Rais Jacob Zuma akiwa na mai waifu wake mpya Tobeka Madiba wakilisakata javu la Kizulu leo huko jimbo la Kwazulu Natal
Bi harusi na wapambwe wakiwasili sehemu ya tukio

bwana harusi akijimwayamwaya kwa furaha ya kupata kitu kipya. bahati mbaya alijikwa na kula mweleka. ila mzee mzima hakuumia


maharusi wakiimba nyimbo za kizulu










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 75 mpaka sasa

  1. ...interesting.

    ReplyDelete
  2. EE bwana huyo ni Zuma au????
    Mbona kama nimemuona pale msitu wa Turiani?

    ReplyDelete
  3. jAMAA ANAkula "BATA"

    ReplyDelete
  4. Waafrika bwana, wenzetu wa Magharibi wanashindana kudesign jengo refu ulimwenguni, kurusha roketi mwezini, au wanakesha lab kuvumbua dawa za kutibu magonjwa hatari, mwafrika yeye anacheza ngoma kufurahia uroda wa mke wa tano. Afrika itaendelea kweli.

    ReplyDelete
  5. Nilikua najiuliza kila siku hivi wazungu waliwezaje kutawala bondeni miaka yote hiyo bila kizuizi kutoka kwa weusi, sasa nimeelewa hawa wenzetu huko South Africa akili zao ziko kwingine kabisa,kwenye kuhesabu mke wa ngapi,kesho nilale kwa mke gani,mwakani nioe binti wa nani. Maendeleo ya nchi yanapangwa lini kiongozi yuko busy na kuoa wanawake na kuacha.

    ReplyDelete
  6. Huko South Africa kutaharibika sasa hivi, kama kipaumbele cha nchi ndio hivi, TUMEKWISHA, makaburu wamewaachia nchi nzuri, economy nzuri wataiharibu muda sio mrefu na kuendekeza haya mambo yao ya kienyeji.Zimbabwe ilikua nzuri sasa ona wako wapi sasa.

    ReplyDelete
  7. there we go again, yaani rais anaoa mke wa tano sijui wa ngapi!! haya ndo maendeleo ya mwanaume wa kiafrica

    sasa hapa ataconcentrate vp kwenye wake zake na serikali?? au ndo ameowaolea madreva wake????

    ReplyDelete
  8. Hogera Mr. president kwa kudumisha mila na dasturi za kiafrika. To hell westernised brain washed individuals

    ReplyDelete
  9. kiongozi huyu hajatulia

    ReplyDelete
  10. Michuzi, huyu jamaa anafanya kazi saa ngapi??? hawo ndio vioungozi wetu wa kiafrika

    jama ankula ngoma kama sio raisi wa nchi..... shame

    ReplyDelete
  11. hivi tunakwenda mbele au tunarudi kulekule, lakini naamini gharama haikuwa kubwa siyo ya kifahari

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA MR. PRESIDENT KWA KUPATA JIKO.

    ReplyDelete
  13. Again, "stupidly educated, western civilised brigade" washaanza na upumbavu wao. Kuna kosa gani kwa Zuma kuishi kizulu? Kila kitu cha kiafrika kibaya, cha ki-western kizuri. Je. angesherehekea birthday ya kuzaliwa mwaka wa 66, na kukata keki, na kupuliza mishumaa, kucheza bluuzi msingesema upumbavu wenu huo wa wenzetu wanzungu hivi, mara vile...;
    Chukueni taimu huko, heko kamanda Zuma kwa kuishi kizulu
    ; Wachina wanaishi kichina, wahindi wanaishi kihindi, wazungu wanaishi kizungu; lakini hawa stupidly educated hawataki mwafrika aishi kiafrika.

    Na wewe uliyesema wenzenu wazungu wanagundua majengo marefu; haya, hapa JK na Mizengwe pinda wanakata keki za birthday kila siku kama wazungu; sasa jee hiyo imewasaidia na nyinyi kugundua hizo maabara zenu?

    Ondoeni kasumba zenu hapa, wewe kama unajikataa endelea kujikataa lakini usilazimishe eti wote tujikatae.

    Kila siku mpo bize kuishi kwa expectations za wazungu tuu...!

