DENIS IMAN GEOFFREY AMBAYE ANACHEZEA CHUO KIKUU CHA GREENSBORO NORTH CALORINA AKIFANYA VITU VYAKE
WADAU WENZANGU WAPENDA SOKA, TFF NA SELIKALI YA AWAMU YA NNE.

LEO MIMI NAKUJA NA HOJA HII MPYA INAYOHUSU UENDELEZAJI WA WANASOKA WETU VIJANA ILI KUFIKIA KIWANGO CHA KIMATAIFA. TUMESHAONA KUTOKA KATIKA MATAIFA YA WENZETU KUWA SOMETIME WANAJUMUISHA WANASOKA WACHANGA ILI KUWA PROMOTE NA KUWAPA EXPOSURE.

UKIANGALIA KATIKA TIMU ZA TAIFA ZINAZOCHUANA HUKO GHANA KUNA VIJANA WENGI WANAOCHEZA KATIKA TIMU NDOGO NA COLLEGES ABROAD LAKINI MAKOCHA WAMEWAITA ILI KUWA PROMOTE. HII NJIA IMEKUWA INATUMIWA SANA NA MATAIFA YA WENZETU HASA HUKO WEST AFRICA NA SIO KUSUBIRI MPAKA MCHEZAJI AFIKE KIWANGO CHA PROFESSIONAL NDIO AITWE TAIFA STARS.


MIMI BINAFSI LEO NAPENDA KUMTUMIA KIJANA WETU DENIS IMAN GEOFFREY, AMBAYE ANACHEZEA CHUO KIKUU CHA GREENSBORO NORTH CALORINA. KWAKWELI KIJANA HUYU ANAKIPAJI KIKUBWA CHA SOKA NA ANA UWEZO MKUBWA WA KULISAIDIA TAIFA HILI KAMA AKIPEWA NAFASI. DENIS AMBAYE AMEKULIA MAISHA YAKE HUKU USA AMEAANZA KUCHEZA ORGANIZED SOKA TOKA AKIWA MDOGO YANI HIGH SCHOOL NA SASA COLLEGE NA PAMOJA NA KUCHEZA SOKA CHUONI PIA ANACHEZA SEMI PROFESSIONAL LEAGUE IJULIKANAYO KAMA PDL.


KWA KUSEMA KWELI VIJANA KAMA HAWA WANA UWEZO MZURI TU WA KUELEWA MIFUMO YA UCHEZAJI KWANI WAMESHAZOEA KUFUNDISHWA NA MAKOCHA WA KIGENI.


PILI UELEVU WAO WA LUGHA IKIWEMO ENGLISH UTASAIDIA MAKOCHA WA TAIFA STARS KWANI MIMI BINAFSI HILI NDIO NALIONA KUWA NDIO TATIZO KUBWA HASA HAPO NYUMBANI.


TATU HATA KAMA HAWATAPATA NAFASI ZA KUCHEZA NJE HIVI SASA BASI WANAWEZA KUPEWA MIKATABA MIFUPI MIFUPI NA TIMU ZA HAPO NYUMBANI PINDI WAKIWA LIKIZO HUKO MASHULENI. JE WADAU HILI MNALIONAJE??

MDAU WA MAREKANI



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Hii nipingana nayo taja wachezaji wambao wapo African cup wa Ghana wanachezea Vyuo vya Ufundi USA? kama Maximo atachaguwa mtu nje Daraja la Kwanza au Ufundi basi na hapa Tanzania afanye hivyohivyo. Kigi.

    ReplyDelete
  2. Wapumbavu bwana utawajua tuu. Mpumbavu akishindwa kufanya kitu, basi sababu yake ni "English". Tuondokee na english yako hapa.

