DAR HAIWEZI KUKUZA SOKA,
TWENDE MIKOANI SASA
Michuzi,
Naomba kuweka mada ifuatayo mezani wadau waijadili. Kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa ikijitahidi kuinua kiwango chake cha soka, lakini juhudi zinazofikiwa ni kidogo sana, pamoja na kwamba rais wetu mpendwa amejitoa kikamilifu kusaidia sekta ya michezo.
Tumeona vijana wetu wanavyojitahidi, pamoja na walimu wao, bila kujali wako katika timu gani, lakini tunaendelea kufanya vibaya kimataifa.
Maoni yangu ni kuwa labda tungehamia sasa mikoani kwenye hali ya hewa tofauti na staili ya maisha tofauti, na huko tujaribu kuimarisha timu za huko kwa kutafuta vijana waliojengeka vizuri kimwini, wenye nidhamu na hata wenye IQ ya juu.
Ningewashauri wadau wenye pesa zao, kama wale walio na timu za Manyema na Azam kufikiria kuweka juhudi kama hizo katika mikoa kama vile Mwanza, Arusha, Kigoma, Mbeya na hata Manyara.
Kwa uzoefu nilionao, Dar es Salaam haijawahi kutoa wachezaji nyota weeengi vile. Mastaa wengi wamekuwa watokea mikoa ya Mtwara, Tanga, Kigoma, Mbeya, Kagera, Mwanza na hata Shinyanga na Singida.
Hebu sasa tuachane na Dar es Salaam kidogo na tuangalie tena huko mikoani tuone tutafika wapi. Ninachojua ni kuwa hata wachezaji wazuri wakija Dar baada ya muda kiwango chao huwa kinashuka.
Kama ni hali ya hewa au mengineyo sijui ila POINTI yangu ni kwamba sasa tuangalie ni kwa kiasi gani tuanweza tukaunda timu imara huko huko mikoani, na hata timu ya taifa iwe trained outside Dar es Salaam. Wadau mnaonaje????
Nitoe mifano michache. Ghana wachezaji wanatoka Kumasi na Tamale na sio mji mkuu wa nchi hiyo Accra. Nigeria wengi wanatoka Ibo land na sio Abuja au Lagos. Zambia wachezaji wazuri hawapo Lusaka ila Copper Belt.

Mdau Deo Peters
Monduli
Mdau Deo itabidi uuombe radhi mkoa wa Morogoro kwa kuukose yaani unweza kuandika mikoa inayotoa wachezaji ukaiacha Moro unaweka Singida na shinyanga. Hivi hawa kina King kibadeni.Manga,Sembuli,Gaga,Mogela.Omary hussen.Ngurungu.Shilingi.Shiwa. Hao ni baadhi tu nikisema ni wapange foleni kuanzia Kariakoo shimoni nafikili watafika Mbagala zakhem.
ReplyDeleteMdau
kisiju pwani
kuna hali ya kuipendelea dar kwa kila kitu.Kama serikali yenyewe haitaki kuendeleza viwanja kwanza vya mikoani,unategemea nini?IPO SIKU,LIGI ITAKUWA NA TIMU ZA DAR TU.NCHI HII MPIRA UTAPANDA SANA SIKU VILABU VIWILI SIMBA NA YANGA KIMOJAWAPO KIKITEREMKA DARAJA.ONA SASA LIGI HAINA HATA LADHA,YANGA NA SIMBA NDIYO ZINAZOPEWA PESA,NA NDIZO ZINAZOSHINDA KILA MECHI.HAKUNA USAWA HAPA.NA TULIVYO WASHAMBA,HUKU MIKOANI ETI UNAKUTA TAWI LA WANACHAMA WA SIMBA AU YANGA.KAZI YAO NI KUHUJUMU TIMU ZA MKOANI ZISHINDWE ZINAPOKUTANA NA HIZI YANGA AU SIMBA,SASA KWA HALI HII MPIRA UTAKUA?LIPULI ILISHUKA DARAJA KWA AJILI YA MAMBO HAYA YA KISHABIKI YA YANGA NA SIMBA
ReplyDeleteMdau wa soka
ARUSHA
NAAM MIE NI MWENYEJI WA KANDA YA KASKAZINI LAKINI NAIFAGILIA KANDA YA ZIWA TANGU ZILIPOKUFA TIMU ZA PAMBA YA MWANZA NA ILE YA MBEYA (WANALINDANDA) MIE SIJAONA MASHINDANO YA LIGI KUU YAKIWA NA MVUTO TENA! NAFIKIRI CHIPS MAYAI ZA DAR NDIZO ZINAZOHARIBU WACHEZAJI MARA BAADA YA MAZOEZI. KANDA YA ZIWA UGALI KWA SAMAKI NDIO LISHE KWA NINI MCHEZAJI ASIWE NA NGUVU? NA HII VILE VILE KULE MBEYA UGALI UPO WA KUTOSHA SASA SIE TWA NG'ANG'ANIA CHIPS. HATUTAFIKA MBALI.
ReplyDelete