MAJ. PERFECT ANTHONY SHAYO
25/08/1955 – 23/11/2009

Sisi Familia ya Shayo, tunapenda kuwashukuruni nyote kwa upendo wenu, kwa kushirikiana nasi tangu mlipopokea taarifa ya kifor cha baba yetu mpendwa, Maj. Perfect Anthony Shayo kilichotokea Hospitali ya Muhimbili tarehe 23/11/2009 na kuzikwa (Kimaroroni – Kilema) Moshi, Mkoani Kilimanjaro tarehe 27/11/2009.

Tunawashukuru kwa kutukimbilia nyumbani na kutoa salam zenu za rambirambi na kushiriki kwa hali na mali katika maandalizi na mazishi yake.

Tunamshukuru Dr. Kisanga na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Muhimbili. Dr. Green wa Hospitali ya Temeke. Uongozi wote na Wafanyakazi wa JWTZ. Viongozi, wafanyakazi na waumini wote wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) – Kurasini. Uongozi na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Maurusi – Kurasini. Parokia ya Mtakatifu Bernadeta Kilema – Moshi. Viongozi na wanajumuiya wote wa Jumuiya za mtaa wa Mtoni na Sabasaba, Jumuiya ya Mtakatifu Benedict. Majirani zetu wote wa Mtoni Dsm na Kilema Moshi. Ndugu jamaa na marafiki zetu wote ambao mlishiriki nasi kikamilifu katika kuomboleza, kuandaa na kushiriki katika kufanikisha mipango ya mazishi ya Baba yetu mpendwa hapa Dar es Salaam na Moshi – Kilema.

Tunapenda kumshukuru kila mtu na kumtambua binafsi. Hatuna maneno zaidi ya kuelezea vya kutosha jinsi tulivyoguswa na upendo wenu mioyoni mwetu, tunachoweza kusema ni Asanteni Sana. Tulifarijika sana kwa upendo wenu na kushiriki nasi katika kipindi hicho kigumu tulichopita.
Mungu awabariki nyote.

Misa ya Kumuombea Marehemu Baba yetu mpendwa itafanyika Jumamosi tarehe 9/01/2010. Saa nne Asubuhi, Nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ally.

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PERFECT ANTHONY SHAYO MAHALI PEMA PEPONI.
AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. R.I.P mzee shayo.
    Belinda na Gisela poleni sana dadazangu kwa msiba wa mzee wenu ndo kwanza napata taarifa saiv kny michuzi apa. Dah mipango ya mola yote, sipo nchini ndo maana hata info imekuwa ngumu kupata.
    POLEENI SANA jamani.

    Chebich.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...