uchafu na uchakavu
ndani meng'emeng'e...

Habari Anko, shwalama? (Mix ya Shwari? na salama?)

jamani jamani.....

Eti nyie shirika la ndege ambao mnasema mmepewa tuzo ya shirika bora la ndege, jamani mmegoma hata kuzipita "Isuzu Journey" zinazoenda mwenge-posta kwa matunzo/ubora/n.k?

Hizi ni picha ya ndege yao ambayo inakula vichwa kama haina akili nzuri, inapiga dar/shinyanga/mwanza, kote kote with break za dk 15 15 kila inapofika airport husika..
Mi wasiwasi wangu ni huu uchakavu, au labda ma-fundi ndege mniambie; Je, kuchoka huku hakuhusiani na ubora/umadhubuti wa ndege?

Haya sasa na mende je, au usafi na hizi repair zinasubiri kwenda kufanyiwa sijui ufaransa/ujerumani na kwingineko? si mna ma'engineer? Yani unahisi kama uko kwenye DCM vile...kwanza hakuna, sio ka DCM, DCM haliwi na mende unless liwe halijaamshwa na suka.

Muwalipe nafuu/vizuri ma-pilot wa kitanzania na staff wenu wengine kwenye hivi vyombo vyenu vya usafiri, maana wanafanya Over-over-over-over time (over time iliyopitiliza overtime - "msibishe"). ushawasikia mapilot wao wakitoa report ya safari kwa abiria?

mnawaelewa vizuri iwapo ki-ingeredha chako sio sharp? ukiwa na GUBU (ma-pilot yani), unafikiri utamchangamkiaje mtu ambaye humfahamu wala humwoni.

Abiria mwenye GUBU na vyombo vichakavu vya usafiri ANGANI.
(**Hamna second chance kule kikibuma**)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ebwana eeeh unatania ama kweli hio ndege au caterpilar hunitii humo hata kwa mijeledi sio kwakulipa bure pia

    ReplyDelete
  2. hiyo ni precision air ndiyo ndege dar via shiyanga ukweli ndio uo ndege imechoka haya ma-ATR kelele mtindo mmoja ni sawa na Dcm kwa sababu hata kiwandani hawatengenezi tena mpaka uweke special order kutoka Ufaransa na PW ndio wanaongoza africa Kwa Kuwa nayo mengi lakini EU Na America marufuku kwa sababu ya kelele.

    ReplyDelete
  3. mimi nilishapanda huo mzigo sina ham tena yaani ukianza kupaa kama unakwamakwama njiani au fiat inapanda mlima, kwanza nikuulize siku hizi mle ndani wameweka kapeti maana chini ilikuwa ni chuma tu kapeti unaliona kwa juu, halafu wahudumu mle ndani ni wauza sura tuu waliopewa mapande wanatoa huduma kwa kumuangalia mtu kama ni kijana au hujavaa suti unamwita muhudumu ankuangalia machoni tuu, inakera sana

    ReplyDelete
  4. HATA KWA NGUMI SIPANDI HATA UNIWEKEE BUNDUKI KICHWANI SIPANDI NG'OOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  5. kama ushawahi kuangalia NATIONAL GEOGRAPHIC CHANNEL....program za AIRCRASH INVESTIGATION,utaona vitu vidogo vinavyoangusha ndege na haki ya Mungu hutapanda tena hio ndege.

    ReplyDelete
  6. Asante mdau hata mimi nililiona hilo last week. Hivi unapokuwa na mkurugenzi mkenya "Alphonce Kioko ambaye wasifu wake wa kuongoza mashirika ya ndege huko aliko toka haujulikani unategemea nini?" Hata hawo marubani na wanaanga wao ni msala mtupu. Kuna wakati rubani alizima wakati dude linatoka mwanza anaitwa Capt Mosha ilikuwa mwaka jana tukalazimika kutua kwa dharura mwanza ilikuwa jioni. Siku hiyo hata mende waliogoa maana walikuwa ni miongoni mwa waliokuwa wanashuka kwa ghafa na haraka. Tukaishia kupelekwa hotel lakairo tukisubiri rubani toka kenya aletwe mwanza tuweze kwenda KIA.
    Bwana Michael Ngaleku shirima niwakati sasa kama mwenye kiti wa shirika uoneshe uwezo wako. Hivi kuna haja gani ya kutumia jina KQ wakati wao ni PAA?
    Hebu wabongo tuamke wakenya wasitukenye

    ReplyDelete
  7. What is this? What a crap!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. mungu wangu walah mtu aliyewah kuangalia national g,hawez panda ndege chakavu jamn kitu kidogo tu kinaweza kukusababisha ndege ipate crash..jaman jamn itakuja kutuletea mafa..wenye uwezo wawahabarishe wahusika.

