kukutumia huduma za benki? Na benki bado ni zile zile za enzi ya ujima mlizoziacha? Na mishahara yetu bado ni ile ile ya chini ya laki moja? Unakopa benki, tena benki nyingi zinakopesha sasa hivi kama Barclays, Stanbic, Standard Charter, na unaweza ukahama benki wewe na mkopo wako kuhamia benki nyingine. Mimi nimejenga kwa kutumia mikopo ya benki za Standard Chartered, na Stanbink, hapo mkopo na mshahara wako baada ya kukatwa unaongezea.

    Vile vile bank kama CRDB wewe kama nyumba yako haijaisha, wanakupa mkopo wa kuimalizia, lakini unaingia mkataba wa namna ya kuwalipa pesa zao. Na benki nyingine wanakukopesha pesa ya kununua nyumba kabisa mradi tu uwe na feasibility study itakayoonyesha jinsi utakavyolipa pesa zao, unaweza kuopt kuipangisha, kodi inakwenda benki, deni likiisha nyumba yako unakaa mwenyewe.

    Kalaghabaho na ubozi wenu mtakalia hivyo hivyo kutuita mafisadi kwa wivu wenu lakini sisi tunasonga mbele, na nyumba yangu siwezi kukupa bure ukizingatia huo mkopo nililipa na interests pia.


    Nyie mmekalia pesa zenu kunywa tusker, sie wenzenu wala huzioni mshahara wako unakatwa deni huko huko benki unabaki na pesa ya kutumia tu. Hebu fanya hesabu ya wine na tusker mnazokunywa kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi, hata kwa mwaka, kama hutaweza kusave.

    Na wengi wenu kosa kubwa mnalolifanya mnawapa ndugu zenu pesa wawajengee kwa ubahili, matokeo yake wanajenga nyumba zao au wanazila tu kisha wanawaacha solemba. Wewe umekaa unajua una nyumba kumbe unaletewa picha za nyumba ya watu. Tumieni makontracta wanaoaminika, wako vijana wamemaliza University wana makampuni madogo madogo ya ujenzi, atakuandalia mchoro, kupitisha upate kibali mpaka kukujengea, ila acheni ubahili!

    ReplyDelete
  14. mdau eehhh njenje wanapatikana paleee salender bridge kiwanja cha mashushushu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...