Bwana Michuzi habari za kazi?
Blog hii ya jamii hakika ni jukwaa huru la mawazo. Baada ya kusoma mada kadhaa za kijamii na kuvutiwa nazo kwa sana, nami napenda kutoa dukuduku langu la moyo.
Mimi ni kijana wa miaka 30 na naishi Mwanza mjini na kazi yangu ni Mtaalam wa ujenzi. Kipato changu hakina wasiwasi namshukuru Mungu. Mimi ni mkristo mkatoliki mzuri tuu. Mke wangu naye ni katoliki.
Nilioa mwaka jana baada ya kukutana na ambaye ni mke wangu kwa sasa huko Marekani ambapo nilikuwa nafanya degree yangu ya pili na bibie naye alikuwa nafanya sheria (Masters) na kwa sasa anafanya kazi hapa Mwanza na kipato chake kizuri. Mke wangu pia ni wa kabila langu.
Kuna mdudu ameingia ndani ya ndoa yetu baada ya mke wangu kujifungua mwaka jana mwezi wa saba. Nimegundua kuwa mke wangu huyu hana kabisa mapenzi ya kimama na hutu mtoto wetu, kwani toka alipojifungua naona anamwachia zaidi house girl kumtunza mtoto kuliko yeye.
Kuna siku mtoto akiwa na miezi mitatu nilimkuta yupo sebleni na house girl, huku mama akiuchapa usingizi. Mtoto alikuwa analia sana na ilinipa uchungu kweli. Kumwuliza mke wangu alinijibu kwa kiburi kuwa alihitaji kupumzika kidogo.
Hali hii ya kutomjali mtoto wetu nimei-note kwa muda sasa na inanishangaza kwa kweli jamani. Worse enough juzi mama yangu mzazi alikuja nyumbani kwetu kututakia hali na mke wangu alionyesha dharau fulani kwa mama yangu, jambo ambalo limenihuzunisha sana.
Nimejaribu kuwashirikisha ndugu zangu tabia hizi za ajabu za mke wangu, na wenyewe wamekuja na kushughudia ukweli kuwa mke wangu ana tabia ya ajabu kidogo.
Ndugu zangu baada ya kuona hali hii wameniambia kuwa ni bora nikaachana na mke wangu mapema, kwani anaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa katika maisha yangu.
Kwa kifupi mimi sijawahi kugombana naye, ila kwa vile ni mtoto wa kigogo fulani mwenye pesa ana maringo ya ajabu kwangu.
Sasa wadau nifanyeje kuhusu hali hii???
Blog hii ya jamii hakika ni jukwaa huru la mawazo. Baada ya kusoma mada kadhaa za kijamii na kuvutiwa nazo kwa sana, nami napenda kutoa dukuduku langu la moyo.
Mimi ni kijana wa miaka 30 na naishi Mwanza mjini na kazi yangu ni Mtaalam wa ujenzi. Kipato changu hakina wasiwasi namshukuru Mungu. Mimi ni mkristo mkatoliki mzuri tuu. Mke wangu naye ni katoliki.
Nilioa mwaka jana baada ya kukutana na ambaye ni mke wangu kwa sasa huko Marekani ambapo nilikuwa nafanya degree yangu ya pili na bibie naye alikuwa nafanya sheria (Masters) na kwa sasa anafanya kazi hapa Mwanza na kipato chake kizuri. Mke wangu pia ni wa kabila langu.
Kuna mdudu ameingia ndani ya ndoa yetu baada ya mke wangu kujifungua mwaka jana mwezi wa saba. Nimegundua kuwa mke wangu huyu hana kabisa mapenzi ya kimama na hutu mtoto wetu, kwani toka alipojifungua naona anamwachia zaidi house girl kumtunza mtoto kuliko yeye.
Kuna siku mtoto akiwa na miezi mitatu nilimkuta yupo sebleni na house girl, huku mama akiuchapa usingizi. Mtoto alikuwa analia sana na ilinipa uchungu kweli. Kumwuliza mke wangu alinijibu kwa kiburi kuwa alihitaji kupumzika kidogo.
Hali hii ya kutomjali mtoto wetu nimei-note kwa muda sasa na inanishangaza kwa kweli jamani. Worse enough juzi mama yangu mzazi alikuja nyumbani kwetu kututakia hali na mke wangu alionyesha dharau fulani kwa mama yangu, jambo ambalo limenihuzunisha sana.
Nimejaribu kuwashirikisha ndugu zangu tabia hizi za ajabu za mke wangu, na wenyewe wamekuja na kushughudia ukweli kuwa mke wangu ana tabia ya ajabu kidogo.
Ndugu zangu baada ya kuona hali hii wameniambia kuwa ni bora nikaachana na mke wangu mapema, kwani anaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa katika maisha yangu.
Kwa kifupi mimi sijawahi kugombana naye, ila kwa vile ni mtoto wa kigogo fulani mwenye pesa ana maringo ya ajabu kwangu.
Sasa wadau nifanyeje kuhusu hali hii???
Ndugu pole kwa situation hiyo na mkeo. Ushauri wangu ni kuwa mtafute counselling kwanza kwani kuna watu baada ya kujifungua wanashindwa kubond na mtoto. Hii haitokei kwa wanawake tu hata wanaume inaweza kutokea. Halafu kuna depression inayoweza kuwatokea wanawake baada ya kujifungua. Kwa hiyo tatizo linaweza kuwa ni kushindwa kubond na mtoto au amepata depression baada ya kuzaa. Ningeshauri kwa pamoja mtafute msaada kwanza before mfikirie kuachana.
ReplyDeletePole sana kaka! Matizo katika ndoa yapo, na yapo ili yajadiliwe na kusuruhishwa, ningekushauri jaribu kuongea na mkeo umweleze jinsi anavyokukwanza kuhusu kuacha mtoto na HG, lakini nafikiri swala sio mapenzi na mtoto nafikiri swala ni stress za kazi, kumbuka huyu mama bila shaka anaamuka mara kwa mara usiku kumhudumia mtoto, halafu asubuhi inabidi aende kazini, akirudi ni lazima hawe amechoma hivyo anapaswa kupumzika kwa ajili ya usiku (najua watoto wadogo usumbua sana usiku) Sasa basi kwa faida yako na ya mtoto wako, ukitoka kazini jaribu kumsaidia mkeo uwe na mtoto, na akiamuka basi mpe mtoto.