    ReplyDelete
  3. Huyu ni Mmarekani mwenye asili ya Kitanzania. Nchi yetu haina dual citizenship kwa hiyo hawezi chezea TAIFA STARS

    ReplyDelete
  4. jamani huyu jamaa ameomba mtoe mawazo yenu na sio kuponda,ufike wakati tujiheshimu jama,na ndio maana hatuendelei kwa kung'ang'ania ubishi na kuukataa ukweli,huu muda ni wa kuukubali ukweli na mageuzi kwenye soka letu jaman,wakati wa tanzania ndio huu kufanya mageuzi ya soka...mdau Ommie Jr from M

    ReplyDelete
  5. Wazo la kutumia wanamichezo wetu walio nje ya nchi ni wazo nzuri,lakini mtowa wazo kafirisika kwa kufikiri lugha ya kiingereza ndiyo ya kufundishia! Je vjana wetu walio nchi zisizotumia kiingereza wasipewe nafasi hiyo? Elewa kuwa makocha wengi maarufu hawaongei kiingereza na wengi wao wanafundisha hata hizo timu za uingereza kwa lugha yao.Hata huyo kocha Maximo anaongea zaidi kireno,kuliko kiingereza.Hivyo basi mtoa hoja,usitumie uelewa wa kiingereza ndicho kigezo cha wanamichezo wetu kuwa rahisi kufundishika.Pia ili mwanamichezo ajulikane inabidi awe ameonyesha uwezo na kuonekana na wengi kuwa anaweza.Pia pawe na uwezekano wa kumtangaza huko nyumbani ili makocha waweze kutathimini uchezaji wake kabla yakumwita kwenye timu."Narudia tena kiingereza kisiwe kigezo"

    ReplyDelete
  6. Ankal mi naomba usinibanie maoni yangu. Kwanza napenda kumpongeza mdau kwa juhudi anazofanya za kutuchimbulia vipaji vyetu vya kitanzania kokote vilipo. Mi nadhani moyo kama huu ndio unatakiwa kwa Watanzania wote kwani tukisubiri watu wengine watutafutie basi kila siku tutabakia wasindikizaji. Pili nampongeza kijana Denis kwa mafanikio haya aliyofikia ila asife moyo kwani safari bado anayo ndefu. Kwa mdau wa kwanza hapo juu naamini ni Kigi Makassy au metumia jina tu usimkunjie bwana mdogo! Wewe kama mpira umekushinda basi usiogope kunyang'anywa number!!We si unakimbia kimbia tu uwanjani acha wenzio waje wakuonyeshe mpira! Forward gani ufungi goli mpaka mcheze na Mauritius?? Sasa nakujibu jibu lako kiufundi: kuhusu Maximo kuchagua wachezaji toka vyuoni kwa huko Nyumbani haliwezekani kwani hakuna utaratibu bora wa michuoano ya vyuo kama huku USA. Mashindano ya Vyuo huko nyumbani ni kama kupast time na sio competative games. na kama ulishapata muda kwenda kuangalia utaona vyuo vinakodisha majeshi na sio wanavyuo wanaocheza. Pili kwa ninavyofahamu mimi ligi ya soka ya MLS haina daraja la pili kwa hiyo daraja la pili unaweza kusema ni timu za vyuo. Timu zote za MLS zinatoa wachezaji toka timu za vyuo kwa hiyo nadhani unaweza kuona kuwa level aliyokuwapo Kijana sio ya chini.
    Tukija kwa Mdau wa kiingereza wewe ndio wale wale waliokuwa wanamtukana kijana Thabit enzi hizo! Mara hawezi mara nini lakini mlivyoanza kuona kuwa anakaribia kumake NBA mkaanza kwenda na mabendera yenu "Wanafiki wakubwa". Leo kila mtu anajifanya rafiki. Watanzania tuache tabia ya unafiki na tujifunze tabia ya kuringia chetu wenyewe tusisubiri mpaka Mzungu akithamini na sisi ndio tunajifanya kukibabaikia! Kama wewe mpira umeshakushinda endelea kubeba boksi kaka ukimaliza mnakutana Baa mnakata kilauri mitumbo imefumuka kama pipa na ndio maana taifa halifanikiwi katika michezo. Mnachojua nyie nyinyi ni ngono tu na bia! Acha dogo aendeleze kipaji!!
    Mdau wa tatu nani kakuambia kama dogo anahitaji Dual Citizenship?? Acha kupayuka na kukurupuka kama kidampa! Dogo hana citizenship bado ana ganda la kijani tu kwa hiyo bado ana urahia wa Bongo!!
    Mwisho napennda kutoa pongezi kwa mdau kwa moyo huo natumai wabongo wote tutajifunza kuvitambua vipaji vyetu kokote vilipo!!

