
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh.Prof David Mwakyusa akipokea vifaa vya dharura na upasuaji kutoka kwa mwakilishi wa Shirika la afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dr. Martins Ovberedjo.Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 153 za kitanzania,vifaa hivyo vitapelekwa kwenye wilaya za kanda nane nchini .Makabidhiano hayo yamefanyika wizara ya afya na ustawi wa jamii makao makuu jijini leo.


ankal, nje ya mada kidogo: hoja ya haja - wakati suala la kasri ya gavana wa bot lilipoibuka ulitutundukia picha na mchakato wa malumbano pamoja na taarifa rasmi iliyotolewa na utawala wa bot. je unaweza kututundikia ufafanuzi ambao prof ndulu ameutoa juzi mbele ya kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma ili tuutolee maoni? ninatanguriza shukrani
ReplyDeletemlalahoi
kwa mfugamafisadi
STOP!
ReplyDeleteHii tabia ya kupewa misaada na kuinadi itaisha lini Tanzania? Waziri wa afya anapokea msaada wa sh milioni 153 anapiga na picha kama vile ni kitu cha kujivunia. Shilingi milioni 153 kwa serikali ni pesa kidogo sana. Mtoto wa kitanzania akiona haya matangazo ya misaada anakuwa na tabia ya kuomba omba matokeo yake hulka ya kuomba inakuwa ni sehemu ya utamaduni wa mtanzania.
Ombi:
Acha kutangaza misaada badala yake wakulima, wavuvi, wachuuzi wanapofaanikiwa katika shughuli zao za kila siku mafaanikio yao yatangazwe kila kona kuwamotivate watanzania wengine. Waziri anayehusika aje na mi kamera, waandishi wa habari, na apige picha na huyo mkulima.
Mwalimu Nyerere katika uhai wake alisisitiza sana kujitegemea. Ninauhakika kama Mwl akifufuka leo, atasikitishwa sana na hii hatua tuliyopiga ya ukaomba omba miaka 50 baada ya uhuru.
Acha kutangaza misaada, tangaza mafanikio yanayotokana na juhudi zetu wenyewe.