Mgambo wa Manispaa ya Ilala wakiendesha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauuzaji wa Vocha za simu katika mitaa ya Posta Mpya jijini Dar mchana huu kwa lengo la kuliweka jiji katika hali ya usafi.
dada akijaribu kuomba rasilimali yake isichukuliwe kibabe na mgambo hao
vitendea kazi vikitaifishwa na mgambo wa jiji
wakati zoezi la kamatakama ya wafanyabisahara ndogondogo likiendelea wakazi wa jiji wameendelea kusota na madimbwi makubwa ya mvua kutokana na miundombinu ya kale na ambayo wahusika wa jiji wanaonesha hawana mpango wa kukarabati




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Camon ,kikwete a r u happy na haya,embu tuambie kwa lugha ya kitaifa ambayo inaema nguvu mali,je inakuwaje watu wasio na hatima ya ujambazi ,ukabaji,uhalifu wa mali za watu wanateswa kinoma namna hii na kunyan'gwanya miladi yao ya kuwapa riziki ya kila siku ila mnaona poa kuweka picha za vibaka wamepigwa na karibia kuchomwa moto ndo iankuwa habari ya mji .ila sie wafanza kazi ndogondogo tunatendewa kama vilaka vya kuuza uchi makababuli ya kinondoni..so embu niambieni niuze uchi au niuze vocha za vodacome,,lazima niwatege wateja manake awaji kwenye mauzo mliotaka tufanze biashara hizi.uonevu mtupu yaaaani.

    ReplyDelete
  2. ...not again! We are yet to digest the fate of the lady in bra who stood up against these bullies...With all due respect, the city ought to enforce the law in a more orderly manner than what we have seen for years...

    ReplyDelete
  3. Wafanya biashara ndogondogo wapo hata katika miji mikubwa duniani kama New York. Kinachosababisha uchafu na muonekano mbaya wa miji yetu si hao wafanyabiashara ndogo ndogo..tatizo ni kuwa infrustructure yenyewe ni mbaya. Kwamfano system ya maji machafu (maji-taka) haifanyi kazi na mvua zikinyesha unakuta madimbwi kila mahali...Serikali ianzie hapo kwanza. Tengenezeni Sewer system inayoweza ku-support output ya uchafu jijini, acheni kuwaonea wazawa. Mdau-USA

    ReplyDelete
  4. I WISH KIKWETE NA WAFUASI WAKE WANASOMA HIZI COMMENT ZA WADAU.

    ReplyDelete
  5. yani wananitia hasira askari wa jiji kama wao ni wababe kweli kwanini wasiende kuwashika mafisadi wana kazi yakuwaonea watu wanaojitafutia riziki zao kwa njia ya halali kweli tutafika ?tutaogopa kurudi nyumbani ,MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  6. Kikwete unafanya nini? Kumbuka 2lipanga mistari kukuchagua leo hii machinga 2nachukuliwa ridhiki ze2 unaona je 2fanye nini? Unataka 2we majambazi au wezi? Mimi nataka sababu kwanini machinga awaruhisiwi kuuza biashara zao mjini? Biasharza za machinga ni kwenye muvumenti. Uwezi ukaenda kuwamwga wamachinga sehemu kama ya Kigogo au magomeni uwaambie wafanya biashara zao kule. Umefungua Ilala plazza kwaajili ya machinga. Jengo alijafunguriwa bado wahindi washapata milango. Unataka 2fanye nini? Au mpaka 2mwage damu ndio kieleweke. Watz hamkeni, lazima 2ongee na kulalamika juu ya swala hili. Wamachinga nendeni ktk offisi ya rais kulalamika au 22me ujumbe Geneva ndio 2tasikilizwa, au serikali mmesahau 1995 2livofanya vurugu mtaa wa Congo je mnataka 2fanye tena? Cpendi kuona Tz kuna vita sababu 2shazowea amani, ila kusema kweli mateso kwa machinga yanazidi. Wallah huu ni uwonevu, hii yote sababu ya viongozi wa Tz awajapitia kwenye ari ya shida ndiomaana haya awayatolei macho. Viongozi wengi wa Tz wametokea kwenye familia za kula kulala a.k.a. kuku mayai, wangepitia msoto nahisi wange2onea huruma. Tokea nazaliwa mpaka nakuwa viongozi majina yao ni yale yale.

