Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara (35) - pichani - amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akikabiliwa na tuhuma sita tofauti za utapeli wa magari na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 48.9.

Mwendesha Mashitaka, Batseba Kasanga, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Benadicta Beda, kuwa katika mashitaka ya kwanza Novemba 27 mwaka jana Magomeni, Manara alijipatia gari aina ya Toyota OPA namba T 527 AUB kutoka kwa Abdul Ngalawa, kwa lengo la kuliuza Sh milioni 10 lakini baada ya kuliuza alitumia fedha hizo kwa matumizi binafsi bila kumrudishia mlalamikaji.

Katika mashitaka ya pili ilidaiwa kuwa Desemba 19 mwaka jana Magomeni, kwa nia ya kudhulumu, alimdanganya Asma Miraji amwazime magari mawili aina ya Toyota IPSAM namba T 866 BEB la thamani ya Sh milioni 14 na Toyota Nadia namba T 746 AVU la thamani ya Sh milioni 12 kwa makubaliano ya kuyarudisha baada ya siku 10 lakini hakurudisha.

Ilidaiwa katika mashitaka ya tatu kuwa Januari mosi mwaka huu, kwa lengo la kujipatia Sh milioni 5 kutoka kwa Jacob Manyanga aliweka dhamana ya gari kwa mlalamikaji na kumwahidi kumuuzia gari hilo wakati akijua kuwa si lake.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hili nitukio lakwanza kubwa kwa Haji japo yako mengi madogomadogo,anakoelekea watu wake wakaribu tunakujua hima wazee wa kigoma mleteni mtoto ujiji nyumbani afanyiwe matambiko ya kimila na kumuombea madua kwa mwenyezi mungu amnusuru kurithi tabia hiyo,mleteni hapa msikiti mkuu wa ujiji kama akipata dhamana,vinginevyo ataelekea kulekule.

    ReplyDelete
  2. Tapeli la kufa mtu akanyee debe tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...