    PUMBAF

    Amandla.... Ngawethu

    ReplyDelete
  14. mtu mweusi na maendeleo wapi kwa wapi? sisi watu wa ngoma na chini hongera president ongeza mwingine ila chukua dogo dogo we mwenyewe mzee unachukua tena mzee ndo iweje...we vipi?

    ReplyDelete
  15. HONGERA MHE. ZUMA KWA KUDUMISHA MILA. ACHANA NA WALEVI WA KASUMBA YA MAGHARIBI. ONA WAO WA 'MKE MMOJA MUME MMOJA' WANASHIKWA UGONI KILA KUKICHA. SI UZUSHI, TUNAPEPERUSHIWA NA CNN!!!!!

    ReplyDelete
  16. Huyu Raisi kweli mtambo, utavunja mguu buree umri wenyewe umeshaenda hebu tulia 'bata' ingawa mtamu waachie vijana

    ReplyDelete
  17. duh! kuna pumbavu humu wanadhania maendeleo ya nchi yanaletwa na Rais

    ReplyDelete
  18. Ohh 37 yrs old and 68 yrs old ...aghhhhrrrrrrr.....ohhh FOOL ME ONCE, SHAME ON YOU! FOOL ME TWICE, SHAME ON ME! 37 yrs old virgin????????? They gonna help him doing the JOB and the HIV/Aids knock knock knock ...mhhhhhhh

    ReplyDelete
  19. Okay watoto 19. Mke wa mmoja 67 yrs old (no children), mke wa mwingine 34 yrs old (3 children) married 2008, mke mwingine the Home Affairs Minister (4 kids) divorced in 1998, mwingine alijiua in 2000 (left 5 kids), the newly bride is not that new as the couple have 3 children together and he is engaged to at least one other woman.

    Ukimwi huu utatuua

    ReplyDelete
  20. Angalia michosho hii? ya miaka ya karne zilizopita bado tu wanaishikiria, utafikiri ya kwamba hawajui binadam ana mabadiriko, sasa huu utmaduni wa kuoa kila wakati si umeshapita na wakati, tena yeye kama kiongozi wa nchi!!!! kweli,africa bado, uncoverd.

    ReplyDelete
  21. Mlikuwa mnamlaumu baba wa pili wa taifa (Mwinyi) sasa kwa Zuma mnashindwa kusema hata adumishe utamaduni wao.

    Ikija kwa utamaduni wa kibongo mko mbele kuutetea wakati mntahiri wasichana. Huu wa kizulu ndo utamaduni sio majungu.

    Watu mnaleta mahubiri yenu ya mke mmoja ya kanisani kwenye mila za watu.

    Mbona nchi yao imeendelea saana tu kuliko waswahili!

    ReplyDelete
  22. Hii ni moja ya utajiri mkubwa ambao sisi watu wa Africa tumejaliwa. There is no problem whatsoever ya kuwa na wake wa tano, hasa ukifuatia kwamba hizi mila zimekuwa zikidumishwa milele na milele, toka henzi za mababu zetu wa Kizulu na Kingoni. Namuungua mkono mchangiaji wa mada hapo juu aliyesema: "To hell the westernised brain washed individuals." Wengi wenye kupinga tamaduni hii, wanaringanisha na tamaduni za ulaya, Wazungu. Why do you have to use the decrepit western cultures as a mirror? Why????

    ReplyDelete
  23. Aluta Continua...Hongera Raisi kwa kufanikiwa kufikisha nusu ya lengo ulilojiwekea la kuoa wanawake kumi.Afilika oyeee.......

    ReplyDelete
  24. Mzee huyu ajatulia. watatu usawa wenyewe huu.HATARI.

    ReplyDelete
  25. Mtu mzima namna hiyo halafu mambo yake ni hovyo kabisa.You can now see a real "villager".

    Mdau Dave
    duniayetukubwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  26. Ndugu hapo juu ni mtizamo wa wapi unaoeleza kuwa ukiwa raisi ni aibu kucheza ngoma kwa stail unayotaka?

    ReplyDelete
  27. Seriously, kama uzungu na maendeleo ni ndoa za jinsia moja let african men marry everyday.