ReplyDeleteSwala la maringo, dharau au mtoto wa kigogo ni mawazo yako tu.
Na kama alimuonyesha mama yako dharau basi mwambie na umsikilize yeye anatasemaje inawezekana kabisa labada hakuwa na maana maya au hakukusudia kufanya hivyo.
Kumbuka muhimu katika ndoa ni kukaa nchini na kuongea nyie wawili, Kuheshimana, kusikilizana, kuvumilian, kupendana na kuaminiana ndio msingi wa ndoa.
MPIGE CHINI BWANA HUYU. WANAWAKE MBONA WAKO WENGI SANA. TENA UKISHABIGA CHINI TAFUATA KASICHANA KADOGO UKISOME KWA MUDA WA MIAKA MIWILI KWANZA HALAFU NDIYO UNAOA.
ReplyDeleteBAADHI YA WANAWAKE WALISOMA TENA ZAIDI WALISOMA SHERIA WANAKIBURI FULANI HIVI.
WEWE SI RIJALI BWANA, MPIGE CHINI UACHANE NA MATITAZO MAPEMA.
sidhani kama umesoma. Ungekuwa na elimu ugekuwa pia na akili ya kurekebisha maisha yenu ya ndoa, na sio kutafuta mawazo kwa wadau.Mke ni wako, mama yako anahusika nini? Basi umemuolea familia na sio mkeo huyo.
ReplyDeletePole sana na tatizo unalolikabili katika ndoa yako, still inawezekana ikawa ni tatizo dogo kwa maana Dunia ya siku hizi Baba, Mama kila mtu anapigania maisha, mambo ya kazi saa nyingine inakuwa ni vigumu kubalance familia na kazi. Imagini Viongozi mbali mbali wabunge kwa mawaziri na kusafiri kote huko saa ngapi atapata muda wa kutosha kulea mtoto. Ndo maana wenzetu wazungu mtoto mmoja au wawili tu wanatosha. Mpe tu muda labda huko mbeleni atapata kujua namna ya kubalance.
ReplyDeleteTatizo kubwa litakuwa kuna akina mama wachache unakuta hawana motherly instict. Mimi ni muathirika wa aina hiyo ya mama, niko mtu mzima mwenye mafanikio na familia yangu, utakuta mama maisha yake yote ni pesa zake tu na starehe zake mpaka siku ya kaburi itakapofika. Wajukuu unashindwa hata kupeleka wasije ona uliyowaona maanake yanaweza kuja waharibia maisha yao.
Ukishampa mkeo muda ukaona kuna tatizo kubwa kama hili basi hakikisha unampa/wapa wanao mapenzi toosha maanake wao ndio huko mbeleni watakuwa victims kama nilivyoishia mimi. Lakini watakuwa imara watakapokukumbuka angalau baba yetu alikuwapo. Hizi ni isssue ambazo inabidi wengine tupambane nazo na unapata moyo unapoona wenzio wenye mafanikio either walikuwa adopted, mama zao walikwa alcoholics, au kwenye drugs, abused, vilema and still they make it good in life.
Hivyo mpe mke muda na support hiki kinaweza tu kuwa kipindi cha kupita na baada ya muda mkaweza kuwalea watoto wenu vizuri.
Ndugu mi naona afadhali upige chini mapemaa!! Maana hapo inaonekana watu washaanza kukusaidia!! hahahha haya uamuzi ni wako kama kusuka au kunyoa!!
ReplyDeletewe kaka tumia akili hujui maisha kusaidiana au bado una mambo ya kizamani watuu hawaendi hivyo wanasaidiana kulea sio kujikosha kwa watu msaidie kumbeba mtoto au kuwa nae ukishindwa hause girl awasaidie. Sasa anafanya kazi gani kama mnamlipa halafu hafanyi kitu mwache apumzike tena kwa raha zake hujui hivi hujui kama ni kusaidiana.
ReplyDeleteUshauri wangu usiachane na mke wako mwanamke anapojifungu mara nyingi inatokezea kitu kama hicho sio kama hamjali no, anajali ila anahitaji muda wa kupumzika ili aweze kudeal na mtoto vizuri usipopumzika anaweza kuumwa na wewe unahitaji kukaa na mtoto umsaidie kwa sababu usiku mara nyingi anakuwa macho msaidiane usichoke ndio maisha.
ReplyDeleteKama ulivyojieleza umesoma kidogo sasa nenda ka-research POST NATAL DEPRESSION utapata majibu yote. Endelea kumpenda mkeo na vumilia hilo wimbi litapita, maisha ni milima na mabonde.
ReplyDeleteKwa vile mlikutana Marekani, pia nyote ni 'wasomi' vipi mnashindwa kujadili kuhusu 'mapokezi' ya tamaduni za Kimarekani vinavyoweza kuleta mambo 'chanya' na mambo 'hasi' ktk ndoa yenu.
ReplyDeleteMimi hapa Uingereza siku nyingine hukaanga chips na kuoka kuku, huku mamsapu yupo sebuleni anatizama TV vipindi vya 'eastenders'.
Chakula kikiwa tayari namwita bibie chakula tayari, ili mamsapu na wanetu wajipakulie mlo. Sio kupika tu hata kufua nguo, kufanya usafi n.k mzee mzima nafanya, hata wakati mwingine mamsapu hujisahau akitoka shopping mie nikiwa nyumbani naangalia mpira huniuliza kama 'nimepika au bado'.
Lakini pamoja na hayo huwa tunajdiliana hivi tukienda likizo Bongo nyumbani tutaendelea na jinsi tunavyoishi hapa Uingereza?.
Bahati nzuri Mamsapu husema katu hawezi kupeleka mambo ya kizungu Bongo, kwamba katu hataniruhusu 'kukarangiza' vitu Bongo.
Na kweli tumeenda mara kibao Bongo mambo ya 'kizungu' hatupeleki Tanzania. Hata hapahapa Uingereza wakija rafiki zetu wa kizungu na wakiswahili, sie hufuata mila za kiafrika kuwa dume ni dume tu hatuonyeshi mambo ya kizungu kwa marafiki zetu.
Hivyo ushauri wangu kwako ni kuyajadili mambo yenu, pia sioni ubaya mtoto kubembelezwa na huyo dada mliyemuajiri, ukiona dada anazidiwa na kilio cha mtoto, mbembeleze wewe, ukiona umezidiwa mbinu, basi nenda na mtoto chumbani, nadhani mkeo akiona hizo juhudi zako zimeshindikana basi ataamka kufanya ujanja wa kumtuliza mtoto.
