Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (kulia), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika dina la mchana liliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi (wa pili kulia) kwa ajili ya walemavu na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, akiwaongoza viongozi wengine kupakua chakula, leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum
Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, akisevu dina la mchana alilowaandalia watu wenye ulemavu leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Wengine wanaotoa huduma naye walioshika sahani za vyakula nyuma yake ni Bi. Joyce Mhavile, Mkurugenzi wa ITV (kapelo nyekundu) na Kiondo Mshana Mkurugenzi wa Guardian Newspapers.

Msanii Khalid Mohamed 'TID', akitumbuiza katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi kwa ajili ya watu wenye ulamavu, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.
Wasanii wa kikundi cha TMK Family akitumbuiza katika hafla ya hiyo wakiwa na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. mgosi wa kayaJanuary 17, 2010

    well done Mr.Mengi tunatumaini watu wengine wenye uwezo wataiga mfano huu

    ReplyDelete
  2. Very well done bwana mengi hata mungu anakuzidishia mara dufu kwa hilo tu! maana kuna watu umewavusha maisha kwa siku hii ya leo kwa tukio hilo. maoni yangu next year fanya sehemu nyingine ikiwezekana vijijini waliko uliwa maalbino. Watu wale chakula na dua kwa madhehebu yoote na tumbuizo za ngoma za kienyeji na pengine toka kwa walemavu wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Anafanya jambo jema sana, ni mfano mzuri wa kuigwa! Keep it up Mengi huo ni uungwana na Mungu atakujaalia!!

    ReplyDelete
  4. mfano wa kuigwa

    ReplyDelete
  5. UNAFIKI KWA MUNGU. Juzi amewafukuza wafanyakazi watzanzania zaidi ya 100 kutoka IPPMEDIA bila hatia yoyote, halafu leo anatupiga changa la macho na lunch ya walemavu, nadhani ndiyo maana JK alishtukia akaingia mtini. Aibu kubwa.

    ReplyDelete
  6. kip it up mr.Mengi mfano wa kuigwa hata kama we fisadi lakini fisadi unaekula na wenzio, ua great.
    hata kama amefukuza watu yupo kazini watz hatupo makini kazini, usihisishe mambo ya kzi na msaada,hata Mungu anajua kila mtu atamhukumu vipi, we subiri hukumu yako usiangalie ya mwenzio.

    ReplyDelete
  7. safi sana bwana mengi mungu akuzidishie

    ReplyDelete
  8. MUNGU akubariki Ndugu yetu ,Mzee wetu Mengi endelea na moyo wa upendo kama huo,achana na kelele za MAFISADI ,tunajua mchango wako kwetu sisi watanzania ,wewe ni MZALENDO HALISI,tunakuahidi mzee wetu kuwa TUNAKUPENDA na tunakuthamini kwa kila unachokinya,kutoa kwako si kwamba unacho kingi sana !la hasha! ni UPENDO uliokuwa nao kwetu
    MUNGU AKUBARIKI WEWE,FAMILIA YAKO NA SHUNGHULI ZAKO ZOTE ZA KILA SIKU

    ReplyDelete
  9. anony mon jan 18, 01:10:00 PM. hao waliofukuzwa kama wamekosewa kuna mahakama acha ku-judge ile ni kampuni binafsi na kama wameshindwa kufikisha malengo ana haki ya kuwatimua akaajiri wengine! Ndo maana unaona The Guardian leo hii imefikisha miaka 15! Ni kwa ajili ya kuzingatia hilo tuacheni siasa makazini tujifunze kutonyea mikono inayopeleka tonge tumboni! Keep it up Bwana Mengi! Wema hauwezi kuonekana leo hisoria itakuhukumu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...