    ReplyDelete
  28. NASISITIZA SIO UTAMADUNI BALI NI UMALAYA WA MTU

    KAMA NI UTAMADUNI MBONA MANDELA HAKUOA OA HIVYO

    KADHALIKA RAIS ALIYEPITA HAKUOA OA HIVYO

    NI UMALAYA WA MTU BINAFSI

    ZEE ZIMA LINAACHA KUFIKIRIA MZIGO WA TAIFA?

    ReplyDelete
  29. president hajatulia huyo, sasa kwa nini alitembea na binti wa rafiki yake tena bila kutumia condom kwa kisingizio kuwa alienda kunawa mara baada ya ku-do! kwa mtindo huo mr. president ataweza kweli kuhamasisha kuhusu kuzuia maambukizi ya ukimwi? AFRICA ZAIDI YA TUIJUAVYO

    ReplyDelete
  30. Kwangu mimi naona kwa staili hii Africa tutabaki nyuma siku zote. kama Rais nategemea ana majukumu mengi sana na anahitaji muda wa kuyafanya kwa ajili ya kuendeleza watu wake. Lakini huyu mwenzetu kuoa imekuwa kama sera ya maendeleo ya nchi, huyu ni wa tano, nasikia anamchumba mwingine sijui ataoa lini. Sasa kazi ya kuongoza nchi ataifanya saa ngapi.

    Nalaani kitendo hiki na wala siyo sifa ni uzandiki tu.

    ReplyDelete
  31. tatizo lililopo afrika hasa Tz mtu akiweka mambo yake hazarani anaonekana ni mkosefu, mzinzi,muasherati saaana... ni marais wangapi afrika ambao mbele ya wengi wanaonekana wana mke mmoja? funua pazia uone jinsi ngozi ya kondoo ilivyoficha maovu ukiwakusanya vimada wa rais mmoja unaweza kujaza fuso na wengine kubaki... si maraisi tu bali hata viongozi wengine wa kisiasa,je ni mashehe,mapadri,wachungaji wangapi wamefumaniwa? na vyombo vya habari vinaripoti kila siku wakati wakiwa mbele ya madhabahu au misikiti ndio wakwanza kukemea na kuponda.

    ReplyDelete
  32. Wamagharibi wana mambo yao na sisi waafrika tuna mambo yetu.
    Sisi tunacheza ngoma kwa sababu ni zakiasili kabisa na hatujaziiga kutoka kwa mtu yeyote. Mila za kizulu zinaruhusu mwamme rijali kuoa wanawake wengi kadri anavyoweza. Hii si sheria ya Zuma au Mandela, ni utaratibu wa tangu enzi na enzi za mababu zao. Kama mtu anaona kudumisha mila ni aibu basi afanye kama wanavyofanya wa magharibi kula denda hadharani, kuoana watu wa jinsi moja nk nk, mbona hayo hamyashangai?

    ReplyDelete
  33. huo ni upumbavu sana yaani jamaa anawaza ngono tu hao wanne hawamtoshi duh! ama kweli angekuwa Rais wetu tungeshampindua ningejitoa hata muhanga kuliko kuona Taifa linateketea kwa kuoa tuuuuuuuu.
    du! Mungu umetupa viongozi

    ReplyDelete
  34. He is too local

    ReplyDelete
  35. Kaka Michuzi na wadau wengine, namna hii Africa kuendele kwa juhudi zetu wenyewe hatuwezi katu. Yaani kiongozi kabsaa wa nchi ambaye watu wake kila kukicha wanatia tifu juu ya ajira yeye hawazi lolote wala kuumia juu ya hayo. Anawaza raha tu na uroda!!!

    Ona sasa waafrika tnavyobweteka, badala ya kujenga uchumi, na kuwaza jinsi gani kuimarisha uchumi, kiongozi anawaza kukamilisha kuvutia wanawake ndani ya nyumba!! Ni bahati tu kwa kuwa Makaburu walidumu mno Sauzi ndiyo maana angalau hali iko tambarare.

    Mimi nafikiri haukuwa wakati mwafaka wa kuzidi kuongeza wake. hivi wadau mnijuze, je, wote wanaitwa first ladies, au kuna mmoja tu? Ni yupi sasa kati ya hao? Yupi anastahili kukaa jumba jeupe?

