Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( kulia) akimtambulisha Waziri wa Tamisemi, Celina Kombani ( kushoto) mbele ya waathirika wa mafuriko yaliyozikumba Kata nane za Wilaya ya Kilosa wanaoishi katika kambi ya muda ya shule ya Msingi Kondoa , wakazi Waziri Mkuu walipowatembelea kuwapa pole waathirika hao
Mke wa Waziri Mkuu , Mama Tunu Pinda ( wakwanza mbele) akiwasalimia waathirika wa mafuriko waliopo katika kambi ya muda ya shule ya Msingi Kondoa , juzi ( Jan 9) wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara katika Wilaya ya Kilosa kuwatembelea waathirika hao na kutoa pole.

Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa ( watatu kutoka kushoto) akizungmza jambo na Waziri wa Tamisemi, Celina Kombani ( wapili kutoka kushoto) kuhusiana na athari za kibinadamu na miundombinu kabla ya waziri Mkuu, Mizengo Pinda ( hayupo pichani) kuwahutubia waathirika wa mafuriko waliopo kwenye kambi ya muda ya shule ya Msingi Kondoa juzi ( Jan 9), wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omary Chambo.
juu na chini ni sehemu ya kambi ya muda ya waathirika wa mafuriko kilosa






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Candid ScopeJanuary 10, 2010

    Mheshimiwa Nanihi, nashangaa kuona viongozi waendao kutembelea sehemu ya nafuriko Kilosa wanatanguliza kwanza kuandaliwa sehemu ya kukaa kwa starehe wakati waadhirika wanalala chini kwenye matope na mvua hii. Bado tuko mbali sana kwani kutembelea sehemu kama hiyo kwa viongozi ni shauri ya ratiba. Nilishuhudia Bush alipotembelea waadhirika huko Luisiana kasimama na kutembelea bila kuandaliwa viti na meza zilizotandikwa vitambaa.
    Nimeshuhudia wakubwa wanaposhiriki kupanda miti wanavaa suti na tai wakati wanaenda mashambani wanakotakiwa kushiriki kwa vitendo. Halafu wanatandikiwa mkeka au karatasi wasichafuke.
    Mbona bushi alipoenda kuwaona masai kule Arusha alivaa jinsi hapo wakubwa mpo?????????????

    ReplyDelete
  2. I like the simplicity of the scene in pic 1, good guys!!

    Poleni wana Kilosa.

    ReplyDelete
  3. Reading London UKJanuary 10, 2010

    hivi kaka michuzi nikiwaandikia barua hawa refugees wataipataje hapo mimi mdau ninaishi reading london uk.

    ReplyDelete
  4. KAMA ITIFAKI(PROTOCAL ILIVYO ) IMEENDA SAHIHI KABISA AMEBAKIA RAISI TU KWENDA KUTOA POLE. WALE WAVIZIAJI WA KISIASA (POLITICAL SNIPERS) WALIOLALAMIKA KWANINI RAIS HAJAENDA HUKU KWANZA HII NDIO THIBITISHO LA ITIFAKI.

    ReplyDelete
  5. wewe candida huna hoja mnyonge myongeni haki yake mpeni hawa viongozi wamejitahidi vya kutosha kuwapatia hifadhi na huduma za dawa, ukianagalia hata hiyo sehemu walipo ni kambi ya waathirika na sio jumba la mikutano.., wewe ulitaka waandaliwe mkeka? wakati mazungumzo yalizidi masaa mawili? umeshasema bush marecani ,sio tz . mlosa wa kweli ugaibuni

    ReplyDelete
  6. mzee pinda kwa kweli unanigusa kwa ukarimu wako ukigombea uraisi bila kupinga kura yangu nitakupa unajali Mungu hakubariki,poleni watu wa kilosa hata sisi huku UK tunafunikwa na barafu mhhh tunatani kweli nyumbani tanzania tambarare

    ReplyDelete
  7. SASA INJINIA/KATIBU MKUU HUKO KWENYE MAAFA UNAGONGA SUTI YA NINI???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...