TIME LIMIT FOR SENDING PATIENTS ABROAD FOR TREATMENT
(TUTATUMA WAGONJWA NJE YA NCHI HADI LINI??)
By Raphael Mallaba Jr
Ni miaka mingi sana wakati nikiwa kijana mdogo nilikuwa nikisikia tu kuwa wagonjwa Fulani wenye magonjwa mbalimbali wanapelekwa nje ya nchi kwa ajiri ya matibabu, aidha katika kipindi hicho katika mawazo yangu mafinyu nilijua kuwa Tanzania haina madaktari wakutibu magonjwa hayo au hakuna vipimo husika.
Kweli sana tuko karne ya 21 na taifa letu likiwa linasherehekea uhuru wake wa karibu miaka 50 lakini kila mwaka ninaendelea kusikia kuwa wagonjwa wanapelekwa nje ya nchi kutibiwa kama India na nchi zingine.Maswali yangu ni mengi sana ila siwezi kuyaandika yote katika hii makala moja ila yananipa wasiwasi sana wa hii nchi yangu Tanzania kwani ni aibu sana kwa taifa kutuma wagonjwa nje ya nchi kila mwaka utafikiri taifa halina madaktari .
Moja, je tatizo hakuna madaktari wa magonjwa hayo husika? Au je tatizo ni la hao madaktari kutojiamini na wanalofanya?Nasema hivyo nikimaanisha kuwa kama ni madaktari nauhakika kabisa wapo na wanaweza kabisa kutibu au kufanya upasuaji wa wagonjwa husika. Nakubaliana kipindi cha nyuma kulikuwa na upungufu sana wa madaktari wa upasuaji wa magonjwa ya moyo( cardio surgeon) lakini kuna madaktari zaidi ya 100 walimaliza masomo yao miaka miwili iliyopita nchini India na sasa wapo hapo hospitali ya Taifa ambao walikuwa wameandaliwa maalumu ili kuanzishwa kwa huduma za upasuaji wa moyo Muhimbiri.
Sasa bado kuna haja gani ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi?
Pili, Inawezekana wakasema tatizo ni vyombo vya huduma vya magonjwa husika labda havipo nchini mfano MRI,CT,Laparascopy,Endoscopy,and other Radiological Imaging.Kweli vyombo vingi vya kisasa ni gharama sana na hiyo ndo inayosababisha gaharama kubwa za matibu sababu kabla ya kupata diagnosis lazima kwanza upitie vipimo husika.Hivi vifaa nauhakika kabisa kwa mahospitali makubwa kama Mhimbili,Bugando, KCMC n.k vyote vipo labda kwa new generation vinaweza kukosa.
Hata kama havipo je serikari na wizara husika inamalengo gani? Je Tanzania itaendelea kuwa nchi ya kutuma wagonjwa kila mwaka nje ya nchi? Je mnatambua kuwa gharama za mamilioni manazotumia kila mwaka kutuma wagonjwa nje ya nchi si zaidi ya miaka miwili vifaa vyote mhimu vingeweza kununuliwa?na watu hao kuendelea kutibiwa nyumbani kwa gharama nafuu kabisa?
Tatu, Kwa nini tuwe wategemezi kila siku au ni kutojiamini kwetu ndo kunakosababisha haya yote ?
Kama hakuna mda maalum wa kusitishwa kutuma wagonjwa nje,basi hili litakuwa ni dili la watu wakubwa maana kila wanapotuma wagonjwa kunakuwa na percentage yao wanayopata kwa hiyo kazi hii itakuwa ni ya kudumu,hata kama kuna madaktari na vifaa vya kutosha bado wagonjwa watapelekwa nje ya nchi.
Hii ni aibu sana kwa nchi na madaktari nchini kwani inaonyesha kuwa tatifa zima halina madaktari bingwa wakuweza kutibu wagonjwa wao.
Inanikumbusha siku moja rafiki yangu alikuwa akipata matibabu nchini China na madaktari wakamuuliza je nchini kwenu hakuna madaktari wa kumfanyia hii operation au hamna vifaa? Lilikuwa ni swali gumu sana kwangu ukizingatia gharama nchini China ni ghari sana ukilinganisha na nyumbani.
Naomba waziri wa afya na wizara husika ilifikirie kwa undani hili swala, kwani nilazima ifikie mahali mabo ya kuzoeleka tuyaache kabisa na tufanye vitu vyenye tija kwa taifa letu. Au mnataka hili nalo mpaka aje mwekezaji kutoka nje awaambie ndo mkumbuke kuwa uwezo mnao??
God bless Tanzania
drmallaba@yahoo.com
P.R.CHINA.

Kuna wakati fulani mgonjwa alipelekwa India alipofika kule wakamwambia operation yako inabidi tumuagize expert wake toka nje ya nchi cha ajabu aliitwa daktari mtanzania toka tanzania kufanya ile operation!!!!!??? Hebu fikiria gharama za matibabu na usafiri zilizotumika wakati ile operation ingeweza kufanyikia Muhimbili!! Du jamani maisha bora kwa kila mtanzania na Kilimo kwanza ELIMU na MATIBABU baaden.
ReplyDeletemadaktari bingwa wapo wengi sana bongo ila tatizo ni vifaa na mazingira hivyo basi wengi wanajikuta wakifanya kazi zilizo nje ya profession zao au wanakimbilia nje ya nchi ambapo watatumia taaluma yao
ReplyDeletemdau kwanza nakupongeza kwa kuweza kuandika na kutoa dukuduku lako kuhusu swala la wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa mimi naomba nikuambie yafuatayo
ReplyDelete1. madaktari wa kitanzania ni wazembe sana kwa kila walichosomea ushaidi ninao na mkubwa zaidi ya aliyekosea kichwa na mguu,pia mi nilipo wagonjwa wengi sana wanakuja hapa india wagonjwa wengi wanakuja baada ya kushindikana kwa matatizo madogo sana lkn yamewashinda ni aibu sio kubwa kiasi kwamba mpaka nashangaa ni kwanini? serikali imasomesha madaktari na wanafikia kuitwa madaktari bingwa
2. wivu
ukifuatilia kwa karibu yule daktari aliyekosea ilifanywa ujuma hili aonekane mzembe
3.kupata pesa kwa haraka bila kuangalia utu
ukiangalia hospitali zetu za private hakuna hata moja inayofanya maajabu kwa kusema ukienda na ugonjwa ukiachilia malaria unaweza ukasema wamejitaidi je na huko ni serikali au na ukienda unaumwa kichwa tu cha kawaida unaandikiwa dawa hili stock yao ya phamacy iishe waagize nyingine
4.kutosikiliza wagonjwa matatizo yao
unajua hili ndio tatizo kubwa madaktari wengi awasikilizi wagonjwa nini matatizo yao ukisema tu najisikia vibaya unaambiwa kuwa maralia ndio ugonjwa wanaujua na ukisema wakapime damu wao wanajua ni ukimwi tu
kwakweli kazi hii inataka mtu mwenye moyo sana na inaitaji mtu kijitoa na sio suala la maslahi tu mimi naamini kuwa kupenda kazi na kujitoa kwa kutoa hii uduma mungu anaweza kukulipa kwa namna yoyote hile tatizo la madaktari wetu awatafuti self actualization