    ReplyDelete
  36. Tulizeni mizuka...Mzee endeleza mila acha waosha vinywa waendelee, mbona wazungu wanaoana wanaume kwa wanaume hawasemi kitu? Acheni hizo kila mtu na asili yake...mkasirike mcheke mila zipo pale pale...waswahili tunasema 'asiye na mila mtumwa' teh teh teh! Nkosi Sikelel' iAfrika

    ReplyDelete
  37. KWA KWELI AFADHALI YA ZUMA, YUKO WAZI.

    YEYE NYUMBA NDOGO ANAZIHAMISHIA NYUMBANI NA ZINAKUWA ZINAELEWEKA.

    WENZAKE WANAWEZA KUWA NA WANAWAKE WENGI ZAIDI KULIKO YEYE. WANAFICHA WAKIJIFANYA WAKO SAFI.

    PESA UNAZO, UNAKULA UNASHIBA, KESHO HAIKUPI SHIDA, WHAT ELSE??

    KWATUAAA!!!

    ReplyDelete
  38. Mzee Wa Zeze, New Albany- OhioJanuary 05, 2010

    NINGELIKUWA HUKO SAUZI, LAZIMA NINGEMCHAPIA HUYU RAISI "KIWEMBE" NA NINGEFANYA JUU CHINI NIKAMZALISHA HUYU MKE MPYA NA MTOTO AKAFANANA NA MIMI KAMA KAWAIDA YANGU.
    TEH TEH TEH!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  39. watu wengine kwa ubongo wao wa ndege wanakuja na upuuzi eti mila za Kiafrika! Hizi ndizo zilikuwa zikitwa za kishenzi. Kusema kwamba tangu zamanimila hizo zilikuwepo tangu zamani ni upuuzi. Kwa hiyo kwavile zilikuwepo na zile za kurithi mke nazo ziendelezwe?

    ReplyDelete
  40. i do congratulate mr , president zuma, kwa uamuzi wake, ni ngapi mnanzini, labda tukubali waafrica culture yetu ni kuwa na wake wengi........wazungu wana divorce, sisi tunasema dini hairuhusu, ila ni wangapi mna nyumba ndogo wanawake wa nje, ya nii kuzini kama mnaweza kuhalalisha.

    ReplyDelete
  41. Ni mke wake wa tatu ingawa ni mara yke ya tano kuoa, sio kwamba saivi ana wake watano. Big up Zuma, just liive your life and let them talk because they have the mouth

    ReplyDelete
  42. Jamani, Zuma asisakamwe sana maana kila binadamu in staili yake ya kusihi. Mbona akina Mswati wana wake kibao na life goes on kama kawaida.

    ReplyDelete
  43. dada matilda naomba nipingane nawe kabisaaaaa....kama mila zinamruhusu na uwezo (kingono na kifedha) anao hamna shida..mila na tamaduni weka kando maendeleo ni umakini wa watu tu--angalia uarabuni mila zinawaruhusu kuoa zaidi ya mwanamke mmoja (angalia maendeleo yao), rais wa bolivia (Morales) anacheza ngoma na kula majani ya coca (ambayo yanatumika kutengeneza cocaine) kama sehemu ya utamaduni wa watu wake lakini sehemu zote hizi maendelo sio kama sisi ingawa wanafata mila na tamaduni..acheni wazimu wa kuzani kila wanachosema na kufanya wazungu basi ndo sahihi..fata mila akili kichwani..

    ReplyDelete
  44. nyinyi mnaomponda mnaojifanya mmeelimika mnaishi kizungu ni watumwa wa utamaduni. BIG UPZ ZUMA..

    ReplyDelete
  45. kuna baadhi ya vimila vya kiafrika ni vibovu kama mnataka kudumisha mila sana tembeeni peku msivae viatu vaeni magome ya miti kama kina kipepe na mademu vifua wazi msiendeshe magari endesheni baskeli za mbao ili mdumishe mila vizuri manake bado hapa mnaiga umagharibi tu asikudanganye mtu mila za kimagharibi ziko juu tu full maendeleo kuna baadhi ya mambo mabaya na mazuri kadhalika na zetu hivyohivyo

    ReplyDelete
  46. Kwani kuwa villager ni vibaya? Corrupted minds...kuna mdau hapo juu kasema "mwangalie huyu a real villager" Sawa wewe wa borntown lakini umefulia yeye a real villager lakini ni Prezida wa Bondeni.See that?

