Swetu Fundikira, mtoto wa nduguye Chifu Abdallah Fundikira, yuko hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) jijini Dar alikolazwa usiku wa kuamkia leo kufuatio kipigo cha mbwa mwizi alichokipata toka kwa watu wanne, mmoja mwanamama, wanaosemekana kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi.
Habari zinasema watu wanne hao wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho wamefunguliwa mashtaka kituo cha polisi cha Oysterbay wakati uchunguzi ukiendelea. Na wao pia inasemekana wamegfungua mashitaka dhidi ya Swetu ya kufanyiwa fujo na kutukanwa.

Hivi sasa Swetu Fundikira yuko ICU hapo MOI akifanyiwa uchunguzi wa kina kutokana na kipigo hicho, ambapo uchunguzi wa awali unaonesha amevunjwa taya na uso wake hautamaniki kwa uvimbe.
Kaka wa mjeruhiwa, Ismail Fundikira, amethibitisha habari hii sasa hivi na kwamba ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika hospitali wakimuombea ndugu yao ambaye yuko katika hali mbaya sana.
Ismail hakuweza kuweka bayana chanzo cha yote hayo, akisisitiza kwamba polisi wako kazini na hawezi kuwaingilia katika uchunguzi. Hata hivyo habari zinasema sakata lilianza pale Swetu na mwenzie mmoja ambaye jina lake halijatambulika walipokuwa wakitoka dansini usiku maeneo ya Kinondoni na kujikuta wanapambana na gari ingine barabarani ambalo inasemekana liliwachomekea na kisha kusimama mbele yao na kuwaziba.
Walipotoka kujihami kwa dhana labda ni majambazi, makonde yakaanza na mwenzie alipoona wanazidiwa nguvu akakimbia kuomba msaada. Walipofika eneo la tukio wakakuta Swetu hayupo na gari la hao waliogombana nao halipo.
Baada ya kuhahah huku na kule wakapata habari kwamba Swetu yuko kituo kidogo cha Salender ambako walipokwenda wakapata habari kwamba watuhumiwa walimchukua hadi kituo cha mabasi cha Palm Beach na kuanza kumpiga. Bahati nzuri dereva wa teksi aliyekuwa anapita hapo akakimbilia kituo cha polisi cha Salender na polisi wakaja kumuokoa Swetu na kumkimbiza hospitali akiwa hoi bin taabani.
Ndugu wa Swetu wameshafungua mashtaka na watuhumiwa inasemekana wamewekwa korokoroni. Habari zingine zitafuata kadri zitavyopatikana.

tabia mbaya sana hivi walitaka kumtoa mwenzao roho kwa nini jamani hope wafungwe miaka mingi jela huu ni uonevu halafu usiku walitaka tu kumchomoa mwenzao roho Mungu awapige radi
ReplyDeletekama ni hao wanajeshi naomba wakomeshwe maana wana ubabe wa kijinga,hawana kazi wanakula bure afadhali wapelekwe afghanstan sio kuonea wananchi
ReplyDeleteWanajeshi wetu hawapatiwi mafunzo ya kuishi na raia.Wanatumia nguvu nyingi uraini kuliko akili,Waliwahi kuwampiga sakali wa usalama barabarani ili kuonesha ubabe,walimloanisha kwenye dimbwi la maji raia mmoja kwa vilile aliwapita na gari lake na kuwarushia maji yaliyochafua viatu vyao.Kwa wale mliopitia JKT mnakumbuka maafande hawa walivyokua wakichukia wasomi.Walitoboa MV Bukoba kwa kutumia nguvu nyingi physics kidogo.Sina uhakika kama wamepelekwa Kilosa kusaidia walioathirika na mafuriko kama wenzetu kule Haiti.
ReplyDeleteTanzania ni nchi isiyo na sheria wala haki.Sheria zimeandikwa vitabuni tu.Huo unaweza kuuwawa hivi hivi tu bila ya sababu yeyote.Kama hapo mahakamani hamna haki kabisa huyo muathirika itabidi ainunue haki yake,Bullshit ndio maana niliamua kuishi nchi zilizostaarabika na zina haki,sheria na demokrasia ya kweli.
ReplyDeletepoleni sana,wanajeshi wa bongo wana uonevu wa kujinga hayo ndo mafunzo walioenda kujifunza huko!!hao ni wa kufungwa tu hawana hata nyuso za haya!mnaenda kumpiga mtu pasipo bila sababu jamani,nia yao walikua wamuue?jamani hebu angalia huu si uonevu loh,ok mungu atamsaidia atapona inshallah,jirani zangu swetu mungu yupo na nyinyi na wala hao watu msiwaachie kuleni nao sahani 1 mpaka kieleweke jela tu hao wasokuwa na nyuso za haya!hizo njaa zao si wakalie na serikali yao sio kuleta hasira kwenye miili ya watu loh bongo nuksi!!!!
ReplyDeleteTATIZO LA WANAJESHI WETU NI ELIMU KIDUCHU. WANADHANI UBABE NDIO UASKARI! AJAB KWEL KWELI. POLE SANA SWETU.
