keki ya beatrice
BEATRICE P. MAKANI

Nikitimiza Miaka 55, Napenda kumshukuru Mungu kwa umri huo
Napenda pia kuwashukuru watoto wangu walioniwezesha siku hiyo kuwa ya kukumbukwa kwa maisha yangu yote.


Niliamka siku hiyo nikiwa mnyonge, na mpweke, kwa vile wanangu hawakuwepo nchini na sikuwa na uwezo wa kushereheka siku hiyo kama nilivyotaka mwenyewe.


Nikajiamulia kwenda kukaa na rafiki zangu hapo Salendar Bridge
Mara Niece wangu Lola akaja na rafiki za watoto wangu pale nilipokuwa
Nilishangaa na kujiuliza nitawapa nini wageni wangu hawa
Mara mmoja wao Denis akaondoka na kurudi na
CAKE HIYO
Nilipigwa na butwa na kufedheheka sana
Ndipo siri ikafichuka

Watoto wangu wakiwasiliana kwa njia mbalimbali na rafiki zao wa hapa nchini, wakishirikiana na Lola walipanga hayo yote. Wakijua mimi ni mpenzi wa Serengeti tangu ilipoanzishwa, wakanizawadia Cake mnayoiona hapo. Mpaka leo sijui ni nani ali ‘order’ wala alielipia ninachojua ni wapi ilipotengenezwa.


Nawashukuru sana wanangu Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwazidishia sana hasa Upendo, watoto wema kama ninyi ili nanyi siku moja mfurahi kama mnavyonitendea mimi. ‘Big Ups’ Wajukuu zangu
Nawashukuru watoto wa wanawake wenzangu waliokubali na kuja kuona mwaka wangu wa 55 sipo mpweke.

Miaka 55 nimepitia matamu na machungu mengi sana
Kwani nyani mzee amesharukia miti mingi
Yote yamenijengea uimara wa Mwili na Roho
Kubwa na Uvumilivu na Upendo
Slogan ya Serengeti
‘Good times last longer’
Thanks
Beatrice P. Makani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. hongera sana, nimeipenda kweli keki yako, hata mimi ni mpenzi wa Serengeti,michuzi ningependa sana ungetuwekea tangazo la serengeti maana linanifurahisha sana.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Bibite kwa kwa kutimiza miaka 55, mungu akujalie mingine 55 yenye afya na baraka. I always admire your ways mama big up!!
    mimi hunifahamu lakini mimi nakufahamu ila kwa chati.lol
    one day nitakutafuta tufahamiane nipate inspiration.
    ni mimi mdada

    ReplyDelete
  3. dada ongela sana kwa besidei yako, epi besdei 2 u
    epi besdei 2 u
    epi besdei dada makani,
    epi besdei 2 u

    sasa dada hopsitali ya temeke haina maji wala vitanda vya kutosha tuongee na nabii yohana mashaka ambaye ndiy mgombea mkuu wa temeke alte maji na kutengeneza balabala yetu, foleni mbaya sana na mashimo,,

    ReplyDelete
  4. Mzee Ambali, Lizu Hotel, MafiaFebruary 24, 2010

    Hongera Mama mwenye watoto na wajukuu kwa kutimiza umri huo.
    Sasa achana na pombe na umrudie Mola wako na ufanye ibada kwa wingi. Hata nyani wazee huacha kurukia miti wakishafikisha umri mkubwa kama wako.
    Happy Birthday 2 U

    ReplyDelete
  5. thats so nice,,,,,, wud luv to do it 4 my mam... hongera sana

    ReplyDelete
  6. You are not just a mother and a granny, to us, your children, you are a WORLD!! We love you mom!!

    Austin

    ReplyDelete
  7. Wow Auntie Bite! It surely meant alot to you! Happy birthday again and thanks for appreciating the day!!!!!Ni mimi Niece wako umenipa ujiko! Lola

    ReplyDelete
  8. NICE KEKI SORRY IMETENGENEZEWA WAPI NAOMBA CONTACT PLEASE PLEASE

    ReplyDelete
  9. kuna watu wengine wanapenda kuisemea mioyo ya wenzao ; sasa wewe inakuhusu nini kuwambia mama wa watu habari ya pombo aisee kila mtu kaburini anaingia peke yake wewe ya kwako unayajua ? acha unafiki ,,,,,,

    ila mama ummenda age duu na hizo nywele zako au mambo ya mchina

    hongera mama yangu ... i wish was my mom maana wangu alishatangulia mbele ya haki !