    ReplyDelete
  7. We anony wa hapo juuu inaonekana uelewa wako ni mdogo.Muandishi ameandiga habari vizuri sana nami namuunga mkona.Lugha ni kizingiti kwa wachezaji wetu wa bongo. angalia Maximo anavyo pata tabu kufundisha hadi awe na mkalimani.Unafikili kuna teamitakuchukua kama wewe hujui lugha...? you have to be extrimly good yaani kama PELE,otherwise,hakuna coach atakaye kuchukua kama kuna mchezajeji anacheza level moja na wewe na anajua lugha. language counts.Angalia Nonda shabaani, unafikili alikua mzuri kuliko mmachinga au lunyamila au Muso. aiweza kuzungumza kifarance kwa hiyo ilirahisisha comunication. kunamchezaji wa stars anaweza kuongea france au kingereza proficint?Itakuwa ngumu....

    ReplyDelete
  8. HIVI NI KIASI GANI SISI HATUJUI KUTENGANISHA PUMBA NA MCHELE! WATANZANIA LAZIMA TUJU KUWA UNAPOSOMA NDANI YA NCHI YOYOTE ILE BASI UNATAKIWA USHIRIKI KWENYE SHUGHULI ZOTE NCHINI HUMO. TANZANIA WAPO WANAFUNZI WENGI TU TOKA NCHI MBALIMBALI WANACHEZA MPIRA HAPA HAO HATUWEZI KUSEMA WANAFANYA VITU VYAO HAPA. ILI AWEZE KUITWA KUWA ANAFANYA VITU VYAKE HUKO BASI LAZIMA AFANYE KAMA HASHEEM NA SI KUPIGA PICHA UNACHEZA NA WAZUNGU KISHA UNATUAMBIA UNAFANYA VITU VYAKO, KUCHEZA MPIRA NA WAZEE WA KIZUNGU SI KIPIMO CHA UJUZI WA KUCHEZA MPIRA.

    ReplyDelete
  9. Nafikiri tuache ushamba wa kuongea bila ya kufikiri kama watu wengi walivyo nyumbani.Kwanza upeo wa kuelewa kwa baadhi ya watu ni kutokana na malezi ya jinsi gani ya kufikiri kabla ya kuongea, ili uepuke kutwanga pumba. Swala la kumchagua huyu kijana kwenye timu ya taifa ni bora na zuri kwa sababu leo hii akichukuliwa na timu za ulaya na akawa nyota mtaendelea kusema hizo pumba kuwa hatuna dual au hajazoea mpira wa nyumbani? Je, akikata kuchezea timu ya taifa wakati huo akiwa nacheza nje mtamuitaje? Nawaombeni ndugu zangu muache mawazo finyu na kuweni makini na werevu katika kuchangia mambo.Pia tukumbuke kuwa sio kila mtu anaweza kucheza mpira ndio maana wachache sana wanabarikiwa kuwa na kiwango cha hali ya juu kuliko wengine. Nafikiri wanaopinga hoja hii kazi yao ni kushika jezi kuanzia utotoni hadi ukubwani. Wenu Mwanasoka mkwonge.

    ReplyDelete
  10. Mawazo ya wengi ni ya jaziba sijui ni kwanini hii nchi mmeichukia kiasi hicho.
    kijana aliyekulia USA naona ni vigumu kukubali kuja kuishi hapa kwa mategemeo ya kucheza mpira. Huyo anayesoma naona mpira kwake ni kujifurahisha na kwa sababu anauweza na kuupenda anacheza akiwa na nafasi, swala la kuacha chuo aje huku kucheza mpira hata angekuwa ndugu yako sijui kama mngemshauri hivyo. Kuna vijana wengi hata hapa Bongo wamecheza sana mpira hata club kubwa zikawanyemelea lakini ilipofikia shule walichagua shule.
    Mimi sina taarifa nzuri lakini tufikiri hata hao professional players wa nje wangapi wameenda shule??
    Mie naona shule na Mpira wa miguu vinachengana. Michezo mingine sawa.
    NAWASILISHA

    ReplyDelete
  11. ANON JAN 18 05:50:00 YOU'RE RIGHT MAN, BIG UP??

