Ankal samahani kama nitakuwa nakusumbua,
Katika kipindi cha jioni cha Jahazi cha Clouds FM wiki hii kumekuwa na swali ambalo wadau wametakiwa kutafuta jibu lake, nami swali hilo limenikuna sana nikaona labda nililete kwenye Blogu yetu ya Jamii ili nako lipate kujadiliwa na wataalamu ambao huku wamejaa lukiki.
Swali ni; JE TOFAUTI YA TUNDU NA TOBO ni nini?
Nawasilisha huku nikiomba msaada tutani....
Mdau Msasani


tundu linaweza kua tobo au sehemu ya kujihifadhia kama tundu la ndege. Tobo ni halina hifadhi lazima litokee upande wa pili lol!!!
ReplyDeleteTobo ni kubwa kuliko tundu.
ReplyDeleteNdio maana wanasema tundu ya simdano kwa kuwa ni dogo na haisemmwi tobo la sindano.
(US Blogger)
Tofauti hakuna yote yanamaana moja! tundu la sindano tobo la sindando! kalale ndugu!
ReplyDeletetundu halina upenyo/uwazi kwa upande wake wa pili hali tobo lina uwazi. maana unaweza ingia upande mmoja na kutokea mwingine
ReplyDeleteKuna Wengine wana Ma Tobo na hutokei upande wa pili hapo je? hahaaha, Tundu ya sikio Tobo Bao kazi kwelikweli Kiswahili chetu wenyewe kinatupiga Matobo. Pazi.
ReplyDeleteMimi naona mbele ni Tundu na nyuma ni ndio Tobo. simpo.
ReplyDeleteManeno hayo mawili mara nyingi yana maana moja. Ila kama uwazi umetokana na kitu kilichokuwa hakina uwazi kutengenezewa uwazi kwa kutumia kitu kingine kinachotengenezwa ni tobo na sio tundu (kutoboa hutengeneza tobo). Uwazi ukitengenezwa moja kwa moja kinachotokea ni tundu mfano tundu la choo.
ReplyDeleteTobo vilevile ni pale mwanasoka anapopitisha mpira katikati ya miguu ya mchezaji anayemkaba.
UKITAKA KUTOFAUTISHA YASEME YOTE MANENO MAWILI IKIWA NI KAMA KITENDO AU VERB, TOBO UNAWEZA SEMA TOBOA, UKIMAANISHA ADI UPANDE WA PILI, NDEGE AKIWA TUNDUNI INAMAANA KUNA MLANGO MMOJA. ASANTE.
ReplyDeleteTobo lina uwazi pande zote mbili yaana waweza ingiza/tolea upande mmoja na kutokea upande wa pili wakati Tundu lina uwazi pande moja tu ya kuingia tu.
ReplyDeletekwahiyo huwa tunaingiza kwenye tobo au tunduni?
ReplyDeletemimi naomba kuongezea neno lingine zaidi ya hayo mawILI YAANI NINI TOFAUTI KATI YA TOBO TUNDU NA SHIMO.
ReplyDeleteMdau
Astaghafulilah wabara mshalaaniwa nyinyi, Yakhe inabidi mje zanzibari tuwaonyesheni hayo matundu na matobo yenu
ReplyDeleteTundu na Tobo ni maneno ambayo yanafanana sana kimaana na unaweza tumi moja badala ya lingine.Kinachotofautisha ni mazingira ya matumizi kulingana na asili ya tukio.Tobo mara nyingi ni uwazi unaotokea upande wa pili ingawa hata tundu lawezatokea upande wa pili.Mfano ukikata kipande cha bomba,ule uwazi ni tundu na unatokea upande wa pili.Lakini katika lile bomba ukilitoboa utaita tobo,kwamba ukiangalia kwa ubavuni ni tobo na ukiangatalia katikati ni tundu..Pia tundu asili yake ni mviringo tobo sio lazima liwe na mviringo.Ndio maana Malenga tunasema "Tobo pevu ni tundu angavu" Mdau uliyeongeza neno Shimo. Shimo ni tundu kubwa lililo chimbwa ardhini.Mf shimo la choo au la taka
ReplyDeleteYOTE NI MATUSI, UKISEMA TUNDU, TOBO AU SHIMO YOTE YANANISISIMUA
ReplyDeleteHapo ni watu waliharibu kiswahili hamna kitu kinachoitwa tobo, bali ni toboa(verb)matokeo ya kutoboa unapata tundu(noun) ....Nyingine hiyo nini tofauti ya ng'ombe na mbuzi?
ReplyDeleteTUNDU-kama ilivyo neno hili ni tata.kwa maana yaweza kuwa na maana zaidi ya moja.Na tofauti yake yaweza eleweka kutokana na mtumiaji wa neno hili, au msikilizaji na wakati wa kulitumia.