    ReplyDelete
  10. Hongera sana kwa kufikisha miaka 55. Tanzania huo ni umri mkubwa tu. Kwenye nchi za watu bado kijana sana.

    Lakini hiyo keki ya bia????? halafu unamshukuru MUNGU kwa kukupa miaka 55 hapa duniani tayari, nashindwa kubalance hesabu hapo!!!!!

    ReplyDelete
  11. mama yetu usijali hao wachache wanaohoji ya duniani, yao hawayajui wanakalia boriti za wengine. hongera sana mama tulikupenda, tunakupenda na tutaendelea kukupenda. Mungu akujalie miaka mingi zaidi yenye amani na furaha. stay blessed Mum.

    mwanao ughaibuni-nitakufacebook.

    ReplyDelete
  12. Congratulations Mama Rena...I know you went through alot in your family-(Loosing your hubby $ daughter), but keep doing what you are doing.Thats why we have family and friends for support. Happy 55th birthday. May the Lord bless you.

    The cake looks great..Yummy!!

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Beatrice na mshukuru Mungu, kwani wengi wamekutangulia mbele ya haki, baadhi wadogo kwako na wengine walikuzidi kidogo... ila kila mtu na wakati wake. Kila tusherehekeapo tuwakumbuke waliotutangulia, and that will make us appreciate life more.

    Stay blessed.

    UK

    ReplyDelete
  14. hongera kwa kutimiza 55,we bado kijana tu unaweza endelea kurukia miti zaidi sema tu sikuhizi miti mingine noma sana ina mpaka trojan horse.
    celebrate life and mourn death!!! ila mungu na serengeti nadhani haimechishi:-)))

    ReplyDelete
  15. Hongera Aunt Bite kwa kusheherekea b'day yako. Mungu akuongezee mingine 50. Joana

    ReplyDelete
  16. Flavia MwombelaFebruary 25, 2010

    May God continue to bless you my auntie... I dont understand - why are people soooooo afraid to say who they are... if you want to make a comment... tell us who you really are. And for those with negative comments about my aunt...you don't even know her.... so get a life. Love you tons auntie!!!

    ReplyDelete
  17. happy birthday mamaaaa.u look great mtu hawezi amini u r 55 kip it up ni maajaliwa au kujitunza?me niko 35 watu huwa hawaamini wanadhani nadanganya wanafikiri niko 25 natamani nikiwa 55 nionekane kijana kama wewe

    ReplyDelete
  18. Hongera sana Bibite! Mimi ni mmoja wa watoto wako pia, am so happy for you...you are still going strong...ntakuja kukupa serengeti soon hapo salenda....

    Haters...Pleaaase!!!!!! That's her life haiwahusu whether she drinks or not.....fanyeni ya kwenu...you don't know jack about her... ni hayo tu

    ReplyDelete
  19. jamani hivi wapi kumeandikwa pombe hairuhusiwi kabisaaa kama ni kanisani mi najua hapana,kuna ule wakati wa kushiriki kuna mvinyo una alcohol kibao,inachokatazwa ni matokeo na matendo mabaya ambayo watu wanafanya wakinywa pombe kama unaimudu hufanyi mabaya kunywaaaa mpaka basi,ni swala binafsi sana na kwa maana hiyo mi naona halikatazi ukaribu na mungu,
    hey it seems huyu ni good mama na bibi on her age anajua vitu vingi so kunywa serengeti mi naona ndo starehe yake msifuatefuate kwanza big up kwa kutumia product ya tz na uchumi ukue
    as for msiokunywa pombe mkifiri mtaenda peponi there is more to that than being sober
    happy birthday mama

    ReplyDelete
  20. Wabongo bana...sasa nyiemlitaka amshukuru nani..shetani?? acheni kuwa na akili fupi kama funza...mungu lazima ashukuriwe kwa kila jambo na kila wakati hata kama unakunywa bia waweza kumshukuru na akakusikia binadamu ndio mnataka kuleta ubaguzi...yani kuna watua ambao wangepewa hata dakika moja tu ya kua God watu kama milioni ishirini ivi wangekua wameshaangamia...mwacheni mungu aitwe mungu....

