Kinyaunyau
Mwanamuziki mkongwe wa Kilimanjaro Band "Wana Njenje" Mabrouk Omar amepata mstuko katika enka ya mguu wake wa kushoto baada kuteleza na kuanguka kwenye ngazi za kupandia jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cho kipya cha maraha wanapotumbuiza siku hizi kila Jumamosi cha Salender Bridge Club maarufu siku hizi kama daraja la manyoya....
Kiongozi wa bendi hiyo maarufu, Waziri Ally, kaiambia Globu ya Jamii sasa hivi kwamba Babu Njenje hivi sasa yuko nyumbani kwake akipumzika baada ya kuruhusiwa na madaktari ambao wamempima na kukuta hana madhara makubwa isipokuwa enka yake hiyo imepata mstuko katika ligamenti baada ya kuteleza na kuanguka.
"Babu Njenje hajambo na kwa kweli tunawashukuru mno wapenzi wetu kibao ambao wamekuwa wakifuatilia hali yake kwa njia ya simu ndani na nje ya nchi" amesema Waziri, akiongezea kuwa Babu Njenje hajambo na hamna haja ya kuwa na wasiwasi wote na kwamba Jumamosi ataonekana Jukwaani kama kawa hapo Salender Bridge club.
Zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pole sana Babu Njenje Mwenyezi Mungu mkubwa amekunusuru na hilo akunusuru na mengine zaidi na Inshaallah kwa uwezo wake Mola utapona na kurudi katika afya njema nasi wapenzi wako tunazidi kukuombea.

    ReplyDelete
  2. Duuh, babu Njenje pole na tunashukuru hakuna maradha makubwa yaliyotokea, M'nyazi Mungu azidi kukuafu ili uendelee kutuburudisha. Kaka Waziri upooo?? Nduguyo na shabiki wa siku nyingi London.

    UK

    ReplyDelete
  3. Aya we!
    Washamwendea NGENDE hapo.

    Waswahili kwa wivu bwana!

    ReplyDelete
  4. Pole babu njenje...Nafikiri ishu ya manyoa bado inawatesa watu pale....mara Joti,mara babu njenje....more to come....

    ReplyDelete
  5. pole,nyimbo zenu me zinanikosha balaa

    ndo mahali pa kujifuzia viuno

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...