Stars United
Uganda
Zambia Stars

Timu ya Stars United inayoundwa na wachezaji Wabongo kutoka kila State hapa Marekani,april 24 mwaka huu itakua mjini Boston kwa mechi ya matayarisho na safari ya Sweden,ambayo inatarajiwa kuondoka july 22 mwaka huu baada ya mashindano ya kombe la Dunia,kuelekea mjini Stockholm
Katika kujipima ubavu, Stars United itacheza mechi mbili dhidi ya Uganda na Zambia Stars Na tayari imewaongeza Francis Makala, Ally Hilary,Said Shela (kutoka Massachusetts), Walter(Houston),Victor Kileo na Aristot Maruma(Dc) na Godfrey Oswald(Minnesota).

Tunaomba wachezaji Hamisi (Dallas Texas), Michael Mngodo(Columbus Ohio) na Hakim Majaliwa kuwasiliana na uongozi wa Stars haraka iwezekanavyo kwa ajili kujiunga na kambi itakayokua chini ya Kocha Juma Maswanya (Houston). Wasiliana na Salum Salum,Ma,(617 308 2971) au Luka Kinyang'anyiro,Dc,(240 595 9874)au barua pepe starsunited@live.com

Kabla ya kuelekea Massachusetts Stars itakuwa na mechi nyingine April 3,Dc,dhidi ya Timu ya Maryland United, timu inayoundwa na wachezaji kutoka mataifa yote DMV.(DC,Md,Va) hii siku ni Re-union ya timu hii ya Maryland united. Siku hiyo kutakua na nyama choma kibao na uongozi wa Md united itakabidhi zawadi mbali mbali kwa wachezaji wote wa zamani.

Uongozi wa Stars United umeisha wasiliana na mwenyekiti Jumuia ya Watanzania Sweden, Zam Khalfa na timu kepteni Jameer,tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu,na matarajie kandanda safi kiwango cha TBS.

Asante
Uongozi Stars United

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. MASALIMIENI JUMA MASWANYA MY CLASSMATE AT MZUMBE SECONDARY SCHOOL, HE WAS PLAYING FOR A SCHOOL TEAM WHEN WE WERE THERE AT MZUMBE SECONDARY SCHOOL. HE LOVED FOOTBALL.

    ReplyDelete
  2. Michuzi,
    Najua hii comment utaiminya lakini poa tu ujumbe utakuwa umekufikia. Unatuletea michezo isiyoeleweka unaacha kuleta habari za premier league ya kwetu.
    Ushabiki wako ni wa ovyo kwa mtu unajidai hii ni blog ya jamii. Yanga ikicheza na kushinda mbiombio unatoa taarifa. Simba imecheza na majimaji zii. Imecheza na Prisons kimya. Manyema na mtibwa umetoa. Kama Simba inakukera ki hivyo basi meza wembe.

    ReplyDelete
  3. asante uongozi ..kuna wachezaji wawili kutoka zanzibar wanataka kujiunga wako dfw area /arlington tx...wasliana nasi kwa number 817 524 7146

    ReplyDelete
  4. Hamisi (Dallas) yuko TZ kwa likizo akirudi atapewa ujumbe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...