    THAT PROBLEM IS THERE, PEOPLE JUMPING ON THINGS!!

    ReplyDelete
  12. WACHEZAJI WANGAPI WANA E-MAIL ADRESS LIGI KUU TZA AU TAIFA STARS?

    ReplyDelete
  13. Kipaji nyumbani cha mpira kipo. Kinachomiss sana ni the "tactical aspect" of the game. Asilimia kubwa sana ya wachezaji professinal wa marekani walipitia college. Ndio system yao ilivyo, unaenda huko unakuwa drafted. Basketball, football, Soccer n.k.

    Scholarship za mpira wa miguu zipo, sema kuna minimum requiriements na hapo swala la lugha (english) ni muhimu maana bila hio minimum requirments kuingia chuo kwa scholarship is near impossible labda uwe na maradona type skills.

    Ligi ya marekani inakuwa kila siku, na asilimia kubwa ya wachezaji wake inawatoa kwenye hio draft ya mashule.

    kwahio kama sisi tungejitahidi kuwapigisha vijana wetu (secondary school) wenye talent ya mpira brush ya kitabu kidogo(english) ukweli ni tunawapa nafasi kidogo ya kuomba na kupata scholarshp ya mpira.

    Sasa wakitoka college kama ni wazuri wakaenda ligi ya marekani, bado sisi kama nchi tutafaidika maana ingawa the technical aspect of the game sio ya juu the tactical aspect is very high (much higher than uarabuni au even 3rd division za ligi za ulaya).

    Bado kama Tanzania tutanufaika. Nani kasema kunafaika kwetu ni mpaka mtu achezee Taifa Stars mwishoni? Kijana akiweza kupata scholarship ya shule kwa mpira, hapo kama nchi tumenufaika.

    Kama kawaida yetu badala ya kujengea kwa juu kile madu alichokileta kwa kuongeza vinginevyo vinavyoweza kutusogeza mbele, tunakimbilia kuponda kipande hiki au kile. Kazi tunayo.

    ReplyDelete
  14. kiingereza ingekuwa ndiyo kizingiti kama "stupid" wetu humu wanavyosema, basi arsenal ingekuwa imeshashuka daraja tangu miaka 8 iliyopita.

    ReplyDelete
  15. Kuwa mwanachuo, ukacheza mpira na kutoka kwenye local paper ni kitu cha kawaida sana duniani kote. Kufanya vitu vyako katika michezo ya mikondo, mabweni and baina ya vyuo ni mambo ambayo yamekuwepo siku zote. Wapo wachezaji walioibuka kutoka humo na wapo wengi (kama mimi) tuliopita humo na kuishia njiani. Mchezaji wa taifa huchaguliwa kwa viwango ambavyo meneja ameviweka na anakubaliana navyo. Mfano, Brazil, Italia, Ujerumani hawawezi kuchezesha timu ya taifa mtu anayecheza daraja la pili ligi ya Ulaya au daraja la kwanza Dubai au Afrika ya Kusini - lakini sisi na nchi nyingine tunaweza. Kama nitampigia debe mchezaji wa chuo kikuu Amerika asiye na timu ya daraja japo la pili, nitakuwa na wazimu. Wazimu wangu unaweza kuonekana mdogo iwapo nitampigia debe achezeaye chuo kikuu cha Rio de Janeiro ambaye kwa uhakika atakuwa na timu ya kueleweka.

    Neno nje ya nchi lisiwe lulu na lisipoteze lengo la timu.