Hivyo fanyeni mazungumzo kwa hali ya upendo, kwamba mwenzio kachoka, kuna dada mliyemuairi na pia mjadili kuhusu mambo chanya na hasi ya tamaduni za kimarekani na kitanzania, kutegemeana na mahali mlipo TZ au USA.
Pia ni mara chache mama kumwonea wivu wa attention mtoto wake, lakini inawezakana pia wewe bwa-mzee unatoa attention kubwa kwa mtoto kuliko mama, hivyo tafuteni ushauri kwa 'wataalamu'.
Mdau
Mkangarizaji
inaonekana wewe ndio mwenye tatizo maana huelewi na aliyekushauri hapo ukasome POST NATAL DEPRESSION ndio hasa unachotakiwa kuelewa,hayo ni matatizo ya kawaida sana kwa kina mama wanaojifungua hata actress Brooke Shield yalimkuta hayo,na kazi ya kulea ni yenu wote sio kumlaumu mwezako tuu eti analala na anamwachia mtoto housegirl,kama kachoka unataka afanye nini?sio machine hiyo ni binadamu tuu kama wewe,na hiyo tabia ya kumwona eti hana heshikma kwa mama yako na kumuona anajidai eti mtoto wa kigogo is upuuzi wa hali ya juu na inaonekana una inferiority complex na hujiamini,hizi tabia za kumsema mwenzako na ndugu zako wa familia yenu hazitakusaidia chochote zaidi ya kuvunja ndoa yako na mwanamke unayempenda na ukumbuke ndoa sio lelemama na matatizo yapo na yataendelea kuwepo ila uache tabia ya kulaumu laumu mkeo,msaidie na ujitahidi kuelewa tatizo ni nini na utumie watu wenye kuelewa sio opinions za majungu majungu tuu kutoka kwa ambao tayari wanamwona ana dharau na ni mtoto wa kigogo....na kulea ni wote wawili sio peke yake.
ReplyDeleteWADAU MBONA MIE BADO SIJALIONA TATIZO HAPO JAMANI??SWALA LA KUMKUTA MTOTO NA HOUSEGAL WAKATI MAMA KAJIPUMZISHA NI LA KAWAIDA SANA UTAKUTA SIAJABU MTOTO ALIMSUMBUA MAMA USIKU KUCHA NA MAMA HAKULALA SASA MCHANA AKAONA AJIPUMZISHE NA WATOTO KWAVILE HAWAWEZI KUONGEA KULIA KWAO NI KAWAIDA MM NILICHOGUNDUA WW UNA MFUMO DUME SIDHANI KM UNAMSAIDIA MKEO VYA KUTOSHA KUHUSU SWALA LA KUMLEA MTOTO WENU,NA KUMDHARAU MAMA YAKO HUJAFAFANUA KAMDHARAUJE JE KM MAMA NDIO ALIANZA DHARAU JE?MDAU HUNA JIPYA JAMII YETU YA WATANZANIA INA MATATIZO ZAIDI YA HILI LAKO KM KWENYE BLOGU USHATOKA SASA KAA KIMYA TUNZA FAMILIA YAKO NDOA YAHITAJI UVUMILIVU KULIKO MASOMO ULIOSOMA ...ASANTE
ReplyDeleteWanawake viburi na Jeuri kama hao wapo sana yani mdau ninakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, sijui huwa wanakuwa na matatizo gani?? ni kweli unakuta hamjali kabisa mtoto yani ni roho mbaya sana sana. hata kumnyonyesha unakuta anamwachisha ziwa mtoto wa miezi 3 kisa matiti yake yataanguka akiendelea kunyonyesha. sasa unajiuliza swali kwanini uwe na wasiwasi matiti kuanguka kwani unataka bado kupendwa na wananume wengine wakati umeolewa??
ReplyDeleteNa ninakuambia kweli mdau amini ninayosema mwanamke wa namna hiyo hafai hafai hafai, ni bora ulale mbele mapema wanamke wa namna hiyo ni headache na mara nyingi ni wajeuri na ni viburi kupindukia!! mimi nimeyaona yaani tabia kama za mkeo TYPICAL yani utadhani wamezaliwa tumbo moja na huyo mkeo na sasa cha moto ninakipata. Na huwa hayana mapenzi na mtoto na si mtoto tu hata kwako ujue mapenzi ni ziro!!! na akishaona ametokea familia nzuri basi hapo humwambiii kitu na ninakuhakikishia mwanamke wa namna hiyo haogopi taraka hata kidogo na ukichelewachelewa utajikuta yeye ndo anakubandika taraka.
kwakweli ningekushauri ulale mbele mapema ndugu yangu, na kama huamini ninakupa miaka mingine 3 ipo siku utatupostia makubwa zaidi hapa kwenye huu mtandao. kama hukutuambia kuwa umepigwa talaka na mkeo sijui, mimi nilioa mke wa hivyohivyo yani copyright!!!
Pole sana.
Issa.
Pole sana ndugu na matatizo hayo. Hiyo hali ya mkeo kutojali mtoto huwa inatokea kwa baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na "Postpartum Depression." Anonymous wa Kwanza ameongea vyema kuwa mkeo anahitaji counseling even some medical interventions.
ReplyDeleteMdau DC
Various treatment options for Postpartum depression include:
ReplyDelete* Medical evaluation to rule out physiological problems
* Cognitive behavioral therapy (aka: Psychotherapy)
* Possible medication
* Support groups
* Home visits/Home visitors
* Healthy diet
* Consistent/healthy sleep patterns
Source: Wikipedia
Look good in people weee unachokiona ni mabaya tu. Hujaelezea hata zuri la mkeo...Na weee mbona husemi ya kwako mabaya tuyaone?
ReplyDeleteKwanza kama umesoma ungejua kuwa hamna anayechukia mtoto wake bali kuna kuchoka na mtu anahitaji kupumzika. Na kama umesoma ungejua kuna depression and bonding. Weee hujaelimika japo umesoma. Kaa yote marekani hukujua hayo? Wakati kila siku kwenye TV wanaonyesha dalili za postpartum depression
Mimi hapa nimejifungua mwaka jana pia mtoto. Na huyu ni mtoto wa kwanza na tulitumia IVF ...so you know the whole thing and money that goes into it. Nampenda sana mtoto wangu but sometimes I need a rest na anaweza kulia hapo na wala nisisikie. Na huyo mkeo anamsaidizi mwachie mwenzio apumzike. Unajua kubeba mimba wewe? It's not easy... ungetakiwa uvae empathy belly siku moja uelewe....Mimi nipo marekani na wala hatuna baby sitter bali nikusaidiana na mume wangu tu. Yeye akija nyumbani anaanza na mtoto na miye nipumzike. Ukiingia home do your share. Sio umwachie tu mkeo na nanny tu wafanye kazi za mtoto. Ulivyoona analia kwanini usimchukue ukambembeleza? You are the daddy right!!
