songombingo la magari katikati ya jiji la dar. hapo daladala hazijajumuishwa na ni karibu na posta mpya. kifanyike nini kuondoa msongamano jijini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. waimprove public transport, naona watu watapark magari yao nyumbani na kuchukua usafiri wa public kama ni mzuri

    ReplyDelete
  2. Kazi rahisi hilo ghorofa hapo mbele libomolewe limejengwa barabarani then magari yatapita fresh..

    ReplyDelete
  3. Michuzi wake fee kuingia city centre .

    mdau EU

    ReplyDelete
  4. mimi nahisi tujenge fly over tu hlo ndo suluhisho kwani nchi zilizoendelea si ndo walivyofanya ila wasiwasi wngu huu mradi ni kama wa miaka mitatu utachukua miaka kumi haujaisha na hela haijulikanai wapi imepotelea.
    HYD

    ReplyDelete
  5. 1. Madereva wafuate sheria (Vyombo husika vihakikishe hilo kwa kutunga sheria kali (Adhabu, faini) dhidi ya utovu wa nidhamu barabarani(Kuchomekea, kufurukuta, kupakia na kushusha sehemu zisizo vituo, kupaki gari sehemu si stahili nk).

    2. Uwekwe utaratibu mabasi yawe na njia zake tofauti. Mafano barabara za njia 2, moja itengwe kwa ajili ya mabasi na taxi.

    3. Ziachwe taa kufanya kazi, badala ya trafiki kuongoza magari. Hii ikiambatana na pendekezo namba moja hapo juu, mambo shwari.

    4. Zijengwe njia za pembeni. (Sio lazima fly overs kwani ni gharama. Mfano, mtu anayetokea barabara ya kawawa kinondoni kwenda Muhimbili, hana haja ya kupita magomeni/Jangwani/fire ikiwa kutakuwa na njia fupi tu pale (Daraja lingine). Hali kadhalika, mtu wa kutokea kimara kwenda mwenge/tegeta/mbezi beach hatakuwa na haja ya kupita Ubungo ikiwa kutakuwa na mchepuo mfano kutoka Kibo hadi samnujoma mbele ya daraja nk.

    Wadau toeni mapendekezo katika maada hii muhimu. Huenda authorities zikachukua yale ya kujenga,'

    Mdau wa Isimani.

    ReplyDelete
  6. Asante sana Anko Michuzi kwa kuendelea kuhabarisha kupitia globu ya jamii.
    Hii ndiyo athari ya kukua kwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.Kila mwenye gari anaona ni vema alitumie hata pale ambapo si lazima sana kuingia na gari lake hapa Dar City Center.Uamuzi huu wa kibnafsi kwa kila mdau mwenye usafiri wake ni matokeo ya kukosekana kwa usafiri wa umma unaolingana na hadhi ya Jiji na usio na ratiba wala mwelekeo na kuwaacha wadau kukimbizana kuanzia kombora hadi lala salama.Usafiri wa daladala ni kero tupu kuanzia wahudumu wake wasiozingatia usafi wao binafsi,magari yao na lugha zao zilizosheheni kero tupu.Kwa ujumla SUMATRA imekosa wanazuoni mahiri makini katika tasnia ya usimamizi wa usafirishaji abiria mijini nchini Tanzania.Wao wamekeza kwenye makusanyo ya faini na adhabu badala ya elimu kwa umma.Imeshindwa kuishawishi serikali iondoe kodi na ushuru kwenye mabasi mapya yenye uwezo wa kusafirisha abiria 50 na kuendelea ili kuwa na usafiri wenye hadhi na staha ya mjini.Mamlaka za miji nazo zinaendeleza kigugumizi katika kubuni na kukarabati barabara za miji husika kulingana na mahitaji ya wakati husika.Mimi nahisi sasa ni wakati ufaao kwa kila kata kupewa uwezo wa kusimamiana na kuboresha miundo mbinu ya barabara kwa ushindani ili kuwafahamu viongozi wazembe na wasiotimiza majukumu yao ifaavyo kwa jamii.Huu ni wakati ufaao kwa mamlaka za miji kubuni vyanzo vya mapato kwa ajili ya kuboresha na kudiumisha miundo mbinu ya barabara kwa kila kata na kufanya tathimini baada ya kila robo mwaka na mwishoni mwa mwaka.Mwalimu Nyerere alisema:"I CAN BE DONE PLAY YOUR PART" na Nkwame Nkurumah alisema:"DAIMA MBELE NYUMA KAMWE".Anko naomba kuwasilisha hija na kuendelea kuomba nguvu za hoja na hoja za nguvu kutoka kwa wadau wa globu ya jamii.

