Kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Askofu Zakari Kakobe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kanisani hapo jana baada ya kuwatimua mafundi wa Tanesco waliokuwa wapitishe nguzo kanisani hapo. Watumishi wa watatu wakampuni inayopitisha nguzo za umeme za tanesco leo wamejeruhiwa na walinzi hao wa Kakobe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. BONGO TAMBARAREEEEEEEEE!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kupendelea dini moja na kuonea dini nyingine mfululizo siyo sawa!
    hongera Kakobe

    ReplyDelete
  3. Naomba kuuliza swali. Hivi ni mhubiri gani vile aliyeitisha press conference kushinikiza viongozi wa DECI wakamatwe na wafungwe bila huruma? Kama sikosei kuna mstari unahimiza kuangalia mbegu unazopanda.

    ReplyDelete
  4. Ni DINI.....UBABE......au KIBURI??

    ReplyDelete
  5. Huyu Askofu Kakobe inaelekea ni mbinafsi. Na lile jeshi la wafuasi wake ni kama wamerogwa. Ukisoma biblia kitabu cha Warumi 13:1-7 tumeamriwa kutii mamlaka ya serikali. Sasa mbona yeye anakuwa mkaidi?

    Kila mtu na atii mamlaka inayotawala, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, nazo mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu. 2Kwa hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe. 3Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu. 4Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya. 5Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu iwezayo kutolewa, bali pia kwa ajili ya dhamiri.
    6Kwa sababu hii mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu, ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.

    ReplyDelete
  6. Jamani mi naona sielewi hili sakata?? tatizo nini na kwa nini Kakobe hataki nyaya zipite?? labda angepewa nafasi ya kufafanua ili nasi tuelewe maana tunaweza kunamuona mkorofi kumbe anamaana yake.

    Ankal hebu tuletee wadau wanaoweza kuchambua hii mada ili na sisi tuelewe maana naona kama tuko gizni vile??

    ReplyDelete
  7. What has Tanesco overhead power lines got to do with a church and its worshippers? Should we assume that their 'signals'will be distorted by the electricity?
    I think this is a ridiculous farce and the Govt., should act professinally..Where did God say D not go forth and develope?

    ReplyDelete
  8. Anon wa Fri Feb 19, 09:26:00 AM

    Ishu iko namna hii..

    Kakobe anatetea heshima yake. Assessment ya kwanza kuhusu upitishwaji wa hizo nyaya ulionesha kwamba nyaya zinafaa kupita Sinza ... yaani ziambae na barabara ya Morogoro mpaka Shelikalngo halafu zile kona na shekilango road mpaka zitakakoishia Makumbusho.

    Sasa Sinza kuna wasomi wengi, wakatoa hoja kwamba hizo nyaya zina madhara... zinaweza kuwasababishia kansa na kero za kuingilia vyombo vyao vya electronic kama vile radio, tv, na simu.

    Kwa sababu wasomi wanajuana wakapiga kampeni chini chini kupitia mitandao yao, hivyo mpango wa kupitisha Sinza ukapigwa chini.

    Ndio ikaamuliwa zipite Sam Nujoma Rd., ikiwemo mbele ya kanisa la Kakobe.

    Sasa Kakobe kupitia mtandao wake akagundua njama iliyofanyika ndio maana kachachamaa.

    Hoja yake ya msingi ni kwamba, "Wametuona sisi mbumbumbu ndio wanataka kutupitishia hii miwaya. Hatukubali"

    ReplyDelete
  9. Baba koku apo juu kanichanganya na kingishi naomba. Tafsiri

    ReplyDelete
  10. wewe hapo inaelekea una data nyingi za tanesco basi njoo wewe na kakobe mtupe ukweli wenu kuhusu hii mada

    ReplyDelete
  11. Sasa inakuwaje kanisani tena watu wanapiga na kuumiza wengine?

    ReplyDelete
  12. Sasa ina maana hizo nyaya zinapita kwenye kanisa la kakobe tu au vipi? mimi ninachoona hapo ni ubinafsi tu wa kakobe na waumini wake,tatizo la umeme si la watu wa dini moja wala si la waumini wa kakobe nila watu wote ,hebu tuwafikirie na wengine jamani, hapo taratibu za kisheria zikichukuliwa watu watasema kwa kuwa raisi ni muislamu basi anaonea wakristo na kusahau ukweli wa mambo na kupofushwa na imani.Mbona mambo kama haya yanaeleweka kwa maendeleo ya nchi bila kujali itikadi zetu.