Na huyo mama yako hayo unayajumlisha ili upate sababu ya kuongezea shari... You know what sio ujidai kumwacha ...hata yeye anaweza kukuacha...wanaume wako wengi tu siku hizi na kuachika na kuolewa mara hata tatu sio jambo la ajabu tena na kuishi single lady wala sio shida....Acha kuchezesha kibiriti na nyamaza utunze mtoto wako na mkeo kama familia.....Ugemind tiny things before you got the baby ...no time for blah blah blaha.
Aghhhhhhhhhh
Inabidi uone ile movie ya "Talaka tatu" ndio utaelewa..miaka 30 ulikimbilia luoa sasa unatamani uwe single
x
Read here about Post natal Depression, here about <a hefr="http://motherinlawhell.com/>Mother in laws Hell</A> and read about THE MAN CODE
ReplyDeleteMimi nakushauri jaribu kukaa na mtoto wako siku nzima na ufanye kila kitu mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote, au ukitoka kazini uhamanike naye uone mziki wake. Inawezekana mke wako yuko stressed na kama kawajibu ndugu zako vibaya au mama yako inaelekea hawamsaidii hata kumlea huyo mtoto wanamuwekea usiku kwa hiyo anashindwa kuwaambia ukweli anaamua kutoa majibu yaliyoambatana na hasira juu yao. Kama amerudi kazini ukichunguza vizuri utakuta hata kiwango cha utendaji wa kazi kimepungua.
ReplyDeleteWewe kama mumewe unatakiwa uwe karibu naye sana hayo mawazo ya kuwa mtoto wa kigogo kwani ulipomuoa ulikuwa hujui hizi ni inferiority complex zako na ujinga unaojazwa na ndugu zako, unapooa unatakiwa muwe kitu kimoja mkishaingiza ndugu humo ndani utajikuta unaoa mara sita, nashangaa hao ndugu zako wanakushauri umwache ni wa dini gani maana dini zote zinataka muafa kwanza kukimbia tatizo sio solution.Tena umesoma Marekani umeona grow up brother acha ushamba!!
Kaka jitahidi kumsaidia mkeo kumwangalia mtoto muda mwingine. Tumetofautiana katika kuhimili mikiki. Mara nyingi sana mama mwenye mtoto mchanga usiku huwa halali kabisa au ana lala kidogo tu kutegemeana na mtoto kama huwa analala au la. Usiku inabidi awe anaamka mara kwa mara kumhudumia mtoto na asubuhi awahi kazini kama kawaida kwa kuwa wote tumeumbwa na mwili wa nyama nae anachoka. Kweli anahitaji kusaidiwa na wewe pia, tena kama wewe usiku unachapa usingizi muda wote siku zote hata husemi mwenzangu pumzika kidogo na mimi nimbembeleze mtoto sasa hio depression ndio inazidi. Anaweza asiseme lakini moyoni anakwazika.
ReplyDeleteUsiwashirikishe watu wengine kwenye suala hili kwa vile utapewa majibu rahisi ya makto kama vile mpige chini na tafuta mwingine. Siku zote matatizo ya ndoa yakabili mwenyewe. Kwanza ndoa yako bado changa na unaweza ukairekebisha. Ongea na mkeo. Huoni kuwaambia watu wengine umetoa siri ya ndoa yako nje?
ReplyDeleteKuhusu mama yako. Sawa mheshimu lakini mpende mkeo zaidi kwa sababu ni mwili wako huo mzee. Au hukufundwa wewe kabla ya kuoa?
Mimi siku zote nimekuwa nasema jamani kitchen party kwa bibi harusi sawa lakini wanaume nao wanahitaji darasa kabla ya kuoa kwa sababu wanakutana na matatizo mengi baada ya kuoa.
Ukimwacha huo na ukaoa mwingine naye pia utamwacha. Wanaume wanaoacha wake zao hawajiamini na wana ubinafsi. Chunguza sana.
I am married for more than 30 years. Siyo kwamba sijawahi kukutana na migogoro. Hapana. Wakati mwingine ni mimi ndiye ninaesababisha na wakati mwingine ni wife. Pamoja na hayo sijawahi kufikiria kumtosa never. Wala hatushirikishi watu wengine. Wenyewe tunakuwa na ujasiri na kukabiliana. Washauri wa nje hawafai asilani.
usione wazazi wako wameishi cku zote pamoja sio kwamba siku zote wameishi kwa furuha ni kwa kuvumiliana tu!na watoto ndio huwa ni kiunhanisho kikubwa ktk ndoa!kuishi na m2 yoyote mwenye nafsi tofauti na na yako n backgroung tofauti ni kazi mno yahitaji uvumulivu kwa hiyo kaka angu endelea kumvumilia tu huyo wifi maana no one is perfect!
ReplyDeleteKAKA POLE SANA. HAYA MAMBO YAPO KATIKA NDOA, NA SULUHISHO LAKE SI KUACHANA NA MKEO AU KUSHIRIKISHA NDUGU (WENGI WATA-REACT VILE WEWE UTAKAVYO WA-GUIDE, HAPA TUMEONA GUIDANCE YAKO...) HASA KATIKA HATUA HII AMBAPO MSHALETA KIUMBE DUNIANI. UKIFUATA USHAURI WA KUMWACHA MKEO, MTAMPA TABU SANA HUYO MTOTO ASIYE NA HATIA (TRUST ME ON THIS). KUNA MABADILIKO MENGI SANA YANATOKEA KWA WENZETU (KINA MAMA) KATIKA KIPINDI CHA UJA UZITO, NA HATA BAADA YA KUJIFUNGUA. jARIBU KUSOMA KUHUSU MABADILIKO HAYO (YA KITABIA) KABLA YA KUANZA KU-CONCLUDE (samahani wadau kwa kiswanglish) UKISHAELEWA, TAFUTA NAFASI NA MKEO (MNAWEZA FANYA KAMA OUTING FLANI YA JIONI AU HATA MWISHO WA JUMA KAMA MNA MUDA), MKAKAE MAHALI PENYE UTULIVU (SIYO NYUMBANI), MWELEZE JINSI UNAVYOMPENDA NA MZUNGUMZE KUHUSU NYUMBA YENU. MTAPATA SULUHU TU.. NAWATAKIA HERI KTK MAISHA YENU NA MUMLEE HUYO MTOTO KUJA KUWA NA FAMILIA YAKE BORA HUKO MBELENI.