    ReplyDelete
  21. wewe annon apo juu acha fiksi wewee kanisa gani linakunywa pombe,labda lenu tu!!ni mvinyo usiotiwa chachu yani ni km champagne ya matunda,,,

    mh hii keki sijui!!

    ReplyDelete
  22. Hongera daada, Mungu akuweke na akuzidishie umri na afya njema;

    Nyie mnaongelea pombe hayo ni maamuzi binafsi ya mtu msiyaingilie pommbe haikufuanyi usimche Mungu unaweza usiwe mnywaji pombe lakini ukawa mzinzi na muasherati ipi bora?

    ReplyDelete
  23. Hongera Mama Bite... Mdogo wangu Austin hongera... Nimeipenda sana zawadi ya aina yake tena kwa mama wa 55yrs... I wish na mimi nimfanyie hivi Mama yangu akitimiza miaka 60 Mwakani...

    Anony wa Wed Feb 24, 02:41:00 PM - Michuzi hawezi kuweka tangazo la SERENGETI ambao wapinzani HATARISHI wa Ndovu ambayo ni wadhamini wa Blog hii.

    Kwa upande wa wale wanaodhani Dada Bite hatakiwi kunywa...kusherehekea B'day yake hivyo... Kaeni chini mjiulize duniani mmekuja kufanya nini??? Ni hayo tu... MDAU wa V2 Bariiiiidi...

    ReplyDelete
  24. Patrick TsereFebruary 25, 2010

    Dada Bitte hongera. You are only 55 years young.Endelea kufurahia maisha dada. Umri ni takwimu tu. What you have in your mind is what you are. Hakuna cha kujutia. Do what you like best my sister.

    "Whether you think you can or think you cant, either way you are right" (Henry Ford[1863-1947]). Kama unaipenda safari kunywa kama huipendi yote sawa dada. Live from inside out and not the other way round. Cheers! cheers! cheers!

    ReplyDelete
  25. You mean a world to all of us,we love you and thank God for having you in our life may god bless you auntie and Protect you so that we can keep hearing your wise words.

    Hapi besidei

    Queenrahel

    ReplyDelete
  26. Bite, kula maisha mama yangu..manake maisha yenyewe ni mafupi na hayana guarantee!! why should you stress yourself na hujui kama kesho utaamka ama vipi?? spoil yourself and always be happy sweetheart! you deserve it big time!! Love you loads.... mwanao Reena!

    ReplyDelete
  27. Woooote nimewasikia wajukuu wangu!!
    Kuna wacha mungu na wasio, japo sina kipimo.
    Umri wa mama huyu kwa hali ya maisha ya mtz wa kawaida anastahili kupongezwa, namsifu kwa weredi wake kama alivyoeleza hapo juu. Nanyi wachangiaji toka kila pembe ya dunia hii tujiulize kabla hatujatoa maoni yetu, maana yaweza hata wakati mwingine kuchafua hali ya hewa ktk blog hii ya jamii. Nionavyo mimi kuna watu wanajiona wako juu kuliko wengine wakati sivyo, hawa unawatambua kwa maoni yao tu, na hii ni kwa jeuri ya vijesenti walivyo navyo kwa wakati anatoa maoni na hali aliyonayo wakati huo.... yawezekana akawa kiserengeti zaidi au la...
    kuna kundi lingine wao wanajiita walokole.Kwao kitendo cha kuona nembo ya SERE... basi walishahukumu.
    JAMANI WAJUKUU ZANGU HAYA NI MAPITO JARIBUNI SANA KUFANYA YALIYO MEMA, KWANI HATA MAAZIMISHO YA MIAKA 55 HAYAKUWA UTAMADUNI WETU. TUSIKWAZANE KWA ULIMBUKENI WETU, TUYATAMBUE KAMA MAPOKEO NA NDIO JAMII TUNAMOISHI " THE LIFE IS HOW YOU MAKE IT N IT REFLECTS HOW U HAVE BEEN SOCIALIZED" Kwa leo naomba niishie hapa.