    ReplyDelete
  13. Watanzania wengi tupo nyuma ya habari,jamani tusome magazeti au kucheck taarifa za habari kwenye TV,tuache uvivu wa kusoma,kwa wenzetu mlio ughabuni,sakata lenyewe hivi

    Tanesco wanampango wa kupitisha nyanya za umeme wa High Tension/voltage kama ule wa kutoka Kidatu au Kihansi,plan yao ya kwanza ilikuwa utoke Ubungo -UDSM area-Mwenge-then to other area,plan ya kupitisha eneo la UDSM iligonga mwamba kwani walipambana na wasomi -madoctor,professors,kwani wanajua madhara ya umeme wa High Tension,lakini waliwapa ushauri wa kupitisha chini,lakini gharama za kuweka nyanya chini ni expensive kuliko kutumia nguzo,na inavyosemakana mradi utagharimu 50bl na jamaa wameshafuna baadhi ya hela za upembuzi yakinifu,
    baada ya chuo kikuu kugoma ndio wakaamua kupitisha kwenye makazi ya watu,ikiwa ni pamoja na mbele ya Kanisa la Kakobe-Full Gospal Bibble Fellowship Church,ndipo walipambana na kigingi,msomi au muelewa mwenzao ambaye anajua njama yao.
    Baada ya kuona mchakato huo Kakobe alipeleka malalamiko TANESCO pamoja na wazara husika,ambapo waziri Ngereja anajua hiyo issue.Kakobe aliitwa kwenye kikao,ambapo Waziri Ngereja,Naibu wake,mabosi wa Taneso walikaa pamoja kujadili huu mchakato,na Taneso walimwomba awe mpole kwani walikubali kubadili plan,na wangefanya survey upya,lakini toka huu mchakato huu uanze waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakilinda eneo hilo kwa mantiki wasije wakakaidi maamuzi ya kikao,ndio juzi kuna wafanyakazi 3 walikuwa wanaendelea na kazi kwenye eneo hilo ambapo walimwambia hawawezi kupitisha usoni mwa kanisa lake,

    Guys mimi sio supporter wa Kakobe,lakini naona kakobe yupo right ,navyojua wanapopitisha umeme huu lazima uwe mbali na makazi ya watu,mtakuwa shahidi kama mnavyoona jinsi nyumba maeneo ya Kimara,Ubungo,Mabibo,Kigogo zilivyombali na umeme wa kutoka Kidatu,Tanesco wanafanya danganya toto coz baada ya kumaliza kujenga watakuja na hoja nyingine kuwa nyumba zilikaribu na umeme zibomolewe,je kabla kujenga walikuwa hawajui madhara?Nyepesi zinasema kuna hela zilitolewa kulipa fidia wajanja wametafuna,
    So guys kwa wale wanaojua umeme hii ni hatari,kama unavyojua umeme huu ni hatari,kwanza unapita unasikia sauti,au muungurumo,kwa wasio jua sogea karibu na wire za ubungo kutoka Kidatu.
    Therefore,ilitakiwa watu watu wa maaeneo hayo wamuunge mkono Kakobe,otherwise in near future watavunjiwa nyumba zao,kwa kigezo una madhara au mwenyewe utahama kwa kuhofia madhara,
    Swali kizushi-Kama huo hauna madhara kwa nini hawaruhusu watu kujenga nyumba kwenye viwanja vya Ubungo,Kimara ambapo umeme huu umepita?

    Mdau,
    Kisenga

    ReplyDelete
  14. kanisa gani linaleta fujo mpaka kushambulia wenzao???????? Kakobe jibu swali hilo

    ReplyDelete
  15. Wewe mdau unayejiita Kisenga story yako naona kama hadithi ya Abunuwasi vile!!....Hainiingii akilini na wala siwezi kuamini kama umeme unaouzungumzia ni ule unaotoka kidatu ambao ni marufuku nyumba kuusogelea!!!...ile ni hadithi nyingine bwana....usolelee usiku usikie UNAVYONGURUMA na hakuna nyumba iliyosubutu kuusogelea....ndo unataka kupamba hadithi eti upitie Sam-Nujoma??...No...hii nakukatalia...itakuwa ni line ndogo bwana....it means kama ni umeme huo basi ile line yooote ya Kakobe na nyuma yake WAMEUIMIA...Na kama ni kweli itakuwaje mitaa yote miwili inyamaze kimya apige kelele Kakobe peke yake!..hawa watu wa dini sometimes ni viburi sana!!!(Sorry Michuzi but this is a plain fact!)