    ReplyDelete
  47. Utakuta majoriti wanaopinga ni wanawake hili ndo dume.

    ReplyDelete
  48. Sawa kabisa Mh. Zuma unatulindia heshima wazee, maana kijana wa miaka 27 halali yake kuwa na mke mmoja, lakini kadri anavyokua-kukomaa-kujiamini akifika miaka 35 anaongeza mke wa pili na akifika 42 mke wa tatu, huo ndio ukomavu.

    Kijana akijaliwa umri kama wa Mzee Zuma wake watano kutimiza hapo hata sisi wazee wa baraza tutamkaribisha tuchangie kata ya pombe ya umkomboti, maana anaonyesha ukomavu wa kuweza kuhimili kashikashi za 'mji wake' wenye wake zaidi ya mmoja na watoto 19 na ushee. Wazee wengi wenye mke mmoja huwa hawakanyagi kijiwe chetu kwa sababu tunawatania kuwa bado ni 'watoto' maana iweje Mzee wa miaka 55 ana mke mmoja wakati kijana wake wa miaka 32 tayari ana wake wawili!

    Hiyo ni mojawapo ya 'litmus-test' kuonyesha kuwa umekomaa hata nchi ukipewa utaweza kuiongoza, maana ukiwa na mke mmoja mawazo ya 'kiwivu-wivu' mengi mpaka kuongoza shughuli zako za kibiashara inakuwa ngumu sembuse upewe nchi.

    Mdau
    kijijini Amanzimtoti
    Kwa-Zulu Natal

    Mzee Zuma ni

    ReplyDelete
  49. Acheni wivu wanawake asipooa mnataka aolewe, uzungu unatusaidia nini zaidi ya kuidistroy dunia, maendeleo gani zaidi ya haya afrika inayoyataka, hii pati ya natural sio viagra,ni lazima na sisi tuwe na kitu tofauti na wazungu nahichi mkitaka msitake wazungu hawatufikii,bravo keep it up dude.

    ReplyDelete
  50. sasa kama tayari alikuwa na wake wengine 4 kisa cha kubaka kilikuwa nini?

    ReplyDelete
  51. huo ni utamaduni wao huyu jamaa anatoka kwenye royal family huko kwa zulu yeye ni kama king flani hivi,mi sioni kama kuna ubaya kuliko wazungu wanakuwa wameoana lakini wanainvite watu waengine kitam=ndani yaani three some wanaita, au unakuta kila siku wanaoa na kuachana si bora huyo wake zake wanapendana na hajawaforce kuishi pamoja

    ReplyDelete
  52. ankal meseji yangu umenibania kwa sababu imemtaja JK na pinda wanakata keki za birthday.

    poa tuu lakini lengo langu lilikuwa ni kuwaelimisha waafrika wenzangu, na wala sina chochote against jk.

    ReplyDelete
  53. Big up Zuma!!!
    Hawa wanaokataa ulilolifanya hawajui nature ya mwanamume hasa; siye yule anaepapaswa na wenziwe kusikotakiwa halafu akacheka eti ndio kwenda na wakati?
    Hapa ni maneno ya Bush, "You are with us or with them" no middle option. Yaani wewe ni Rijali hasa au another Elton John?

    ReplyDelete
  54. msichanganye utamaduni na common sense tafadhali.....

    ReplyDelete
  55. Mhh wabeba Maboksi mnanyoodo nyie!!!! Akioa wake watano wanaojulikana rasmi maneno kedekede. Nyie mlio na vidumu kila kona ya mtaa??? Wengine mkihesabiwa hata kumi wanafika!!! AAACHENI HIIZOOOOO.!!!!!