    ReplyDelete
  7. Msongamano huu utaisha iwapo tu maofisi nyeti yatahamishwa kwenye pande mbali mbali za Mji badala ya kujazana mjini...Tunashangaa vipi msongamano wa Magari hali ya kuwa ingebidi tushangae kwanza msongamano wa majumba huku katikati ya mjini??

    ReplyDelete
  8. Mji wa Dar centre lazima uwe traffic free zone totally. Dar iwe for walkers only. Nje ya mji kuwe na shehemu madaladala yatashusha watu na wafanyakazi wanaotaka kuingia ndani ja mji. Ndani ya mji kuwe na mabasi kama ma4 kazi yake ni kushusha watu/wafanyakazi ndani ya jiji vituo mbalimbali. Mabasi yawe ya Uuma na kupanda hilo basi lenye aircondition lazima nauli. Pesa za nauli zitachanganywa kwenye budjet ya mfuko wa pesa wa kumentain Dar city na mabasi hayo. only solution City centre free of traffic, hebu watanzania tujiendeleze. Hatuwezi pata underground train au metro in the city lakini we can make it a traffic free zone. its a beautiful city in Africa. I*m proud.

    ReplyDelete
  9. Kuna haja ya kujenga kuendeleza mji midogo, ama centers nje ya central business district, iliiweza kujitosheleza na kila huduma ambayo watu hufuata katikati ya mji.

    Pili barabara zinahitaji kupanuliwa na kuongezwa. Mfumo mzuri wa kuiingiza magari na watu ndani ya central business district na kuwatoa. Hii ni pamoja na kujenga majengo ya parking, na kuendeleza public transport kama trams, bus na treni, ili watu wasitegemea zaidi magari.

    ReplyDelete
  10. Watu wa ardhi waache kabisa kutoa vibali vya ujenzi wa maghorofa katikati ya jiji ili kupunguza idadi ya ongezeko la huduma ya huduma city centre.
    Ofisi zote za Serikali zingeamishwa toka City centre kama ilivyofanya Tanesco.
    Vyuo kama CBE,IFM,UHAZILI,DAR TECH,shule za Msingi, secondary,zingehamishwa katikati ya jiji,
    Barabara zingekua aina mbili tu yaani za kuingilia mjini na za kutokea tu kama ilivyo samora ambayo haihusishi magari yanayokwenda na kurudi wakati mmoja. Maeneo maalum ya parking yngetengwa ili kupunguza idadi ya magari yanayopaki kila nje ya ofisi ili kupunguza ile ingia toka ya magari ambayo nayo inachangia vijifoleni vya hapa na pale ambavyo mwisho huzaa msongamano kama huo. Nadhani kwa kuanzia yakifanyika hayo yatasaidia kupunguza msongamano.Japo kuna mambo mengi kama ujenzi wa fly overs, underground network ya treni. Kupiga marufuku private cars ndani ya city centre vitu ambavyo nadhani ni vya mbele sana, na vinaitaji mji mpya kwani kuufanya huu uliopo ambao hata ramani za mifereji ya maji taka hazijulikani zilipo itakua ni kazi ngumu.