    ReplyDelete
  16. Kinachonishangaza ni kwamba serikali haimpi nafasi kakobe kujieleza. Globu hii ya jamii na yenyewe imekataa kutoa nafasi aeleze. TBC1 iliandaa kipindi kimoja cha usiku wa habari juu ya suala hili lakini kipindi kikakatishwa kiaina aina tukahisi kuna amri ya mkuu inayopinga hili. Kwa nini globu hii na vyombo vingine vinamnyima Kakobe nafasi ya kujieleza?
    Hata maoni yangu sijui kama yataona mwanga.

    ReplyDelete
  17. Michuzi kwa kubania mambo mengine. Mchango wangu wa kwanza umetia kapuni.
    Mimi sipingi madai ya Kakobe ila njia aliyoitumia mimi ndio napinga kwa sababu ni hatari kama tutaendekeza hasa hizi jumuia mbali mbali za kidini na kisiasa hata zile za vyuo tu, ipo siku yatatokea maafa makubwa, kama serikali haitazinduka kwa sasa.
    HATA HIVYO UKWELI UNABAKI PALE PALE ASIYEFANYA KAZI NA ASILE NA TABIA YA KAKOBE KUWAWEKA WATU PALE USIKU NA MCHANA NA USIKU SIO USTAARABU HATA KAMA ANADAI HAKI YAKE NA ANAONEWA. TUWE MAKINI IPO SIKU ATAWAFUNGIA NDANI NA KUWATIA KIBERITI KAMA KIBWETERE.
    HEBU FIKIRIA NI KWA VILE HATUNA MTU WA NDANI PALE ATAKAYETUELEZA UKWELI, ITAKUWA WENGI SANA WAMEUGUA MALARIA. SASA OPERESHENI MALARIA ZINDUKA YA KAZI GANI. KAKOBE KAMA NI MSOMI MSTAARABU ANAYEMJUA MUNGU AMEKOSA NJIA NYINGINE YA KISTAARABU YA KUDAI HAKI BILA KUWAUMIZA WAUMINI?
    Mimi hofu yangu ni matumizi ya nguvu ya kuheshimika kwa mtu(kiongozi) kufanya jambo ambalo kweli jamii husika imeonewa kulitatua kwa njia inayoleta maafa direct au indirect kwa jamii nzima.
    Hatuhitaji kusubiri mpaka FFU waende pale kuwaumiza waumini ambao mimi naamini hawaelewi kiundani wanachotetea.
    Lile kanisa lina waumini wengi sana wasomi na wenye uwezo lakini ukienda pale ukweli utakao waona pale wengi wao ni wale wa hali ya chini na kati. Na siamini kama Kakobe amekuwa akikesha nao siku zote tangu waanze kukaa pale.
    JAMANI KWA HILI YATUPASA KUPIGANA NALO, WALE WATU WANATESWA NA KAKOBE NA WALA SIO SERIKALI. HEBU TUAMKE JAMANI.
    MWISHO NAMWOMBA KAKOBE ATAFUTE NJIA NYINGINE ZA KISTAARABU KUDAI HAKI YAKE. ASIWATESE WAUMINI.
    Najua na hii michuzi utatupa kapuni. Sawa bwana!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. Wadau msichanganye maelezo. Serikali siku zote ina plans zake za maendeleo kwa utaratibu itakaoona unafaa. Kila Barabara inawekewa vipimo vyake vya ukomo pande zote mbili. Eneo ambapo Tanesco wanaweka nguzo liko ndani ya road reserve. Suala la muingiliano na vinasa sauti, ni matokeo ya wajenzi kutojali ukomo/vipimo vilivyowekwa na serikali. Kakobe hana hoja, bali ni kiburi tu kinachotokana na machungu ya sehemu yake ya kanisa kuvunjwa hapo nyuma kupisha upanuzi wa barabara. Hata kama asingekuwa ndani ya road reserve, serikali inayo nguvu na sababu ya kufanya maamuzi yeyote kwa ajili ya maendeleo kwa taifa kwa ujumla bila kuangalia athari kwa mmoja mmoja. Awali Kakobe alijua yuko mbali sana na barabara na kwakuwa tumeshazoea kujenga majumba na kujitanua kwa eneo huku tukijifariji kuwa sio rahisi serikali kufanya maendeleo yoyote ndani ya kipindi cha uhai wako katika eneo lake ambalo unaliona "lako"!. Matokeo yake mwenye mali akiamua kufanya atakacho ndani ya eneo lake, tunaona tunaonewa kwa kuingiliwa "maeneo" yetu!!. Nashauri serikali iendelee na azma yake na Kakobe akiona hali ni mbaya ki-athari kanisani, viwanja viko vingi akajenge kanisa kwingine. Hao akina mama wanaolinda na watoto wao wachanga, nawashauri tu wakapumzike nyumbani baada ya sala wasijeumia kwa nguvu ya Dola.

