Ankal,
Nakupongeza sana kwa kazi ngumu ya kuwatoa watu usingizini kwa kuwaelimisha kupitia blong yako Hongera sana!!!!!!!

Mimi kama mdau na mpenzi wa kufuatilia mambo kwa ukaribu, napenda kuungana na mdau wa Tokyo kuwa ukiangali kwa makini taarifa nzima ya habari iliyorushwa na TBC1 hakuna mahala popote panapoonyesha kuwa sasa wale police wanapokea pesa, isipokuwa wanaonekana wakipokea nyaraka mbali mbali kama leseni nk.
Na kupanda na kuchungulia ndani ya gari kama kuna vitu vyovyote na huu ni wajibu wao na ni sehemu ya kazi ya traffic. Je kama ni kweli mbona hata Mr Jerry hajasema kuwa “ona sasa hapo police anapokea rushwa!!” Au police walipokuwa wanafunga milango ndiyo rushwa?

IGP mwema tafadhari ninapenda kutoa ushauri kuwa ni vema zile picha zikapitiwa upya na wataalam kabla ya kutoa maamzi ya kuwaadhibu hawa traffic. Pili ni vema kazi za traffic zikawekwa wazi kwa wananchi ( Elimishwa ) ili kuondoa migongano na udhalilishaji wa Wapiganaji wetu.

Mwisho ningependa kumshauri Mr Jerry kuwa rushwa haipo traffic peke yake, ajaribu kuingia anga zenye rushwa kubwa kubwa kama TRA, TANROAD n.k mfano:-mtu anaajiriwa mwezi mmoja tu akitokea chuo na alikuwa msaga lami mara unasitukia ana nyumba ya ghorofa na gari mbili za kutembelea, Hizo ndiyo rushwaaaaa... tia timu na huko ndiyo tutajua kweli uko fiti.

Mdau nawakilisha
Miha JM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. nakubaliana na ww mdau na mdau wa tokyo,tusikurupuke tu kujaji bila ushahidi,hakuna sehemu hio clip ikionyesha wakipokea rushwa,nakubali kuna mazingira ya rushwa lakini hamna concrete evidence,bahasha inaweza kuwa na kadi na makaratasi mengine ya gari au mzigo,hata hela ila hakuna ushahidi

    ReplyDelete
  2. wewe kwann unamkazania jamaa kama ataaza na Tanroad na TRA B´ndio utamuona yupo fiti, yeye kaaamua kunza na huko kwa trafiki then atakuja na huko mnakotaka nyie. Rushwa ni rushwa tu hata iwe shiling 5 au hao jamaa wa TRA na Tanroad wamekuchukulia kimwana chako nn na mahela yao.

    ReplyDelete
  3. Mimi Nawashangaa watu wote wanaomchachamalia Jerry Muro. Yaani eti kwa sababu rushwa iko sehemu nyingi basi polisi/Trafiki wasiguswe mpaka na hao wengine washughulikiwe kwanza. Muro amejisikia aanze na mapolisikwanimambo yao yako dhahiri kabisa. Na nyie wakereketwa mnaowafahamu wala rushwa wengine igeni mfano huu-kawafichueni. Kuhusu rushwa kutokuonekana ikitolewa..hiyo sio hoja ya msingi kwani ni nani asiyefahamu mazingira ya utoaji na upokeaji rushwa yalivyo? Watanzania acheni unafiki. Au mpaka apongezwe mnayemtaka nyinyi ndio mfurahi? Kwani ni nani asiyefahamu mikakati yenu ya 2010? Acheni unafiki. Rushwa itaondolewa hatua kwa hatua, kitengo baada ya kitengo kwa ushirikiano na mchango kutoka kwa kila mmoja wetu!

    ReplyDelete
  4. we mdau uliyeandika hii habari ni traffik nin? au una ndugu yako trafik?Wale jamaa sio uongo wanakera wanapokea rushwa sana sasa unapotokea wewe kuwatetea unashindwa kueleweka.Mwache Jerry muro afanye kazi anaanzia traffik baadae ataenda kwenye rushwa kubwa tu usijali acha atuondolee hizi kero za barabaran kwanza.

    ReplyDelete
  5. You got to be kidding !!!. Nashindwa kuamini kuwa kuna watu ambao walishindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kinatokea pale!!! au ni kutaka tu kujifanya kuwa wao waliweza kuona vizuri zaidi kuliko wengine. Mdau unakataa kuwa haikuwa pesa bali ni leseni na nyaraka mbalimbali, wewe uliwezaje kujua kuwa zile zilikuwa ni leseni. Tuambie basi ni leseni ngapi au nyaraka ngapi uliona zinarudishwa na polisi wale baada ya kuzipokea!. ukiangalia vizuri katika clip ile, kuna karatasi moja tu ndo ilirudishwa tena akibaki na kitu katika mkono wake. Mimi sijawahi kuona polisi anachukua leseni halafu anaifutika katika mfuko wake anafunga mlango wa gari na dereva anaondoka, labda basi ilikuwa ni copy, ambayo labda kuna utaratibu siku hizi za kuachwa mikononi mwa askari.

    Halafu ukiangalia kwa makini ni kuwa wale madereva wanajua kabisa kinachoendelea pale. Haiwezekani gari isimame tu askari anakuja kufungua mlango na kupokea kitu kwa dereva moja kwa moja.
    Huku ni kutetea rushwa kuliko vuka mpka. Labda mdau na mwenzake wa Tokyo wana sababu nyingine ya kumlaumu Jerry. Kumwambia mwandishi aende TRA, TANROAD na kwengine sio hoja ya msingi , wewe unajuaje pengine baada ya hao Traffic kinachofuatia ni huko unakomshauri aende.
    Wake up people!!!!

