na Mike Chuma (shoto) na mgeni wao jijini Dar hivi karibuni enzi za uhai wake
Kwa masikitiko makubwa tunatangaza msiba mzito wa ndugu,mwenzetu na rafiki yetu kipenzi Clement Mwanangaya (Kile) mwenye t-shirt ya njano ya brazil pichani..
Msiba huu mzito umetokea siku ya alhamis jioni hospital ya muhimbili Daresalaam marehem alifikwa na mauti hayo baada ya kuugua malaria kali kwa siku chache tu zilizopita
Tunaungana na familia ya marehemu, Sinza stars FC ambayo marehem alipata kuichezea kipindi chote cha uhai wake tangia akiwa shuleni hadi mauti yalipomfika katika kipindi hiki kigumu sana cha maombolezo.
Maziko yatafanyika leo jumapili
Msiba huu mzito umetokea siku ya alhamis jioni hospital ya muhimbili Daresalaam marehem alifikwa na mauti hayo baada ya kuugua malaria kali kwa siku chache tu zilizopita
Tunaungana na familia ya marehemu, Sinza stars FC ambayo marehem alipata kuichezea kipindi chote cha uhai wake tangia akiwa shuleni hadi mauti yalipomfika katika kipindi hiki kigumu sana cha maombolezo.
Maziko yatafanyika leo jumapili
saa tisa alasiri katika makaburi ya uzuri.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA!!!
Mike Chuma
Denmark
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA!!!
Mike Chuma
Denmark



Bwana ametoa na bwana ametwaa Amen!
ReplyDeleteRest In Peace Clement Mwanangaya!!! u ll always be in our heart
Poleni sana wanafamilia. Malaria si mchezo has ikiwa sugu. Rest in eternal peace. Amen.
ReplyDeleteRIP Kile..Bwana ametwaa kilicho chake...
ReplyDeleteHabari zenu ndugu zangu?,
ReplyDeleteYes Mwanangaya Clement jana mida ya saa kumi na nusu ndiyo tumemlaza katika nyumba yake ya milele pale katika makaburi ambayo yapo karibu na kwao maeneo ya Sweet Corner maeneo ya Sinza uzuri kwa wale wanaofahamu maeneo hayo vizuri, kwa kweli hali ilikuwa ya kusikitisha sana katika msiba huo ambao ulitugusa sana familia yake na sisi pia marafiki zake kutokana na jinsi Clement ambaye wengi walimjua zaidi kwa jina la Mwanangaya, Mwanangaya alikuwa mkimya na pia tabia yake ya kuongea na kila mtu wa rika na tabia yoyote bila ubaguzi.
Kwa upande wangu nimemfahamu Mwanangaya kwa muda wa zaidi miaka 20 sasa kwa sababu alisoma darasa moja na mdogo wangu pia katika shule hiyo hiyo shule ambayo nilisoma hata mimi inajulikana kwa jina la Mugabe Primary iliyopo Sinza lakini wakati namaliza darasa la saba Mwanangaya alikuwa ndiyo anaanza darasa la kwanza hivyo huyu alikuwa ni kama mdogo wangu kwa vile hajawahi kunidharau wala sijawahi nikimsikia akigombana mtu yoyote.
Mwisho napenda kuwashukuru sana vijana wa Timu ya Sinza Stars kwa umoja wao waliouonyesha kuanzia siku mwanangaya alipoanza kuumwa mpaka siku ya jana alipolazwa kwenye nyumba ya milele hakika Sinza Stars wana upendo wa ajabu sijapata kuona na nawaomba waendelee na upendo huu isiwe tu kwa Mwanangaya pekee bali iwe pia kwa wana Sinza Stars wote.
Asanten sana na polenei wana Sinza Stars wenzangu,TUPO PAMOJA.
Mdau,
Japhet Stephen.
POLENI SANA WANA SINZA STARS NA FAMILIA
ReplyDelete