ReplyDeleteKUHUSU KUPELEKWA KILOSA NINA UHAKIKA WAPO, ILA KIKUBWA WALICHOFUATA NI POSHO NA SIKILIZIA BAADA YA MIEZI 18 HALAFU TEMBELEA MAENEO WALIOKUWEPO HUKO KILOSA, UTAVIKUTA VITOTO KIBAO MATUMBO WAZI. UKIULIZA HAWANA BABA. UJUE WAJESHI WESHAPITA HAPO.
watoa maoni hapo juu,p/se msikurupuke tu kwa vile labda mna access,ingependeza kama mgefikiri mnachotaka kuandika na kama kina mantiki sawa,"poleni" maana mnachokijua kinakaribia na sifuri_mpo dunia gani hadi hamjui jeshi na wajibu wake nini na ndani yake kuna nini..,ama ndiyo kejeli tuu? tafuteni habari..
ReplyDelete"soja mwenyewe"
TUSUBIRI UCHUNGUZI UFANYIKE..., LAKINI WANAJESHI WAKUMBUKE KWAMBA "MOJA" YA KAZI/KIAPO CHAO NI ULINZI WA NCHI/RAIA NA MALI ZAO...
ReplyDeleteI think the issue here is beyond kuchomekea.
ReplyDeleteFind out.
kosa walofanya hao wanajeshi ni kumpiga mtoto wa kigogo tu. kila mtanzania anajuwa namna wanajeshi wanavyotesa raia. wanajifanya kama ni nchi yao peke yao, kila siku watu wanalalamika na jinsi wanavyonyanyaswa na wanajeshi na hakuna hatuwa yeyote inayochukuliwa.
ReplyDeleteKwanza nafikiri cha msingi si kwa sababu ni mtoto wa mzee Fundikira bali ni vitendo vibaya hasa tukitegemea hawa watu ndio tuna wategemea katika kulinda usalama wa raia. Kama hata kuna kosa ambalo labda huyo kijana/vijana wamefanya basi ilitakiwa hawa askari watumie njia zinazo faa. Wangewapeleka hata polisi ili washitakiwe si kuchukua sheria mkononi. Hawa askari nafikiri hawaeliwe kama sasa tupo katika karne 21 ambapo swala la maguvu bila kutumia akiri vimepitwa na wakati. Mimi ninaomba kama wakipatikana na hatia lazima wafundishwe nizamu.
ReplyDeleteAhsanten sana
Awe mtoto wa kigogo, asiwe mtoto wa kigogo, askari wa kiafrika ndivyo tulivyo. Kumalizia hasira zetu za ugumu wa maisha kwa wananchi.
ReplyDeletemimi kama mtoto wa swetu ningependelea waachiwe tu njiani ao watu na wao wapigwe kama walivyo mpiga mwenzao, na hao sio binaadam bali ni wanyama kwani binaadam ana roho hawezi kumfanyia kitendo kama hicho binaadam mwenzie. serikali ipime kuwaachia tu ndio hapo watakapo fanya la maana lazima walipiziwe kisasi na pia hatutachoka kumuomba maulana atawachapa pia kwa fimbo yake ya mbali na apa kwa mwenyezi mungu kuwa sitochoka kumuomba nao awalipe hapa hapa dunia, habari zao tutazisikia kwamichuzi. insha allah kwa nguvu za mwenyezi watahukumiwa
ReplyDeleteI think it is time to make our leaders accountable for this kind of inhuman behavior . These people makes life miserable for a lot of citizens , including their wife and kids .These people been doing this for a long time and nothing happen to them , ministry of home affair is one of the most poorly managed institution in Tanzania,there is too much abuse of power ,from immigrations , TPDF , courts and all of it's urgency .These soldiers think that they are the law, they are god . I hope Mr Kikwete and his government will get at the bottom of this .
ReplyDeleteThose soldier need to be slapped with attempted murder , it seem they intended to kill him .I hope they will spend all their life in jail .
MTU HATA KAMA AMEKUCHOKOZA KWA MATUSI HUWEZI KUCHUKUWA SHERIA MIKONONI MWAKO KUNA VYOMBO VYA SHERIA VYA KUTAFUTA NA KUKUPA HAKI YAKO, NA HATA KAMA SEHEMU YA UCHOKOZI HUO NI KINONDONI IWEJE TENA WAMCHUKUWE NA KWENDA KUMPIGIA PALM BEACH? TAFUTENI MWANASHERIA MAKINI ILI JAMII IONYESHWE KUWA SEHEMU YA HAKI NI MAHAKAMANI SI MIKONONI MWETU
ReplyDeleteSwetu pole sana mshikaji wangu!Nakumbuka tulikuwa wote JABAL HIRA morogoro.Si na wewe ulienda CCP lakini ?ilikuwa je tena?Pole sana na mungu akupe nguvu.-Athuman-Quebec
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeletetaarifa zilizopatikana sasa hivi ni kuwa Swetu amefariki dunia.Mungu amlaze mahali pema peponi.Amina.