    ReplyDelete
  56. HAO WATAJUTA MUDA SI MREFU KAMA NCHI ZINGINE ZA AFRICA,KWANI KWENDA KULICHAGUA ILO JENDAWAZIMU KUWA RAIS WA NCHI SI UJINGA HUO.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  57. NIMEMPENDA ZUMA KWA KUFANYA MAMBO YAKE AYAPENDAYO HAZARANI. AU MLITAKA AOE MKE MWINGINE KIMYAKIMYA KAMA WANAVYOFANYA VIONGOZI WENGINE WENYE NAFAZI KAMA YAKE? MARAISI WANAO ONGEZA WAKE WENGINE KIMYA KIMYA HAWAJIAMINI.HEBU FIKIRIA UNASIKIA RAIS WA NCHI AMEONGEZA MKE MWINGINE KIMYAKIMYA HIYO INA IMPLICATION GANI? Michuzi huwa unanibania sana coment zangu hivi ni kwanini? sitaki kuamini kwamba hata hii utahisi itahatarisha uhai wako

    ReplyDelete
  58. Sisi waafrika sio watu wa maendeleo kwa ajili ya nchi ni uselfish tu. Na ndo maana ukitaka nchi iendelee waachie wazungu wenyewe brain zao zimetulia. Huko South waliifanya ikawa kama Europe lakini baada ya muda sio mrefu kwa mwendo huu itaanza kuharibika kama ni ajira, wizi na ujambazi.
    Kitendo cha huyu bwana ni mila za kiafrika zilizopitwa na wakati. Watoto 19 sio mchezo na sio mfano wa kuigwa.
    Pia wanawake wenyewe wanatakiwa kuendelea kujikomboa kielimu, kazi na biashara na kupigia haki zao ili kuwa na sauti katika mila kama hizi.

    ReplyDelete
  59. Zuma is another Lunatic just happen kujua politics akachaguliwa lakini other skills ni zero. Ukisoma historia ya mwanamke aliemuacha anaeleza jinsi mateso aliyoyapata. Hizi skendo zote za kubaka na kuzaa ovyo kama kuku ndio mila?I do not care kama anajua uongozi kuna watu wanajua kazi zao vizuri sana lakini nyumbani kama baba ni zero.I do not care anavyocheza na mila ila historia yake inasikitisha.Anon aliyesema kuna mila nzuri na mbaya nakusupport 100%. Huu ni ulimbukeni wa 67year old kwanza hana nguvu tena anahitaji watu wakumtunza tu.Hivi hao wanounga mkono wangependa watoto wao wakike waolewe na mtu kama zuma?

    ReplyDelete
  60. Kwa nyongeza kwa Wadau JuaKali and co.

    Hao wakeze Mh. Jacob Zuma wote wana elimu ya kutosha (mpaka vyuoni) na walikuwa/wana kazi zao nzuri tu, mmoja wapo Waziri wa serikali.

    Hivyo msiwadharau wake-wenza hao mkadhani hawajui Haki zao, hao wameridhika kipendacho-roho na utamaduni waliokuliwa kumbuka huyo mke mdogo ana umri wa miaka 37 tu.

    Pia hao kina mama wana elimu ya shule kuliko Mh. Zuma ambaye ilibidi apate elimu-duniya kutokana na sera za ubaguzi zilizomfanya awe mkimbizi nje ya Afrika ya Kusini akiwa kijana mbichi na baadaye kupewa cheo cha mkuu wa usalama wa Umkhoto We Sizwe yaani jeshi la ukombozi la ANC uhamishoni.

    Mimi mzee mzima kuna mwenzetu hulalamika kwa mkewe kuwa anadharauliwa na wazee wenziwe kwa kuwa na mke mmoja miaka yote 30 ya ndoa kuna mdau pia amegusia hilo.

    Hivyo kina mama wa kitanzania msiache mila zetu za kiafrika, ndoa ya wake wengi nzuri- kupiga soga na wenzio, ukienda likizo mke mwenza anakutazamia watoto, ukijifungua mke mwenza anakuchemshia maji ya moto, maji DAWASO yakikatika zamu kumtengea mume maji,yaani listi ya mema ktk uke-wenza ni ndefu mpaka raha.

    Mdau
    Mumewangu

    ReplyDelete
  61. Hii ni safi sana kuliko zxa wengine wenye ku-"ape" za Ulaya au Uarabuni!