    ReplyDelete
  16. Ahsanteni Wadau! Tatizo la mliochangia humu hamjui hata kuicheza hiyo soka ila ni washabiki wa soka! Lililoko hapa sio tu kuwa kijana anacheza Chuo bali kijana ana Kipaji kikubwa na cha kutisha! Mimi mwenyewe nimemuona huyu kijana akicheza Walivyokuja Houston. Ana potential kubwa na ndio maana mdau akaamua kumuanika. Na hakika kuna vijana wengi wakitanzania wanacheza mpira vyuoni lakini hiyo sio sababu hapa ila sababu ni kipaji cha ajabu alichonacho kijana Denis. Kwa mpira anaocheza kama angekuwa huko nyumbani na hakika angekuwa gumzo katika magazeti huko nyumbani. Angalia wenzetu waliondelea pindi waonapo kipaji huwa wanakiendeleza na hakuna formula kuwa mchezaji mpaka awe na timu ndio achezee timu ya Taifa. Kumbuka Ronaldo aliitwa timu ya Taifa Brazil akiwa anamika 17 ingawa hakucheza lakini walishamuona kuwa dogo ana potential. Kwa ninvyoelewa mimi kijana Denis ana uwezo mkubwa ila kwa Chuo anachochezea na mizengwe mingine ataishia porini tu sasa ni kazi yetu sisi Watanzania tukiona kitu ambacho labda kinafaida kwetu tukiendeleze. Kwani kumbuka kuna wachezaji wengi wanauwezo wa kucheza professional league or hata NBA lakini labda hawakuonekana au walikuwa katika wrong places kama kijana wetu hapa!! Na hiyo sio kwa sababu yuko nje la hasha! hata kama kuna vipaji kama hivi hapo nyumbani lakini bado viko mchangani basi uanzishwe utaratibu wa kuvifanyia majaribio na sio tusuiri mpaka eti afike Yanga au Simba. Acheni ukiritimba wenu kuchezea Yanga au Simba sio kwamba mtu anajua soka kuliko mchezaji wa mchangani!! Tuamke washikaji wakati wa mizengwe umeshakwisha tusipokuwa na machungu na chetu sijui kama Mbrazil ataweza! Sisi kama Watanzania ndio kazi yetu tukiona kipaji kokote kilipo ni wajibu wetu kuki scout! Wenzetu wa Magharibi walishaanza hili long time na mnaona matunda yao! Ukiangalia timu zao zimejaa Watoto wengine wa Wachezaji wakubwa ambao waliwazalia nje ya nchi na sasa wananufaika nao!! Sisi tutabakia jerous tuuu ....ah huyu akifanikiwa mimi nitaonekana mjinga... acha ufala!! Tuamke!!

    ReplyDelete
  17. mimi bado nipo kwenye lugha na nasisitiza wewe na kiswahili chako kama hujui kingereza au kifaransa itakuwa ngumu kupata team. COMUNICATION IS THE KEY. Ngasa kaishia wapi? lunyamila? china? hawataki kutuambia ukweli hao.kamahujui international language you have to be PELE au Maradona kupata team ambayo itakuwekea mkalimani na kumlipa lakini kama unacheza kama Nizar, pawasa, au haroona moshi hakuna eam itakubali kuingia gharama ya kuhire mkalimani kwa ajili yako. acheni upumbavu sisitizieni wachezaji waende shule. asilimia kubwa ya wachezaji bongo ni darasa la saba na form four. unafikili std 7 anaweza fundishika? pumbafu. Denis anaadvantage kuliko wachezaji wa bongo. he onlyt needs national team experience... ili atengeneze CV au resyme for tryout.

    ReplyDelete
  18. Kuna watoto wengi wanakipiga mchangani kuliko huyo anayecheza college za wazungu. Kuna waziri mmoja alishawahi kusema mtoto wangu shule Tanzania ni wa mwisho lakini akienda Marekani anakuwa wa kwanza.