ReplyDeleteMfano-Njiwa kaingia "Tunduni".Kumbuka tundu hutengenezwa na na binadamu kw madhumuni ya kufugia ndege wafugwao.Ndege wa porini wanajenga VIOTA, sio matundu.
Kitu muhimu Tundu linaweza likawa na matobo, lakini matobo hayawezi kuwa na tundu.
Maana nyingine ya TUNDU, ni uwazi uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kazi fulani,mafano tundu la sindano, au tundu la funguo.
TOBO-mara nyingi hutokea bila ya kukusudia, na kitu kikiwa na tobo basi kwa asilimia kubwa hakikidhi haja ya matumizi iliyokusudiwa.Shati likiwa na tobo halivaliki, lakini pale tunaposhikiza vifungo vya shati ni matundu ya shati na sio matobo yale.
Nimejaribu kuwa as simple as i can but najuwa kuna wajuaji humu wataleta "meanings beside primary meanings"-Nawasilisha.
Hakuna tofauti hapo, ni sawa na sumni na senti hamsini.
ReplyDeleteTundu imekaa kimpagilio wakati Tobo limekaa ovyo ovyo.
ReplyDeleteMdau
Kibandamaiti
Tundu ni tobo ambalo halitokei upande wa pili au kwa maana nyingine linahifadhi.
ReplyDeleteTobo lina sehemu ya pili ya kutokea hata liwe refu.
Yakhee,Kondaa.
ReplyDeleteTuweke Michenzani hapo tobo la pili.
Mzee wa kubonyeza Kizenji
mdau wa msasani usijifanye mchanja sana na wamjini nishakustukizia wewe hutaki maana ya maneno haya ila una lako jambo basi kamtafute wa kutoboa umtiye tundu sawa.
ReplyDeletebro weke hii comment
Unaweza kutoboa tobo lakini sijasikia kutundua tundu. Sasa kuna jamaa flani huwaga wanatoboa masikio. Yaani masikio yanakuwa na matobo, lakini kwa mfano mfuko ukitoboka huwaga unakuwa na tundu.
ReplyDeletejamani tunatofautiana viswahili,na matamshi pia,ila kwa wenzetu wazanzibar imetia fora, unapanda hiace unasikia shusha tobo la pili,mmh nikastuka nikawa natafuta hilo tobo liko wapi? kumbe ni njia iliyoko katikati ya flat. sasa hapa maana halisi ya tobo na tundu sijalipata wadau labda muelewa utuambie kama yapo kwenye kamusi ya kiswahili tufahamu
ReplyDeleteTOFAUTI "TUNDU Vs TOBO"
ReplyDeleteIpo tofauti kubwa kati ya "TUNDU" na "TOBO". Tukianza na TUNDU, ni sehemu yenye upenyo au uwazi unaoweza 'kufunga na kufunguka' na TOBO ni mithili kama hiyo hiyo yenye uwazi, lakini uwazi wake ni ule wa moja kwa moja, wenyewe huwa upo wazi mda wote hapafungi wala kufunguka, pako "TOBO" tu liwazi mwaa! Na mfano wa "TUNDU" ni kama vile sehemu ya kupitishia haja kubwa wakati mfano wa "TOBO" kama vile "Tunnel" (Passageway), unaingilia huku unakwenda kutokea kuleee! yaani ni mbele kwa mbele huko kwa huko, hakuna haja ya kurejea ulikoingilia na pia huwa liwazi 24/7 tofauti na TUNDU. Nadhani nimefahamika kwa kiasi fulani. Shukran.
Oprah, hujakosea ni kweli ukati mwingine tunatofautiana viswahili, matamshi na hata lafdhi pia na kama utakuwa umelitizama uzuri lilivyo hilo TOBO la pili ulilolielezea hapo,(najuwa ni pale Michenzani kama sikosei) basi lile ndio TOBO na TUNDU kama mfano la PUANI au hata sehemu nyingine lilipokuwa located,khususan katika mwili wa binaadam, kuna ma-TUNDU kadhaa (Ashakum si matusi), ila tu tofauti ya TUNDU, linafunguka na kufunga iwe 'automatically' or 'manually', wakati TOBO, siku zote au daima huwa lipo waziii! unaingilia huku unakwenda kutokezea kulee! Nadhani umenipata kwa kiasi fulani, shukran.
ReplyDeleteuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii u made my day uwiiiiii me wala sijawaelewa kabisaaaa labda tukasome ktk kamusi la kiswahili lol
ReplyDeleteila wee Oprah zenji "eti shusha tobo la pili jicho likakutoka kuona ilo TOBO" hahahaaaaaaa
hahahahaaa hii ya 2010