    ReplyDelete
  62. hao wazungu wasiooa kila siku mmewasahau nini wanavyocheat? Clinton, Sarkozy mmewasahau ehe?
    Zuma alishasema politicians wengi wana vimada na watoto kibao nje wanawaficha, yeye ameamua kuwa mkweli, kama kuna mtu amezaa nae mtajua, kama kuna mtu amemtole mahari mtajua na badala ya kucheat anaongeza wake tu!
    i dont see anything bad about that as along as amekubaliana na wake zake na anaendesha nchi vizuri!

    ReplyDelete
  63. msisahau Tiger Woods alikuwa na wanawake 10.

    ReplyDelete
  64. NAKUMBUKA WAKATI ANASALIMIANA NA MISS MMOJA TOKA UGANDA KUNA MTOA COMMENT AKASEMA FISI ANASLIMIANA NA MBUZI KUMBE NIMEAMINI.JITU ZIMA UTAFIKIRI GANGA LA JADI.KUNA TAMADUNI ZA KUTUNZA NA NYINGINE NI AIBU.RAISI ANAOA KAMA KUKU?WAMEPIMA?

    ReplyDelete
  65. RAIS KAMA HUYO ATAACHA KUIBA PESA ZA UMMA WAKE WOTE HAO NA WATOTO WOTE HAO, HIVI WAKE KIBAO ANAO NA BADO ALIM-RAPE YULE BINTI MWENYE UKIMWI!!! HAFAI KUWA RAIS, SOUTH AFRIKA ITASHUKA CHINI MI YANGU MACHO UTAONA HIYO NCHI INTAVYOZAMA KIUCHUMI NA KI-POPULARITY. ALING'ANG'ANIA URAIS KWA VILE ALIKUWA MKUU WA MAJESHI YA UMKOTWE- WE-SINZWE(NOT SURE WITH THE SPELLS) NDO ALIONA NI HAKI YAKE NAYE AUPITIE URAIS LAKINI IS NOT QUALIFIED FOR THE THAT TOP JOB.

    ReplyDelete
  66. Watu wanashindwa kuelewa tofauti ya kuelimika na kuuvaa uzungu. wewe kama unadhania kuwa etu Zuma fala, embu soma historia yake. Zuma ni mjeshi tena ni kiboko.

    Sababu mojawapo ya mapigano ya ukombozi wa Afrika kusini ni kuwawezesha waafrika waweze kubakia waafrika. Sasa wenzetu "wathomi" mlioelimika ambao uafrika ni kitu kichafu kisichostaarabika kwenu, endeleeni kujikataa. Na huo upumbavu wenu ndo maana mnaamini kuwa majina kama Stewart au idris ni majina yanayowasogeza karibu na mungu.

    Poleni.

    ReplyDelete
  67. Naona mzungu kazi yake Afrika kashamaliza maana mapigano yake yote sasa yanafanywa na the "educated mwafrika".

    Hao ndio tishio kwetu sisi(villagers) maana wanakemea kile ambacho wanaona kimemkwamisha katika jitihada zake za kuwa mzungu mweusi.

    We soma tu comments zao hapa na zile za kina John Smith au Mary Hickebery from The Guardian U.K. Tofauti haipo maana huyo John Smith kweli anaweza kuwa ni mbongo.

    Job well done mzungu.

    ReplyDelete
  68. Rest in Peace Simba wa Vita, idadi ya watoto wa kwenye ndoa kama 15 hivi,na idadi kamili au ya watoto iliyokamilika fanya kama mara mbili ya hao 15.

    At least we can safely say watoto wako tunao kwenye kutafuta Maisha hujaiba na kuliachia Taifa Hasara. Katika Viongozi wooote wakubwa waliopita Tanzania Ni watoto wa kwako tu Mzee Kawawa,Wa Marehemu Edward Sokoine na wa Baba Yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere ambao wanaishi maisha ya Mtanzania wa kawaida.
    Mwenyezi Mungu atawaipia mema yote mliotutendea na kuukataa UFISADI. Amen..