    ReplyDelete
  19. SOKA NA SKULI BONGO WAPI NA WAPI SI MNAONA ALLY MAYAI TEMBELE KAACHA SOKA SIO KWAMBA KIWANGO KILISHUKA BALI ALIANGALIA KWA KINA KIPI BORA KWA BONGO NDIO MAANA AKAACHANA NA SOKA LA BONGO SASA HUYO ANASAKA NONDOZZZZZZZZZZZZ

    ReplyDelete
  20. Na mie nacheza mchangani hapa westbourne park chini ya flyover jijini london, TFF Tanzania na Maximo mnitumie tiketi nije chezea Taifa stars.

    Mdau
    Wamchngani
    Jijini London

    ReplyDelete
  21. Mdau wa Jan 18, 6:07 Pm. Tatizo sio kukipiga hapa ILA ni kukipiga na kucheza Organized soccer! Tatizo ni kwamba hujui College hapa USA zina timu zilizokuwa organized kuliko hiyi Simba na Yanga. Yani kiakili mchezaji anakuwa yupo katika mfumo wa ki professional zaidi ya hao Yanga na Simba unaowajua wewe. Na huyo Waziri wako aliyema hivyo nae Kihiyo tu, tatizo sio urahisi wa masomo bali ni Ufanisi na Miundo mbinu ianayofanya masomo yawe rahisi huku. Wewe hapo UD computer moja tu wakati huku kila mwanafunzi ana lap top yake sasa unategemea wanafunzi wasifauru!! Acha kuchemka!!

    ReplyDelete
  22. Andrey Arshavin aliulizwa, "jee unasumbuliwa unapokosolewa na washabiki au vyombo vya habari?"

    Jibu lake akajibu "Huwa sijui kama nalaumiwa kwa sababu sielewi kinachoandikwa gazetini na wala nikiagalia TV sielewi kinachozungumzwa".

    Halafu wewe stupid unayesema kama hujui kiingereza hupati timu.

    ReplyDelete
  23. Wewe mdau wa 04:18 kungekuwa na tofauti gani kama wachangiaji wangekuwa wachezaji wa mpira wa kulipwa? Hakuna aliyesema kuwa mchezaji lazima awe Yanga au Simba. Ronaldo aliitwa kijana mdogo lakini alikuwa na timu, Diego Maradona alikuwa mdogo zaidi lakini alikuwa Boca Junior. Kwa nini unataka watu waamini kauli yako kwa sababu umemwona akicheza? Narudia kuwa hapana anayesema kuwa hafai timu ya Taifa, lakini naamini hata wewe ungekuwa kocha wa taifa usingechagua wachezaji kwa kampeni za Facebook na kadhalika. Kama kweli anastahili kuchezea Stars au hata timu ya US - time will tell. Kama ana kipaji kikubwa na kikapotea, there must be a problem. Nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji academies hususan kwa vipaji vya nyumbani, lakini kwa vipaji vilivyo katika nchi nyingine sidhani kama TFF itakuwa na resources za kutosha kuvi0scout vyote.

    ReplyDelete
  24. Inabidi tujifunze kuthamini na kuamini vya kwetu watanzania.Pamoja na huyo kijana, kuna kocha maarufu mtanzania yuko Ottawa-JOHN KALONGA.Anaheshimika mno kule, kwa ku scout vijana, but sidhani hata kama Tanzania wanalijua hilo.Hayo ndio mambo ya kufuatilia ili kukuza vyetu badala ya kukaa kushangilia akina Drobga kila siku.
    Lini tutashangilia vya kwetu?

