BANZA STONE AKICHENGUA MASHABIKI

Msanii maarufu wa Muziki wa Dansi Nchini Ramadhani Massanja Maarufu kama Banzastone Jumapili ya siku ya Wapendanao anatarajia kufanya onyesho maalum katika kusherehekea siku ya wapendanao katika Manispaa ya Iringa.

Banzastone ambaye alijizolea umaarufu mkubwa alipokuwa katika Bendi za African Stars twanga Pepeta pamoja na TOT Plus ameahidi kufanya kweli katika onyesho hilo na amedai yuko kwenye maandalizi makali ili kuweza kukonga nyoyo za mashabiki wake wa Iringa.

Onyesho hilo maandalizi yake yote yamekwisha kamilika na limeandaliwa na Bendi ya Sweet Noise yenye maskani yake mjini Iringa ambayo siku ya Onyesho Banza anatarajia kuimba nayo live.

Onyesho hilo linatarajiwa kufanya katika CLUB VIP na itawashirikisha pia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya ambao bado wako kwenye mazungumzo.

Maandalizi yote ya onyesho hilo yamekwisha kukamilika na wapenzi wa Iringa wanashauku kubwa ya kumouna Banza live akiburudisha baada ya muda mrefu kuwa mgonjwa na hivyo kumpelekea kushindwa kupanda jukwaani kutoa burudani.

Banza mara baada ya kuwasili manispaa ya Iringa anatarajiwa kuimba nyimbo zake zote zilizompatia umaaruku mkubwa kama, Mtu Pesa, Mtaji wa Masikini, Kumekucha, Elimu ya Mjinga na nyinginezo nyingi.

Ziara ya Banza Iringa imedhaminiwa na EBONY FM.

HASSAN REHANI
MRATIBU WA ONYESHO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. duh mjomba kachoka!! keli bongo shemsha bongo

    ReplyDelete
  2. Jamani mbona amechoka sana? Mwili haujngwi kwa matofali jamani, mlo muhimu

    ReplyDelete
  3. Mambo yetu yale ukipiga unakuwa huna hamu ya kula....kwanza unajiona upo New York, Paris, London....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...