Ni matumaini yangu kuwa mwaka umeanza vizuri kwako, kila kitu kipo sawa. Sasa kaka mimi nilikuwa na Hoja moja ndogo nataka kushare na wana jamii katika blog letu la Michuzi ambalo lipo juu kila kona haswa kwa sisi wadau wa ughaibuni.
Kuna mtu alinikumbusha msemo mmoja wa wahenga (yaani wale wazee wetu wa zamani) , usemao kuwa : "akiri ni nywele, kila mtu anazake"; sasa swali linakuja kama akiri ni nywele, inakuwaje kwa wale watu ambao wana nywele chache na wale ambao wana Vipara?
ina maana watukuwa na mapungufu au huu msemo ni potofu?
embu wape wana jamii tusikie nao wanasemaje. hahaha.
Kazi njema kaka.
see you next time.
yours andrew c.
see you next time.
yours andrew c.
wewe nawe sidhani hata unaelewa unachosema! Hiyo ni lugha ya picha! Haina maaana kuwa kuwa ukipoteza nywele akili pia itapotea! Kwa mtazamao wako huo watu wote wenye vipara wangekuwa vichaa! Kipara kidogo! Kichaa kidogo! asiye na nywele kabisa huyo ni bonge la kichaa sio! Kwele majuu hamnazo!
ReplyDelete...nywele...nywere...oh, dear!
ReplyDeleteWalisema akili ni nywele...sasa kwa vile unaulizia "akiri" mimi hata sijui wasio na "nywere" "akiri" zao ni vipi...but I've seen some smart bolded people out there...but I guess we all born with hair that is what counts the most...ss kama umepoteza ur hair along the way that is not big no more...
ReplyDeletekwanza tuwekane sawa:
ReplyDelete"akiri ni nywele, kila mtu anazake'', una maana mtu ''amekiri ni nywele'' tunapokuja 'kila mtu anazake'' hapo umenipoteza kabisa.
Sasa kwa kubahatisha una maana msemo wa 'Akili ni Nywele, Kila mtu ana Zake' kama ni msemo huo nifahamishe ili tukupatie maana ya msemo huo.
Mdau
Tangamano
Mimi naomba nikurekebishe mdau mwenye swali tupate kuelimisha matamshi ya methali sahihi ni "Akili ni nywele kila mtu ana zake" na sio AKIRI... kwa wale tunaojifunza kiswahili fasaha...
ReplyDeleteBwana Andrew kama unavyojiita ! Sijawahi kusikia huo msemo " akiri ni nywele" msemo ninaoufahamu ni "akili ni nywele" hivyo ni vigumu kukupa jibu kwa vile unazungumzia "akiri" ambayo sijui maana yake.
ReplyDeletePole bob!!!
Mdau uliyeuliza hili swali , kwanza ungetueleza nini maana ya NYWERE na AKIRI ndipo baadae tungeweza kukupa jibu la swali lako.
ReplyDeletemdau mwenzio wa Musoma .
"akiri" ni "nywere" yaani the way kiswahili is being murdered these days is atrocious!!!
ReplyDeleteProper ki-swashili..... AKILI NI NYWELE.....
ndg andrew,akili ni nywele KILA MTU ANA ZAKE.....soma vizuri capital letters hizo ndio maana ya huo msemo,yaani wewe na mimi kila mtu ana akili zake kama vile nywele wewe unazako na mimi nina zangu.
ReplyDeleteha ha ha ha mtafute mwalimu wako wa kiswahili umchape viboko manake sijui ni uzembe wako au wa mwalimu wako shule uliosoma au ndio mambo ya ughaibuni unashindwa mpaka kufikiri?
ReplyDeleteWadau taratibuni msiwe wakali sana kwa muuliza swali.
ReplyDeleteHuyo lazima atakuwa ni wa-Tarime(Mkurya).Wao ni RRRRRRRRRRRRRRRR kwa kwenda mbele.Hata hivyo msemo sahihi ni "Akili ni nywele,kila mtu ana zake"
Hiyo ni lugha ya picha na ufundi wa kupunguza maneno.Tukirefusha msemo tunaweza kupata,"Akili ni kama nywele,kila mtu ana za kwake ambazo ni tofauti na za wengine"
Mdau
Mndengestan.
hahaha..na wale wenye rasta (zile extensions ambazo wanatumia hasa wakinadada)...hehehehe...
ReplyDeletePamoja na "r" zako za unakotokea naweza kukusaidia kwa kifupi sana:
ReplyDeleteAKILI NI NYWELE, ILA NYWELE SIO AKILI.
Osaki
Mdau kwanza inabidi uelewe kwamba hiyo ni nahau na kwa kuwa ni nahau maana haipatikani kwa kutfsiri maneno yaliyotumika moja kwa moja utapotea kama inavyokutokea.
ReplyDeleteMaana ya nahau hii ni kwamba kila mtu ana akili tofauti na mwingine na mtu huwezi kujua huyu anawaza nini katika kutathmini maswala na ndiyo maana kila mtu anakuwa na maoni tofauti na mwingine pamoja na kwamba mnaweza kuwa mnakaa pamoja mmezaliwa pamoja, mmefundishwa na mwalimu mmoja mnakula chakula chakula cha aina moja na kadhalika, yaani mazingira hayawafanyi mfanane akili kwa namna yoyote ile sawa na nywele ambapo unakuta kila mtu ana nywele lakini nywele hazitufanyi kuwa wamoja kiakili hata kama wote tunaweza kuwa na nywele zinazotufanya pengine tufananishwe lakini kila mtu anazo za kwake wengnie nyeusi sana wengine kipilipili wengine za mtelezo lakini zote zinaitwa nywele!
Waswahili bwana kwa maneno, hivi mnaotaka kujua mdau alikuwa na maana gani? imekuwaje tena mnafafanua kuwa Akili ni nywele?? Kama hamukuelewa alimaanisha nini mbona mmemkosoa na tena kuandika alimaanisha nini?
ReplyDeleteakiri...akili
ReplyDeletemweee kweli wewe ni mwisho...
ujiju
ASSUME YOU MEANT "AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE".
ReplyDeleteACHA UBWEGE, TULETEE HOJA ZA MAANA.
KWANI NYWELE ZA BINADAMU ZIKO KICHWANI PEKEE??
NDIYO, UNAZALIWA NA NYWELE ZA KICHWANI AND THEN UNAPOKUWA UNAKUA ZINAONGEKA NYWELE SEHEMU NYINGINE ZA MWILI.
BINADAMU ANAKUWA NA NYWELE MUDA WOTE WA MAISHA YAKE.
HUO MSEMO WA KISWAHILI UKO SAHIHI KABISA.
uyu jamaa msukuma,anatumia sana nguvu kutoa matamshi yake,kila akiongea kidogo anasikia njaa kwa ajili ya energy anayotumia.te te te
ReplyDelete............akiri ndio nini?
ReplyDelete................home work nyingine bana ! sijui mwalim ana mning'inio !?
ReplyDelete