WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA DR. MARY NAGU AKIMKARIBISHA WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA WA CHINA MHE. CHEN DEMING KWENYE UZINDUZI WA UJENZI WA JENGO LA MIKUTANO LA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVETION CENTRE JIJINI DAR LEO. JENGO HILI LITAKUWA KWENYE KIWANJA KARIBU NA UMOJA HOUSE AMA HOSPITALI YA TSPCA ZAMANI, JIRANI NA CHUO CHA IFM
WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA DR. MARY NAGU PAMOJA NA WAZIRI WA VIWANDA WA CHINA MHE. CHEN DEMING WAKIFURAHI BAADA YA KUZINDUA JENGO LA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVETION CENTRE LEO JIJINI DAR.
PICHA NA ANNA ITENDA WA MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwanini wanarundika kila kitu mahali hapo? Hii ndio ingalikuw anafasi ya kujenga nje ya mji ili kupunguza msongamano mjini aaaaghhh eeeeeeeer

    ReplyDelete
  2. naombea pia iwe sehemu yakufanyia concerts

    ReplyDelete
  3. hakuna jina lingine zaidi ya nyerere? mpk inakera sasa
    tafuteni sehemu za kujenga nje ya mji, hapo hata security itakuwa mbovu mlundikano ni mkubwa sana nakufikia eneo hilo ni ngumu mafoleni sijui baada ya miaka 5 itakuweje

    ReplyDelete
  4. Convention Centre ki kawaida huwa inakuwa downtown. Au hamjatembelea mamiji ya wengine mkaona. Anyway katika Africa kusini mwa jangwa la sahara hizi convention Centre ziko kule kwa Mzee Zuma pekee. Mfano pale Jopburg kuna hii Sandton Convention Centre katikati ya Sandton City kwenye ma-shoping kibao, kule Cape Town kuna hii Cape Town Concentionm centre nayo iko katikati ya jiji la Cape Town, pale Durban ile International Convention centre nayo iko katikati ya jiji la Durban...sasa kipi cha ajabu hapo.
    Kinachotakiwa kufanyika ni kuweka barabara zote za jiji katika hali inayotakiwa na kuwashauri madereva wa DAR waache tabia yao ya kuendesha magari kama walevi....ndo wenzetu wanafanya hivyo ebo...jamani bado jiji la Dar lina nafasio kibao. Tunataka kila kona iwe na jengo kama PPF tower, Mfuta hse, extelecom, exim tower, nk nk

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu Anon wa Fri Jan 15, 10:08:00 pm. Hata mimi nashangaa. Wangetafuta ardhi maeneo ya Chanika na wajenge a multipurpose convention centre. Sijui kama nafasi ya pale pa sasa panatosha. Kungekuwa na faida nyingi sana za kujenga Chanika kama vile:1. Ukaribu na Airport 2 kuepuka msongamano3Miundombinu mizuri ingepatikana na kwa njia hio hata Kisarawe na uzaramoni kunge grow4 Wawekezaji kama vile property developers wangewekeza maeneo hayo. Kufuatana na Presidential Order ya 2000 maeneo ya Chanika, Pugu, Majohe na ya pembezoni ya DSM hayana sifa ya kuwa vijiji tena bali miji. Sasa mimi ningekuwa mtoa maamuzi ningewashawishi Wachina tukaijenge hico kituo huko. Halafu baadhi ya facilities ambazo tungejenga hukoi ni hoteli ya 5 star, kumbi za Cinema, Casino, Kumbi kwa ajili ya big time entertainers wa calibre ya akina Michael Jackson, kumbi za michezo kama ya ngumi, Ice na hockey skating. Facility kama hii ingevutia sana mikutano na burudani nyinginezo. Sasa sijui kama huu wa Nyerere utakuwa na vikolombwezo(superstructures) hivyo.

    ReplyDelete
  6. Du,Tanzania, Tanzania Tanzania, Viongozi na Wabongo wote nahisi aliyetulaani ameshakufa. Hivi ninajiuliza ina maana hili jengo tungejenga nje ya jiji la Dar es sallam tungekufa?
    Ikitokea tuna mkutano mkubwa wa viongozi wa afrika tutakuwa na mapunziko hatutakwenda kazini? maanake hiyo misururu tu ya kusubiri wapite si tutalaala?
    Pata picha kwenda kumzika kiongozi maarufu tu Mzee wetu pale MADALe wengine tulikaa barabarani masaa tukisubiri viongozi wetu watoke kuzika.
    Bush tu alipokuja mjini tulifungiwa barabara sasa leo jengo hili si kusimamisha uchumi wa nchi?
    Wanaharaki, wanataaluma tuko wapi tuamke tuandamane tupinge maamuzi kama haya yasiyohitaji hata nguvu kufikiria?
    HELA NYINGI ZA TAIFA ZINATUMIKA KUJENGA KITU AMBACHO HATUJAANGALIA MADHARA YAKE KIUCHUMI,
    IMETOSHA JAMANI HII SASA NIA AIBU.
    HAWA NI VIONGOZI BORA AU BORA VIONGOZI?

    ReplyDelete
  7. hata sioni nafasi ya kujenga hilo jengo iko wapi pale. Nahisi tumelogwa si bure. Hata kufikiri hatuwezi. Mapori yote yaliyopo hata hapo bagamoyo. Sijui naona giza mbele kwa maendeleo ya Nchi yetu hii.

    ReplyDelete
  8. Wenzetu wanajitahidi kupunguza msongamano wa majengo katikati ya miji,sisi pamoja na kujaliwa ardhi sehemu lukuki za jiji bado tunajiminya posta tuu.parking,miundombinu hewa..! kweli wahandisi + siasa haviendi!!!

    ReplyDelete
  9. Candid ScopeJanuary 16, 2010

    Wanamipango miji wanafurahia kwa kujienzi kuweka mikakati ya majengo marefu bila kufikiria usafiri na nafasi ya kupaki makagri. Huko wanakotaka jenga hiyo center kutakuwa na parking ya kutosha ya magari au watu waache magari kariakoo na jangwani kisha wadandie vipanya kwena huko?

    ReplyDelete
  10. Waheshimiwa, wekeni sawa na miundombinu kwanza, jamani mipangilio gani hiyo isiyo na kichwa wala miguu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...