Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya na mbunge wa Kibaha Mh. Dk. Ibrahim Msabaha na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Vijijini Mh. Halima Kihemba wakiangalia bomba jipya la maji Soga leo. Chini akiongea na wakazi na viongozi wa hapo
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya amewaambia wakazi wa Kijiji cha Soga mkoani Pwani kuwa Serikali haijawasahau hasa katika upande wa tatizo la Maji.

Waziri Mwandosya ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya siku moja mkoani Pwani kuangalia miradi mbalimbali ya Maji, na kuongeza kuwa changamoto ya maeneo ya Pwani ni shida ya maji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya mkoa wa Pwani kuwa karibu na bahari ya Hindi hivyo kusababisha maji yanayopatikana sehemu kubwa kuwa ni ya chumvi.

Hata hivyo Waziri Mwandosya ameongeza kuwa licha ya tatizo hilo la maji kuwa ya chumvi bado wakazi wa Pwani wana bahati kwa kuwa Mto Ruvu upo katika mkoa wao na maji huwa yanapatikana karibu kipindi chote cha mwaka.

Aliongeza kuwa hivyo kiasi cha maji kinachopatikana katika Mto huo kitagawanywa pande zote Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es saalam, ili watu wote wafaidi huduma hiyo ya maji.

Wakazi wa Soga awali walimweleza Waziri Mwandosya kuwa kilio chao kikubwa ni tatizo la maji na kumuomba kuhakikisha anawatatulia tatizo hilo kwa kuwa wizara yake ndio yenye dhamana hiyo.

Akiwajibu kuhusiana na hilo Waziri Mwandosya aliwahakikishia kuwa mradi wa maji unaendelea hivi sasa katika vjiji 10 mkoani Pwani chini wahandisi kutoka china, wataalam hao hawataondoka mpaka wawe wameshawapatia wananchi huduma za maji katika maeneo yote husika.

Katika ziara hiyo Waziri Mwandosya aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi Halima Kihemba, Mbunge wa Kibaha Vijijini Dk.Ibrahim Msabaha, Mtendaji Mkuu wa DAWASA Archard Mutalemwa, Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Alex Kaaya na viongozi wengine kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mkoa wa Pwani .

Waziri Mwandosya alitembelea Shule ya Sekondari ya Al Akbar Hashem Rafsanjan , shule ya Msingi Soga, Stesheni ya Reli ya Soga, Shamba la Mkonge la Alavi pamoja na shamba la Mhe Dk Msabaha .







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi huyu waziri amejiuliza hii nyumba ilivyo. Sasa hilo bomba la maji siku lipasuka hii nyumba itakuwaje?

    ReplyDelete
  2. Hii aibu gani tanzania,yaani hata picha tena mnapiga haya bomba moja watatumia wanakijiji wangapi?MAMA ZETU MNAWAUMIZA SANA,MAJI UMEME NI HAKI YA KILA MWANANCHI NA SIO KAMPENI YA UCHAGUZI.MAANA VIONGOZI WAMEWEKA MBELE TUTAKULETEENI MAJI WAKATI NI HAKI YA MWANANCHI YOYOTE,NAKUMBUKA LAST TWO MONTHS KIKWETE ALIKUA ANAMTWISHA NDOO YAMAJI MWANAMAMA MMOJA SASA KAMA WE NI RAISI BADO UNAFUNGUA VISIMA,JAMANI TUFANYE NINI?(NURAMO)

    ReplyDelete
  3. Michuzi naomba nimsahihishe mtoa habari hii. sio "wakiangalia bomba jipya la maji"
    alitakiwa kuandika "wakiangalia kabomba kapya ka maji"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...