    ReplyDelete
  69. Kuna ndugu yangu alisema tatizo la Afrika sio uongozi ni watu.. sasa naamini. Kuna wanaosema haya mambo ni mila na yadumishwe, na kuna wanaokemea hili jambo. Mimi binafsi namuona huyu bwana hafai kuwa kiongozi na kuna watu watasema mimi ninafikra za kitumwa. Swali langu nani anataka kupinga kuwa hii nchi ya Afrika Kusini itaharibika tu chini ya Uongozi wa watu kama hawa? Sisi Waafrika ndio maana wenzetu walioendelea wanatucheka tu na naona wanaamini kabisa sisi akili zetu nusu. Wakati walioendelea wakifunga balozi zao Kampala, mke wa Amini kakutwa kafa kwenye buti la gari sisi tulimchagua kuwa mwenyekiti wa OAU!!!
    Nchi inaangamia na ukimwi, Rais anaendekeza ngono, na watu wanashangilia. Nawapa SA miaka kumi tu na viongozi hawa, watakuja Bongo kutuomba msosi; si mmeona Zimbabwe?

    ReplyDelete
  70. big up sana mtoa maoni no Tue Jan 05, 11:10:00 PM: hili suala la fikra za mwafrika kutawaliwa na uzungu naona limeshika kasi haswa..mimi mkristo na ntakuambia kitu:leo hii ukienda kumbatiza mtoto ukampa jina la MAGANGA (MAANA YAKE JIWE KWA LUGHA FLANI YA WATANI ZANGU) utaambiwa sio jina la kikiristo lakini ukamuita PETER (JIWE HIVYO HIVYO KWA "KIDHUNGU") ama PIERRE (nadhani "spelingi" nimepatia) ambayo ni kifaransa na maana hiyo hiyo utaambiwa sawa hilo jina la kikiristo..cha ajabu anayekubishia usitumie jina la MAGANGA ni mweusi mwenzio...!!!!
    KWANGU MIMI nadhani mjadala wa ZUMA unafanana kabisa na mfano huo wa majina!WAAFRIKA BADO TUKO KWENYE DIMBWI LA UTUMWA WA FIKRA!na ole wetu na hizi tamthlia za kina "SALVADO" uafrika wetu wote kwisha!
    big up ma men ZUMA!

    ReplyDelete
  71. Wewe uliyeejiita akili, umekosea jina lako mwenyewe. Wewe unaitwa "akili za kizungu". Ni vizuri kwamba unajielewa kama una akili za kitumwa kwa sababu huo ni mwanzo wa kurekebisha upumbavu wako.

    Ukimwi upo dunia nzima, na usenge ndiyo chanzo kikubwa cha kueneza ukimwi. Lakini kwa kuwa Mungu wenu Mzungu ni msenge na anaruhusu usenge, hamuoni kama hilo ni tatizo.

    Ankal CCM usinibanie meseji yangu.

    ReplyDelete
  72. Michuzi are you serious? how could you have allowed comment ya anonymous ya jan 06 01:24 PM.. I mean really? I never comment on this website,though i usually come and read your articles and people's opinions ila leo nimeshindwa kuvumilia. I had thought so much of you, until i saw that comment! kwahiyo huyo Mungu Mzungu ni nani? I dont think you would have liked that comment if you were any other religion apart from Muislamu. Mnaudhi sana kila siku mnalia kuwa mnatengwa,mnanyanyaswa yet you are the ones who are associated with all the sinister things.. from kutukana wenzenu,to terrorism and all that crap. Yet you put up such a comment on your website? SHAME ON YOU. wether you put this message up or not,i could care less,ILA MESSAGE DELIVERED.

    ReplyDelete
  73. KUmbe Zuma anapenda Uislamu?

    hehehe


    (US Blogger)

    ReplyDelete
  74. wewe mtoa maoni wa Wed Jan 06, 08:53:00 PM

    Hivi umetoroka mirembe au vipi? kuna uhusiano gani wa uislamu na huyo jamaa aliyetukana wazunngu?

    Michuzi ni mwandishi aliyebobea, na tangu mimi nipo mtoto nakumbuka kuangalia picha zake gazetini (Na Muhidin Issa Michuzi)

    Anaielewa taaluma yake ipasavyo na anatundika maoni yenye mitazamo tofauti. kama umekasirika saga chupa ubwie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...