    ReplyDelete
  9. Aah! who cares, don`t forget it!s Tanzania by the way. Everything goes. No matter how dangerous it may look and operate. Sisi tumtafute mchawi aliyeturoga tu !!

    ReplyDelete
  10. Ankol! raha ya blog yako ni ukweli na uwazi,Precision kwa muda wamekuwa ni mkombozi wa usafi wa anga sisemi wa haraka kwani yameshawahi kunikuta ya delay zao mpaka unakata na tamaa lakini is fine,lakini hili la uchakavu wa ndege si tu linatishia usalama wa shirika lenyewe lakini pia linatishia un=hai na usalama wa abiria ambao ndio sisi,ni ukweli usio na chembe ya hila ya kuwachafulia sura nzuri ya kibiashara mlionayo Precision Air ndege zenu haswa za za ruti za dar-shinyanga mwanza,dar- kigoma ni kwakuwa tu hatuna mbadala lakini mtatuua wenzenu kisha mje kutoa rambirambi na mashada ya maua kama kwamba hayo maua yatarudisha roho zetu. Sawa yawezekana huko kwenye engine na mitambo mingine mkawa mko vizuri kwani hamna record ya ajali mpaka sasa,lakini nitapataje imani hiyo ili hali ndani ya ndege kuna mende ,siti chakavu ukiangalia hayo magurudumu yamejaa tope hata lori la mkaa ni afadhili,najua mnamajukumu mengi lakini ni ndege hizo zinazowafanya muwepo.USALAMA KWANZA,KISHA BIASHARA.

    ReplyDelete
  11. ndo maana nachukia panda ndege!!

    hii cha mtoto mshapanda kenya airwyas ya west afrika?utajuuuta kupanda jaman kelele izo adi KITUKO,utafikiri dege lataka pasuka angani

    why?????

    ReplyDelete
  12. Asante kwa kulileta hili. Jamani ni kweli hizi ndege zimechoka si mchezo. Kuna siku nilishapanda moja toka Dar kwenda Mwanza kalikuwa kadogo kidogo kanatumia kama masaa mawili. Aisee si utani by the time nawasili Mwanza kichwa kinauma. Yaani nilikuwa nimekaa pale chini ya mabawa, makelele hata roli au DCM afadhali. Mbaya zaidi hakukuwa na AC na kulikuwa na abiria alikuwa na mafua. Jamani this is too much!!! Na hao wahudumu wao sijui wana nyodo au gubu!!!

    ReplyDelete
  13. ni kweli jamani hawa presishen sasa too much
    wakenya wamejaa kwenye kampuni hawajali kitu hakuna mipango bora ni bora wao wamejinufaisha tu,presishe hata hawawezi kuenda sauzi eti makubaliano aahh why feeding kq while they can fly direct to South?its high time shirima afanye uchunguzi na kujua nini hasa kinaendelea kwenye shirika lakena aujue ukweli wa mambo.nawakilisha

    ReplyDelete
  14. MBOVU, MBOVU!!! TOKENI HAPA. WOTE MNATOA USHUHUDA MMEPANDA HILO HILO BOVU NA MKAFIKA. SASA MAKELELE YA NINI?? MSHASIKIA TZ NDEGE YA ABIRIA IMEANGUKA??? HIYO MIJIDEGE YENU YA KIFAHARI MBONA KILA KUKICHA TWASIKIA IMEANGUKA NA KUUWA WATU. INAMAANA HAO MARUBANI HAWAJUI USALAMA WA NDEGE HIZO, MBONA WANARUKA KILA SIKU, ACHENI HIZO, USHAMBA HUO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...