Kinyaunyau
Mwanamuziki mkongwe wa Kilimanjaro Band "Wana Njenje" Mabrouk Omar amepata mstuko katika enka ya mguu wake wa kushoto baada kuteleza na kuanguka kwenye ngazi za kupandia jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cho kipya cha maraha wanapotumbuiza siku hizi kila Jumamosi cha Salender Bridge Club maarufu siku hizi kama daraja la manyoya....Kiongozi wa bendi hiyo maarufu, Waziri Ally, kaiambia Globu ya Jamii sasa hivi kwamba Babu Njenje hivi sasa yuko nyumbani kwake akipumzika baada ya kuruhusiwa na madaktari ambao wamempima na kukuta hana madhara makubwa isipokuwa enka yake hiyo imepata mstuko katika ligamenti baada ya kuteleza na kuanguka.
"Babu Njenje hajambo na kwa kweli tunawashukuru mno wapenzi wetu kibao ambao wamekuwa wakifuatilia hali yake kwa njia ya simu ndani na nje ya nchi" amesema Waziri, akiongezea kuwa Babu Njenje hajambo na hamna haja ya kuwa na wasiwasi wote na kwamba Jumamosi ataonekana Jukwaani kama kawa hapo Salender Bridge club.
Zaidi


Pole sana Babu Njenje Mwenyezi Mungu mkubwa amekunusuru na hilo akunusuru na mengine zaidi na Inshaallah kwa uwezo wake Mola utapona na kurudi katika afya njema nasi wapenzi wako tunazidi kukuombea.
ReplyDeleteDuuh, babu Njenje pole na tunashukuru hakuna maradha makubwa yaliyotokea, M'nyazi Mungu azidi kukuafu ili uendelee kutuburudisha. Kaka Waziri upooo?? Nduguyo na shabiki wa siku nyingi London.
ReplyDeleteUK
Aya we!
ReplyDeleteWashamwendea NGENDE hapo.
Waswahili kwa wivu bwana!
Pole babu njenje...Nafikiri ishu ya manyoa bado inawatesa watu pale....mara Joti,mara babu njenje....more to come....
ReplyDeletepole,nyimbo zenu me zinanikosha balaa
ReplyDeletendo mahali pa kujifuzia viuno