    ReplyDelete
  28. "Walevi na waleweshaji hawataingia ufalme wa mbinguni"

    ReplyDelete
  29. huyu ndo mama reeeeeeeeeeeeeena wa upanga.hongera

    ReplyDelete
  30. aloo hivyo huyu ndio mama yake marehemu salome makani?

    ReplyDelete
  31. Samahani..kuuliza siyo ujinga....hivi huyu ndiye mama wa Grace Makani?

    ReplyDelete
  32. huyu si mama yake Grace Makani,huyu ni mama yake marehemu Salome Makani.

    ReplyDelete
  33. Mama, Hongera.....nina mwaka mmoja sasa tangu nimeanza kufurahia Serengeti na sijajutia.....
    Good Times Last Longer.....

    Hongera kwa kutimiza 55years.....

    ReplyDelete
  34. Dada Beatrice!!!
    Hongera sana na Mungu akubariki!!
    Pokea salaam zetu za dhati!!
    Ni sisi Classmates wako wa St Xaviers===Class of 1972
    Fawzi
    kwa niaba ya Soledad Brothers [Pita, Mika, Marco, Hamisi}

    ReplyDelete
  35. Happy bday mama.. yaani bdate yako ni sawa na ya rafiki yangu anaitwa Pamela Salehe yuko pale Hazina makao makuu.. tena anafanana sana na wewe hata wanao.. Again Happy bday mama n Pam!

    ReplyDelete
  36. Beatrice P. MakaniMarch 01, 2010

    Ankal Michuzi Asalam Aleikhum!
    Wasomaji wa Blog hii ya jamii Asalam Aleikhum.
    Nakushukuru ankal kwa kuweka hepi besdei ya kuzaliwa kwangu katika blog yako hii mahususi. Pia napenda kuwashukuru NYOTE kwa 'comments' zenu. Mlionipa hongera Asanteni sana, waliotoa maoni mbali mbali asanteni sana. Wale waliokasirika, poleni sana lakini pia nashukuru mmepata pahala pa kupumua, ingekuwa sio hiyo mgekuwa bado mnaumia.. poleni sana kutoka katika sakafu ya moyo wangu.Wale walioumia kwa niaba yangu kutokana na maoni mbali mbali pia nawapa pole sana mjue 'Nyani mzee amepitia mishale mingi' Ndio mishale hiyo. Ili mradi mnaishi dunia hii, na kuwa na umri mkubwa, mishale kama hiyo ipo, uzuri mishale hiyo wala haina sumu mtapona tuu. 'UVUMILIVU' muhimu. Tupo duniani kama 'CHARACTERS' au wasanii wa 'MOVIE' au sinema moja inaitwa 'ULIMWENGUNI' Nami 'character' yangu ndio hiyo nawe yako ni hiyo uliyonayo. Onyesha au usionyeshe lakini kila mmoja ana sehemu yake ambayo ni nadra kufanana kwa kila jambo na 'character' ya mwingine. Ili mradi uitumie kwa kuleta furaha,amani,upendo na maendeleo kwa wote walioma katika 'movie' yenyewe.
    Uhusiano wangu au wako na Mwenyenzi Mungu ni 'PERSONAL' wa kipee haufanani wala haulinganishi na mwingine, kwa wale wanaosoma Biblia Mungu alisema nitaweka Nira yangu moyoni MWAKO hakusema mioyoni mwenu la hasha. Nira ni dhumuni lake juu yako. Kila mtu amepewa 'TALANTA' yake pia. Basi zalisha kadri ujaliwavyo.. usikae na kumlaumu aliekupa hiyo Talanta kuwa hafai au mbona Beatrice anakunya Serengeti sio kazi ya talanta uliyopewa. AMRI TUPENDANE, Watanzania tunashindwa kutekeleza amri hii ndio maana tunapata taabu sana kupata maendeleo ya haraka. Happy birthday to you too 2010.
    Beatrice mama Reena 'Salome' Austin, David na Anthony.. mke wa the 'late' 'Nicco'
    Thanks for your time. Love you all

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...