    ReplyDelete
  19. KAKOBE PLIZ= WHERE IGNORANCE IS BLISS, ITS FOOLY TO BE WISE..

    ANKO= KWA UZOEFU, MADHARA YATOKANAYO NA UMEME NI MAKALI MNO.. NA HATA SHOTI KUBWA ZITOKEAPO NA MOTO KUWAKA- FIDIA ZA MALI ZETU NI NDOTO, LABDA KWA WAKWASI WACHACHE WENYE COVERS/ INSURANCE..

    TANESCO= WAPITISHE HUO UMEME CHINI REGARDLESS OF THE EXPENSES..AU WAFANYE MAONGEZI UPYA NA MFADILI KHS ONGEZEKO LA GHARAMA KWA UNDERGROUND CABLES.. AU WATAFUTE MRADI MWINGINE.. ZAIDI YA 50% YA TZ BADO HAINA UMEME, FEDHA NYINGI ZINAPOTEA KWENYE MIRADI TATA INAYOONGEZA HOFU KWA WATEJA BADALA YA KUONGEZA WAPYA..

    MDAU,
    AMANI.

    ReplyDelete
  20. Huo mradi usitishwe kwani umeme si muhimu kama maisha ya watu. Ni heri tuendelee kutumia vibatari vyetu tu. Ila bwana kakobe angeweka msimamo wa kweli aache kabisa kutumia umeme wa tenesko.

    ReplyDelete
  21. pande zote ziende kwenye vyombo vya sheria kama ndo suruhu, kama inafikia wafuasi wa kakobe kutimua serikali, sipati picha hapo

    ReplyDelete
  22. kwa wale wasiojua ukweli halisi kama mimi nadhani ni vyema kutolaumu upande mmoja.
    kama ni kweli umeme huo ni ule TAIFA KUBWA,basi ni hatari mno kupita ktk makazi.hivyo basi huyo kobe mdogodogo(Kakobe) yupo sahihi kupinga kitu hicho.
    na kama hali ndo hiyo,kwanini hao wakazi wengine wasimpe tafu Kakobe?hapa kuna ulakini fulani.
    suna oo leta,tuliopo mbali na Bongo tutajua ukweli halisi.

    ReplyDelete
  23. mimi ni maamuma katika hii ishu sijui kitu ila hao wanaosema kwanini wengine wasiungane na kakobe waliokaribu na eneno hilo......Jamani kila kunguru huwa anaruka kwa ukubwa wa mbawa zake.inawezekana wanatka kumuunga mkono kakobe lakini je kama ni wenzangu na mie hasa hapo iisue itakapofika kupelekana vituo vya polise hadi mahakani wakitakiwa wajizamini kwa milioni 5 watakuwa nazo? kakobe yeye hata milioni 50 atajidhamini au mnataka uwe mtego wa panya? kuigia aliekuwemo na asiekuwemo? siku zote kwa kunguru muoga hakwendi kilio.

