Kipa wa manyema Rangers, Odo Nombo akiusindikiza kwa macho mpira wa penati uliopigwa na Mrisho Ngasa na kuzaa bao la pili katika mchezo uliofanyika kwenye dimba la neshno ya zamani la Uhuru leo jioni. Yanga imeshinda bao 3-1
Beki wa manyema Rangers, Buji Ally (kushoto) akijaribu kumzuia mshambuliajui wa Yanga, Kigi Makassy katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo uliofanyika leo kwenye dimba la Uhuru leo jioni.
Mshambuliaji wa Yanga, Nurdin Bakari (katikati) akijaribu kuwatoka walinzi wa Manyema Rangers, Adam Matunga (15) na Julius Mrupe wakati wa kinyang'anyiro cha Ligi Kuu ya Vodacom mchezo uliofanyika leo jioni kwenye dimba la Uhuru jijini Dar.
Kocha wa Manyema Rangers "mkuki wa sumu" Abdallah 'King' Kibadeni (kushoto) na benchi lake la ufundi wakifuatilia mchezo kati ya timu yake na Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar. Yanga imeshinda 3-1. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mwendo Mzuri yanga bila shaka tutafika tu kwenye Ubingwa>Yanga oyeee.
    Mwana Yanga asili.

    ReplyDelete
  2. Jana simba kashinda mbona haukuposti?

    ReplyDelete
  3. hongera yanga,nafasi ya pili ni yenu,maana mwendo ni mzuri

    ReplyDelete
  4. Ankal hii ni blog ya jamii sasa mbona unaleta unazi za yanga umeziweka za simba mbona umezibania inakuaje kuaje hapo?

    ReplyDelete
  5. Aahh! Baba-Abdalah King Kibaden Mputa. Maneno ya Sinza Kwa Remmy ayo baba!

    ReplyDelete
  6. kocha yuko kwenye benchi huku ameshika mobile phone?? ina maana anaweza kupigiwa simu na akaipokea!!

    wacha timu yake ifungwe!!!

    ReplyDelete
  7. No way,this is unfair,au ndio unazi wenyewe?Mbona Simba wameshinda juzi hukupost kwenye blog yako?kuwa fair michuzi tunakuaminia ktk kutujuza habari mbalimbali,usituangushe bwana na si Simba tu,hata matokeo ya mechi nyengine tutafurahi zaidi.Asante.

    ReplyDelete
  8. king kibaden ni mchezaji wa kuigwa tz.

    ReplyDelete
  9. UNCLE MICHUZI BLOG YAKO HUWA INATOA MATOKEO YA YANGA TU... MATOKEO YA MNYAMA (SIMBA) HUYAWEKI KAKA AU UNASUBIRI MPAKA SIKU TUFUNGWE? HUTUTENDEI HAKI.

    NDIYO TUNAJUA WEWE NI YANGA LAKINI UNASAHAU KUWA HII BLOGU NI YA JAMII SIYO YA YEBOYEBO PEKE YAO UNCLE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...