ReplyDeleteMdau, Deslam
hiyo ni postpartum dipression huwa inachukua miaka miwili mitatu kutulia worry not
ReplyDeleteUnajua hadi jamaa kaamua kupost mi naamini kuwa he's doin' his share....Unapojikuta wewe unafanya majukumu mengi ya mama wakati yeye hana time na mtoto ni wakati wa kuamka smell some coffee na kufanya decision...
ReplyDeleteWell malawyer bana wapende tu wakiwa mahakamani ila sio nyumbani,They always argue,Kila kitu kwao lazima kiwe na logic,Gender balance Equality sijui!
Kwakua huyo ni mkeo huna jinsi Kaa nae chini.Communication is key.Unatakiwa umwambie kuwa u're not happy with the situation lately...
I mean Ndoa ndoano babu aliesema hivyo hakuwa anatania...Ukiona kitu kina mkataba ujue Hicho kitaa kiko sensitive kidogo...
I hope mtapata solution...Ila usiogope TALAKA,Huoi ili ukae na mtu kama ndugu yako Bali kama mpenzi wako....Ukijua hilo Life mbona EASY SANA!!
Mmmmh!! ANOTHER LAZY!! THAT'S HOW YOU SOUND.
ReplyDeleteMAN, I MUST BE VERY HONEST.
YOUR EQUALLY RESPONSIBLE FOR THE CARE OF THE CHILD, NO EXCUSES.
MNA ELIMU SAWA NA WOTE MNAFANYA KAZI, MAJUKUMU SAWA. SASA MWENZAKO ANAPOKUWA AMECHOKA SI UNAMSAIDIA NDUGU YANGU.
VINGINEVYO UNGEOA A FULL TIME HOUSEWIFE NA HATA HIVYO BADO UNAWAJIBIKA KUMSAIDIA MAMAA.
ACHA KUBWETEKA!!
Mwanangu nakushukuru sana kwa kutoa lile linalokusibu ndani ya roho yako. Napenda nikuambie kuwa hali ya mke wako ni nzuri sana na anajua kabisa ana mtoto kwani alidiriki kuibeba hiyo mimba mpaka akazaa.Jua tu kuwa yeye ni binadamu na kuna kuchoka katika majukumu ya kazi na kuna kuchoka kwa akili. Nakuomba kuwa wewe na yeye mmeshakuwa kitu kimoja.Pale ambapo unaona anazembea jaribu kuongea nae kwa taratibu na ikiwezekana kufanya kwa kufuatilia lolote katika malezi ya mtoto. Lakini ukiendekeza maneno ya marafiki ama sisi wazazi utaharibu ndoa yako. Mnapendana na hamjagombana chanzo cha maudhi kisiwe ni huyo mtoto kwani mnaweza kusaidiana kwa kurekebishana taratibu hadi atazoea. Hayo mawazo ya kuwa ni mtoto wa fulani achana nayo kabisa kwani ni mawazo potofu na hayatenga unyumba wenu. Muelewe kuwa maisha yake amelelewa vipi ndio umuajust taratibu kwani pengine malezi yake ni tofauti na ya kwako.Nikuambie kuna harusi ya wenzio ya kuwa chakula kiagizwe toka mahotelini je uliona wapi hiyo? Lakini wanaishi pamoja ni malezi ambayo mwenzi wake hajawahi kupika na hajui kupika.
ReplyDeleteNdugu yangu,pamoja na shule yote hiyo, lakini naona una weakness ya maamuzi ya kifamilia, nijuavyo mie tabia za sis waafrica ni kujaribu kuwa na control ya maisha ya ndugu wenye mafanikio.Kwa kitendo chako cha kuamua kushirikisha ndugu katika kutatua matatizo yako ya kifamilia, yatakugharimu ndugu yangu, hebu angalia, kwa kitu kama cha kumkosea heshma mama mzazi, ndugu wamehsaamua umuache mkeo, hakuna kitu kama hichi, ndugu yangu, ndugu katika familia huwa wana mipaka kaka, na kuacha mke sio suluhisho la ndoa. Sit down with your wife,and resolve the issue, ndugu watakuchanganya, and they will make it more worse.
ReplyDeleteMkeo kuwa mtoto wa kigogo, haimpi kibali cha kutoheshimu wazazi wako. Yeye ni kama mtoto, anastahili kuheshim wazazi wako, kama anavyowaheshimu wazazi wake. Na kama na wewe utachukulia kwa sababu yeye ni mtoto wa kigogo basi haambiwi, you will be in trouble mzee. You need to have a stand, na sio kuruhusu utajiri wa baba mkwe ukuharibie ndoa. Kumbuka
mmeshazaa kaka.
Pole sana, na hizi ndio challenges za maisha, najua kama mwanaume unapenda kuona katika nyumba yako, kila mtu anajisikia huru kufika.
Pole sana rafiki yangu. Wote wamesema lakini bora utafakari sana suala la kuachana kwani halipendezi (si ajabu yule anayeshabikia muachane yeye anataka!). Inaelekea una tatizo jingine linalokukera sasa hili dogo umelitumilia kutafuta ushauri wa jumla jumla. Nakushauri ukae chini ufikiri kwa undani bila ushawishi (haswa ndugu)nini kiini cha tatizo. Pia jaribu kupitia majarida na articles zinazohusu ndoa specifically za kidini zitakusaidia mno rafiki yangu.