    ReplyDelete
  7. Ilala Plazza imefunguliwa kwaajili ya wamachinga. Jengo bado alijakamirika ila wahindi na wadau wenye ela zao washawai milango na kila mlango ni zaidi ya million mbili. Sasa mzee kikwete je hii ni haki?

    ReplyDelete
  8. Akale wapi??? Akiiba mnamchoma moto. Kweli kama wewe ni masikini ni masikini tu. Poor lady.

    ReplyDelete
  9. This sort of action leads to unemplyoment, leads to crime, prostitution, dependency and other undesirable consequences. It is disempoweing. Kesho tutalalamika kuhusu uhalifu, ukahaba, matumizi ya madawa ya kulevya na kadhalika; wakati ambapo vijana wakitaka kujipatia rizki kwa amani mnawakwamisha. Watengeeni vijana maeneo ya kufanya shughuli zao kila kona ya jiji- siyo Ilala tu, maana wateja wametapakaa kila kona ya jiji. It is just poor distribution kuwatengea wafanya biashara ndogo ndogo soko Ilala tu; it frustrates the logic of the machinga business, which is a mini mobile shop following the customer rather than waiting for the customer to go to the shop. These people are rendering a great social service apart from earning a living. They should be encouraged and enabled and not frustrated. The City Fathers are just not thinking and certainly not thinking about the common man or his interests or interests of the city's denizens.

    ReplyDelete
  10. sikatai jiji kutekeleza sheria zao lakini huu upuuzi wa kuchukua mali zao hauna maana,wapige fine au vifungo lakini waachieni mali zao....upuuzi wa hali ya juu huu

    ReplyDelete
  11. Hii inaonyesha ni jinsi gani makampuni yetu pamoja na serakali zisivyokuwa na social responsibility policy ambazo zingetumika kuendesha biashara.
    hayo matoroli yanayotumika kuuzia vocha ni mali ya voda kwani yana nembo ya kampuni yao.Sasa najiuliza wakati voda ilivyosambaza hayo matoroli bila kukaa na serekali kuspecify wapi yatumike bila kuleta athari zozote katika mazingira ilitegemea hao watu wayatumie wapi?
    je serekali haina policy yoyote ya kuzuia makampuni kama voda ambayo yanatumia mali zao kupitia kwa wananchi ili kutangaza biashara zao bila kujali athari zake kwa mazingira?
    what i can see here serekali za mitaa is just dealing with rough person which is just a quick fix and that will not going to solve the problem becouse voda and other company will still provide those facility and people will go back to the same streets.
    guys its time to use commonsense not force.

    ReplyDelete
  12. Ebwana hiii ni balaa mbona huku Ulaya wamachinga wanapeta tuu na biashara zaooo ndogooo za kupata riziki yaoo ya kila siku katika kila high streets .Mimi ninaona tatizo lipo kwa wafanyakazi wa jiji na mpangilio mzima wa serikali yetu ya kiumimi ambayooo badooo inakasumba kama mtu mwenye pesa ndioo kila kitu wanasahau kama wote tumetoka katika sehemu moja wanashindwa kufanya vitu vya maana.Ila nazani ukikaribia uchaguzi kwenye mwezi wa tano kila kitu kitakuwa poa jamani kwani viongozi watakua wanabembeleza kura.Mhhhh mimi ninaona ile system ambayooo ilikuwa inatumika ya majina ndioo katika nchi yetu badooo inatumiaka indirect angalau marehemu kigoma malima alijaribu kutufumbua machooo kwa kuitoa katika maswala mazima ya shuleni na tukawa tunasahishwa mitiani kutokana na namba ambayoo ilisaidia kutoa mfume dume wa majina katika system nzima ya viongozi na wizara mbalimbali,imeshindwa kuworkout sasa dahhhhh ..kweli aliye juu utamsubiriiii mpaka unaingia kabulini...umpatiiiii kabisa

    ReplyDelete
  13. MJI KARIBU NA BAHARI UNWEZAJE KUSHINDWA KUONGOZA MAJI BAHARINI KWA KUCHIMBA MIFEREJI MIKUBWA ARDHINI? NI UZEMBE MKUBWA NA ULAJI TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...