Na Veronica Kazimoto – MAELEZO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Aloyce Mwamanga kuwa mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia mkoa wa mbeya utakaodumu kwa muda wa miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Florens Turuka imemwelezea Mhandisi Aloyce kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya PEMACO BEVI Limited na ni Raisi wa TCCIA.

Wakati huo huo waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa. Peter Msolla amewateua wajumbe tisa kuwa wajumbe wa Baraza hilo laTaasisi ya Sayansi na Teknolojia.

Wajumbe hao ni Bwana Suleiman Mmwiri kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Bwana Ignatus Herman kutoka Chuo cha teknolojia ya uhandisi cha Mtakatifu Joseph, Profesa Evelyn Mbede kutoka Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Bibi Monica Mbelle kutoka VETA kanda ya Kusini.

Wengine ni Mhandisi Asantiel Elias kutoka kampuni ya saruji mbeya, Bibi Margaret Mgaya kutoka Taasisi ya kilimo uyole, Prof. Joseph Msambichaka kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya, Dkt Lusajo Minga kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya na Venance Mwakosya kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...