    ReplyDelete
  11. "kifanyike nini kuondoa msongamano jijini?"......SIMPO, MOJA. Tusimamishe kutoa vibali vya majengo makubwa/marefu katikati ya jiji, wenye pesa za kujenga maghorofa wakajenge nje ya jiji (Kimara, Ubungo, Bunju,.......listi inaendelea) maeneo yapo kibao. PILI.
    Tuachane na haya masuala ya trafiki laits, tujenge fly-overs na under-pass kwenye junctions kubwa ili magari mengi yawe yanapita kwa wakati mmoja (tukiwa na NIA thabiti tunaweza, resources TUNAZO, wataalamu wapo, WASIKILIZWE).....NI MTAZAMO WANGU

    Chiggs

    ReplyDelete
  12. Wakati tunasubiri ufumbuzi wa kudumu, ambao ni flyovers a traffic officer should be posted hapo.

    ReplyDelete
  13. serikali iangalie magari yanayoingizwa manake mengine ni maozo hayafai hatakuwepo barabarani, insuanrance pia kodi ya old models zipandishwe sana

    ReplyDelete
  14. Badala ya wahandishi wa habari kukazania habari za kaj_mb@ nani, wangeangaza na macho kwenye hili.

    Ningependa siku moja watu wenye vipindi vilivyonda shule kama Mzee Adam Simbeye, wangewaita mwakilishi mmoja mmoja kutoka TANROOADS, Kinondoni, ilala, Temeke, na mwananchichi mmoja mmoja (aliyetulia) kutoka hizo wilaya wayazungumze pale kwenye TV.

    ReplyDelete
  15. Hii mnayoiita msongamano wa magari DAR ES SALAAM hadi inakuwa kero imesabibishwa na inaendelea kusababishwa na MGAWANYO MBAYA WA RASILIMALI NA VITEGAUCHUMI VYA TAIFA.
    Kila kukicha project mpya zinaanzishwa DAR, wizara zote ziko DAR, Shule na vyuo vikubwa vyote viko DAR,yaani kwa ufupi kila uchafu wote uko Dar.
    Sasa kwa mtaji huo unategemea msongamano utaisha kweli??? kwanini wasitawanye hizo wizara huko mikoani?? mfano wizara ya kilimo iwe huko mbeya/iringa/rukwa maana huko ndo wanazalisha chakula kwa wingi na waziri nae aishi huko huko!na wizara zote zingine zitawanywe pia.DAR wabakina bandari na mambo ya Financy ofcourse ikiweno Ikulu kwa kufanya hivyo hata ajira zitapatikana hukohuko mikoani na siyo Dar tu na hivyo pia balance ya magari na watu itakuwepo.
    Miji ya mikoani ingewezeshwa wala kusingekuwa na sababu ya watu kukimbilia Dar kama sehemu ya kupatia riziki yao.
    Kwahiyo hata kama wakijenga barabara za juu na chini na hata kama wakichimba tunnels kama mtindo utakuwa ndo huohuo wa kila project na kila kiwanda kuwekwa Dar huo msongamano utaendela kuwepo milele na watu watazidi kumiminika kila siku katika hhilo jiji lenu.
    Mdau mwenye kuona kushoto!wa kutoka kijiji cha BUSAWE-NGOREME-SERENGETI.

    ReplyDelete
  16. Kweri bongo tambalale!!! Tupende tusipende, wakati umewadia wa kukubali kuacha vijigari vyetu vya anasa Kwa Azizi Ali, Buguruni, Ubungo, na Mwenge na kuingia katikati ya jiji ama kwa daladala au DART (kama kweli itakuja) au hata kwa baiskeli. Nilimsikia kiongozi mmoja akitaja katika hotuba yake kuwa hiyo hali ni ushahidi wa mafanikioa ya nambari wani kuwaletea maendeleo wabongo!!!