    ReplyDelete
  25. OYA WABONGO ACHENI CHUKI ZENI SIZIZO NA MPANGO! KWANI TATIZO NINI AKIITWA ASIITWE?? NI TIMU YA TAIFA KWAHIYO KILA MTU ANA HAKI YA KUCHEZEA HATA KAMA NYIE MNAUJUA OMBENI TU MTAPEWA. DOGO KAMA ANJIAMINI BASI APEWE MAJARIBIO. SI TULISHAONA WAKINA MIKE CHUMA NA WENGINE WENGI WALIITWA NA KUCHEZA?? SASA MIMI SIONI SABABU YA KUPIGIZANA KELELE HUMU WAKATI HII NI TIMU YA KILA MTANZANIA KAMA KIPAJI UNACHO WE SONGA MABELE KAWAKILISHE TAIFA SIO KUMBANIA DOGO HUMU!! WAPUMBAVU SANA NYIE MNAPIGA KELELE UTADHANI TIMU YENYEWE IMEKUWA BRAZIL KUMBE NI KITIMU CHA CHALLENGE TU HUKO AFRIKA MASHARIKI. MI NADHANI MDAU ALICHOFANYA SI KIBAYA SOTE TUNAJUA NCHI YETU INA TATIZO LA WAFUNGAJI WATU WANAKIMBIA KIMBIA TUUU!! NA MAXIMO ALISHWATUKANA NA KUSEMA KATAFUTA NCHI NZIMA HAKUONA FORWARD SASA KAMA WAKO NJE SI BORA WAPEWE KIPAUMBELE?? AU MANATAKA KILA SIKU TUFURAHIE HUO USHINDI WA 0-1? ""dah ..leo hatujafungwa mengi""?? Masikini rahisi wenu sijui lini atashika jezi ya Mchezaji kama Denis badala ya Drobda?? Ghalagha bao wote kwa chuki zisizo na mpango!!

    ReplyDelete
  26. Madu wa 12:39 Usitake kufananisha Mtu anaeongea kirusi au kifaransa na Kiswahili. Kumbuka kuwa any professional clu ni organisation kubwa kwa hiyo ni rahis kumpata mtu mmoja anaeongea lugha moja kata ya lugha kuu saba na sio kiswahili. Kitu kingine kinachowaangusha wachezaji wetu ni umbumbumbu na sio lugha pekee!! Hii inamfanya manager wa timu akose confidence nae!!
    Mdau 2:31 na kataa hakuna sheria kuwa mchezaji lazima awe na timu ndio aliwakilishe taifa! Of corse mpaka kuitwa mchezaji basi ana timu hata kama sio professional team. Ligi yetu ya nyumbani sio Prof bali ni yalidhaa sasa kuna tofauti gani kati ya Yanga , Simba na Faru Dume Fc?? Pili kama ni mfuatiliaji mzuri utakumbuka kwamba hata Maximo aliwachukua Jerry Tegete na Kigi Makassy wakiwa bado hawana timu wakati huo wakiwa Makongo Secondary....upo hapo?? Sasa sioni sababu ya wewe kubana eti huyu Mtanzania asipewe nafasi. Au una personal issue ndugu yangu??

    ReplyDelete
  27. Ghana timu hii iliyoko angola sasa kushiriki CAN ina kocha kutoka serbia hajui kiingereza anatumia msaidizi katika kutafsiri kumbuka ghana lugha yao ya taifa ni kiinglish soccer halina lugha ni kama mafundi mafundi hawana lugha lugha kuu ya fundi ni mchoro nazani mainjinia mtanielewa zaidi

    ReplyDelete
  28. ANON JAN 19, 12:09:00PM. HE IS COACH.UNALINGANISHA NA MCHEZAJI AMBAE KIWANGO CHAKE NI CHAKAWAIDA? NANI AINGIE GHARAMA YA KUMTAFUTIA MKALIMANI?MFANO DEO NGASA NA MICHAEL OWEN.... OWEN ANAADVANTAGE TAYARE HAITAJI MKALIMANI UNAFIKILI WATAMCHUKUA NGASA WAMUACHE OWEN AMBAYE COMUNICATION INMFEVA? WACHA UPUMBAFU WACHEZJI BONGO LAZIMA WAENDE SHULE ILI WAKUZE UELEWA WAO. IS NOT ABOUT JUST PLAYING SOCCER IS ABOUT UNDERSTANDING THE GAME, SAIKOLOGY, SOCIALOGY, INTERECTURAL. HAKUNA STD 7 AMBAE ATAKUA NA QULITY ZOTE HIZO. AGAIN HE IS A CHOAH NA NI SPECIAL NAFASI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...