    ReplyDelete
  24. MNASEMA TANZANIA KUNA DEMOKRASIA, UTAWALA WA HAKI NA UWAZI, HIYO NI KWELI NA KAMA NI KWELI HAYA YASINGETOKEA, NASEMA HIVYO KWA SABABU ZIJAZO, NI KWAMBA KWENYA NCHI ZILIZO NA DEMOKRASIA, UTAWALA BORA NA WA HAKI, KUNAPOKUWA NA MRADI WOWOTE ULE UNATAKIWA KUJENGWA, SERIKALI KUU NA YA MITAA UITISHA MIKUTANO KWA WATU WATAOATHIRIKA NA MRADI HUO NA KUELEZWA FROM "A" TO "B" MRADI UTAKUWAJE, UNAFAIDA GANI NA HASARA GANI NA WANAPEWA UCHAMBUZI MZIMA WA MRADI KWENDA KU-USOMA NYUMBANI NA BAADA YA MKUTANO MATANGAZO UBANDIKWA SEHEMU ZA PUBLIC NA MAGAZETINI KUELEZA MAHALA FULANI PATAJENGWA KITU FULANI KINAELZWA CHOTE NA MWISHO WANASEMA MWENYE MAONI NA MALALANIKO AU ANATAKA KUZUWIA USIJENGWE NA ATOWE SABABU ZAKE, WANAPEWA MUDA WA KUFANYA HIVYO, NA KAMA KUTAKUWA NA MAONI MENGI YA KUUKATAA KWA SABABU FULANI FULANI KIKAO KITAITWA TENA NA KUJADILI NA MWISHO KUPIGA KUNA ZA NDIYO NA HAPANA WATAKAOSHINDA WANAPEWA USHINDI NA HAPO PIA SI MWISHO UPANDE HAUJALIDHIKI WANAWEZA KUFANYA-APPEAL KUTOKANA NA UTARATIBU HADI NGAZI YA MWISHO NA MAAMUZI YA MWISHO YATAKUBALIWA NA PANDE ZOTE MBILI. TATIZO LA TANZANIA NI SERIKALI KUTO WADHAMINI WANANCHI INAJIFANYA YENYEWE INAJUWA KILA KITU. THAT IS A SIGN OF LACK OF LEADERSHIP NA NI MTINDO WA KIZAMANI WA UONGOZI TULIOURIDHI TOKA KWA WAKOLONI AMBAO HATA WAO WENYEWE WAMEUACHA. NOW IT IS DOWN TOP LEADERSHIP STYLE NO TOP DOWN, WANANCHI WENYEWE NDO WAAMUWE MAMBO YAO KWA FAIDA YAO. HILILINAFANYIKA NCHI NYINGI TU, HATA KUJENGA NYUMBA MTU BINAFSI HUTOWA TAARIFA KWA PUBLIC NA KUOMBA MAONI YAO NA MWENYE KIPINGAMIZI HUTOWA NA USIKILIZWA. KAMA NI KWELI WASOMI WAMEKATAA USIPITE KWAO SO WAKO TAYARI RAIA WENZAO WAPATE MATATIZO, NA HWAO NDO WENZETU NA WASOMI WETU, NAAMINI JIRANI WA KAKOBE HAWAJUWI KINACHOENDELEA NDO MAANA HAWALALAMIKI NA HII NI KUTOKANA NA MUUNDO MBAYA WA SERIKALI KUTO WAELEZA KIWAZI KINACHOENDELEA

    ReplyDelete
  25. Suala hapa si la dini au asasi ya dini. Maswali ni : 1. Je hizo nyaya ni za high tension kwenye pylons au ni hizi za kawaida (local mains)? 2. Zitapita umbali gani kutoka kanisani? Pande zote mbili zikae pamoja na kuelimishana. Kuwapiga wafanyakazi wa Tanesco haitasaidia kitu na si mfano mzuri kwa jamii. We anon wa pili, 5:12 a.m. mbona makaburi sehemu tatu DSM ya watu wa dini moja yalipofukuliwa miaka 10 iliyopita ili barabara zipanuliwe na wenye maiti zao wakaambiwa wakachukue mabaki ya wapendwa wao kwa fidia ya 70,000 tshs watu hawakutia udini? Ni kwa sababu hawakutaka kuleta chuki za kijinga sehemu isiyostahili. Ndiyo maana wa-TZ tutaendelea kuishi pamoja, kula pamoja, kushereheka pamoja, kuomboleza pamoja kama ilivyo kwa 99% ya waTZ. Nyinyi kina Anon wa 5:12 a.m. ni 1%tu na mtadorora. God bless TZ. Simba Tayari.

    ReplyDelete
  26. kama ni high voltage kulikuwa hakuna mbinu za kakobe na watu wake kulalamika bila kupiga watu hili ni kanisa linalomwamini Mungu aliye hai yule ninayemwamini mimi au? maana walitaka kuua kwa kumpiga jamaa kichwa kakobe angalia sana ndo maana watu wanasema unatumia nguvu za giza

    ReplyDelete
  27. Yaani mnataka kuonea kanisa kwa sababu mnajuwa hawawezi kupigana? Nani alikwambia kupigana ukitetea haki yako ni dhambi?

    Ujinga wa kutokuelewa neno la Mungu ndiyo unafikiri kupigania haki yako ni dhambi. Mbona sisi walokole tuko kwenye majeshi yote na tukitumwa kupigana na serikali tunapigana! Serikali ilitufukuza walokole kusali mashuleni. Wapinzani wa ulokole wakafurahi sana. Sasa tumejenga majengo yetu wenyewe serikali inakuja kutufanyia vurugu za kila aina.

    Kumdharau Mungu kuna madhara makubwa. Watanzania bado hawajaonja gharama za kumtukana Mungu. Ndio maana Wachungaji na watumishi wa Mungu wanadharauliwa sana nchi hii ya Tanzania.

    Nawakumbusha tu watanzania muangalie sana mbegu mnazopanda siku moja zitaota!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...