    ReplyDelete
  17. Brother Michuzi
    Swala la Foleni kwa miji yetu has Dar es salaam ufumbuzi wake ni mmoja tu na rahisi ingawa unagharimu FLY-OVERS. wewe umetembea umeona miji yenye magari mengi kuliko Dar lakini hakuna foleni za kijinga namna hiyo
    Halafu tuwe na taa za kuongozea magari za kutosha na watu waziheshimu.
    Topiki hii inanigusa sana kiasi ambacho nnankua na mashaka na elimu za wataalamu na viongozi wetu hakuna uchawi ni kujipanga kila mwaka tutengeneze fly over moja labda ubungo nakuhakikishia hela ipo na itapatikana mbona kwenye mafuta tunachangia road Toll tutashindwa kuchangia kitu muhimu kama hicho.
    Watu hawataki kuongelea kabisa hata kuwaomba wafadhili kama wenyewe tumeshindwa,
    Unaona hiyo picha kama ulivyosema Daladala hawapo . Je wakiwepo ingekuaje. Kwahiyo hata mradi wa mabasi yaendayo kasi ni Bure kwani yenyewe yataruka juu. na watu wenye magari binafsi unawafanyaje ukiyapa hayo mabasi njia yake? mashaka yangu watu wanajitengenezea ulaji tu kwani UDA mbona imewashinda kwa nini wasitumie UDA kufanya mradi huo huoni kuna jambo.Tuliwahi kuanzisha mabasi ya wanafunzi Yako Wapi?
    Bro Michuzi nnamengi lakini naona hii nafasi haitoshi na sehemu nyingine ya kuongelea hakuna
    Wenu katika ujenzi wa Taifa
    JPMM

    ReplyDelete
  18. BRAVO ANKO MICHUZI;
    NAWASHUKURU SANA WADAU WOTE KWA KUIDADAVUA VEMA MADA HIIMUHIMU SANA KWA WAKAZI WOTE WA BANDARI SALAMA.MIMI NATOA OMBI RASMI KWA WANAZUONI MAHIRI NA MAKINI KUTOKA SUMATRA,CHUO CHA USAFIRISHAJI, ARDHI,POLISI NA JIJI WAKAE KWENYE MEZA YA MVIRINGO NA WAIBUKE NA MPANGO WENYE MAJIBU YA KITAALUMA.
    ------------------------------
    R.E.Njau
    Dar City Centre.

    ReplyDelete
  19. Jamani maofisi yaamie na sehemu nyingine kama tegeta, mwenge ili kuwe na mgawanyiko wa magari especially asb na jioni.Lakini hivi sasa kero hii imezidi na nashangaa majengo mjini yanazidi kujengwa jamani kuna nini huko???? embu ona Tanesco na wale wa pale TCRA sam numoja wanavyotesa!!!

    Vyuo km IFM,CBE vihamie Bunju huko, huko town wabaki students wa Masters tu.

    Traffic polices naona wamezidiwa sana na magari, foleni zimezidi mno na wao kazi kupendelea pande moja tu utadhani na wengine hawaendi huko town e.g barabara ya Kinondoni jamani trafffic wanavyoisahau.

    Hivi na barabara ya bagamoyo asb hakufai jamani, na wiki hii ht traffic wanaokaaga pale junction ya kwenda Kawe wameingia mitini afterall walikua hawasaidii kwani magari yanatanua wanayaachia tu.

    Solution ni kuweka fly overs e.g pale ubungo. Bagamoyo road waweke double lanes km sio 6 lanes na barabarani wakae FFU instead of traffic lakini wakiachia taa zifanye kazi, wao wawe wanakaa tu kuangalia wafanya fujo mana traffic kazi imewashinda.

    ReplyDelete
  20. simpo!!! viongozi waache porojo, tamaa na rushwa wafanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watu na wakubali kuachia ngazi pale wanaposhindwa ili wenye uwezo waongoze. basi. ni hilo tu ndo linaisumbua tanzania.

    ReplyDelete
  21. JE HAIWEZEKANI KUZIFANZA WILAYA TATU ZA MKOA WA DAR ES SALAAM KUWA MIKOA MITATU KAMILI YA KIUTAWALA?

