Ankal nimesikia hii ngoma kali yaweza kuwa ya kuanzia mwaka toka kwa watu wa Afrika Mashariki na Maziwa Makuu, hebu tu-share na wadau wa globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nimeikubali mzee mzima, imetulia

    ReplyDelete
  2. Jamani! huyu kidumu anasauti inayoendana na kuimba,,kweli mziki umetulia vyakutosha.duhhhh.

    ReplyDelete
  3. asante sana aliependekeza wimbo huu hapa kwenye hii blog!! I love the song!! thanks so much ...Mmmmmwaaaaa

    ReplyDelete
  4. Napenda kumpongeza mtunzi wa huu wimbo, na ningependa kama kuna uwezekano, aandike nyimbo zaidi yenye huu mwelekeo. Kaka hongera sana, tafadhali usikate tamaa, tumia sauti yako kuihamasisha jamii yetu.

    John Mashaka

    ReplyDelete
  5. huyu jamaa ni mnyarwanda lakini wimbo bombo saaana na kiswahili hakijui vizuri lakini katoka sana wasaniii wenzangu wa bongo kelele tu hata ujumbe hakuna hakuna shame on bongo fleva baadhi lakini si wote.

    ReplyDelete
  6. yah, Ni track nzuri, imepangwa vizuri, kivyombo na uimbaji. Lakini tatizo moja kubwa ambalo nimekuwa nikiliona kwa nyimbo nyingi za Bongo Flavor ni kwamba hazichezeki. Nenda Club, utakuta zinapigwa nyimbo za west africa, carribean nk. Bongo flava watu wanakaa. Hili ni tatizo kubwa sana. Kwa nini wakongo wanatesa hapa. Nyimbo zao zinachezeka. Hongera Asha baraka, ameweza kupambana na miziki ya wa kongo. Mimi natoa changa moto kwa bongo flavor pamoja na FM stations zetu. Acheni kupromoti hizi slow type of Zouk ambazo wasanii wetu wengi wanapiga. Haiendi mbali. Promoti miziki inayochezeka. huwezi amini mpaka leo kuna remix za saida karoli (Unanichambua kama Karanga) na nyimbo za Mr. Nice zinapigwa kwenye maclub west Africa. ZINACHEZEKA!
    Nachangia.

    ReplyDelete
  7. ebwana weeh wee kiboko kweli kidumu.tupe mambo ya zouk machine maana haya makitu tumezoea kuaskia kutoka kwa wa carribeani tu.ebwana big up mtu mzima.

    mdau kigali makazi boxini

    ReplyDelete
  8. Hivi wewe unayesema eti huyu Kidumu ni mnyarwanda hujui,,,ukweli Kidumu ni mrundi lakini anaishi kenya,,na ni msanii wa kenya wa siku nyingi tu.Na usiongee uongo eti hajui kiswahili vizuli yuko fleshi tu kiswahili chake hakina kasolo yoyote.

    ReplyDelete
  9. wimbo safi sauti safi jamani huyu juliana ana nsauti kali kumzidi binti machozi huo ndo ukweli halisi sauti lainiiii haina sio ya kupayuka huh!!

    ReplyDelete
  10. michu tunaomba utoe single!

    ReplyDelete
  11. wewe anonymous wa hapo juu wasanii wengi wa kike wa bongo hawajui kuimba,lamda Ray naweza sema,binti machozi kazi anayo

    ReplyDelete
  12. Kwa
    Ankal na Wadau wa Blogu ya Jamii.

    Nimeona 'MichuziEffect' wakati nimeingia Youtube kuangalia hii clip ya Juliana Ft Kidum.

    Katika Video ya "Hatutrudi Nyuma' chini kuna sehemu ya Statistics& Data: Blogu ya Jamii kuanzia 19/02/2010 imesababisha grafu ya hiki kibao kupanda juu kwa kasi ya ajabu!

    Hii inaashiria kuwa kibao hiki ni kitamu, chenye ma-'feeling' kibao na kinakubalika kwa sana.

    Hivyo kama msanii/wasanii wamefanya kazi nzuri, wakipeleka kazi yao Youtube, basi wapitishe pia na clip yao ktk Blogu ya Jamii kujua kama pia kazi yao itapata 'MichuziEffect'.

    Pia tangu kusikia kibao hiki, pamoja na baridi ya huku, mie nimekuwa nakicheza mara kadhaa na kupasha moto mwili kwa kukicheza.

    Hongera Juliana na Kidum.

    ReplyDelete
  13. Eeeeh Bwana weeh!
    -vizuli; fleshi; kasolo.

    Mi hapo, ndio niko hoi na hizi ndimi za watu wengine! Zina nini? Zimelegea?
    (usibanie comment yangu Ankal). Ebu jitahidini kuongea kiswahili fasaha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...