ReplyDeleteRegards
KWELI WEWE BWEGE UNATUELEZA NDUNGU ZAKO PIA WAMEONA HANA TABIA MBAYA KWANI WAO NDIO WAMEMUOWA TENA NINGEKUJUWA NINGEKUPIGA NA KIATU MAANA JAMBO KAMA HILO LA NDUNGU NDILO LILILONIFANYA MIMI KUACHANA NA MUME WANGU NIKIWA NA MTOTO WA MIEZI MITATU SHEZI WEWE FIKIRI NYIE NDIO MNASABABISHA SINGLE MUM KUONGEZEKA SHAME ON YOU
ReplyDeleteWote waliokushauri umwache mkeo huenda wanakabiliwa na tabia kama ya kwako. Lakini watu wengine wamekupa ushauri mzuri kama utaufanyia kazi mambo yataenda sawa tu. Muhimu saidiana na mkeo kulea mtoto. Pia msaidizi nae anaumuhimu wake kama umelea utajua tu. Kuna watoto mama yake akimchukua kumlisha anataka kunyonya tu wazo la kula linatoweka. Ukipewa nafasi ya kuchagua utaacha mtoto abaki na njaa kwa kuwa unalazimishia mama yake amlishe? Au utamwacha binti msaidizi ampe chakula mtoto ale vizuri? Kitu muhimu ni kuelewa mwenzako kwa nini anafanya jambo fulani. Na utaelewa kama unashiriki kwa vitendo na si kwa macho tu.
ReplyDeleteBadili mwenendo wako utaona mabadiliko.
WE BWANA WACHA UBWANYENYE! MSAIDIE MKEO . NAE PIA ANACHOKA, YEYE SIO BULL DOZER! ACT LIKE A FAMILY MAN
ReplyDeletehttp://www.tubeislam.com/video/6848/Tips-to-keep-your-wife-happy
ReplyDeleteNdugu yangu hao wanaokuambia mambo ya post-natal depression wanakuingiza "chaka bovu", hizo ni excuses za wazungu kwa wao kukosa mapendo, na kwa sababu wanaona kawaida wanatafuta scientif explanation for it; naona wadau wengi washaathirika na hizi bla-blah za wanaojiita wataalam wa kizungu
ReplyDeleteUshauri wangu, 1. Wewe umeoa ndoa ya kikristo, biblia inakataza kumwacha mwanamke isipokuwa kwa sababu moja tu,uzinzi(Matthew 5:32 na 19:9). Kwahiyo hata mkeo awe na roho mbaya,awe mchawi,ana dharau sijui as long as ni muaminifu katika ndoa futa kabisa wazo la kumuacha
2. Usimuambie mkeo kuwa hana mapenzi, nakwambia that will do more harm than good in the long run. Cha kufanya jaribu kumuonyesha kwa matendo jinsi ya kumpenda na kumjali mtoto, na unaweza ukawa unajaribu kumfikishia ujumbe katika maongezi lakini usimwambie moja kwa moja unamzungumzia yeye. Usiache kumpenda mkeo, Biblia inasema waume wapendeni wake zenu, na wake waheshimuni waume zenu. Onyesha upendo wa nguvu kwa mkeo pamoja na mapungufu yake, taratibu atabadilika tu, na uwe mvumilivu. Na mwisho na muhimu zaidi zama katika sala ndugu muombe Mungu kila wakati.
Mdau G/Mboto
kumwacha sio solution,hilo ni tatizo wanawake wengi linawatokea kama alivyosema mdau wa kwanza mkeo atakuwa ana ugonjwa unaitwa post natal depression,inabidi mwende kwenye counselling,jalibu kuongea nae but sio kwenda kutafuta maguberi nje,na huo ukimwi noma
ReplyDeleteNimepitia hoja yako,angalau umejitaidi kufuata taratibu za kuonyana kindugu kwa taratibu za kikatoliki.Lakini sijaona sehemu ambapo kanisa umelishirikisha.check Mathayo 18:15-17. haya ya 15 inasema,nguduyo akikukosa enenda ukamwonye wewe na yeye peke yetu;akikusikia umempata nduguyo(mkeo nimeongeza).Haya ya 16 la kama hakusikii,chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wa2 au wa3 ili vinywa vya mashaidi wa2 au wa3 kila neno lithibitike.Melezo yako yanaonyesha umefuata izi haya mbili.Haya ya 17 inasema,na asipowasikiliza wao, liambie kanisa(si ndipo ulipofunga ndoa?);na asipolisikiliza kanisa pia,na awe kwako kama mtu wa mataifa.Kwa maelezo yako so far kanisa hujalishirikisha.Hakuna sehemu ulioonyesha kama ulishawai ulimshirikisha padri au sheikh.Pili inawezekana kuna sababu nyingine zaidi ndio mana unataka kumwacha(may be unahisi jamaa wanakusaidia?) kwa maana kikatoliki ndoa haivinjwi isipokua kwa sababu ya uwasherati(Mathayo 19:9).
ReplyDeleteunataka kuacha mke ambae ni mwili wako kwa sababu ya maneno ya wazazi,sijui mtoto wa kigogo nk???ivi na ww unajiita msomi ilhali wasikiliza eti mashauri tena ya ndugu zako,uko dunia gani?nenda kanisani/msikitini upate ushauri basi wa watumishi wa mungu sio ivo vindugu vivunja ndoa...
ReplyDeleteuna akili wewe kweli?au ulilazimisha ndoa au kuoa kama "na wewe wakuone uko ndoani" nini?
suala la kipuuzi sana hili eti analala na anamwacha mtoto,wee unafanyaga nini?hujui madhara ya pre na post natal depression,au wafikili mkeo ana mwili wa CHUMA na damu ya BARAFU???ivi unaujua mziki wa kulea mtoto mchanga ww?kuamka,kulisha,kulaza,kutibu nk???
ndo nyie uwa mwatutia aibu wasomi,kazi kuklemu buku wee na mitihani basii nmnabweteka mnasahau kusoma mambo ya kijamii na familia...nyambafu umeniudhi sana apa khaaaa
anyway,kaa ongea na mkeo na utimize wajibu wako pia alaaaa!!
ITABIDI UVUMILIE TU HATA AKIFANYA NINI KWANI SI ULITAKA MWENYEWE KUOWA MSOMI? UKIOWA MSOMI NDANI YA NYUMBA UJUWE NI MWANAUME MWENZIO KWANI HUMWAMBII KITU. WANAWAKE WAPO KIBAO VIJIJINI TENA WAZURI MNO KUANZIA MAUMBO MPAKA TABIA KWA JINSI UNAVYOTAKA WEWE ILIBIDI UOWE KIJIJINI. POLE SANA MDOGO WANGU SINA MSAADA KWAKO.
ReplyDeletekwa nini wewe hukumchukua mtoto kama alikuwa analia, hata wewe humjali mtoto wako pia, mambokusaidianabwana. wote munaitaji councelling ya hali yajuu, kwani wote hamuwezikudili na watoto.