    MIMI NAAMINI MPANGO HUU UKIFANIKIWA UNAWEZA KUCHANGIA KUPELEZA BAADHI YA HUDUMA ZA JAMII KARIBU ZAIDI NA WANANCHI.

    KUNA MSEMO UNAOSEMA KUWA NCHI INAYOTAFUTA MAENDELEO HAIUTAMBUI USIKU.JE HUU SI WAKATI MUAFAKA KWA MABASI YOTE YA MIKOANI KUSAFIRI KWA SAA 24 NA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MABASI ASUBUHI KATIKA ENEO LA UBUNGO?

    JE HAKUNA NJIA MBADALA YA VIONGOZI WETU KWENDA NA KURUDI UWANJA WA NDEGE BILA BARABARA KUFUNGWA NA KUSABABISHA MSONGAMANO BAADAE?

    JE SUMATRA NA JIJI WAMESHINDWA KABISA KUWA NA MPANGO MZUNGUKO MZURI WA DALADALA KUINGIA NA KUTOKA KATIKA YA JIJI BILA KUFUATANA MITHILI YA MAANDAMANO YA SIAFU?

    JE SI WAKATI UFAAO WA JIJI KUWEKA KIGEZO RASMI CHA KUWA NA MAEGESHO MAALUMU KWA KILA JENGO LA GHOROFA KAMA ILIVYO KWENYE JENGO LA EXTELECOM MTAA WA SAMORA?

    JE SI WAKATI UFAAO KWA SUMATRA KUBORESHA USAFIRI WA UMMA JIJINI ILI UWAAFAE WENYE TAI ZAO ILI WASHAWISHIKE KUUTUMIA?

    JE SI WAKATI UFAAO KWA ENEO LA POSTA KUWA FREE TRAFFIC ZONE KWA MABASI YA UMMA TU NA MAGARI BINAFSI YAISHIE PEMBEZONI?

    ReplyDelete
  22. very simple wabeba BOX wote turudi getto kuchukue nchi tuifanye kama mamtoni full stop

    ReplyDelete
  23. Flyover hazisaidii, ni kama kutibu symptoms badala ya kufika kwenye kiini cha tatizo.
    Mdau wa tano ametoa mawazo mazuri sana. Nchi kama Marekani kuna sehemu unakuta kuna 4-way stop. Kila anayefika kwenye makutano hayo lazima asimame, hata kama hakuna gari popote. Halafu wanapishana kwa utaratibu wa first come first served. Mi nshapigiwa honi kwa kusimama kwenye taa nyekundu!!!

    ReplyDelete
  24. Wale wenye senti zao wazidi kuingiza magari nchini na maghorofa yazidi kujengwa katikati ya jiji!!Maana yake sisi hatujufunzi hata mara moja kutokana na makosa ya wale waliotutangulia kimaendeleo,na tubaki hivyo!Amen

    ReplyDelete
  25. florian rweyemamuFebruary 20, 2010

    viongozi wetu wamekariri, na wanashindwa kufikiria nje ya box. Kwani miundombinu ni barabara tu? mfano mie naishi Tegeta!!! na ninaamka 0400 kila asubuhi kuingia barabara ya bagamoyo. ingekuwa vyema kama tungeitumia bahari yetu ya asilia tuliyopewa na Mungu kwa kuweka pantoni.Sie wakazi wa Tegeta tungepaki magari kwenye maegesho huko huko tegeta na kuja huko mjini na pantoni. Halmashauri ya Jiji ingepata mapato ya maegesho, mradi wa pantoni ungeleta kipato, na kizuri zaidi tungetunza mazingira kwani ni kweli magari mengi ni mabovu. Faida nyingine ya kutumia bahari ni kwamba barabara zetu hasa hii ya bagamoyo ingeponyeshwa na tatizo la uchakavu.yaani kasi ya ukarabati wake ungepungua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...