KONGAMANO LA KUJADILI
MAKUBALIANO YA CCM NA CUF KUFANYIKA KESHO.
Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) ya Zanzibar imeandaa kongamano la kidini la kitaifa ambalo litajadili makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa chama cha CUF.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bwana Azzan Hamdan ambaye ni Naibu Kiongozi wa Jumuiya hiyo amesema, kongamano hilo litafanyika tarehe 09.01.2010 katika ukumbi wa Suza Majestic ulioko Zanzibar.
Bwana Hamdan amesema, kongamano hilo litasindikizwa na Sala ya Ijumaa itakayofanyika tarehe 15.01.2010 katika viwanja vya Maisara ambapo dua maalum ya kuiombea Zanzibar itasomwa.
Aidha Bwana Hamdan amefafanua kuwa, JUMIKI watajitahidi kudumisha maelewano yaliyopatikana na kuhakikisha umoja na mshikamano wa Wazanzibari unakuwa wa kudumu kwa maslahi ya Wazanzibar wote.
“Tutakuwa karibu na Raisi Karume ili kumsaidia katika kuhakikisha umoja wa wanzanzibari unapatikana na watu wanaishi kwa kupendana na kushirikiana ili kujenga Zanzibar mpya,” ameongeza Bwana Hamdan.
Amesisitiza kuwa JUMIKI wako tayari kupambana na mtu yeyote atakayejaribu kuvunja msingi mzuri uliojengwa na viongozi wa CCM na CUF na watamtangaza mtu huyo kuwa ni adui wa Zanzibar na watu wake.
Vilevile Bwana Hamdan amesema kuwa, Jumuiya ya JUMIKI itaendeleza msisitizo wa kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kabla ya uchaguzi mkuu ili kujenga nguzo madhubuti ya umoja na mshikamano

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...