ReplyDeletemimi nilifikiri kachelewa kurudi nyumbani,au karudi kalewa kumbe ni upumbavu wa kushindwa kusaidiana kulea huyu anaonyesha ana gubu na kuhesabu vitu kila kukicha hawata fika mbali akiendelea kuwa hivi upuzii mtupu ulaya aliyo kaa yeye ipi mbona abadiliki.
ReplyDeleteStart being a team player not a spectator...in doing so you will appreciate the hardwork of bringing up a baby! the and only then can you also testify that the baby has growup and can think of making another one.Stop being a baby by running to your Mama to "show" her the problem.Be a MAN and Sort issues out with your wife.
ReplyDeleteJAMBO LA KWANZA POLE KWA TATIZO HILO UNALOKABILIANA NALO. LA PILI NATAKA NIKUFAHAMISHE NI KUWA SISI BINAADAMU TUNA MAMBO MENGI YANATUPITIA. KWAHARAKA HARA NINGEPENDA KUKUDOKEZEA HUENDA MKE WAKO KUNA KITU KIMWENDEA KWENYE KICHWA CHAKE, KINAWEZEKANA MAMBO YA KAZI, AU "KUNA PAKA FULANI ANAMZINGUA" NA MENGINEO. UKIANGALIA SASA UNA MTOTO NINGEKUSHAURI MTANGULIZE MTOTO MWANZO KWANI UZINGATIE SANA WATU WENGI HUONA SOLUTION KUMWACHA MWANAMKE NA KUANZA KUMTESA MTOTO KIAKILI. KWAKUSHAURI NDUGU YANGU VUMILIA KWANI KAMA KUNA MTU ANAYEHARIBU NDOA YENU SIMUDA UTALIFAHAMU. NA KAMA MWANAMKE AMECHOKA BASI NALO UTALIFAHAMU...LAKINI KUWA MSTAHAMILIVU. USIWASIKILIZE WATU WANOKUAMBIA MWACHE MKE MARA MOJA...DECISION YAKO YA HARAKA ISIJE IKAWA MAJUTO YAKO YA BAADAE.NA UAMUZI MZURI HAUTAKI PUPA.
ReplyDeleteNDUGU YANGU MIMI SIONI TATIZO LOLOTE HAPO KWANI NDOA NDIO JINSI ZILIVYO NA NAKUSHAURI HIVI:
ReplyDelete1.SIRI ZA NDANI YA NDOA YAKO USIMWELEZE KILA MTU KWANI SI KILA MTU ANAKUTAKIA MEMA.
2.JAMBO AMBALO UNATAKA LIFANYIKE NDANI YA NYUMBA KAMA HALITEKELEZWI BASI WEWE FANYA,KWANI KUBEMBELEZA MTOTO NANI KASEMA NI KAZI YAKINA MAMA TU?
3.LAZIMA UJIFUNZE TABIA YA MKEWAKO MAANA KIPINDI CHA UCHUMBA HAYO YANAPUUZWA HIVYO INATAKA MUDA.
4.MPENDE MKEO NA MWANAO.
MWANAMME MZIMAAA UVIVU TUU OVYOO!!KWANI ULIPOMUOA HUKUJUA KAMA MTOTO WA KIGOGO MBONA UMEMUOA!!???MIMBA AKUBEEE!!KAZI AFANYEE !!HATA KULALA ASILALE DUU HIZI NDOA MBONA ZINA MAMBOO 'HII SIO NDOA UTUMWAA!!BE RESPONSIBLE NA MWANAO!!MBONA MKEO HAKULALAMIKA KWA MICHUZI KUWA MIMBA KASHIKA YEYE MIEZI 9 YOTEE AU ULIMSAIDIA KUBEBA ANGALAU MIEZI 2??!!OVYOO KAMA MCHUZI WA JOGOO!!!KWELI EDUCATION DOESNT MAKE SOMEONE WISE!!
ReplyDeletePole Mdau,
ReplyDeleteNdoa ina mengi ndo maana wahenga wakasema ndoa ndoano,mikingamo ni mingi ndani ya ndoa,inahitaji uvumilivu na subira,juu ya yote mawasiliano chanya baina yenu wawili.
Ninachoona mimi ni kuwa kunatatizo na kunakiri tamaduni zinazopelekea kuakisi tabia mpya miongoni mwa wanajamii hasa wasomi waliopata elimu ya juu (kimagharibi) either hapa nyumbani au ughaibuni,lakini yote ni yote mume atabaki kuwa mume na mke kuwa mke,hata vitabu vya dini vinasema hivyo.Tatizo lako na mkeo linaweza jitokeza kama tabia yake ya kuzaliwa au kuakisi (kuiga)inawezekana kwao watoto ulelewa na yaya au kama zilivyofamilia nyingi za kiafrika bibi yake na mama mtoto au baba ya mtoto,tunaona watu wa ughaibuni utuma nauli mabibi waende kusaidia kazi za kulea,hivyo ulezi sio jukumu lake pekee,ni kazi ngumu jaribu kukaa chini na kujadili hili na mkeo.Kuacha mtoto kwa HG sio shida kama HG nae sio mtoto,na ana uzoefu wa kulea mtoto,vinginevyo mtoto atakuwa na utapiamlo(ama wa uzito pungufu and zaidi ya umri wake)
Tatizo lingine linaweza kuwa ni lake binafsi,ni mtu asiye na upendo(watu hushangaa mama hana upendo/uchungu na mwanae?),hii utokea iwapo mama hakuwa tayari kulea familia na mimba ilijitokeza bila kutegemea kama zilivyo nyingi Tanzania,au kwa asili nafsi yake uchagua wa kumpenda hivyo basi jaribu kusaidiana nae kumjenga kisaikolojia,mpe msaada zaidi,msaidie kubeba mtoto,kucheza na mtoto,kumlisha,kubadili nguo na nepi,kumuimbia,na kuamka usiku kutoa msaada (acha kukoroma)hili litamvutia mkeo na polepole ataanza kuonyesha kujali huko unakotaka wewe. Pia rudi nyumbani mapema.Ni hayo tu,
Mdau
KKK
Umeoa mtoto wa kigogo/tajiri naomba ujiulize swali lifuatalo, Malezi yake yalikuwaje?
