Profesa Benno Ndulu
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuteua mthamini huru ambaye atachunguza na kupitia taratibu na hesabu zilizotumika katika ujenzi wa nyumba mbili za viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kamati hiyo ilitoa agizo hilo jana baada ya kupokea maelezo ya Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, kuhusu ujenzi wa nyumba hizo – ya Gavana na ya Naibu wake - ambazo zinadaiwa kukarabatiwa kwa zaidi ya Sh bilioni moja.
Kamati hiyo ilitoa agizo hilo jana baada ya kupokea maelezo ya Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, kuhusu ujenzi wa nyumba hizo – ya Gavana na ya Naibu wake - ambazo zinadaiwa kukarabatiwa kwa zaidi ya Sh bilioni moja.
Habari kamili



Kaaaazi kweli kweli.
ReplyDeleteHapo wanatumia tu fedha za walipa kodi bila msingi. Hao walio lamba huo mlungula hawakulamba kienyeji.
Tunachotaka kujua sisi ni priorities katika matumizi ya fedha za umma. Nani anapanga billion 1.2 kukarabati nyumba badala ya kujenga shule au barabara?
tunarudi kulekule,inaundwa tume/kamati ambayo inachunguza hela ambazo zishapotea/fisadiwa, kamati itatumia fedha nyingi then watatuambia hakuna ufisadi....
ReplyDeleteNi faraja kusikia Prof Ndullu anatetea mchakato mzima wa ujenzi wa nyumba za vigogo hao wa bot kwamba sheria za manunuzi nk za miaka 2003, 2004, 2006, na 2007 zilizingatiwa. Tunaamini kuwa Prof Ndulu hajavunja sheria yo yote kwanza kabisa kama maamuzi yalifanywa miaka ya 2007, basi aliyefanya maamuzi hayo ni gavana aliyemtangulia, hayati Balali - ambaye pia alikuwa mchezaji wa kiungo katika kashfa za EPA na minara-pacha ya BOT ambayo leo hii imempeleka Bw. Liyumba mbele ya pilato. Hapana shaka na ujenzi wa minara-pacha ulizingatia sheria fulani za miaka fulani!!
ReplyDeleteHiyo ndio sifa kuu ya mfumo ambao wataalamu wa mambo ya siasa na utawala wanauita kwa kiingereza kleptocracy (na sisi tumepata jina lake sadifu - ufisadi)ndani ya jaketi la utawala bora. Kila tendo la kifisadi hupatiwa maelezo mazuri na ya 'kitaalamu'! Juzi tumesikia Mhe. Msekwa akitoa maelezo mazuri ya kutetea kwa nini hajamaliza deni la serikali alilokopa miaka saba iliyopita kwa ajili ya matibabu ya kijana wake! Hajavunja sheria. Kelele za wananchi sio juu ya kufuata sheria za mwaka xyz, bali wanahoji hata hizo sheria mnazozitaja (ambalo sio kosa la mtu binafsi) ambazo ndio security system ya ufisadi. Ni nani atakayebadilisha mwelekeo huu wa sheria za kifisadi kama sio maprofesa kama prof ndulu? ulipochukua madaraka ungeweza kukataa baadhi ya vitu ambavyo ni vya kifisadi na kuwa-influence akina Zitto na wenzake kurejea bungeni na kuunda sheria upya zinazozingatia maslahi ya umma. Hukufanya hivyo, na badala yake unatetea maamuzi yaliyofanywa na waliotangulia ambao sifa zao zinafahamika hata kwa watoto wa shule ya msingi!!! Prof hujavunja sheria, lakini unatetea ufisadi. Kwa maoni yako hayo tunashangaa kwa nini hajamtetea Liyumba kuwa alikuwa anafuata sheria za mwaka 2003.
KITU NI KWAMBA SI NYUMBA ZIMEGHARAMIWA KIASI GANI CHA PESA, TATIZO NI KWAMBA KULIKUWA NA UMUHIMU GANI WA KUJENGA HIZO NYUMBA MPYA? PAMOJA NA HAYO LAZIMA KULIKUWA NA ULAJI PIA HAPO ULIOPELEKEA UJENZI HUO, HUWEZI KUJENGA NYUMBA KWA MABILIONI YOTE HAYO WAKATI WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI WANASOMEA PORINI, LAZIMA TUWE NA PRIORITY. BAADAYA YA UCHAGUZI WAPIGWE CHINI HAWA, NA TUELEZWE HIYO WAKATI WA KAMPENI ILI TUAMUE NANI TUMPE KURA ZETU
ReplyDelete