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  6. Labda nielimishe jamii kuwa Rushwa haiwezi kwisha Polisi.Sababu ya kutokwisha kwa rushwa ndani ya polisi ni mfumo wa polisi. Nakumbuka wakati naenda kujiunga na jeshi la polisi, ndani ya basi major aliyokuwa akitusindika alidai tuchange hela ili akatusaidie kusajiliwa mara tufikapo CCP. Nilitoa japo sikuona umuhimu wake kwani nilikuwa na vyeti sahihi na sifa zote. Nilipokuwa chuoni mwalimu mmoja(afande) bila aibu aliomba hela darasani ili tusifeli mtihani. nilitoa hela japo nilijua siwezi kufeli mitihani yake. Kwa hiyo askari anajengwa na kukuzwa kirushwarushwa. Haiwezekani akaacha rushwa. Hata kwenye kupangwa kwenye malindo mazuri ni lazima umpe major kitu kidogo ili akupange. Je unategemea polisi atapata wapi pesa ya kumpa major-jibu liko wazi ni kutoka kwa wananchi hasa walalahoi. Naamini mnaelewa kuwa matajiri huwa hawatoi rushwa. Traffic huwa hawasimamishi magari mazuri. wenye magari mazuri watakubaliana na mimi. Rushwa haiwezi kwisha polisi mpaka mfumo utakapobadilika. Huyo Muro atapiga picha mpaka atazeeka. Namshauri afanye shughuli zingine la sivyo hatumuokoa tena akitemewa mate na mzungu.Nawasilisha.

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na mdau-Rushwa haiwezi polisi.Ni suala mfumo.

    ReplyDelete
  8. Kusema aende TRA,TANROADS huo ni upeo finyu, kweli rushwa ipo kila sehemu lakini kuna pa kuanzia, ndo hapo sasa ameanza. Kinachotakiwa ni kuwa apewe msaada wa kuweza kuwabaini kwa uthibitisho hao wala rushwa kama alivyofanya kwa Traffic, naamini kuwa kuna msaada kapata mpaka akafikia kuwanasa. Sasa wewe kama unapaona pengine msaidie halafu ndo ulalamike kuwa kashindwa. Kazi ya Muro ni ya pongezi kubwa. Kwa sababu kajitoa, wewe unayewajua hao wala rushwa wa TRA na kwingineko alafu unakaa kinya hufai sababu wewe ndo unawaficha.
    Naona Jerry angeundiwa timu ya vijana wa kazi ili wafanye kazi kama hizo. Wote tuanjua kuwa Tanzania ni kubwa si rahisi kuifikia yote lakini tusaidiane ili kazi aliyoianza Muro isishindwe.
    TAKUKURU MPO??????

    ReplyDelete
  9. hongera jerry muro..naona wala rushwa hapa wanatapatapa..rushwa ni rushwa tu, aijalishi ni traffic au ni TRA, kaza buti jamii ya WaTz iko pamoja nawe, usiwasikilize hawa ni watuhumiwa wenyewe wanajaribu kujiosha

    ReplyDelete
  10. MIHA JM UNASHANGAZA NINI HAPO NA UNACHOTETEA NI NINI HAPO!!!!!! KWANI HUONI WATU WANAPOKEA HAYO MAKARATASI UNAYOYASEMA NA HAWAYARUDISHI KWA DEREVA!!! SASA WANABAKI NAYO KWA SABABU ZIPI, NA HATA YALE YANAYORUDISHWA KWA DEREVA YAMETUMIKA KA VEHICLE YA KUSAFIRISHIA PESA HIZO ZA RUSHWA ZIKICHULIWA YANARUDISHWA, KWANI WAKIPEWA HATA HATUWAONI WAKIYASOMA HAYO MAKARATASI, NI KWAMBA PESA INAWEKWA NDANI YA MAKARATASI HAYO KWA MAELEKEZO YA POLISI NA WANAPOPOKEA HAYO MAKARATASI WANACHUKUWA PESA NA KURUDISHA HAYO MAKARATASI WALA HATA HAWAYASOMI, PAMOJA NA HAYO YOTE MADEREVA WOTE WALIOHOJIWA WAMETHIBITISHA KUTOWA PESA, SASA UNATAKA KUTUELEZA NINI, NINACHOHISI HAPA NYIE MNAOTILIA WASI WASI REPORT YA JERRY MURO NI NYIE WAHUSIKA, PIA JERRY HAJASEMA HAKUNA RUSHWA KATIKA SEHEMU NYINGINE ZA JAMII ZIPO NAZO PIA ZINAPASHWA KUKEMEWA, SAFIRI KATIKA BARABARA ZA TANZANIA UONE RUSHWA ILIVYOSHAMIRI. PIA PAMOJA NA YOTE HAYO KUNA HAJA GANI YA KUWA NA ROAD BLOCKS/CHECK POINTS BARABARANI NDANI YA NCHI HUO NI UONEZI NA SI DEMORASIA, THESE ARE DRACONIAN LAWS UNNECESSARY TO BE THERE, HAMNA POINT YOYOTE YA KUWA NA CHECK POINT NDANI YA NCHI ZIMEKUWA-CREATED NA POLISI KUTENGEZA PESA KWA NJIA YA RUSHWA, TUNAWAOMBA WABUNGE WAZIONDOWE HIZO. SAID MWEMA ANATAKIWA KUTUPATIA MAELEZO SI WANANCHI JUU YA HILI LA RUSHWA LILILOIBULIWA NA JERRY MURO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...