ReplyDeleteHousegirl mmoja, shambaboy mmoja, chakula kupikiwa, nyumba kuoshewa, nguo kufuliwa, usafiri kila mahali mpaka mlangoni, chumba chake binafsi maisha private mambo ya extended ndugu ndugu hakuna, starehe mbalimbali. Kama alijiweza alikwenda shule mpaka Ulaya and with connections sasa atakuwa na kazi nzuri.
Sasa swali langu kwako ni wewe ulitegemeaje?
Ndugu yangu kuna kuna dini hua inadiscourage sana wanawake kufanya kazi, haswa kazi za proff na zenye majukumu makubwa, lakini huonekana ni ya ubaguzi na unyanyasaji! point hapa ni kuwa huwezi kupata malezi mazuri kwa familia yako kama my wife wako atakuwa na majukumu mazito na kipato kizuri. itabidi kila kitu mlipie, mpaka mtu wa kumpa mapenzi na malezi bora mtoto. na hiyo ndio bacground ya mke wako. kupanga ni kuchakua, akili kichwani mwako kaka! wasikudangaje na kuiga maisha ya kimagharibi, hayafanyikazi africa hilo wanalijua, sana sana waafrika wenzako watakuona umechanyikiwa. Kusema yaliyo moyoni kuna saidia kupunguza stress, usiogope kuongea uko sawa!
ReplyDeleteMkatoliki mwenzangu ndoa ni msalaba na kwa wakatoliki kuacha/divorce huwa si jibu la kwanza bali ni la mwisho.
ReplyDeleteVilema na tabia mbaya zote za mwenza wako ni misalaba hivyo beba vyema machungu na mabaya yote.
Bado uliyoyasema hayakatishi tamaa na nashukuru wengi wamekujibu kitaalam ila sana ikiwamo ugonjwa-depression nk.
Huna tatizo kaka wenzako tunafumani kila leo na tunavumilia kaka. Omba mungu akujalie wingi wa busara na ageuze mambo yote ikiwamo psychological problems yasiwepo bali kuwe na amani ktk ndoa yako.
Mungu yuko nawe ukimuhitaji na sala ndio dawa na wala sio ushauri wa mtu wala wa watu ila rekebishaneni wenyewe taratibu
Nilipigia vita kuoa mtoto wa kigogo ama tajiri kutokana na inferiority complex ambayo inawezekana inakuumiza vibaya na kumuona mkeo analinga kutokana na hilo.
ReplyDeleteThey are petty and minor problems hasa kwa mtatoliki ambaye ni askali mwenye moyo mgumu na mvumilivu kama kuta za Roma
Mke wako si mkosefu hivyo wa kumwacha
Beba msalaba-kufa na kuzikana
nyoooo mnakimbilia kuoa tu,hamjui ndoa ngumu?ulitaka mtoto alee peke yake yake?msaidie mkeo mtoto anachosha.
ReplyDeletemimi ni single mother nimeyaona hayo mtoto anaweza kukufanya uwe chizi km huna wa kukusaidia,usiku unakesha asbh kazini muda wa kupumzika huna unajikuta hata huyo mtoto unamchukia msaidie kulea uone kama atamchukia.
wengine manoa kama fasheni sio?
ukishindwa kupika basi unaoa fasta ili upate mpishi,ukishindwa kufanya kazi kujifulia unakimbilia kuoa upate wakukupikia unakuwa hujaangalia faida na hasara za ndoa.
jamani huyo mwanamke kanisikitisha sana ,watu wanatafuta watoto na mapenzi ya mama kwa mtoto huwa makubwa sana hata ukimsikia analia wewe roho inaumia ,huyu mwenzetu vip ? utadhani mama wa kambo?
ReplyDeleteomba mungu akufungulie hili janga pole sana
na hiyo dharau kwa mama mkwe matatizo
Jey
mi nashauri umuoe huyo house girl kama unaona analea mtoto vizuri kuliko mama yake. au uoe ndugu zako ambao ni maskini ili wakuheshimu. na kama unaona vipi ishi na mama yako. simple. ila nafikiri unahitaji ushauri nasaha manake unajaribu kulinganisha vitu ambavyo havihusiani. mama, wife, house girl! u r crazy.
ReplyDeleteNdugu yangu, umesema nyie wote ni wakatoliki, maana yake ni wakristo. Hukusoma kwenye Biblia kuwa 'mume mmoja na mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe?'
ReplyDeleteIsitoshe, sioni sabababu yoyote yenye uzito hadi ufukirie kuachana.
Kumbuka, mlipopendana na kuamua kuoana mlijadiliana na kuridhiana, vipi leo mshindwe kujadiliana?
Pia nikueleze ndugu yangu, katika mambo ya ndoa, jitahidi kutafuta suluhisho wewe mwenyewe, usisikilize sana ushauri wa watu, kwani wengine hawana nia njema, wanapenda sana kuwaona mkigombana na hata kufurahia kuona mkiachana. Chunga nasa.
mkeo anakupenada, na ndiyo maana alikubali kubeba mimba miezi tisa na hatimaye kufika kujifungua. Hilo unalofikiria kuwa hana mapenzi na mtoto ni fikra potofu. Usidhani mchezo ndugu, waswahili walisema kuwa kuzaa ni rahisi sana kazi ni kulea. Katika kulea kuna stress nyingi sana. Usipokuwa makini na kuwa na busara unaweza kukufuru kuwa kwa nini mpepata mtoto. Jitahidini kulea zawadi mliyopewa na MUNGU.
Kuhusu mapenzi na watu katika familia yako, hilo linazungumzika, lisiwafanye kuachana kwa sababu ya mtu ambaye yupo nje ya ndoa yenu.
Kumbuka maneno ya kutoka katika Biblia "mume atawaacha wazazi wake, ataambatana na mke wake, nao watakuwa mwili mmoja, si wawili tena, bali mwili mmoja"
Zingaitia haya na ndoa yako nakuhakikishia itadumu kinyume na washauri wanaokupoteza kuwa utengane na mkeo. Maana hakuna mwenye haki kutamka kuachana, kwani katika kitabu kitakatifu hakuna kuachana bali ni kutengana. hivyo usirubuniwe ukashawishika kutengana na mkeo.
Nakupa siri (KUMBUKA SIKU YENU YA KWANZA ILIKUWAJE? HEBU RECALL JINZI ULIVYOCHANGAMKA. DAIMA KUMBUKA SIKU HIYO, UTAONA HAKUNA SABABU YA KUTENGANA) Haya mengine ni mapito kuelekea kukua na kukomaa kwa ndoa.
Ni mimi Mshauri mwema